'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Mbona bei za mabasi zina regulations, kwani ni mabasi ya umma yale? You can not let free markets forces decide the price of everything. Ndio maana nchi nyingine hasa zinazoacha free markets iamue kiasi cha ada, elimu imekuwa ghali mpaka inawaingiza watu kwenye madeni makubwa.

Elimu ni muhimu hatuwezi kuacha iendeshwe kama biashara ya hotel
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Hizo shule zenu za binafs ambazo ada ni za juu ndo zinashawishi watu kuiba na kujilimbikizia Mali.Bei elekezi ni bora zaidi coz kutakuwa na usawa na wepesi kwa wazaz kusomesha watoto.Hivi kweli ni halali mtoto wa chekechea kulipa ada 4.8m,,hapana hapa lazima kitu kifanyike
 
Bei elekezi kwa hizi shule za binafsi ni lazima,,maana wazazi wanabeba mzigo mzito wasio uweza ambao ndio unasababisha watu kuwa MAJIPU ili waeze kuendana na beat.Inashangaza kwa kweli mtoto wa shule ya awali kulipa ada ya sh 4.8mil zaidi ya ada ya mwanafunzi wa udsm anaenza shahada ya utawala biashara (BBA).Ili twende sawa bei ya ada elekezi kwa shule za binafsi haiepukiki.
 
Hahahaa,Mtoa uzi umeniacha hoi 🙂
Usipaniki,bei elekezi maana yake,utatoza Ada ya shule kulingana na Huduma unayotoa,Vivyo vivyo Kodi mtalipa mwaka huu,hamna ujanja ujanja na kulazimisha kuuza baadhi ya huduma ktk shule zenu
 
Nyinyi ndio mliofanya wafanyakazi wawe wezi, ada kila mwaka juu , kodi za nyumba zinapaa , bidhaa muhimu zinafumka tu bei ....hakuna true free economy dunia nzima ....kuna public goods lazima serikali iwe na mkono ...

India kuna bei elekezi kwenye kila bidhaa,, wanakoelekea wataweka bei elekezi hadi kwa madada poa hawa wafanyabiashara wa kibongo ni wezi sana..!!
 
Ni wapi nimeandika nchi iongozwe na free market pekee?

Unajua kusoma na kuandika?

Umeulizwa kuhusu pure capitalism, unajibu kuhusu capitalism.

Unajua kusoma na kuandika?

Nna mashaka na mwalimu wako wa econ pia uelewa wako juu ya world economy system history pia sina hakika kama ulichokua unakianda kunijibu kama unakielewa na kinatoka ktk akili yako labda nahisi unacopy na kupaste kutoka mahali flani
Hebu nisaidie nini tofauti kati ya pure capitalism na capitalism, ebhu tuanzie hapo kwanza
 
sio ikulu itoe ada elekezi bali kamishna mkuu katika wizara ya elimu ndio anayetakiwa kutoa ada elekezi msipotoshe umma
 
Nna mashaka na mwalimu wako wa econ pia uelewa wako juu ya world economy system history pia sina hakika kama ulichokua unakianda kunijibu kama unakielewa na kinatoka ktk akili yako labda nahisi unacopy na kupaste kutoka mahali flani
Hebu nisaidie nini tofauti kati ya pure capitalism na capitalism, ebhu tuanzie hapo kwanza

Hujajibu maswali niliyokuuliza, na kama uliyojibu, si niliyokuuliza.

Comprehension please.
 
Bei elekezi kwa hizi shule za binafsi ni lazima,,maana wazazi wanabeba mzigo mzito wasio uweza ambao ndio unasababisha watu kuwa MAJIPU ili waeze kuendana na beat.Inashangaza kwa kweli mtoto wa shule ya awali kulipa ada ya sh 4.8mil zaidi ya ada ya mwanafunzi wa udsm anaenza shahada ya utawala biashara (BBA).Ili twende sawa bei ya ada elekezi kwa shule za binafsi haiepukiki.

Serikali isharuka kimanga yakhee
 
Hujajibu maswali niliyokuuliza, na kama uliyojibu, si niliyokuuliza.

