Ujio wa CCJ: Yote unayotaka kujua

Ujio wa CCJ: Yote unayotaka kujua

Itakuwa jambo jema ikiwa wapambanaji wa CCJ baada ya kujiengua kutoka CCM wakashirikiana katika uchaguzi 2010 ili kupata wabunge wengi. Washirikiane katika kampeni nchi nzima. Pia waachiane majimbo pale ambapo upande mmoja unanguvu kuliko mwingine. Kwa hiyo nina wahimiza wabunge wote wa CCM wanaotaka maendeleo katika nchi yetu waondoke CCM, waingie CCJ na kisha waimarishe kambi ya upinzani

Mzee wa Kiraracha kasema....................................CCJ ni chui wa karatasi.........Hahahahahahaaaaaaaaaa !!!!!!!!!!!!!!
 
Jana wakati Mh. Fred Mpendazoe akitangaza kujitoa kwenye chama cha CCM alieleza kwamba, nukuu,

"CCJ siyo Chama cha Upinzani bali ni Chama Mbadala"

Nimejaribu kuitafakari kauli hii kwa makini lakini sijapata mantiki yake vizuri. Maswali ninayojiuliza bilas majibu ni haya:

1: Mpendazoe kusema hivyo anamaanisha kwamba vyama vya upinzani vilivyopo havifai au jina la "Upinzani" halifai?

2: CCJ itafanya mambo yanayolandana na ya CCM?

Wana JF mniweke wazi
 
Kwa kauli hiyo, itabidi iangaliwe vizuri. Wataalamu wa Lugha tusaidieni tafsiri ya hili
 
Hata mimi niliiona hii kauli.Lakini si ya kutilia mashaka sana kwani maneno mengi aliyotumia yanashabihiana n maneno ya viongozi waCHADEMA yaani wale amabo ni WAPINZANI kweli.

CCJ ikitwa chama mbadala what is a big Deal?si hta CHADEMA ni chama mbadala?

Pia nadhani mantiki ya kujiita chama mbadala ni kuondoa ile dhana ya kwamba wapinzani ni wakosoaji tu bila kutoa solution mbadala
 
Sioni shida katika matamshi hayo!

Ni kila mtu atakavyotafsiri, lakini ukweli unabaki pale kwamba CCJ sio CCM, na katiba ya CCJ tumeiona wote hapa jamvini!

Tusianze kunusanusa vitu vya kubuni tu, wakati CCM wameshachanganyikiwa huko, na wanagongana vichwa kwa kitendo cha Mpendazoe kuwakana hadharani!
 
Ni kweli kabisa hakuna cha upinzani.vyama vyote ambavyo haviko madarakani ni vyama mbadala sio CCJ peke yake.
 
Unaweza kuitazama kwa namna mbili. Kwamba CCJ ni Chama kilichoundwa kurejesha misingi ya awali ya waasisi wa CCM na hivyo kuwa mbadala wa CCM inayosemekana kwenda kombo kinyume na matarajio ya wapenzi wake wa awali. Au CCJ ni chama kinachokuja na sera, muundo na mikakati thabiti kushinda vyote ya kufanikisha malengo ya kuung'oa ujinga, umasikini na maradhi. Au vyote. Chama chochote makini lazima kijione mbadala wa kilichopo madarakani. Hadi sasa CHADEMA kimekuwa kikionekana na kujinadi kama chama mbadala. Lakini, kimsingi, vyama vyote vya kisiasa visivyokuwepo madarakani (pamoja na CCJ) vinabakia kuwa vyama vya upinzani.

Tatizo letu, kwa kukosa elimu na ufahamu mzuri, jamii yetu imezugwa na CCM/Serikali kwamba upinzani hauna maana kabisa katika mfumo wetu wa uendeshaji nchi; ni kundi la wachovu, wasioweza kufikiri, ambao kazi yao ni kupinga kila kitu. Hata viongozi wengine wa upinzani wamenasa katika ndoana hiyo na kujaribu kuongeza ukaribu wao na serikali na hivyo kuzidi kuharibu maana ya vyama vya upinzani. Labda wote wakijiita (kwa makosa lakini) vyama mbadala wananchi watawaelewa vizuri zaidi.
 
