Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,109
Tanzania ni nchi pekee ambayo kwa sasa imekaa eneo la kimkakati ambalo lisipolindwa vyema ipo hatari mataifa ya magharibi yakapenya na kutuondolea kabisa amani iliyopo kwenye ukanda wa bahari na Afrika Mashariki.
Tunapowaza kuhusu DP world kuja kiuchumi lazima pia tuangalie kiusalama. Tumeona rasilimali za Mozambique zipo mikononi mwa msbeberu ya ili waweze kuzivuna wameondoa amani na kuweka vikosi vya kigaidi.
Hali hiyo ipo Sudani, Somalia na Congo. Tunaelewa wazi kwamba silaha zinatembezwa kwenye maji zaidi kuliko kwa ndege na usafiri wa Ardhini. Tunaelewa pia kwamba kama siyo juhudi binafsi za Magufuli na utawala wake maghaidi walishakata mizizi Kibiti ambalo ni eneo la mwambao wa bahari
Tunaelewa namna ambavyo shehena au kontena lenye silaha likifanikiwa kupita kwetu kwenda kwa majirani endapo litakamatwa tutavuruga kabisa mahusiano. Lakini tumesikia pia juzi tumeondoa vikwazo kwenye sheria ya kodi na kuruhusu madini yanayozalishwa nchi jirani yaingie Tanzania bila kikwazo; means Kongo na Mozambique wanaweza kuja kuuza madini hapa nchini. Wanapokuja kuuza uwezi jua wauzaji watakuwa waasi au genuine dealers ; uwezi jua wabia wa DP World watawekeza kwenye sekta gani nyingine.
Hivyo bandari yetu si sawa na bandari nyingine kwa sababu ikitumika vibaya itatengeneza maadui wengi ambao ni majirani zetu. Upo uwezekano tukatuhumiana kama anavyotuhumiwa uganda na hata Rwanda kwamba amepeleka watu Kongo kwenda kukwapua rasilimali.
Nataka tuwalete mezani vyombo vya dola vione kwamba wanayo kazi kubwa katika mkataba huu. TLS wameshauri vyema ila vyombo vya ulinzi na usalama wasiliona ili jambo kwa jicho la tatu tunaweza tukawa tunatafuta bajeti yakununulia zaidi silaha za kupambana na makundi ya waasi kuliko kujenga miundombinu
Tuone risks kuliko kuona fursa. Ghadafi alitengeneza mengi ila yalikuja kuharibiwa kwa muda mfupi sana .....bora tuchelewe kuendelea tuendelee tukiwa salama kuliko kuwahi kuendelea then tukalibomoa Taifa kutoka kuwa mkombozi wa Afrika tukageuka mgombanishi wa Afrika.