'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Umeisoma namba eee! Funga hiyo shule yako, madarasa fugia kuku na mbuzi.
 
Sijawahi kuona Uzi ulioshambuliwa Kama huu..ningekuwa Mimi ndio huyo Reagan ningeomba mods wautoe..
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Magufuli aliwa beep wabongo kwa kulipangia bunge bajeti ya kufanya tafrija, kitu ambacho katika checks and balances hana mamlaka nacho.

Alipoona wabongo wanamshangikia, akajua hapa nafanya lolote ninalotaka.

Wengine tulioona makosa tume peotest udikteta huu, lakini nchi ipo katika euphoria, watu hawaelewi.

Sasa hivi hayo mengine hata sishangai.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Kariuni Kampalla na Nairobi, hata hivyo nature itawafundisha kwani mlimkaidi agizo la mzee sokoine na nyerere.
 
Hatukubari ujinga wako huu, Magufuli yupo kwaniaba ya watanzania na si vinginevyo, mmezoea kwenda kinyume na sheria sasa mtatulia tu
 
Tz is not pure capitalist country and there is no any country in world with pure capitalist or socialist economy, therefore govt intervention it's very crucial for the welfare of her citizens as we are in mixed economic
#whatwillmagufulido
 
Wakati wanaanzisha hizo shule binafsi, kulikuwapo na sharti ya bei elekezi, ila ilikuwa ikipindishwa na walarushwa. Anachokifanya Magufuli na Boyz III Men, ni kusisitiza hicho kipengele!

Uvae shati au uwe tumbo wazi, haina impact kwenye maendeleo ya nchi, ndio maana hamna bei elekezi!

Ukiona bei elekezi haifai, tumia majengo na rasilimali zako kwa matumizi mengine!

Pole sana! Maana kwa mwendelezo huu kutakuwa na fursa karibu sawa ya elimu kwa watoto wa maskini na matajiri.

Naona watu mnaumia na hili sababu kubwa itakua wengi ni maskini, Watanzania inabidi wapunguze wivu na wafanye kazi, kumuonea wivu tajiri sio sababu ya kusema wote wawe level moja, mtu tajiri kahangaikia pesa zake kafika alipofika, mnataka muendane kwenye kila kitu?

Elimu iliyopo kwenye shule za kata ni ya ovyo mno, kusema wanafunzi wote tuwaweke kwenye level ile mwisho wa siku hatutobaki na wasomi sasa, mimi nikomae wee kusaka pesa alafu nimpeleke mtoto wangu alishwe ugali na maharage yasiyo na viungo kila siku kama lunch? Au aende kulala kwenye vitanda dorms zenyewe wanaingiliwa hata na wezi usiku, maji ya kunywa hakuna. Wafix kwanza matatizo yote haya ndipo waanze kulalamikia private schools, ukweli utabaki palepale private schools nyingi wanafanya kazi nzuri kuliko shule za serikali. Wengi kinawauma tu kwa kua hawana pesa ya kupeleka watoto private basi hakuna zaidi ya hapo.
 
Huu ni wivu wa kijinga. Matajiri wengi na mafisadi hawataki watoto wao wachangamane na watoto toka familia duni kimapato. Serikali ikitoa bei elekezi kwa shule binafsi,wazazi/wengi wataweza kupeleka watoto wao hapo. Hizi shule binafsi zinajenga matabaka,wenye pesa nao wanataka kuwa wenyewe kwenye shule yao. Hawataki watoto wao wakutane na watoto wa walala hoi,hatimaye waanzishe mahusiano.
Magu ni mwalimu,mtoto wa mkulima. Mtoto wa JK alisoma Feza,pesa kibao,bado akadunda.
 
Hata wewe haujaelewa pia, swala hapa ni sheria za nchi, tuna sheria ya Elimu ambayo inasema kwamba Elimu yetu siyo biashara na serikali ndiyo inayopanga ada au ada elekezi na hakuna anayeruhusiwa kuongeza ada ya shule bila ya idhaa ya kamishna wa Elimu hiyo ndiyo sheria yetu ya Elimu inavyosema na ambayo kila mwenye shule kabla ya kupata kibali cha kufungua shule yake ameipewa akaisoma na kuikubali akasaini na kupewa kibali cha kuanzisha shule, sasa iweje leo hii Serikali inavyotaka kutekeleza jinsi sheria yetu ya Elimu inavyoelekeza wenye shule wapinge?

Elimu siyo biashara ndio lakini sehemu mtoto anapolala, chakula anachokula, huwezi ukapata malazi hayo shule za kata hata moja, kama hayo serikali imeshindwa kufix hadi sasa alafu tuseme elimu sio biashara ni ujinga, hiyo sheria ibadilishwe. Kama ni hivyo wafute na tuition zilizopo mtaani kwa kua na zenyewe zinachaji watoto kwa elimu ileile tu.