-mimi nilishatoa wazo hili tangu mwanzo.pia kama watazuiwa kushiriki uchaguzi mkuu basi wapange kuunga mkono harakati za CHADEMA kwani ndicho chama wanachoshabihiana nacho kimtazamo na kimalengo
 
CCJ wasikurupuke kama NCCR walivyofanya 1995, wafanye maandalizi vizuri ili chama kipate msingi wa kueleweka.

Iwapo watategemea opportunist wanaotoka CCM baada ya kukosa nafasi watajikuta wanafulia baada ya kipindi kifupi sana.
 
Mbadala, means that if you put it in power it will do things differently. If the other is not performing or corrupt, it then perform and not corrupt. Hata hivyo upinzani siyo neno zuri maana inaonyesha kuwa wewe unapingana na kila kitu anachofanya mwenzio hata kama ni nzuri au kwa manufaa ya wengi. Nadhani hii ni changamoto mojawapo ya watu kuogopa kuchagua vyama vingine zaidi ya CCM.
Nadhani it is high time to replace Neno "UPINZANI" kwa Neno "MBADALA"
 
Hayo ni maneno tu "mbadala" au "upinzani" lakini dhana ni moja tu kuweza kutawala.
Wangeweza kuungana na kua kitu kimoja wangekua unstoppable force lakini kwa mtaji huu wa utitiri wa vyama mwisho hakuna tija yoyote. Wangefuata ile methali ya Kiswahili isemayo Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
 
Mbadala, means that if you put it in power it will do things differently. If the other is not performing or corrupt, it then perform and not corrupt. Hata hivyo upinzani siyo neno zuri maana inaonyesha kuwa wewe unapingana na kila kitu anachofanya mwenzio hata kama ni nzuri au kwa manufaa ya wengi. Nadhani hii ni changamoto mojawapo ya watu kuogopa kuchagua vyama vingine zaidi ya CCM.
Nadhani it is high time to replace Neno "UPINZANI" kwa Neno "MBADALA"

"......it will do and accomplish the same thing differently"; Kama neno Upinzani linamadhara kiasi hicho , kuna haja ya kulipigia chapuo neno mbadala (alternative). Kwa hiyo wahusika kwa mfano ambao wamekuwa wakiitwa wapinzani watajulikana kama "Wabadala".
 
Mbadala = kuweka utawala bora na wenye kujali uzalendo na nchi kwa ujumla

CCM = Chama Cha Majambazi (Wengi)
CCJ = Chama Cha Jambazi (Tunaanza na mmoja)
 
Hivi huwa najiuliza CCM ni Chama Cha Mapinduzi. Hayo Mapinduzi walimpindua nani? Au ndo wananchi walipinduliwa? Na wapinduliwa wakakubali kukaa kimya baada ya kupinduliwa! Ni wakati muafaka waweke vizuri jina la chama chao====CCM- Chama Cha Mafisadi. Kwani wanaogopa nini kuweka jina lao halisi wakati wamekalia nchi kwa mabavu--Mapinduzi?
Wamesababisha sivai nguo yenye rangi ya kijani na njano hata kama ikoje......nahisi kujinajisi kwa rangi hizo. Au tuseme CCM ni Chama Cha Mashetani nini?
 
Wanasiasa wote fikra na matendo yanalingana na kinyonga, kujibadilisha rangi kifikra na kimatendo kulingana na mazingira, hivyo falsafa na kauli zao ni kivuli cha nadharia hiyo zaidi ya hapo tazama kauli za wapinzani wanaorudi CCM
 
-mimi nilishatoa wazo hili tangu mwanzo.pia kama watazuiwa kushiriki uchaguzi mkuu basi wapange kuunga mkono harakati za CHADEMA kwani ndicho chama wanachoshabihiana nacho kimtazamo na kimalengo

Mkuu Ben,

Kwanini unasisitiza CHADEMA ?????,ina maana hakuna vyama vingine vya upinzani au na wewe bado uko kwenye njozi za mchana kwamba CHADEMA ndio chama pekee cha upinzani?.

