'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Mtazifunga izo shule zenu za kishenzi zilizoshusha elimu hapa nchini...
 
Ingekuwa mm ningepeleka mswada bungen kwamba ukisha kuwa mtumishi wa uma ni lazima mtoto wako asome shule za serikali,familia zitibiwe kwenye hospital za serikali najua hiyo ingesaidia kuboresha hizo huduma,nakumbuka kipindi tupo shule kipindi hicho tulikuwa tunasoma na watoto wa watumishi wa uma kama wakuu wa mikoa au wilaya lkn siku hizi c dhan kama kuna mtu anapeleka mtoto wake huko..

ubadhirifu na ufisadi,ukwepaji kodi ndio umelileta taifa katika mkwamo huu mkuu
 
Omba radhi... tutake radhi...mtoa mada tuombe radhi...

Haiwezekani mtu apange ada $ 10,000 kwa mwaka ya sekondari...!! Tz sio shamba la bibi tena...

Hizo shule geuzeni bar, au guest house au Hotel tu...!!!

Ada ni sh. 150k for day pupils and 380k for pupils boarding... hutaki unaacha.. mazafantas, marufuku kulipa zaidi ya hapo...

😨😨🚶🚶👍👍 Magufuli safiiiiiiii
 
kila mradi mkubwa unaotaka kufanya kwenye nchi yoyote duniani kuna policy..unatakiwa uzisome na ujiridhishe kama upo tayari kuekeza.
Binafsi naona inachofanya serikali hakuna jipya.... Ni kuwaambia tu watu (waekezaji) wafuate utaratibu na taratibu za mradi husika... Kama vile eura wanavyofanya kazi, tanesco nk...wanapewa bei elekezi
usije kuwa upo kwenye lile kundi la "mangungo wa msovero"....kusaini au kukubali mkataba bila kujua kilichopo ndani.
Ningekuelewa kama ungependekeza huo utaratibu ubadilishwe...ili shule ziende kwa nguvu ya soko

mkuu watu wanapolalamikia situation yoyote hupaswi kuwambia neno sera ama sheria ama lolote ili tu kuendelea kuwakandamiza! Unatakiwa kujua kwamba hicho unachokiita sera au sheria ndicho kinachopingwa. Na kwa hiyo vyovyote kitakavyoitwa hakikubaliki! Hata wakoloni na apartheid walikuwa wakitumia sera na sheria.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!
KITABU CHA BIBILIA KINASEMA

WATU WANGU WANAANGAMIAA.KWA KUKOSA MAARIFAA

NDUGUYANGU RAFIKI YANGU USICHOKIJUA TU ELIMU NI HUDUMA YA JAMII SIO BIASHARAA ..NA NDIOMAANA WANAHIMIZWA WAJUE KUANZISHA SHULE SIO KWA.LENGO LAKUPATA FAIDA.N KUTOA HUDUMA

SASA UNAPOONA EWURA ANAPUNGUZA BEI UNACHEKWLWA.N SABABU ILE NI HUDUMAA NA VILEVILE.NENDA WIZARAN.SOMA IJUE SHERIA.ZAKUANZISHA SHULE UTAELEWA N HUDUMA KILA.MTU ANAiTAJI

TUNAANZA.NA BEI ELEKEZI RASMI KWENYE ADA HIYO AIMEZEKI MKISHINDWA BADILISHEN.YAWE MAKANiSA...TUNACHOOMBA SERIKALI IKAE NA.WAMILIKI WAPUNGUZIWE BAADHI YA.KODI KUFIDIA PUNGUZO..
 
jamani hebu tujiulize nia ya shule za binafsi ni nini?

ilikuwa ni kutoa elimu kwa wa;e waliokuwa wamekosa nafasi ya kuendelea katika shule za serikalia kwa maana nyingine wale waliokuwa wamefeli ama darasa la saba ama form4. wakati shule hizi zilipoanza nyingi zilikuwa za wazazi ama za taasis za kidini kama hasa kanisa la katoliki ama ELCT. miaka ya 1970's baadhi ya shule hizi zilitaifishwa na serikal na hivyo kufanywa za serikali kabisa.

