Ukatili huu!!

Haya yote yanatokea ni kwasababu ya utawala na uongozi wa nchi mbovu. Kama mafisadi wangethibitiwa kuibia nchi yetu tungetumia rasilimali zetu kuwasomesha watoto wetu bure na ajira ingepatikana na hao vijana wanaokwapua simu na kwenda kuuza ili wapate mlo mmoja wa siku wasingekuwepo!! Hivyo basi haya mabo ya vibaka yangepungua kwani mgawanyo wa maliasili ya Taifa ungekuwa equitable na tofauti ya matajili na maskini isingekuwa kubwa kama ilivyo sasa. Mbona wananchi hawaoneshi hasira kwa wale wanaotukwapulia mabilioni ya fedha kwa kusaini mikataba mibovu badala yake wanawaua wakwapua simu?
 
Bwana weee hawa jamaa wakikukwapulia kitu chako cha thamani unachanganyikiwa kabisa.

Na hasa ikiwa umekitokea jasho, umepiga mzigo na kuchanga vihela vyako kwa kujinyima vingi halafu anakuja jamaa kuchukuwa kiulaini. Ule uchungu ulio nao hauna mfano.

Mimi walishawahi kunikwapulia handbag yangu ndani mulikuwa na simu ya gharama, fedha na vitu vyengine kama kadi.

Ee Mungu nisaidie nisiwe na fikra za Ibilisi lakini sijui ningechukuwa hatua gani kama ningemwona wakati anakwapua.
 
Je wewe huwa hufanyi makosa? au wewe ni mtakatifu na je huyu kibaka sijui mwizi dhambi zake ndo KUBWA sana mpaka tusitishe maisha yake?

Maovu yote makubwa yalianza na mambo madogo kama hayo ya kukwapua simu... kama kuna lolote ambalo jamii inaamini inaweza kuwa dawa basi lifanyike hata hilo la kuwanyang,anya viroho vyao...hata wao wakikuwahi wanakuua hao!!!
 
Maovu yote makubwa yalianza na mambo madogo kama hayo ya kukwapua simu... kama kuna lolote ambalo jamii inaamini inaweza kuwa dawa basi lifanyike hata hilo la kuwanyang,anya viroho vyao...hata wao wakikuwahi wanakuua hao!!!
kweli kabisa mie nina uchungu nao walinirudisha nyuma sana hawa jamaa waliniibia gari langu mwenyewe nimekopa nikawa nakatwa hela huku gari limeshaibiwa mpaka leo nina hasira na vibaka/wezi/majambazi nikiona anapigwa uwa nashangilia kama naangalia mpira vile na siku wakijichanganya wakaja nyumbani kwangu nikawastukia lazima nimpe mtu shaba ya kichwa
 
The punishment must fit the crime. Why kill a person who hasn't kill, did not kill and would otherwise not attempt to kill. Majambazi yaki uliwa sawa ila hawa vibaka wa kawaida ambao huiba cha kuvutia bangi?
 
Jamani wewe unapopita mahali ukakuta watu wanampiga kibaka aliyekwapua simu wanamfanyia ukatil huu wewekama mwa JF unafanya nini??


attachment.php

Inauma sana na inasikitisha kuona maisha ya mwanadamu yanakatishwa kikatili.

Lakini upande mwingine wa shilingi ni kwamba vibaka ni watu hatari kuliko unavyoona huruma na hiyo picha.

Kushiriki kumuua au kutokumuua inategemea: Kama ulishawahi kuvamiwa au kuibiwa na kibaka, hakika unaweza kushiriki bila kusita.

Tunaoona huruma ni sisi ambao hatujawahi kupatwa na adha ya vibaka
 
Mimi nitapiga simu polisi, kwani kumtetea huyo kibaka ni sawa na wewe kutaka mvua ya mitofali!
 
Maisha ya mwandamu yoyote yana thamani sawa haijalishi,Tajiri,Masikini,Kibaka.Hakimu,Mwaminifu!!Chamsingi nikujenga utamaduni wakuheshimu sheria na kanuni!!Hata kama umeibiwa hauna ruhusa yakumtoa mwenziyo uhai!!Inasikitisha sana tena sana humu ndani ya JF kukuta Comment zinazoelezea kumkatisha Binadamu mwenziyo uhai!Utadhani tupo facebook!!!!Jali uhai usijali ulichochukuliwa!!nachokijua vibaka wote ninjaa,mifumo mibovu ya elimu,na umasikini uliokithiri na ndiyo maana vibaka wote hukaa sehemu zenye hali mbaya huwezi kumkuta kibaka Oysterbay,masaki,etc.
Hivyo basi nyinyi wan JF nimatumaini yangu kuw niwatu wenye upeo mkubwa mno kiasi hamuwezi kuthaminisha gold Chain na uhai!Je ukipeleka mtoto hospital dawa zikakosekana na mtoto akafariki huwa mnaandamana kufata Daktari ili mmtoe roho??
Mimi nilishakuta mtaani kwangu kibaka kashikwa na mbao kaiba saiti wanataka wamchome na anyetaka kumfanyia hivyo siyo mwenye mali nilisimama mbele ya umati mkubwa nikasema jamani mimi siwazuii ila wewe ndiye kinala ukimfanyia chochote huyu mwizi zaidi yakumpeleka polisi mimi wewe naenda kukushtaki kwa mauaji!!!nanikasema yeyote yule athubutu!!waliogopa wakaishia kumpiga manumi na nikamwambia wewqe ndiye uliyeibiwa mpeleke polisi!!!

