Ujumbe ulio tolewa na serikali kwenye kodi mpya ya miamala

Mulokozi GG

Member
Jul 14, 2021
34
44
“Akufukuzaye hakwambii toka”, ni msemo wa kiswahili wenye maana kuwa ujumbe unaweza kuwasilishwa kwa njia moja ukimaanisha kitu kingine tofauti. Mfano ukienda kumtembelea rafiki yako akakulaza sebureni na vyumba vipo wazi, utaonekana mwenye busara asubuhi ukiaga vizuri na ukarudi kwako.

Sababu kila kinacho fanywa na mtu au serikali huwa kimebeba ujumbe flani ulio jificha au ulio wazi kwa walio wengi kuung'amua. Hili limedhihilika kwenye kodi ya miamala iliyo ongeza serikali kwa madai kuwa ni kodi ya mshikamano.

Kuongeza kodi hii katika hatua ya mwanzo ya utawala wa awamu ya sita ni ujumbe mkubwa sana kwa Watanzania, hasa wale wenye uwezo wa kuelewa ujumbe husika.

Kuongeza kodi katika sekta ya mhimu kama fedha ni ujumbe ulio kati ya yafuatayo;
Moja, Watanzania licha ya wingi ni wavivu na mzigo kwa serikali kiasi cha kushindwa kumdu kodi kidogo kutoka kwa wengi na kukidhi mahitaji ya kuendeshea shughuli za serikali.

Mbili, serikali imeshindwa kudhibiti makusanyo ya mapato na kodi kutoka katika vyanzo vilivyopo na imehamishia kodi kubwa katika vyanzo vichache ambavyo ni rahisi kodi yake kukusanywa na pengine inajiandaa kuacha mianya katika vyanzo vigumu kukusanya kodi sehemu hizo.

Tatu, serikali imeshindwa kuboresha njia zilizopo za mapato ili kuziongezea ufanisi na kubuni njia mpya na rafiki za kuiongezea mapato kwa ajiri ya kuendesha shughuli zake.

Suala hili halihitaji itikadi ya aina yoyote bali uelewa wa kawaida tu, kwani ni wazi hakuna kiongozi yeyote anaye penda kusukuma mzigo mkubwa wa kodi, kuongeza ugumu wa maisha na kupunguza hali ya kukubalika kwake kwa wananchi. Maamuzi kandamizi kiasi hiki wanayafikia sababu hali ni ngumu kwao kuendesha shughuli za serikali kama walivyo zoea, kwa kuwa wamezoea njia nyepesi uamuzi wa kusukuma mzigo wa kodi kwa wananchi ndo unaonekana sahihi kwao.

Je ni nini kifanyike; Hali hii ni ishara tosha kuwa hali serikalini ni ngumu hivyo lazima waachie kuendesha shughuli kwa mazoea, elimu ya ujasiriamali ipewe kipaumbele kikubwa sana ili kuelimisha watu njia bora za kujiingizia kipato na kuongeza pato la Taifa, vyanzo vya mapato vyote visimamiwe vizuri, kwa haki na kisheria na mwisho japo si kwa umuhimu wananchi wajenge utamaduni wa kuwa mstari wa mbele kwa nia ya dhati kuwahamasisha, kuwapongeza na kuwawajibisha viongozi kwa yale wanayo yafanya kwenye jamii.
 
N

Karibu mdau wa JM na nini maoni yako...!?
 
Back
Top Bottom