Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

isifutwe iachwe tu..tusikatishe tamaa junior members....

mpoki hii nchi imeshaingia kwenye utawala wa kifalme if your dad is not or was not WHO IS WHO in tanzania circles bora tu utafutage kazi nyingine..watoto wetu watakuwa WORKING CLASS TU..ruling CLASS tayari ipo ..si unaona wameshawaazishia watoto hadi kwenye siasa...
INASIKITISHA SANA!
 
It is better to base the argument on hard facts i.e. including data. Can samvlachole furnish us with such information?
 
japo nimechelewa naomba nichangia mtizamo wa mwenzangu about this,naisi inawezekana! one comment 4my fellow,ondoa fikra za kuajiriwa tumia that litle or much you have kujiinua kiuchumi si wote walioko madarakani wamepigiwa pande,pia jifunze kutafuta marafiki wa kila aina uwezi jua nani atakuwa nan isitoshe sometimes academic exellence matters,find your position
 
japo nimechelewa naomba nichangia mtizamo wa mwenzangu about this,naisi inawezekana! one comment 4my fellow,ondoa fikra za kuajiriwa tumia that litle or much you have kujiinua kiuchumi si wote walioko madarakani wamepigiwa pande,pia jifunze kutafuta marafiki wa kila aina uwezi jua nani atakuwa nan isitoshe sometimes academic exellence matters,find your position

..ulichosema ni sawa kabisa!ukiwa unajibidiisha kupata maarifa,katika kazi,na kujiinua kiuchumi hutapata muda wa kulalamika kuwa kuna ukabila,blah,blah!

..kimsingi,ukabila upo ila vitu ulivyovitaja ndio huwafanya watu wengi wafike walipo na si ukabila!wachache hutumia vigezo vya ukabila!
 
Ukabila upo lakini si kweli kwamba kila mchagga, mhaya au mnyakyusa anapewa nafasi sawa anapoomba kazi yenye kuongozwa na mtu wa kabila lake. Mitaani wako vijana wa kichagga, kihaya na kinyakyusa wanaoangahika kama vijana wengine.

Vile vile tujaribu kukuza sekta binafsi zitakazoongozwa na wafanyabiashara wa kitanzania. Wafanyabiashara wanataka watu watakaowaletea faida na sio watu wa kabila lao. Bakhresa anaajiri watu wenye ujuzi wa kumletea faida na sio wapemba wenzake kwa sababu ni wapemba. Mengi anaajiri watu wa kumletea faida na sio Mchagga kwa sababu ya mchagga. Hivi ITV ingekuwa na watangazaji wote wachagga, hiyo TV watu si wangeacha kuangalia.

Waajiri wa kazi za serikalini mara nyingi hawaangalii sifa. Nyerere aliwaambia ajira za waalimu wa UPE zitolewe kwa wenye uwezo; waalimu wakuu wakatoa nafasi kwa watoto wao waliochemsha darasa la saba. Sidhani kama shule za binafsi zinaweza kuruhusu vitu kama hivyo.
 
Mwana Mariam,
Hope humaanishi kuwa hakuna ukabila! Kuna ushahidi umetolewa tangu mwanzo wa hii thread!
Ajira za vimemo, ngono, ukabila ni mambo ya kawaida ambapo Watz wameshazoea!
 
Mwana Mariam,
Hope humaanishi kuwa hakuna ukabila! Kuna ushahidi umetolewa tangu mwanzo wa hii thread!
Ajira za vimemo, ngono, ukabila ni mambo ya kawaida ambapo Watz wameshazoea!

Ukabila upo nina ushahidi wa kutosha. Nikiwa shule ya msingi, uwezo wa kishule ulikuwa sio mbaya sana lakini displine yangu ilikuwa mbovu. Na alitokea mwalimu mmoja, Sister wa Roman Catholic na mchagga aliyenisaidia kupiga msasa displine yangu. Na hakunibagua kutokana na dini yangu au kabila langu.

Nilipokuwa chuoni nilipangiwa kufanya practical African Hotel. Ofisa wa uajiri alikuwa mchagga ambaye hakutaka kuona uso wangu ofisini kwake. Kwa bahati akampa nafasi yangu room-mate wangu ambaye alikuwa mchagga na aliyepangiwa sehemu nyingine.

Kwa upande mmoja kuna Sister wa Kichagga aliyenipa elimu ninayobebea mabox ya nguvu huku ughaibuni na upande mwingine yupo aliyenibagua kutokana na ukabila. Aliyenibagua amenisaidia vile vile, kwa mara ya kwanza nilielewa kuwa ubaguzi upo duniani hivyo alinipa JKT ya ubaguzi.

Nyerere alikuwa na elimu kubwa lakini alilipwa mshahara mdogo kwa sababu alikuwa mweusi pale Pugu. Watu walioanzisha klabu ya yanga (Young African). Ni waswahili ambao hawakuruhusiwa kushiriki katika vilabu vya michezo vya wazungu au waasia. Lakini hatua zao zimebadilisha historia ya nchi. Waanzilishi wa yanga, alianzisha AA ambayo ilikuwa TAA baadaye TANU na uhuru ukapatikana. Nyerere angepewa mshahara mkubwa pale Pugu angekuwa na masimamo mwingine.

