Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
C bora wafe madiver wanne lkn wananchi 10 wakaokolewa. Ebu acheni siasa. Hivi unajua wanaccm mtakuja kulia kuliko Opposition. Kwasababu nyie mtakuwa Malia na kusema mwno kwa sababu sanamu mmelichonga wenyewe na kuliweka. Ni hapo sasa mtakapokuwa mnalia, Opposition wanawang'ong'a TULIWAAMBIA!!! Halafu siyo mbali yaani soon
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Wewe na yeye ni mazwazwa tu divers walikua sahihi kusema vile sababu hawakua na vitendea kazi maana naona divers wana boxer tu sasa mkuu wa mkoa anashindwa kusema hatukua na vifaa rafiki kwa kufanyia kazi muda wa usiku wapuuzi tu ndo watatumia neno giza kama kichaka cha kujifichia wenzetu usiku na mchana kunatofautishwa na usingizi tu
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Kweli kabisa, ila kitaifa hakukuwa na msaada wowote kuhakikisha zoezi linaendelea?. Hawa wanaoitwa wenyeviti wa usalama wa mikoa ni usalana wa chama wala sio wa raia.
 
18th century Ulaya ilikumbwa na mageuzi makubwa. Ni baada ya kuibuka kikazi cha INTELLECTUALS kilichoanza kufanya mambo kwa kufikiri badala ya MAZOEA/MIHEMUKO, kiliitwa AGE OF REASONS. Tawala haramu zilianguka kipindi hicho, hivyo Tanzania kuna haja ya kutengeneza kikazi cha AGE OF REASONS kuleta mabadilko Sina maana kwamba kwasasa kuna Tawala haramu hapana ila kuna haja kutengeneza kizazi cha aina hiyo
 
Mongela wasamehe bure.Hizo ni hasira na frustrations zao za kushindwa chaguzi wameaamua KU STEAM OUT FRUSTRATION zao kwenye hiyo ajali.

Wamegeuka ghafla wasomi na wataalamu wa vivuko.Nyoooo!!!! wangekuwa wasomi na wataalamu si wangetumia usomi na utaalamu wao kushinda chaguzi?. Wakshindwa chaguzi hata za udiwani tu hugeuka na kujifanya wasomi na wataalamu waliobobea wa ku analyize mambo ya kitaifa na kimataifa!!!! ha ha ha ha
Huu ni msiba wa kitaifa na hauna siasa isipokuwa kwa small minded people!
 
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
Kama kweli ulikuwepo eneo la tukio, maelezo yako yamenisikitisha sana
 
Tanzania siku hizi kumekuwa na watu wanatetea jambo kwa maslahi binafsi.yuko tayari akukane au atunge uongo kwa faida yake binafsi huku huo uongo ukiwauumiza hata ndugu zake wa karibu.je kutetea Shida au maafa kwa mwenzio ndiyo kujenga mshikamano wa kitaifa au kubomoa
 
Una utaalam wa masuala ya Diving mkuu!?
Au unajaza server za JF na wewe uonekane! Kuna masuala ni ya kitaalam na hayahitaji Siasa na mihemko.
Mkuu wa mkoa alishauriwa na wataalam (Divers) kusitisha zoezi hilo kutokana na hali iliyojitokeza ndani ya maji.
Hayo masuala ya mke wako sijui mke wa jirani yaache huko huko kwenye vijiwe vya kahawa.
Na hilo suala lililojitokeza ndani ya maji ni siri?
 
Back
Top Bottom