Ujumbe wa MO mitandaoni

Ujumbe wa MO mitandaoni

Kidadadeki,me nalipa bonge la kisasi nauaaa.Tena kuanzia alopanga hadi watekelezaji naangamiza.Maisha ni jino Kwa jino.
 
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

IN SUMMARY
Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuandika ujumbe kuhusu anayekufanyia mabaya umlipe kwa mema na kuwagusa watu wa kada mbalimbali

Dar es Salaam. Ujumbe wa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ aliouweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akizungumzia kutenda mema hata kama umefanyiwa ubaya umeibua mjadala mitandaoni.

Katika ujumbe huo Mo ambaye alitekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11, 2018 na kupatikana Oktoba 20, 2018 ameandika, “Hutofanya ubaya kwa aliyekufanyia ubaya, ila utamsamehe na kumfanyia ukarimu.” Mtume Muhammad (S.A.W) JumaahKareem.

Baada ya ujumbe huo watu wa kada mbalimbali wametoa maoni yao akiwemo waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki aliyesema, “Hii ni imani ya ngazi ya juu sana.”

Wengine walioonyesha kuguswa na ujumbe huo ni @MsTayanah aliyeandika, “ila mkuu watanzania bado tungependa kujua walikupeleka wapi mkuu.”

Naye gagula16 ameandika, “Safi sana ndio maana halisi ya hekima. Na ndio maana mfalme Suleiman aliomba hekima na busara kwa mwenyezi Mungu.”

Naye MrMsambwe6% amesema, “Mungu akubariki katika kutufikishia ujumbe katika siku takatifu ya leo Nikutakie ijumaa Kareem.”

“Watu wakarimu tunalipizaga ubaya kwa wema mpaka wanaona aibu,” amesema Bonimawalla.

Soma zaidi: VIDEO: Polisi waonyesha nyumba aliyohifadhiwa ‘Mo’ Dewji
Huyo Mo, baba yake alimfanyia nini marehemu Dr Fupi, Mkemia Mkuu wa Serikali?
Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
 
Aheri wanaoitwa mabeberu kuliko hawa wanafiki wa safari hii.

Majitu yamekuwa na roho za kinyama lla bado kuna maibilisi yanawatetea kisa tu yananufaika na uwepo wao.Ubinafsi wa kiwango cha juu sana huu!!
Wewe ni ibilisi kuliko ibilisi wote walioko duniani!!
 
MO nae hana imani ya kweli,,kwann haweki wazi kipi kilimkuta,,au anawaogopa wanadamu kuliko Mungu??kwamba akiweka wazi yaliyomkuta na waliomteka,,kwamba watamzuru tena au,
 
Huyo Mo, bababyske alimfanyia nini marehemu Dr Fupi, Mkemia Mkuu wa Serikali?
Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Hayo anayopata sasa MO na Baba yake ni malipo kwa udhalimu aliyowafanyia watz kwa kuwalisha mahindi na ngano zilizooza pia alichomfanyia Dr. Fupi. Tena kwa nini hawakumfanyia zaidi yahapo? Mwambieni kuwa wapo ndugu zake na Dr. Fupi waliumia sana kutokana na kumpoteza mpendwa wao!
 
hahahaha TANAPA sasa dandieni malisho hayo hahaha
 
unafikiri Suleman alikuwa haombewi?
Hujui kuwa Daudi kabla ya kufa alimuombea Sulemani?
Unafikiri Rais wetu hajiombei?
Huu upumbavu unaununua genge lipi?
Dah yaan anayelilia kuombewa mwingine anayemtetea anajiombea mwingine yaan raisi ana wasemaji wengi khaaa
 
Kidadadeki,me nalipa bonge la kisasi nauaaa.Tena kuanzia alopanga hadi watekelezaji naangamiza.Maisha ni jino Kwa jino.
Nami nakubaliana nawewe dawa ya moto ni moto, Ubaya then nilepe wema hii hapana
 
Hii ya kutenda mema hata kama umefanyiwa ubaya, nadharia yake ni nyepesi sana, kazi ipo kwenye kutekeleza falsafa hii kwa vitendo. Inaonekana Mo anamaanisha alichoandika, hongera zake sana.

SOMENI VIZURI YEYE KAMNUKUU MTUME MUHAMMAD S,a.w sio maneno yake ni maneno ya mtume alipowausia watu wote
 
Mfalme Suleiman aliomba yeye mwenyewe hekima na busara kwa mwenyezi Mungu huyu wa kwetu anaomba aombewe

kila siku anaomba mungu kwenye hotuba zake pia anaomba watu wamuombee hakuna rais yeyote aliyepita katika nchi hii aliyeweza kumkumbuka mungu daima kwenye hotuba zake kama makufuli, tatizo lenu ni chuki hata hotuba hamsikilizi lakini ukisikia kuna kipindi cha michezo nyie wa kwanza kusikiliza
 
Anatuona mizwazwa[emoji16][emoji16]hata hapo anapoishi kuna wahitaji kibao!!!!angeanza nao.
(Afadhali hata dayamondi kawasaidia watandale wenzake).

Na kama anasaidia watu kisirisiri bila ya mtu kujuwa? We unafikiri Reginald Mengi huyo! Anaependa kujitangaza!!
 
Hutofanya ubaya kwa aliyekufanyia ubaya, ila utamsamehe na kumfanyia ukarimu.” Mtume Muhammad (S.A.W) JumaahKareem

Kweli hii ni imani ya nguzo ya juu sana lakini hawa METL waanze huko kwenye makapuni yao kwa kuwalipa wafanyakazi vizuri hapo MO atakuwa anatekeleza vizuri hiyo imani yake! Watu wanalia huko METL mshahara kiduchu sana.
 
Ujumbe wa MO unafanya nimkumbuke Msanii Suma Mnazaleti katika wimbo wake aliomshirikisha Steve rnb uitwao Hisia za Mtaa.

"Siwalipii Kisasi Walionifanyia Mabaya,

Nitawasaidia hata kwa cash Mwishoni wataona haya"


Wakati Mwingine hate for hate,tooth for tooth Ni njia bora zaiidi ili heshima Isimame mahala Pake.
 
Back
Top Bottom