Ukabila waibuka Bungeni, wachaga wadaiwa kuididimiza Lindi na Mtwara

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Ni mbunge wa viti maalum CCM kutoka Mkoani Lindi.

Ametaja mtandao ambao umeonekana una majina ambayo yanaishia na rafudhi za kichaga kuwa ndio wameurudisha mikoa ya Lindi na Mtwara na wanahusisha mtanadao huo wa watendaji wa serikali walio na mafungamano na CHADEMA. Kawataja watendaji wezi ambao waneiba na kihamishwa ndani ya serikali. Kawataja wakuu wa wilaya na watendaji serikalini amewahusisha na ukabila na wote wakiiba wanahamishwa.

Sasa mimi najiuliza wakuu wa mikoa na wilaya wanachaguliwa na kuteuliwa na nani? Chadema wanahusikaje kwenye uteuzi wa wezi? Chadema kwani ndio wanawahamisha hao watendaji? Chama gani kinaingoza nchi Chadema au CCM?
 
Ndiyo maana tunasena hivi viti maalumu viondolewe ni upuuzi mtupu. Tangu lini serikali ya CCM iliwapa madaraka WACHAGA PEKEE kukusanbya kodi na kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi hii?

Ninaomba unitajie jina huyo mbunge mbumbumbu. Mikoa ya Lindi na Mtwara iko nyuma relatively kimaendeleo kwasababu ya sera mbovu za serikali ya CCM. Jana Mbowe alisema kwamba kama wananchi wa mikoa ya kusini wangefahamu kwamba korosho ni zao la tatu linaloliingizia nchi hii fedha za kigeni sidhani kama kuna mwana kusini angeipigia kura tena CCM kutokana na umasikini walionao watu wa kusini.

Sasa huyo hivi VITU MAALUMU anasema umasikini wa Lindi na Mtwara umeletwa na wachanga!?
 
Mfa maji haachi kutapatapa na mbaazi ukikosa maua husingizia jua! Kazi kwenu wana wa Lindi na Mtwara!
 
Ndo shida ya vitu maalamu! hawajui wanachfanya Walah! Mchaga kafikaji huko Yakhe? Hivi Serikali yetu ina mawaziri wangapi wa kichaga waacheni wachaga tena nazani ktk tanzania ndio kabila linalosambaza maendeleo sana katika sehemu nyingi za nchi mfano kufanya biasha nk
 
Safi sana huu ndio mtindio wa ubongo CCM iliotengeneza hata kwa viongozi wake. Ninajiuliza hivi spika alikuwa wapi kufanya upumbavu huu ukaenda kwenye Hansard? Ee mola utuhurumie siye wanao tunakuachia wewe tu. Wamekosa mashiko sasa hata UCHAWI watatumia hawa wajinga lakini Exodus 14:14 The lord will fight for us! Tanzanians. inatutia moyo
 
Wachaga wanaolewa sana na makabila mengine kuliko makabila mengine
Tuangalie viongozi waliopata wanawake toka kishimundu pekee:

Mh Benjamin Nkapa
Mh Sumaye
Mh Shein

..........
..........
..........
..........
.........
Kila kiongozi anayeingia madarakani ana mke wa kichaga.Sijui mke wa Edward Lowassa mama Regia sijui ni mchaga naye.Lol tunawaonea wivu tuu hawa wachaga.
 
Haya mambo yanachosha.....mm natokea wilaya ya mvomero kule morogoro maeneo ya mgeta........ukweli hamna umeme hadi leo na chama kimeshika hatamu uko balaa....ninachoamini wanaokwamisha maendeleo kule ni sie wenyewe...

Nilienda Himo Moshi nkakaa one week nligundua kinachowasaidia ni mentality yao....kwao ukiwa mbunge unapewa target na kama hujafikisha hizo wanakupiga chini bila kujali chama chako....

Mikoa mingine hasa kusini wanatakiwa kufikiri kwa mtazamo huo na kuachana na dhana ya kulipa fadhira kwa chama kilichowalea....... ila ipo siku mana wameshaanza kuzinduka......... ipo siku watakuwa na uhamuzi wa busara
 
Huyo Mbunge wa Lindi bado anakwepa ukweli kwa 'cover' ya ukabila. Hao watendaji wamewekwa na serikali ya ccm, wanasimamiwa na seriali ya ccm. Sasa kama wameiba lakini serikali ya ccm ikawahamisha badala ya kuwachukulia hatua za kinidhani maana yake serikali ya CCM imeshindwa kazi.

Kuhusu mtando wa hawa watendaji kuhujumu serikali, mbunge anataka watanzania waamini kuwa CCM inajihujumu chenyewe? Maana kama nilivyosema hawa watendaji wamewekwa na serikali ya ccm na ni hao wa hao hao CCM ndio wanatakiwa kuwachukulia hatua. Hoja dhaifu!
 
Ni mbunge wa viti maalum CCM kutoka Mkoani Lindi. Ametaja mtandao ambao umeonekana una majina ambayo yanaishia na rafudhi za kichaga kuwa ndio wameurudisha mikoa ya Lindi na Mtwara na wanahusisha mtanadao huo wa watendaji wa serikali walio na mafungamano na CHADEMA. Kawataja watendaji wezi ambao waneiba na kihamishwa ndani ya serikali. Kawataja wakuu wa wilaya na watendaji serikalini amewahusisha na ukabila na wote wakiiba wanahamishwa.

Sasa mimi najiuliza wakuu wa mikoa na wilaya wanachaguliwa na kuteuliwa na nani? Chadema wanahusikaje kwenye uteuzi wa wezi? Chadema kwani ndio wanawahamisha hao watendaji? Chama gani kinaingoza nchi Chadema au CCM?
mbunge dhaifu.kiukweli hawana sera yoyote ya kuwazima wanachadema na harakati za ukombozi wa taifa letu hili.labda wahamishie kampeni zao misikitini.
 
Wachaga wanaolewa sana na makabila mengine kuliko makabila mengine
Tuangalie viongozi waliopata wanawake toka kishimundu pekee:

Mh Nyalandu

Kila kiongozi anayeingia madarakani ana mke wa kichaga.Sijui mke wa Edward Lowassa mama Regia sijui ni mchaga naye.Lol tunawaonea wivu tuu hawa wachaga.

Huyu hapana......mkewe MBONDEI
 
Riziki lulida mbunge viti maalumu lindi kamtaja ndoskoi,Macha na wengine ambao sikumbuki kwamba wana mtandao wa wezi wa wachaga ambao wameeibia Lindi,Mtwara ,lakini hawa viongozi wa hiyo mikoa wameamua kupambana na wachaga leo Membe asubuhi alikuwa power breakfast kwenye kituo cha clouds alitumia neno kwamba nilienda mtama kufukia mashimo na niliwaambia wananchi kwamba hawa watu wa kaskazini walikuwa wanapangiwa kuja huku na wakakataa kufanya kazi huku kwa hiyo wamechelewesha maendeleo haya maneno ya wana CCM ya kibaguzi sio nzuri kwa ustawi wa nchi yetu
 
wadau kanuni za bunge si zinakataza kutaja jina la mtu ambaye hawezi kuja kujitetea mbele ya bunge , sasa huyu mama hawa watu aliowataja kanuni zinasemaje sijaona mmbunge yoyote kuomba muongozo,
 
Back
Top Bottom