UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

Hivi kwa nini kila mnapohojiwa kuhusu mustakabali lazima muainishe majibu na CCM? ?!!!
Ratiba tofauti wakati time limit inatolewa na tume??!!!!

Mtajifunza tu

UKAWA hawafanyi mambo yao kwa kufuata CCM. Wanajua ratiba ya tume ilishatolewa. Sasa wao hawawezi wakaanza kuvuruga ratiba walizojipangia kwa sbb ya kufuata mihemuko ya CCM. Ndicho nilichokisema. UKAWA hawafanyi mambo kwa kufuata CCM, wanafanya mambo kivyao. Na sisi kwenye technical committee tuko makini sana. Hatuwezi kuwapa MAFISADI nchi halafu tukabaki salama
 
kila mtu anajua mgombea ukawa ni slaa.
labda wamrubuni warioba ama lowasa ndo itakuwa na mvuto kidogo
 
kila mtu anajua mgombea ukawa ni slaa.
labda wamrubuni warioba ama lowasa ndo itakuwa na mvuto kidogo

Huyo Dr.Slaa mnamtaja kwa sababu ya kuogopa kivuli chake cha mwaka 2010. UKAWA wana vichwa vingi watu mtakuja kushangaa. Hata Dr.Slaa alipoingia kwenye ulingo mwaka 2010, CCM hawakutarajia. Bila mazingaombwe yenu yale tungekuwa tunaongea mengine
 
Wanamtangaza nani tena. Mgombea wao wa kudumu si Mzee Slaa?
 
Wanamtangaza nani tena. Mgombea wao wa kudumu si Mzee Slaa?

Mgombea wa kudumu lini? Dr.Slaa amegombea urais mara moja tu, 2010 alipowakimbiza mchakamchaka mpaka ikabidi mfunge kwa kutumia goli la mkono. Kikwete aligombea mara 2, 2005 na 2010, kwa hiyo naye alikuwa mgombea wa kudumu? Pia Dr.Shein anarudi mara ya pili, ni mgombea wa kudumu? Kwa nini iwe nongwa kwa Dr.Slaa kama ataamua kugombea urais mara ya pili?

Kwa nini watu wa CCM mnakuwa vipofu namna hiyo? Acheni siasa nyepesi. Mmekifanya chama kama pango la wezi, mafisadi na wanyang'anyi, na CCM tuliyokuwa tunaifahamu, ikiwa ya wakulima na wafanyakazi sio hii ya leo.
 
haraka ya nini wasubiri news nyingi zitoke dodoma....
 
Time and tide waits for no body weka misamiati weeeee clock is ticking. . . . .

hahahahahahahah kwani mgombea urais kwa ticket ya ccm ni nani? now ndo wapo kwenye mchakato wa kumpata na ilikuwa kwenye ratiba ya ccm kumbuka ukawa ni muungano wa vyama so inabidi wampate mgombea makini mwenye uwezo wa kupambana na wazee wa bao la mkono kumbuka hii ni game so unatumia mapungufu ya mwenzako ku win ktk political games
 
UKAWA hawafanyi mambo yao kwa kufuata CCM. Wanajua ratiba ya tume ilishatolewa. Sasa wao hawawezi wakaanza kuvuruga ratiba walizojipangia kwa sbb ya kufuata mihemuko ya CCM. Ndicho nilichokisema. UKAWA hawafanyi mambo kwa kufuata CCM, wanafanya mambo kivyao. Na sisi kwenye technical committee tuko makini sana. Hatuwezi kuwapa MAFISADI nchi halafu tukabaki salama

Labda, basi tuwe na kasumba ya kujenga hoja bila kuhusianisha ambayo hayajaulizwa, sababu ukitaja unakuwa kama huna muongozo binafsi ila una react kutokana na unayemtaja. Ni hilo tu wazee wa technical committee
 
UKAWA hawaendeshi mambo kwa mihemuko. Bado wako kwenye mchakato na sio Jumamosi kama unavyodhani. Hawo wamekudanganya. Sisi tuko kwenye UKAWA technical committee hatuwezi kuruhusu mbinu zetu zijulikane na maadui. CCM kwanza wachinjane huko Dom sisi tuna ratiba zetu tofauti na vikao vya CCM

Kwani kumtangaza mgombea kwenu kuna mbinu gani?? Mlipokaa kikao mlijadili kuhusu tume huru!!?
 
hahahahahahahah kwani mgombea urais kwa ticket ya ccm ni nani? now ndo wapo kwenye mchakato wa kumpata na ilikuwa kwenye ratiba ya ccm kumbuka ukawa ni muungano wa vyama so inabidi wampate mgombea makini mwenye uwezo wa kupambana na wazee wa bao la mkono kumbuka hii ni game so unatumia mapungufu ya mwenzako ku win ktk political games

1. Exactly mchakato na wao wako one step ahead na kampeni nusu tayari parallel na kusaka wadhamini sasa sijui hapo mapungufu ynakaa upande gani wa equation. . .
2. Wagombea kwa mujibu wa vyama wako wawili tu na umakini wao upo labda ndio maana vyama vyao vimewatumia katika chaguzi zilizopita sasa ukiniambia "makini mwenye uwezo" maana yake ni kuwa mmoja sio makini au hana uwezo nini??!!
3. Game, sawa na ni kweli kuna home and away. . . .marefa, kamisaa, wadhamini, warusha matangazo. . . .wote washika dau. . .
 
