'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

huyu jamaa pumba kabisa yani unamaanisha kindergarten halali kulipa milioni 7??hii nchi lazima kuwepo na utawala wa sheria hivyo lazima mfate masharti kuliko kuwaibia wananchi!

mkuu umechangia nini kujenga hiyo shule?! Kodi yako?!
 
Hakuna hoja yenye mashiko inayotolewa kwenye utetezi wa hii sera ya kuweka ada elekezi.Kwa nini uelekezi uwe kwenye elimu Tu tena shule za msingi?Mbona vyuo vikuu vya private ambavyo hata masikini hupangwa huko hawaweki ada elekezi ilhali tumeona mpaka maandamano kushinikiza zishushe bei?Kwa nini wasianzie huko ambako ndiyo kero? Nani amewahi kuona wananchi wameandamania Ada ya shule za msingi?Sector ya afya inaelekezwa? Pembejeo na zana za kilimo vipi?Watu wanakero ya maji unawaletea umeme,Nonsense kabisa.Huwezi linganisha regulation ya mafuta ama usafiri na hii ya elimu maanake kwenye elimu kuna option kwamba if you can't afford private schools nenda serikalini ambako huduma ni ile ile and also reliable tofauti na usafiri(SUMATRA) ambako huduma za usafirishaji za serikali ni za msimu kama mvua.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!


Inawezekana huna hata mtoto wa kusingiziwa wewe
 
Siku hizi hata shule za mashirika ya DINI zinajipandishia Ada!!

Hakika serikali DHAIFU humfukuza MUNGU!!
 
Anaitwa Reagan C. Mabogo.
Join date: 3rd January 2014
Posts: 108
Rep Power: 422
Likes Received 33
Likes Given: 0
Jamaa kagongwa likes 33 bila majibu.
Ila angenifurahisha zaid angeongelea na mafuta kusiwe na taasisi inayo-regulate prices. Alaf tuone kama tutafika kwa linchi hili, lkn nakubaliana nae kwamba serikali iboreshe shule zake pia.
 
Wengi wa wamiliki wa shule, wapo chini wa viongozi wa serikali (walikuwa).
Ndio maana walikuwa na jeuri ya kupandisha ada kwa jinsi wanavyotaka, kweli binadamu hatosheki.
 
unatafuta sifa za kijinga eti na wewe ushawahi andika post ya kumpinga magufuli.
 
nyinyi ndio mliofanya wafanyakazi wawe wezi, ada kila mwaka juu , kodi za nyumba zinapaa , bidhaa muhimu zinafumka tu bei ....hakuna true free economy dunia nzima ....kuna public goods lazima serikali iwe na mkono ...

la bidhaa kufumka bei ni matokeo ya serikali kushindwa kimfumo! Mkazo zaidi weka kwenye neno "mfumo". Hilo la ada kupanda dawa yake ni moja tu: Peleka mtoto wako kwenye shule za serikali ulikoambiwa eti elimu ni ya bure.
 
Watu mnamtukana mleta mada wakati kaleta mawazo yake. Kwani hizo shule za private ambazo unalipa mamilioni mmelazimishwa kupeleka watoto huko?

Ni sawa na maduka ya nguo yapo yanayouza nguo flani kwa elfu kumi ila nguo hiyohiyo kwingine ikauzwa laki mbili, hujalazimishwa kununua.

Hapa mamlaka husika imekosea kabisa, wapewe shule kila mwanafunzi akilipa buku kwa siku tuone kama wataweza kutumia hiyo hela kumlisha mwanafunzi milo mitatu na kulipa walimu. It is stupid, yani hilo hata kilaza analiona wazi kabisa.

Wakati wanaanzisha hizo shule binafsi, kulikuwapo na sharti ya bei elekezi, ila ilikuwa ikipindishwa na walarushwa. Anachokifanya Magufuli na Boyz III Men, ni kusisitiza hicho kipengele!

Uvae shati au uwe tumbo wazi, haina impact kwenye maendeleo ya nchi, ndio maana hamna bei elekezi!

Ukiona bei elekezi haifai, tumia majengo na rasilimali zako kwa matumizi mengine!

Pole sana! Maana kwa mwendelezo huu kutakuwa na fursa karibu sawa ya elimu kwa watoto wa maskini na matajiri.
 
Mwacheni rais wetu afanye kazi.. Hizi kelele hazisaidii, hatuwezi kua na taifa watu wanajipangia ada milioni 4 chekechea tena kwa dolla, tulieni sindano ziingie
 
da mleta mada atakoma , hamna hata mmoja anayemuunga mkono
 
Mawazo ya kipumbavu hayo,----- wewe,HV mbona watanzania mnaakili za kiboya hivi,nchi zote duniani wananchi wanahitaji unafuu wa maisha katika huduma za jamii bila kujali gharama kubwa lkn sisi watanzania tunajifanya in watetezi sana wa ujinga tu.Tutamlinda Magufuli kwa gharama yoyote ile.
 
