Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 251
- 970
Kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi na malori uliotokea Septemba 28 na 29, 2026, madereva wengi hawakujua maana ya mfumo wa points (Drivers Licence Point System).
Kwa mujibu wa Kifungu cha 31 cha Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 Rekebu ya 2023, leseni yako ya udereva ina pointi 15, na makosa ya barabarani yanaweza kupunguza pointi hizo?
Kwa mujibu wa The Road Traffic (Drivers Licence Point System) Regulations, 2014, G.N. No. 109 of 2014, as amended by G.N. No. 420 of 2025, kosa la barabarani linaweza kukupunguzia pointi 1 au 3, kulingana na aina ya kosa.
Kwa mujibu wa Kanuni hizo, pointi zikifika sifuri, leseni inasimamishwa kwa miezi sita.
Kumbuka: Kukatwa pointi hakuondoi faini au adhabu nyingine inayotokana na kosa husika.
Hata hivyo, mfumo huu haujaanza kutekelezwa rasmi, Septemba 29, 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alielekeza suala la pointi lisitishwe na kufanyiwa tathmini ya kina, kwa kuwashirikisha madereva kupitia viongozi wao pamoja na wadau wengine. Tathmini hiyo pia itaangalia masuala ya elimu na uelimishaji, maoni ya wadau, pamoja na namna mifumo ya usalama barabarani inavyotekelezwa katika nchi nyingine kabla ya hatua zinazofuata.
Imeandaliwa na Advocate Witness wa Aquila_Attorneys