Shule za kata ziko ovyo, chafu, vyakula maharage tu yaliyojazwa maji, maji ya kunya hakuna, taa ikiharibika itakua fixed baada ya wiki mbili, watanzania huu wivu uliojaa kwa watu matajiri utatuponza, badala ya kufanya kazi kupiga pesa ili wote wapeleke watoto kwenye shule ambazo ni standard, tumekalia kutaka kuwavuta matajiri wote waje kwenye umaskini. Kwa nini tusiende juu kuliko kuwavuta chini? Wivu mbaya
 
Sindano imekuaingia unapiga mayowe tulia usukumiwe dawa kwanza
 
Lazima kula sekta iwe na regulatory authority, TCRA, EWURA, SSRA, TIRA na mengine mengi tu...
Hata elimu inalazimika kuwa na chombo cha kuregulate mambo ya ada, ubora wa elimu nk.
 
ada zipunguzwe lakini sio kwa kiwango cha 150,000 kilichowekwa na serikali...
 
jipu mkuu lishapusuka nini..?? hahahaha!! subirini ada elekezi.. sio kujipangia tu mil 5 mili 10
 
Maamuzi ya ada elekezi yana lengo jema ila lazima kuwa realistic
 
Hapa kuna unfair comparison. Unajua education is professional beaurrocracy. Human labour ni muhimu na kubwa ukilinganisha na petrol station au hata kampuni za magari. Ili kumodify hii approach serikari ingelipa mishahara ya walimu wa private ili kuwapunguzia mizigo owners na mameneja wa shule. In other way round, serikali itakuwa imedhibiti walimu wasio na sifa kufundisha hizo private, kukusanya kodi na zile za heslb. Lakini pia ingewapa uhakika wa ajira za walimu wa private halafu hao waajiri wao wa-top up posho na kadharika. Maana msala kwa wamiliki wa shule za private ni mishahara ya walimu. Kuna umuhimu Wa govt.kuintervine ila lazima wamaintain win-win situation other wise figusufigusu lake ni la hatareeee
 
Naona watu mnaumia na hili sababu kubwa itakua wengi ni maskini, Watanzania inabidi wapunguze wivu na wafanye kazi, kumuonea wivu tajiri sio sababu ya kusema wote wawe level moja, mtu tajiri kahangaikia pesa zake kafika alipofika, mnataka muendane kwenye kila kitu?

Elimu iliyopo kwenye shule za kata ni ya ovyo mno, kusema wanafunzi wote tuwaweke kwenye level ile mwisho wa siku hatutobaki na wasomi sasa, mimi nikomae wee kusaka pesa alafu nimpeleke mtoto wangu alishwe ugali na maharage yasiyo na viungo kila siku kama lunch? Au aende kulala kwenye vitanda dorms zenyewe wanaingiliwa hata na wezi usiku, maji ya kunywa hakuna. Wafix kwanza matatizo yote haya ndipo waanze kulalamikia private schools, ukweli utabaki palepale private schools nyingi wanafanya kazi nzuri kuliko shule za serikali. Wengi kinawauma tu kwa kua hawana pesa ya kupeleka watoto private basi hakuna zaidi ya hapo.

Kwani ukubwa wa bei (ada) nidyo ubora wa elimu?

-ishu hapa ni ada ziteremke. Tajiri atanufaika na masikini atamudu!
 
mafuta na usafiri ni tofauti na elimu. kwenda shule binafsi sio lazima, ni uwezo wa mtu. ila kupanda daladala utapanda tu, au la utembee au uwe na gari yako. vile vile kwa mafuta, lazima tu utanunua kama unahitaji na ndiyo maana kuna bei elekezi!

Mmmmm hivi hujui elimu kama ni muhimu na one of public goods?
 
Mkuu nakuomba upitie upya majukumu ya serikali baada ya kufanyika ugatuzi wa madaraka hasa katika sekta ya Elimu ili uelewe vizuri majukumu ya Serikali katika kushughulikia masuala ya elimu.

hoja ya kwamba jukumu la serikali ni kuhakikisha shule binafsi zinazingatia mtaala wa nchi peke yake siyo kweli, serikali ina majukumu zaidi ya hapo na ndio maana imeweza kwenda zaidi ya hapo ulipopazungumzia.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

We mjinga sana wewe.
 
Tz is not pure capitalist country and there is no any country in world with pure capitalist or socialist economy, therefore govt intervention it's very crucial for the welfare of her citizens as we are in mixed economic
#whatwillmagufulido

There is a difference between government intervention and government takeover of the pricing process.

Big difference.

Once economic forces are superseded by governmental pricing, that economy is called a command economy.

What usually ends up happenning is deterioration of services and scarcity.

We have seen this in the early 80s with ulanguzi etc, to a point of rations and quotas in buying sugar and flour.

We do not want to go back there again.
 
Back
Top Bottom