Akitoa tamko hilo jana wakati wa kuapishwa kwa makamanda wa UVCCM mkoani hapa, Kamanda wa UVCCM wa mkoa huo, Gasper Kileo, alisema chama hicho hakikujua kama kinaumia, kwa kuwa kiliteua mbunge asiyekuwa na uchungu na wapiga kura wake.
Alisema Mpendazoe aliwatelekeza wapiga kura wake pamoja na kuwanyima haki yao ya kuwa na mwakilishi bungeni hasa katika kipindi hiki cha bajeti.
Kileo alisema dalili na mwenendo wake vilikuwa tayari vimeshaanza kukinzana na maadili ya chama hicho, hivyo uamuzi aliochukua ni kuipa ahueni CCM na jimbo, kwa kuondokana na viongozi wasiozingatia maadili ya chama na badala yake wanatumia nafasi hiyo kujineemesha wao. " Kwanza tunamshukuru kwa kuitafsiri vizuri katiba ya chama inayomruhusu mtu kujiunga na chama kwa hiari yake na kujitoa kwa hiari yake, siku zote kuna msemo usemao: "Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi," alisema kamanda wa vijana