Hivi kuna watu sijui wanawachukuliaje watu wengine

Hivi kuna watu sijui wanawachukuliaje watu wengine

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,878
Reaction score
4,441
Yaani hii dunia sijui kuna watu wanawachukuliaje watu wengine aisee utakuka kuna lijitu unampigia simu hapokei unampigia simu zaidi ya tatu hapokei na then baadae hakurudii sijui kuna simu zingine hazioneshi missed call au ndio dharau sasa utakuta mtu huyo akikupigia wewe simu wewe usipopokea anaanza kusema kwa watu kwamba Tajiri siku hizi ana dharau kwa sasa ametoboa daah walimwengu bwana

Kuna lijitu lingine unampigia simu vizuri anapokea vizuri tu anakuambia nitakucheki ndiyo mazima hiyo hakutafuti wala nini sasa siku akiwa na shida anajiliza wewe kama mbwa vile 🚮🚮 kuna mijitu mingine inakera kwenye huu ulimwengu dadeki zake

# hii dunia ina dunia ina watu na viatu ujinga mtupu#

Na kuna mijitu wao wanakupigia kwenye shida tu dadeki siku asipokuwa na shida hakupigii na wala kukutafuta na pia kuna wajinga wengine unawachangia harusi zao fresh tu ila wewe ukiwa na jambo lako mpaka mpigizane kelele aisee hii dunia bwana aisee better to love yourself first
 
We nani kakwambia simu yako ni ya muhimu sana kwamba lazima upokelewe?
Kuchangia harusi siyo deni usichange kwa lengo la wewe uje uchangiwe kama huna acha ila kunichangia siyo kigezo cha mimi kukuchangia pia.
 
Baba yangu alikuwa akifika NBC bank anapelekwa kwa Meneja moja kwa moja hata kwenye line hakai. Nilimuuliza kwanini yeye hakai kwenye foleni ya kwa Teller alinijibu pesa ndio heshima.

Wale wazee niliokuwa mdogo nawapa salamu ya unyenyekevu kwa utuuzima wao. Sasa nikiwasalimu wao ndio wanani nyanyapaa. Mleta mada ikumbuke kauli ya baba yangu hapo juu, Ukiona hutafutwi huna cha kusababisha ukatafutwa(hela)
 
Na kweli. Ukiona hupokelewi simu ujue una safari ndefu katika utafutaji. Loh
Yaani kwa mfano unachat na mtu halafu una cha kumwambia lakini unaona ni bora kumpigia kuliko kuandika meseji.

Mlikuwa mnachati hata sekunde 30 hazijapita unampigia simu.

Simu Nita weee lakini wapi, haipokelewi.

Sasa hapo maswali lukuki yanaanza kukaa kichwani……

Kwa mfano, ‘huyu fala si tulikuwa tanachaji sekunde kadhaa tu zilizopita halafu nampigia ila hapokei.

Cha ajabu, simu ikishakata, huyo fala anakutumia meseji halafu anajikausha kama vile hukumpigia simu 😉.

🖕🖕
 
Back
Top Bottom