Ukiuchukulia hatua nzuri ubaguzi unaokupitia unaweza kukufanya ubadilishe dunia, taifa, familia yako au wewe mwenyewe. Mabox naniyonyunyua hapa sitaki kazi yoyote Tanzania labda ugavana wa BOT.
 
Hi wee koma kabisa kumtuhumu mtu kwa mauaji wakati huna ushahidi wowote. Kama angekua muuaji kiasi cha wewe kujua si sheria ingekua imeshachukua mkondo wake?.
 
mimi nafikiri tatizo kubwa sio ukabila kama wengi tunavyofikiri isipokua tatizo kubwa ni umimi na usisi ,angalia uchaguzi wa ccm ulivyo jaa watoto wa vigogo ndugu pamoja na mahawara za vigogo sasa unvyofikiria wewe baadaye 2010 haohao ndio watakao pitishwa kugombea ungozi km ubunge udiwani pamoja na uraisi kwahiyo sisi akina yakhe hatuna nafasi hata ya kushika viatu vya hao vigogo nafamilia za

mibavu mwanachama mpya
 
POINT KABISA YAANI UKABILA NA UDINI HAUJAISHIA HAPO TUU...KUNA MAKAMPUNI MENGI YANAUDINI HASA YA HAWA URABUNI...UTAKUTA MWENZAKO MMEINGIA PAMOJA KAZINI LAKINI ANAWEKWA KARIBU SAANA NAO NA ANAONGEZEWA KIPATO KISA NI WA DINI YAO..YAMENITOKEA KABISA

Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?




-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY
 
Nafikiri mwanakijiji umempa majibu sahihi kabisa mleta hii hoja. Kama nalingine alete likiwa na ushahidi
 
HUU NI UBAGUZI! Bango la nafasi za kazi ya muuzaji kwenye famasia lililobandikwa katika moja ya maduka ya Shoppers Plaza, Dar es Salaam, likionesha sifa mojawapo ya mwombaji ni kuwa Mtanzania mwenye asili ya Asia. (Picha na Emmanuel Kwitema)

Chanzo: Majira, 20/01/2008

Hii habari nimeiweka mahali hapa makusudi kwa sababu suala lenyewe limetokea huku tukiwa katika mjadala wa ukabila na mabo mengine yanayofanana na hayo kwa miezi kadhaa sasa!
Je ubaguzi wa namna hii utakoma lini?
Binafsi nachukia sana ubaguzi!


5357.jpg
 
Chanzo: Majira, 20/01/2008

Hii habari nimeiweka mahali hapa makusudi kwa sababu suala lenyewe limetokea huku tukiwa katika mjadala wa ukabila na mabo mengine yanayofanana na hayo kwa miezi kadhaa sasa!
Je ubaguzi wa namna hii utakoma lini?
Binafsi nachukia sana ubaguzi!

5357.jpg

hii ni hatari sana,Ndio mana wakati mwingine huwa nawachukia ndugu zetu wahindi kwa mambo yao wanayowafanya watanzania wenzangu na wala sio mimi.

hii inabidi ipelekwe wizara ya kazi.JF ni kiboko..TACAIDS wameshabadili Forum yao within 48 hours.
 
hii ni hatari sana,Ndio mana wakati mwingine huwa nawachukia ndugu zetu wahindi kwa mambo yao wanayowafanya watanzania wenzangu na wala sio mimi.

hii inabidi ipelekwe wizara ya kazi.JF ni kiboko..TACAIDS wameshabadili Forum yao within 48 hours.

Ni kweli kabisa Mkuu Gembe, nimepitia ile link ya TACAIDS nikakuta patupu.
Kumbe JF ni moto wa kuotea mbali sana
 
Idimi
Hata kama ni ubaguzi at least it is explicit! Ukabila, rushwa za ngono, n.k je hii hutangwaza ktk magezeti?

Mengi hayatangazwi mkuu!
sasa kama hilo tangazo la ajira ya hapo Shopperz Plaza limetangaza rangi ya mtu, je ni mangapi yamefichika ambayo hayatangazwi ila yanafantika?
Ningependa sana kupata maoni ya Mhe Mwanakijiji katika hili.
Waasia kiboko!
 
jamani ukabila mbaya hebu nadhani sote tumeshuhudia yanayotokea Kenya!

Babalenu, haya mambo yasipoongelewa wazi na kuwekwa sawa mwisho wake ni hayo tuyaonayo Kenya, ambayo kwa kweli yanasikitisha sana na yanapaswa kutemewa mate na kila Mtanzania. Kumekuwa na uhasama wa chinichini kati ya jamii za Kiasia na zile za kiafrika katika masuala ya ubaguzi, nadhani ukifuatilia posts za thread hii za mwanzo mwanzo utaona mambo hayo.
Pitia pia ile post ya Richa Adhia , Miss tanzania mwaka jana uone jinsi watu walivyotoa madukuduku yao, kisa? Wabongo hawaoani na Wahindi!
 
Back
Top Bottom