Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 91
CCJ imeundwa ili kuua nguvu ya CHADEMA. Ila chadema iwe imara sana katika mambo kama haya siamini katika chama kama hiki
Mhhh huu sasa uzushi na sana nitasema ni fikira mgando, nahau zake ni ukabila! kama unabisha kenua meno yako na punguza hasira
Jana wakati Mh. Fred Mpendazoe akitangaza kujitoa kwenye chama cha CCM alieleza kwamba, nukuu,
"CCJ siyo Chama cha Upinzani bali ni Chama Mbadala"
Nimejaribu kuitafakari kauli hii kwa makini lakini sijapata mantiki yake vizuri. Maswali ninayojiuliza bilas majibu ni haya:
1: Mpendazoe kusema hivyo anamaanisha kwamba vyama vya upinzani vilivyopo havifai au jina la "Upinzani" halifai?
2: CCJ itafanya mambo yanayolandana na ya CCM?
Wana JF mniweke wazi
Sijaelewa sawa sawa ila kuna ajenda nyingine kabisa na pia naona kuna umuhimu mkubwa sana na kuwa makini na chama hiki. Siamini katika mambo ya haraka haraka sana ndio maana nasema ni chama ambacho wamekiunda CCM ili kuua nguvu ya CHADEMA. Siamini katika chama hiki, Ni kheri DP ya Mtikila kuliko chama hikiChama cha Upinzani ni chama ambacho kiko kwa ajli ya kupinga na kinyume na chama tawala; chama mbadala ni chama ambacho inaweza kutawala badala ya chama kingine. Yaani, kina uwezo wa kutawala wakati wowote. NI sawasawa na Labour na Conservative kule UK au Republican na Democrat huko US.. vyama hivi vinaweza kubadilishana (mbadala) madaraka bila wananchi kuwa na wasiwasi na wananchi wanaweza kukichagua kimoja badala ya kingine.. n.k
Kwa hivyo CCJ inataka kujiweka kwenye mahali pa kuwa mbadala wa CCM. CCM ni chama cha Kibepari wakati CCJ ni chama cha kijamaa! Vina sera tofauti na mitazamo tofauti kabisa..
MM leo mbona umewaamkia vibaya Chadema? Chadema wamefanya kazi kubwa mno katika nchi hii. Ndio chama kilichoasisi vita dhidi ya ufisadi. Chadema walipeleka hoja za ufisadi Bungeni. Wabunge wa CCM wakamzomea Dr. Slaa. Akishirikiana na wanachama wenzake, hasa Tindu Lisu, wakawataja timu ya watu 11 watuhumiwa wa ufisadi. Chadema pia wamejitahidi kurekebisha kasoro ya kukaa mjini, wanajitatangaza vijijini kupitia operation Sangara.I will not give all that credit to THEM excluding all others.
Niliuliza hili swali huko nyuma ni vipi vitendo hivyo?
I don't think so.. Chadema ni chama cha kibepari kama ilivyo CCM.
angalia jibu langu hapo juu;
chadema wamepewa nafasi yao na wameshindwa kuitumia mara nyingi.. wamebakia kutoa hoja za kisomi na kuvutia wasomi kwa hoja za kisomi.. so.. I don't know..
Ingefaa zaidi kama wangetumia upepo uliopo sasa kufanya merger.
Nasikia siku hizi kwenye CCM ubunge sio cheo tena, hata Kasheshe hajui Mpendazoea alikuwa na cheo gani!! Nasikia mwingine yupo maelezo anajichomoa, ila yeye hajasema anaenda wapi!!
Labda Chadema ndiyo iungania na CCJ!!!
Una maana gani? sentensi yako haieleweki kabisa.