Kwani kumtangaza mgombea kwenu kuna mbinu gani?? Mlipokaa kikao mlijadili kuhusu tume huru!!?

Kumtangaza mgombea kuna hitaji mbinu mkuu. Hata CCM wenyewe hawaamki tu asubuhi wakatangaza mgombea wao. Ni mchakato mrefu unaoambatana na mbinu na mikakati ya kisiasa kwa ajili ya kutafuta ushindi. Suala la Tume wewe mwenyewe unauliza swali ambalo majibu yake unalo.

Hili bunge linaloendelea ndilo kama CCM wangekuwa na nia wangeleta hio mswada, lakini badala yake wameleta miswada ya kifisadi. Nadhani unajua kilichotokea mpk wabunge wa upinzani wakatoka bungeni.

Sasa kutokana na hilo, UKAWA wanajipanga kukabiliana na tatizo hilo kwa njia nyingine, ambazo wahusika watakuja kuwajulisha kupitia waandishi wa habari walipofikia
 
Kupitia waandishi wa habari tena??!!! Hiyo inaweza kuwa na nguvu kuliko katiba sio??!!!
 
Kupitia waandishi wa habari tena??!!! Hiyo inaweza kuwa na nguvu kuliko katiba sio??!!!

Katiba ni mhimu sana mkuu. Lakini wewe mwenyewe unajua fika kuwa katiba haiwezi kufanyiwa marekebisho chini ya utawala huu wa CCM, kwa sababu wao ndio wanufaika wakubwa wa katiba hii. Hii ni katiba inayofanya CCM iwe ni chama dola, na sio chama cha siasa chenye hadhi sawa na vingine katika uwanja wa siasa. Sasa wapinzani hawana namna ya kufanya, nadhani unakumbuka bunge la Katiba kilichofanyika.

Pia ninaposema viongozi wa UKAWA wataongea na waandishi wa habari, ni kwa ajili ya kujulisha umma wa Watanzania michakato mingine ya kiuteuzi kwa Rais, wabunge na madiwani ambayo kwa sasa inaendelea ndani ya kila chama kinachounda UKAWA. Sasa maswala ya Tume hayo sio mahali pake hapa.

Ni mambo ya kiufundi zaidi. Lakini ninachojua kuna mikakati ambayo iliashaanza kufanywa ila kukabiliana na mambo yote ya wizi wa kura, gori la mkono n.k. Sasa sidhani km viongozi wa UKAWA wataweza kuzianika hizo mbinu kwa sasa kwa sbb za kiufundi na kimikakati.
 
Ukawa haina haja ya kumtangaza kwa sababu tayari tunamjua,ni Dr Slaa.

Ila tusichokijua ni kama Profesa Lipumba atagombea urais kupitia CUF, hili litategemea na CCM watamchagua nani.

Muhimu kutambua kuwa chama kitakachotoa mgombea urais ndicho kitasomba wabunge viti maalum wote wanaotokana na kura za mgombea urais na kitasomba ruzuku zote zinazotokana na kura za urais.CUF wasipotoa mgombea wanapoteza haya.
 
Katiba ni mhimu sana mkuu. Lakini wewe mwenyewe unajua fika kuwa katiba haiwezi kufanyiwa marekebisho chini ya utawala huu wa CCM, kwa sababu wao ndio wanufaika wakubwa wa katiba hii. Hii ni katiba inayofanya CCM iwe ni chama dola, na sio chama cha siasa chenye hadhi sawa na vingine katika uwanja wa siasa. Sasa wapinzani hawana namna ya kufanya, nadhani unakumbuka bunge la Katiba kilichofanyika.

Pia ninaposema viongozi wa UKAWA wataongea na waandishi wa habari, ni kwa ajili ya kujulisha umma wa Watanzania michakato mingine ya kiuteuzi kwa Rais, wabunge na madiwani ambayo kwa sasa inaendelea ndani ya kila chama kinachounda UKAWA. Sasa maswala ya Tume hayo sio mahali pake hapa.

Ni mambo ya kiufundi zaidi. Lakini ninachojua kuna mikakati ambayo iliashaanza kufanywa ila kukabiliana na mambo yote ya wizi wa kura, gori la mkono n.k. Sasa sidhani km viongozi wa UKAWA wataweza kuzianika hizo mbinu kwa sasa kwa sbb za kiufundi na kimikakati.

Time factor. . . . .delay tactics. . . .Offside trick. . . .
 
Ukawa kama ligi ya marekani hv wanasubiri akina beckam na gerad watoke EPL
 
Mchungaji Masanilo UKAWA si walisema mpaka August 4 mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Ameharibu kote, angekuwa ni mtu mwenye kufikiri kwa mapana wala asingeleta maoni ya namna hii maana yanahamasisha mgawanyiko badala ya mshikamano ndani ya UKAWA. Fikiria wafuasi wa CUF nao wakija na mawazo ya namna hii hali ya UKAWA itakuwaje?

Tupunguze kuleta maoni yenye mwelekeo wa kuchochea 'Usisi' na 'Uwao', ndiyo mgawanyiko wenyewe huo. Namalizia kwa kusema, maoni yake hayaonekani kuenzi malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa UKAWA, yamejaa chembechembe za kupandikiza migawanyiko ndani ya huo muungano.

Kwa hiyo unafikiri Rais lazima awe mchumi? Vipi afya, elimu, miundo mbinu nk? Kwa nini Prof asiwe waziri wa fedha ili awe technical zaidi?
 
Back
Top Bottom