The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,176
- 4,917
Serikali inapendekeza marekebisho ya Kodi na Ada za Pikipiki (Bodaboda) 2026/2027. Serikali imeamua kutowaingiza wafanyabiashara wa pikipiki (bodaboda) kwenye mfumo wa kodi ya makadirio (presumptive tax), kutokana na ugumu wa utekelezaji wake kwenye sekta hiyo.
Badala ya kodi hiyo, Serikali inapendekeza kufanya marekebisho ya sheria ili kuongeza ada ya usajili wa pikipiki (wa mara moja tu) kutoka Shilingi 95,000 hadi Shilingi 150,000.
Hatua inaelezwa kulenga kulinda biashara hizo ndogo zisiumizwe na kodi za kila mara, huku ikitarajiwa kuingizia Serikali mapato ya ziada ya kiasi cha Shilingi bilioni 17.75.