Soma posts zangu zote katika threah hii utaona msisitizo nilioweka ni CCJ ishirikiane na Chadema. Sikutaja vyama vingine vya siasa, na sababu nimezieleza nilipoulizwa na MM kwa nini ninaona CCJ ishirikiane na Chadema na siyo vyama vingine vya upinzania. Ujumbe uliopo kwenye kichwa cha habari ndio huohuo niliokusudia kwamba CCJ ishirikiane na Chadema.Katika maelezo yako sikuona msisitizo wa moja kwa moja wa kuitaka CCJ ishirikiane na Chadema umetumia neno wapinzani na wapinzani si Chadema lakini ukona bora habari yako isomeke CCJ Washirikiane na Chadema kwa staili ileile ya magazeti yetu Zitto anasurika Kipigo kumbe ni wasafiri wengi nawe badala ya kuitaka CCJ ishirikiane na wapinzani unasema Chadema nadhani nimeeleweka
Chama cha Upinzani ni chama ambacho kiko kwa ajli ya kupinga na kinyume na chama tawala; chama mbadala ni chama ambacho inaweza kutawala badala ya chama kingine. Yaani, kina uwezo wa kutawala wakati wowote. NI sawasawa na Labour na Conservative kule UK au Republican na Democrat huko US.. vyama hivi vinaweza kubadilishana (mbadala) madaraka bila wananchi kuwa na wasiwasi na wananchi wanaweza kukichagua kimoja badala ya kingine.. n.k
Kwa hivyo CCJ inataka kujiweka kwenye mahali pa kuwa mbadala wa CCM. CCM ni chama cha Kibepari wakati CCJ ni chama cha kijamaa! Vina sera tofauti na mitazamo tofauti kabisa..
Mimi nafikiri kuwepo na changes za kiungozi katika chama cha CHADEMA ili kiweze kuimarika na kwenda mbele. Nafikiri kungekuwepo na switching ya Katibu na Mwenyekiti, mimi naona Dr. Slaa akiwa mwenyekiti na Mbowe akachukua ukatibu, mambo yatasonga, maana kumeishakuwa na dalili ya matumizi mabaya ya pesa kwa upande wa Mbowe kwa kutumia cheo chake cha Uenyekiti, lakini kwa upeo wa watanzania nafikir wanamuona kama Dr. Slaa ni mtu ambaye anaweza kuongoza nchi kama akipitishwa kugombea uraisi na akashinda, pia upinzani waweza kukubali kushirikiana kumuungania kama mgombea mmoja. Hata Lipumba atampa zote...na CCJ nafikiri nao watakuwa naye pamoja na vya vingine. Lakini Mbowe..kijana safi lakini hizi kasoro ndogo ndogo zinaaacha doa kwenye fikra za wengi.
Hata hivyo hii thread ni tofauti na hoja zakoAlitoka mzee mzima Njelu Kasaka muasisi wa G55, iwe du!!! haya mbunge ambaye hata NEC alikuwa haingii, hapana wakuuu. kwa kweli siione jambo zito la kuongelea hapa.... raha usikie Malecela, Warioba, Sitta, Kinana, Mwakyembe etc... ndio ametoka... hapo .... nitaangalia hiyo thread kila dk. 5.
..........................................Wakati huo nilizungumzia hii dhana ya chama mbadala, naomba nijinukuu "Nianze kwa kuweka bayana kwamba sipendezwi na jina vyama vya upinzani. Sisi wanachadema tunapenda kukiita CHADEMA- chama mbadala. Vyama hivi vinavyoitwa vya upinzani ni vyama ambavyo kwa malengo ya muda mfupi vinalenga kutoa fikra na sera mbadala. Havijaanzishwa kwa ajili ya kupinga tu!. Hivi ni vyama ambavyo kwa malengo ya muda mrefu vinalenga kuchukua dola na kutekeleza misingi na mipango mbadala. Ni serikali zinazosubiri. Sasa je, vyama mbadala vimekufa au vitakufa? Mimi nasema hapana. Vyama mbadala makini havijafa na haviwezi kufa. Labda vyama magirini. Mwisho wa kunukuu. (Maelezo zaidi unaweza kuyasoma hapa: http://www.jambonetwork.com/blog/?p=291
................................................
habari kama hizi zinafaa kwa shigongo..........................