MIMI SIUNGI MKONO KWA KUUWAWA KIBAKA WAKUKWAPUA SIMU NA HERENI,SIMU!!NAKUWAACHA WALIO HODHI NCHI YETU KULE BURYANULU NA WAZIDIKUACHA MASHIMO NA WANAENDELEA KUTUKEJELI ETI TUWAPE KURA!!Mwana JF funguka!:angry::cheer2:
 
Jamani wewe unapopita mahali ukakuta watu wanampiga kibaka aliyekwapua simu wanamfanyia ukatil huu wewekama mwa JF unafanya nini??


attachment.php

Hii inaonesha hatuna utawala wa sheria. Nchi zenye utawala wa sheria watu hawajichukulii sheria mkononi kwani nao wangekuwa wanaogopa mkono mrefu wa serikali! Lakini kwa hapa Tanzania, watu wanjua serikali yetu ina mkono mfupi sana na ndio maana wanaamua kujichukulia sheria mkononi kwani wanajua mkono mfupi wa serkali hauwezi kuwafikia.
 
Nikiona jiwe karibu naongezea ili asiamuke kabisa. Washenzi sana hawa

Once we appreciate the value of life, then we will reconsider what we normally do. Hapo huyo utakuta ama alikuwa anakwapua simu au fedha au uhalifu mwingine tuu. Ni rahisi kusema anastahili kufa lakini je wizi ulipwe kwa kifo? Ni kosa la kuua kwa kukusudia na uhaini ambayo adhabu yke ni kifo. Nadhani tufikiri mara mbili, kwa nini ameiba? Vipi juu ya hali ngumu ya Maisha? Je kuiba kwake si matokeo ya mfumo wa walio madarakani. Tujiulize kwa makini, na kama tukipata jibu kamili, tena sahihi basi anaestahili kufa hivyo siye aliyeiba, NI HAO WALIOKO MADARAKANI WANAOTEMBEA NA V8 ZINAZOTOKANA NA KODI ZA HUYO ANAESULUBISHWA KWA MAWE HAPO
 
Washenzi hawa, hamna lolote zaidi ya kuonea Wanyonge.

Kama mna ubavu si mkamtwange Rostam Azziz au Lowassa?

Kuna mama Mkapa pale anadunda na Wahindi kibao wakiwa na pesa za EPA.

Mramba na kundi lake wapo tu. Chenge ndiyo kwanza anagonga dada zenu na mnamchekea.

Mnakuja kupiga mawe Kibaka aliyelala njaa jana. Hamna maana kabisa. Si usiku mtoke mpambane na Majambazi?

Au mkisikia cha moto Mnazifyata? Kunguru Dume nyie.......

Si ajabu kama si akina Lowassa na CCM kumpe njaa kijana, asingeliiba. Mnaadhibu siye. Mnakata Majani na si Mzizi.
 
Jamani wewe unapopita mahali ukakuta watu wanampiga kibaka aliyekwapua simu wanamfanyia ukatil huu wewekama mwa JF unafanya nini??


attachment.php
Naomba hili liwe FUNDISHO kwa JK Aache kuwalinda MAFISADI, kwani iko siku tutawafikia. Na mikono Mikono ya Raia Kutoa Judgment Zaidi ya hii.
 