lakini zilipoonekana hizi za binafsi hazitoshelezi hasa pale serikali ilipofanya shule ni za kuchangia kwa maana ya cost sharing ndipo watu binafsi walipoona uhitaj wa kujenga shule kwan hakukuwa na maana tofauti tena kati ya shule za serikal na za binafsi.

elimu ilipofanywa kuwa biashara ilisaidia kupanua wigo wa uhitaj wa elimu. na hivyo kuleta ushindani sana katika jamii. ili sasa shule hizi kuweza kupata wateja ilibidi kuongeza kiwango cha elimu na kuwalipa waalimu wao vizuri.

tofauti iliuojitokeza kati ya shule binafsi na za serikali ilikuwa kwamba shule za binafsi zinategemea kila kitu kutoka kwa mteja na mwisho wa siku mwenye shule apate faida kifedha. shule zaserikal zilibaki kuwa duni kutokana na matatizo ya kimfumo na hivyo kushindwa kuleta ushindan kwenye soko. Licha ya kwamba shule za serikal ni cost sharing lkn mahaitaj muhimu ya shule yalikuwa ni ya shida na bado stahiliz a waalimu zimekuwa ni za tabu na hivyo kupelekea waalimu wengi kwenda kufanya kazi kwenye shule za binafsi kwenye maslahi mazuri zaidi.

shule binafsi zimekuwa na mtindo wa kutoza ada kubwa ili kuweza kulipa waalimu wao vizuri, lkn pia kuboresha mazingira ya kusomea. kitendo sasa cha kusema ada zishushwe kuwepo na bei elekezi ni sawa lakni pia lazima tathmini ya kina ifanywe kuhusu ubora wa elimu itolewayo na maslahi ya waalimu husika. jambo la muhimu la kuzingatia ni kwamba shule hizi zisirudishwe nyuma kiubora ila serikal ijitahidi ipandishe ubora wa shule za zake. Kuna hatari sana shule hizi kuvutwa nyuma ili zilingane na za serikal jambo ambalo litachangia kudidimiza elimu yetu. Ombi langu kwa serikali ni vyema shule za serikali ziboreshwe sana ili kuweza kufikia ubora sawa na ule wa shule za binafsi.

kwangu mimi nafkiri kwamba bado hali hii serikal itaitafakari kwa kina zaidi
 
Nyinyi ndio mliofanya wafanyakazi wawe wezi, ada kila mwaka juu , kodi za nyumba zinapaa , bidhaa muhimu zinafumka tu bei ....hakuna true free economy dunia nzima ....kuna public goods lazima serikali iwe na mkono ...
ukowapi togonge psii calabash umenifurahisha sanaa
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!
Tulia weye wakukamue jipu,acha kulialia hata kabla hujaingia theatre.Tunataka majipu yote yatumbuliwe
 
MAJIPU yanatumbuliwa,tutasikia kelele nyingi sana humu jamvini.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Kwahiyo unamaana hata huduma za usafiri binafsi ziachwe huru na wenye mabasi wajiamulie nauli yao??
 
mleta mada shule yako imekudodea ndio maana unapanic, we fikiria ada ya chekechea mpaka 5mln, ni uhuni huu, kila likizo ya miezi 3 mtoto aende na ream ya karatasi, mwanafunzi wa chekechea anamalizaje hizo ream 3 ? Wizi mtupu.vip mafuta,umeme na maji au vyombo vya usafri vinapopangiwa bei nako unachukia ?

mada iko specific kwenye elimu. Usipate tabu mtoe huko mtoto wako mpeleke kwenye shule zaserikali rais wako kasema eti elimu ni ya bure. Tabu ya nini?!
 
