Kwanini Serikali inakata kodi watumishi wa Serikali?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,325
Hii imekaaje Serikali inakusanya kodi kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo kodi ya mapato (payee) ya wafanyakazi wake yenyewe halafu inarudisha tena pesa hiyo kuwalipa hao wafanyakazi mishahara ikiwemo kiasi ambacho ni kodi ya mapato.

Huu mzunguko kwanini usingefupishwa kwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kamili isiyojumuisha kodi?

Serikali kukata kodi watumishi wake si inakuwa kama kuchuku pesa yako mwenyewe mfuko wa shati kisha kuhamishia mfuko wa suruali?
 
Hahahaha wanataka ili mshahara usome kiwango kikubwa 😂😂😂😂😂. Unalipwa 1,000,000/- ila unaenda home na 70000
 
Back
Top Bottom