Utaratibu wa ada elekezi ulikuwepo hata katika serikali za awamu zilizopita kwa makubaliano ya kwamba hata shule za binafsi zipatiwe ruzuku toka serikalini kufidia pengo.

Tatizo lililokuja kujitokeza ni serikali kutotimiza sera na mpango yake yenyewe kwa kuzipatia ruzuku shule binafsi ili ziweze kujiendesha. Ni lazima tutambue kuwa elimu ndiyo kila kitu na ndiyo msingi wa maendeleo. Na ewekezaji ktk elimu hatuna namna ya kuukwepa kwa gharama yoyote ile. Na kuna usemi huu, kwamba, kama tunadhani elimu ni gharama, basi tujaribu ujinga kwani gharama yake ni kubwa zaidi !!

Na hii iko hata ktk shule za serikali yenyewe kwa maana ya kushindwa kuzihudumia ipasavyo kwa kuzipatia vifaa na fedha za kujiendesha kwa mfumo wa ruzuku.

Serikali yenyewe inachokifanya eti ni kuhakikisha tu walimu wanapata mishahara yao kiduchu, baaasi na kujiona imetekeleza jukumu lake ktk eneo hili. Mengine ni matatizo matupu. Hakuna vitabu, hakuna nyumba za walimu, wazabuni (kwa shule za bweni hawalipwi na mpaka sasa kuna wengine wameishtaki serikali), hakuna maabara na hii mbaya zaidi hasa ktk shule zilizojengwa kati ya mwaka 2005 - 2015 chini ya uongozi wa Kikwete maarufu kama shule za kata. Zingine hata hazina hadhi ya kuitwa shule ni kana kwamba ni mabanda ya kufugia kuku au nguruwe!!

Kwa mtazamo wangu tatizo linaloikabili sekta ya elimu hapa nchini si ada elekezi kwa shule binafsi au "bure" kwa zile za umma. Bali tatizo kubwa ni sera na utashi mbaya wa utekelezaji wa sera na mipango ya serikali. Hapa mchawi ni serikali yenyewe!!

Inawezekana kabisa tukawa na mipango mizuri ktk kutekeleza hili na kusiwe na misigano yoyote kati ya serikali na wamiliki wa shule binafsi ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma hii hautetereki. Mbona katika sekta ya afya imewezekana na kwa nini katika sekta ya elimu isiwezekane?

Kinachoweza kufanyika ku harmonize hii situation ni kwa serikali kwa mfano kuamua kuwa yenyewe itabeba jukumu la kulipa mishahara ya walimu wote ktk shule za umma na binafsi na pia kila mwaka kuzipatia shule za binafsi sehemu ya fedha za maendeleo kama ruzuku ili wanunue vifaa vya kufundishia na kujifunzia na pia kuongeza miundo mbinu ya majengo, madarasa, nyumba za walimu nk.

Ni kwa njia hii utakuta gharama za elimu za shule binafsi au za mashirika ya dini na asasi za kiraia zinaji - regulate zenyewe na hapa lengo la serikali la utoaji huduma za kijamii kwa wananchi wake kwa usawa linaweza kutimilika pasipo mikwaruzano.

Swali kubwa ni hili, kwamba ni kwa vipi hili litawezekana iwapo hili limeshindikana kwa shule za serikali tu yenyewe kwa miaka nenda miaka rudi na hasa hasa katika uongozi wa serikali ya Jakaya Kikwete ambapo ndipo tuliposhuhudia kuvurugika kwa kiwango kikubwa kwa mfumo wa elimu yetu!?

Na mwisho kwa ushauri tu kwa serikali ya JPM ya awamu ya tano ambayo imeonesha matumaini ya kurekebisha mambo mengi, ni kwamba, usimamizi wa elimu hasa elimu ya juu, vyuo, ufundi na sekondari urejeshwe katika wizara moja mama i.e Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi kwa kila kitu kama ilivyokuwa zamani kabla ya Utawala wa Kikwete!!

Hapa ndipo tulipoichaga njia kuu kwani wizara iligawanywa gawanywa kwa lengo tu la kuwapatia nafasi za uongozi watu flani flani kitu ambacho kiliongeza matumizi ya serikali.

Mfano haiwezekani ukawa na waziri anayehusika na elimu TAMISEMI na idara zingine nyingi huko zinazoshughulikia mambo ya elimu wakati tayari tuna wizara husika ya elimu inayojitegemea i.e Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi yenye taasisi na idara zake zote zinazoshghulikia mambo yale yale!!

Hali hii ilisababisha mgongano wa utekelezaji wa majukumu mengi kati ya Wizara ya Elimu na TAMISEMI na hata mambo mengi kukwama kutekelezeka kwa ukamilifu na ufanisi.

Kwa hiyo Rais wetu Dr John J.P. Magufuli anzia hapa kama tunataka kuirejesha elimu yetu ktk mstari wake. Angalia tulipoangukia na wala sioni sababu yeyote ya kugombana na wawekezaji binafsi katika sekta hii. Tatizo lilikuwa ni serikali yenyewe kwa kutosimama ktk maamuzi yake!!
 
Back
Top Bottom