Ukweli unabaki palepale kuwa mwizi ni mwizi tu hata kama kakwapua simu hana tofauti na yule wa EPA.Hao wa EPA wanadunda kwa kuwa wananchi hawana uwezo wa kuwafikia, wangeweza kuwafikia na wao wangewafanya vilevile.Sioni busara yoyote kuwatetea hawa wezi kama wao wanaijua adhabu yao na bado wanakwiba.Binafsi ningewashauri warudi mashambani wakalime kama mji umewashinda. Kuwa na mfumo mbovu wa serikali usihalalishe watu kuibia wenzao wanaotolea jasho pato lao.Ni wangapi wenye hali ngumu lakini wanauvumilia umaskini wao?Hii tabia kama imewashinda jeshi la polisi na mahakama basi wananchi wawamalize tu ili watoe fundisho hata kwa wale waliokuwa na nia ya kuanza fani hiyo.:flame::flame::flame::flame:
 
Wawapige miguu wasiwaue jamani....!
The Following User Says Thank You to NATA For This Useful Post:

CBZ (29th September 2010)

Hongera CBZ umekuwa mtu wa kwanza kabisa kumtwangia thanks NATA, You have made up a remarkable History. Congratulations
 
Nikiona jiwe karibu naongezea ili asiamuke kabisa. Washenzi sana hawa

Kuna siku nilikua napita Coco beach,nikasema nisimame pale , kulikua na show ,ilikua siku ya Iddi . Jioni ilikauimesha ingia , giza nene ,nikiwa nimepaki gari nikashuka nikanza kutembe kuangalia vijana wanao onekana ni wahuni wakisherehekea Idd. Nikafika ufukweni, hapo nikamuona jamaa mmoja anatembea peke yake kama anaelekea nilipo, huku akiongea na simu mbele yangu nikaona kundi kama la watu 10 la vijana wa huni , likija kwa kasi ,lika nipita na kumfuata yule kijana, kilichofuata ni yule kijana kutaka kunyang'anywa simu ,akawa ana bisha , akajaribu kukimbia , alipo kua ana kimbia lile kundi likaanza kumkimbiza na kusema "uyo , uyo , uyo" .

Hapo ndipo kila aliye jirani aliamka na kuanza kumshambulia yule kijana wakidhani ni kibaka, wale wahuni waka mkamata , waka mchukulia simu, raba, jeanz na tishirt halafu waka mwacha, ila watu walio dhani ni kibaka wakaanza kumpiga mawe. uzuri beach hakuna mawe makubwa yule kijana alipigwa mbaka akazimia, huku akitokwa na damu nyingi kichwani tukajua amekufa , ndio wakamwacha. Kilichofuata ni sisi kumbeba na kumkimbiza hospitali , akapelekwa ICU, tunashukuru ni mzima leo .

Je cases kama hizi ni ngapi na kama tuna chukua sheria mkononi je watakufa wangapi bila hatia?
 
huu ni ujinga na kutostaarabika

jamii ilioendelea inajua thamani ya uhai na ina heshimu haki ya kuishi

tujitahidini kuelemisha watu wetu kuhusu thamani ya uhai na kufata sheria

kila kosa lina adhabu yake lkn sio kifo
lkn akikuwahi wewe anakumaliza ujue!!!
 
Washenzi hawa, hamna lolote zaidi ya kuonea Wanyonge.

Kama mna ubavu si mkamtwange Rostam Azziz au Lowassa?

Kuna mama Mkapa pale anadunda na Wahindi kibao wakiwa na pesa za EPA.

Mramba na kundi lake wapo tu. Chenge ndiyo kwanza anagonga dada zenu na mnamchekea.

Mnakuja kupiga mawe Kibaka aliyelala njaa jana. Hamna maana kabisa. Si usiku mtoke mpambane na Majambazi?

Au mkisikia cha moto Mnazifyata? Kunguru Dume nyie.......

Si ajabu kama si akina Lowassa na CCM kumpe njaa kijana, asingeliiba. Mnaadhibu siye. Mnakata Majani na si Mzizi.
jamni, muda mwingine hayahusiana na siasa kabisa, vijana wamejichagulia fungu lao hilo na hawataki kabisa kijishughulisha wala kutumia akili, nina mfano hai kabisa wa jamaa yangu wa karibu ambaye kwao hajakosa kitu chochote, lkn shule alikataa kusoma na maisha alojichagulia ndo kama hayo na anagroup yake ya vijana kama 10 ambao nao kwao hela ya kubadili mboga sio tatizo, mng to evening wanacheza kamari bangi kwa sana, mavazi yao ni vibukta most of the tym, ukikatiza karibu yao imekulaje kwako!?
.
 
Mapambano dhidi ya uovu sio kwa kufanya uovu mwingine - bali kwa kutumia sheria.

Uhai una thamani kubwa jamani sio wa kuondolewa kiholela.
 
Jamani wewe unapopita mahali ukakuta watu wanampiga kibaka aliyekwapua simu wanamfanyia ukatil huu wewekama mwa JF unafanya nini??

Inanifikirisha kwamba wanaofanya haya ni wakatili kuliko watu wa agano la kale ambao dira yao ilikuwa "jino kwa jino" Kuibwa simu kulipizwa kwa kuua!
 
Back
Top Bottom