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa serikali katika juhudi kubwa inazozifanya kuweka usawa katika elimu nchini.Kitendo cha kuzuia shule binafsi kupandisha ada 2016 ili kusubili ada elekezi ktoka wizara ya elimu na ufundi stadi.Hii binafsi nimelipokea kwa furaha kwani kumekuwepo ile kasumba ya wamiliki wa shule binafsi kupandisha ada kwa kila mwaka.mfano ada inapanda kutoka 1600000 kwa mwaka hadi 2000000 kwa mwaka,hapa kuna ongezeko la shs 400000.Tukumbuke kuwa pamoja na kupandisha ada hiyo ado wanafunzi hawapati huduma za msingi zinazoendana na ongezeko hilo.Mfano kuna shule moja hapa Arusha makumila secondary school,ada yao ni tshs 1300000 kwa mwaka {boarding scholars} wakati jengo la bwalo grofa moja linajengwa kwa nguvu ya wanafunzi hivyo kila mwanafunzi alitakiwa aje na tshs 100000 za ujenzi wa jengo hilo na wale wanaorudia mitihani kwa mwaka mmoja.Mie najiuliza hizi shule inajengwa na wanafunzi au mmiliki?.mwakani kila mwanafunzi anatakiwa alipe ada 1800000 kwa mwaka wakati huduma ya chakula ni ile ile kila mwaka hakunaga mabadiliko.mambo ya maradhi ni ghalama ya mwanafunzi mwenyewe ikiwa ni pamoja na godoro,ndoo,neti,jembe na mengine na wakati huo huo analipa 140,000 za uji na 10000 za mlinzi.
Serikali iliamua kuruhusu shule inafsi kwa lengo la kutoa huduma ya msingi kwa jamii,lakini wao kila mmoja anajipangia bei bei zake inategemea ameamkaje kwa siku hiyo. kuna baadhi ya shule wanafunzi analipa hadi millioni 6 kwa mwaka.na hili kuondoa matabaka haya serikali inatakiwa kuweka viwango vya ada elekezi kwa shule binafsi ili kuwafanya wale wasioo na uwezo wa kuwapeleka wanafunzi academy wasijisikie wametengwa na serikali yao.
Wanafunzi hawa wanaosomea shule binafsi kwa ghalama kubwa ndo tunatengeneza majipu mapya ya wizi wa mali za umma kwa kuwaza kuwa walitumia fedha nyingi katika kusoma hadi kukosa uzalendo na huruma kwa watanzania wenzao pale wanaposhika nyadhifa mbalimbali za umma.

Tujadiliane.
 
Serikali lazima iingilie kati haswa kwenye mazingira ambayo watu kama nyie mna abuse concept ya "Free Market" au Soko huria...kwaufupi, lazima muwe regulated...kama hutaki nenda Uganda kaanzishe shule...huko hakuna regulations, unaweza ukaenda uchochoroni ukakutana na shule inaitwa Manchester University college nursery primary high-school....

jamaa atakua kaelewa,watu walizoea kupiga hela wanapoona jpm anaziba mirija lazima wataharuki na kuanza kutafuta upinzani tkt social network ili ionekane watu wanapinga na sisi tunawashona ipasavyo tena wengine wana madeni bank.
 
private mmejiaribia wenyewe toka lini ada ya elimu ya msing, secondary ikawa zaidi ya chuo kikuu. Tuwalipe milioni na nusu afu muajiri form six leavers wafundishe watoto. Pambafu mtaisoma no.

Mkuu hapo umenena. Washenzi sana kwani no kweli ukienda kwenye hivyo vishule St. Mary and the like walimu vilaza waliofeli form 4 na 6 matokeo watoto ni vilaza square na wana term 3 kila baada ya wiki 3 watoto wamefunga shule sasa sijui wanasoma saa ngapi. Vikaratsi vya ada na michango kila kukicha. Magu na serikali yako ada elekezi fuatilia kwa karibu mheshimiwa
 
Pale Upanga kuna shule za kiingereza za Diamond na Olympio ni mali ya serikali maalum kwa wakazi wa Upanga ambao kiuchumi wako karibu na MUNGU
 
Jamaa alikua anaona watu wanaleta mada na matatizo yao wanashauriwa vizuri, akaona ngoja aje muumsaidie kupunguza stress na kumpa moyo. Duh watu wabaya nyie yaani kuanzia post ya kwanza ni za uso tu. Huku serikali imempiga za chembe na ninyi mnammaliza na za uso. Mhurumieni mwenzenu jamani
 
Back
Top Bottom