Mfumo wao wa soko umekomaa na utawala wa sheria pia umekomaa kuzuia upuuzi huu tunaouona hapa kwetu. Soko linadhibiti mtu hasijipangie tu bei anayotaka, hatapata wateja; lakini utawala wa sheria ni komavu unazuia uonevu usio na msingi. Tunavyo vyombo vya udhibiti, badala ya kutekeleza majukumu yake wankimbikia kupanga bei badala ya kuweka mifumo thabiti! Upangaji wa bei isiyo lingana na matakwa ya soko haitadumu, sana sana itaua huduma hiyo.Ada hazina uhusiano na ujamaa kwa jinsi unavyotaka kutuaminisha. Uingereza na Marekani ambao ni mabepari wakubwa hawapangi ada lakini wanayo namna ya kuthibiti ili iwe affordable kufuatana na huduma inayotolewa na taasisi za elimu
Hata huko kwa mabepari serikali zipo na Ndio wahusika.Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!
Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".
Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!
Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!
Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!
Anamaslahi na hizo shule huyoUmeguswa wewe kwenye ilo ndo maana unakuwa mkali kasome masharti ya uanzishwaji wa shule ndo urudi apa.Policy ipo watu walikuwa wakiiby pass.
Kila sector ina bei elekeZi mbona hulalamiki mafuta kupewa bei elekeZi au bse hauko uko?
Basi acha na wenye mafuta wajipangir bei watakavyo tuone kama patakalika apa
Porojo hatutaki!
Hii ni shule ya sekondari ya Marekani. Inaitwa Salisbury School.
Shule binafsi.
KUMBUKA KUNA SHULE ZA BURE! MPELEKE HUKO! OKOA MAPENE!!!Mwenzetu naona taratibu za serikali hujazikamata, lazima kuwe na taratibu za shule binafsi kuanzishwa na kuendeshwa, huwezi jipangia tu fees kama hakuna sheria, ni utoto na ulimbukeni, naona mzee wa msoga aliwadekeza wengi! Maana mpaka wakina mnukulu wanadai wao wana hela sana 80m/- sio kitu, wengine wanadai 10m/- ni hela ya mboga, nyoka mwenye makengeza kudai bilioni ni visenti tu, wengine kugawa mamilioni ya escrow kama njugu, nchi ilikuwa inaendeshwa kama ngoma za kikwere, wengine mishahara ya kubeba na mikokoteni sababu tu wameombwa kurudi bongo, wengine kuomba kusafiri kwenda nchi za nje zaidi ya mara tano! Kisa posho! #HAPAKAZITU..
Wazazi wanaowasomesha hizo shule ndio wakwepa kodi #panamapapers imetupanua macho, kukimbiza hela kule ili wasilipe kodi eti wawasomesha watoto kwenye hizi overpriced schools! Watu duniani wamewastukia wezi, wakwepa kodi na wala rushwa, mtasoma tu shule za kata popote zilizopo nchini kwenu...