Kwa taarifa yako CHADEMA si chama cha upinzani wala si chama mbadala CCJ watakuwa wamefanya kosa kubwa sana kuwaunga mkono CHADEMA badala ya kukiimarisha chama chao.

Waanzilishi wa CCJ wamekimbia ufisadi na demokrasia hafifu CCM iweje leo waungane na CHADEMA ambao wamedhiirisha si chama chenye kufuata misingi ya democrasia,bado hatujasahau mizengwe aliyofanyiwa Bwana mdogo Zitto.

CCJ wanatakiwa waendeshe siasa zao kwa umakini mkubwa,wasikimbilie kuungana na NGO ya kina Ndesamburo.
 
Mkuu Ben,

Kwanini unasisitiza CHADEMA ?????,ina maana hakuna vyama vingine vya upinzani au na wewe bado uko kwenye njozi za mchana kwamba CHADEMA ndio chama pekee cha upinzani?.

Kwa taarifa yako CHADEMA si chama cha upinzani wala si chama mbadala CCJ watakuwa wamefanya kosa kubwa sana kuwaunga mkono CHADEMA badala ya kukiimarisha chama chao.

Waanzilishi wa CCJ wamekimbia ufisadi na demokrasia hafifu CCM iweje leo waungane na CHADEMA ambao wamedhiirisha si chama chenye kufuata misingi ya democrasia,bado hatujasahau mizengwe aliyofanyiwa Bwana mdogo Zitto.

CCJ wanatakiwa waendeshe siasa zao kwa umakini mkubwa,wasikimbilie kuungana na NGO ya kina Ndesamburo.

Mkuu,thanks

Ila umetumia nguvu nyingi sana kutoa hii hoja,si hatari namna hiyo ndugu

Nimependekeza CHADEMA kwa kuwa CHADEMA ni central party.Watawez kuungana na CHADEMA zaidi kuliko NCCRambao ni conservatives au kuliko TLP isiyo eleweka.

Ukifuatilia kwa umakini sera za CHADEMA na yale ambayo CHADEMA wamekuwa wakiyasimamia basi utaona hata wale watu waliojiunga na CCJ kama huyu Fred mpendazoe amekuwa inspired na vitailiyoasisiwa na wanachadema.Still naamini CHADEMA imekuwa na nguvu kubwa bungeni katika kuiwajibisha serikali na katika kutoa suluhisho mbadala la janga la uongozi wa Taifa letu

Ndiyo mana unaona hata CCM iliamua kuiga mambo mengi ya CHADEMA na kuyaweka ktk utekelezaji ingawa walitekeleza kw kufeli kwa kuwa waliiga vitu wasivyo na ujuzi navyo na hawaviamini moyoni mwao

Kuhusu Hoja ya Mbowe na Zitto,mbona basi Zitto alikubali na kuendelea kuwa ndani ya hicho chama?Hoja hii tu haiwezi kuzuia CCJ kuungana na CHADEMA ikiwa watazuiwa kushiriki uchaguzi mkuu ili kupanua wigo wa kuiwajibisha serikali bungeni
 
kimsingi upinzani ni mbadala wa unayempinga. Kwahiyo vyama vyote vya upinzania ni vyama mbadala wa kilichoko madarakani. Upinzani unaleta maana ya kuwa we unapinga kila kitu kinachosemwa na chama tawala hata kama kina mantiki. Vyama mbadala wakati mwingine vyaitwa "ruling party in waiting" maana vinasubiri wakati wao hata kama ni miaka 100 ijayo.
 
Back
Top Bottom