Comprehension please.

ndo maana ninasema una shida ktk uelewa wa hili swala kama hata maneno niliyoyaweka kwa msisitizo wa rangi nyekundu hujui nimekunuu wewe, hii inaonesha hujui hata maana ya ulichokisema hili nalo ni jipu na linapaswa kutumbuliwa watu mlikariri ili mpate credit tu wala hamjaelewa chochote, lazima mfumo ubadilishwe
Hayo mengine uliyouliza ni majibu sio maswali, tafuta swali uulize
 
Wewe ndiye una shida ya kuelewa, hata huelewi kwamba si kila mtu anaona rangi kama unabyoona wewe. Una assume tu. Hilo moja.

Pili, bado hujajibu uliyoulizwa, iliyojibu hujaulizwa.

Tatu, inawezekana unaona sijui ninachokisema kwa sababu una comprehension ndogo, huna uwezo wa kuelewa nuance.

Wewe uliyeelewa chochote mbona hujajibu maswali yangu?
 
Ndugu yangu so kila kitu uache market iongee. Nia ya wafanyabiashara ni kumaximize profit Na sehemu muhimu serikali inabidi iingilie kuwaprotect walaji. Mbona serikali inapoingilia bei ya mafuta tunaona ni sawa? Mbona serikali ikipanga nauli za magari tunaona ni sawa?

Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa kuhakikisha nchi ina usalama, kuna sheria zinazofanya mazingira ya biashara yawe somewhat predictable, kuna sheria zinazokataza wafanyabiashara wachache (oligopoly, duopoly, monopoly, cartels) kujipangia bei zao za ajabu kwa kutumia hila, collusion etc. Hapa ndipo habari za Anti-Trust law zinakuja. Marekani waliivunja kampuni ya simu ya Bell kwa kuwa ilikuwa kubwa sana kiasi ya kwamba iliweza kupanga bei inavyotaka yenyewe in a near monopoly. Na hao ndio champions wa free market. So najua serikali ina role.Serikali inaweza kuweka sheria kwamba asilimia fulani ya mapato ya shule iende kufanya kazi gani, na inaweza hata ku regulate net profit ya shule isiwe outrageous in percentage terms.

Lakini haitakiwi kuweka price ceiling.

Serikali ikiweka a price ceiling ni kama imekubali kushindwa kazi yake ya ku regulate the business environment. Ukiregulate vizuri business environment, kwa nini uhitaji price ceiling? That's the laziest and most business intrusive way of going about it.

Venezuela wananchi wamewatoa wabunge wa chama cha marehemu Hugo Chavez wiki hii kwa sababu ya ujinga huu huu wa serikali kupanga bei za vitu. Imetokea wafanyabiashara wanaona hawapati market price, wanatorosha bidhaa kwenda kuuza Colombia. Venezuela watu wanatenga siku moja ya wiki kusimama mstari ili kununua toilet paper na sabuni, let alone chakula. Unapanga mstari kwa saa tano, halafu ukifika mbele unaambiwa bidhaa zimeisha. Kama enzi zile za miaka ya mwanzo ya themanini Tanzania. Ndiko tunakoelekea huko na habari hizi za kupangiana bei.

Mimi nikitaka kuanzisha shule itakayojikita katika kuwapeleka watu CERN Geneva waende kuwa reseach scientists kwa kuanza tangu sekondari kuwekeza katika shule yenye state of the art labs na world class teachers, halafu nitoze watu shilingi milioni tatu kwa mwaka, watu wenye kujua ninachofanya na thamani ya elimu hiyo watalipa. Serikali inawezaje kunikataza mimi nisitoze hizo milioni tatu ambazo watu wamekubali kulipa?

Serikali inachotakiwa kufanya ni kujenga shule zake, itoe elimu nzuri, itoze hizo ada nafuu, watu wengi wakizikubali, hata hizo za private zitashuka naturally kutokana na forces za demand and supply.

Habari ya serikali kupanga bei itatufanya tukose mwana na maji ya moto, tutupe jongoo na mti wake. Shule za serikali zinaweza kushindwa kukidhi standards za elimu nzuri kwa hiyo ada, na shule nzuri za binafsi zitakongoroka kwa kushindwa kukidhi standards.

Kuna video moja nilikuwa naangalia, imepigwa katika moja ya hizi shule za binafsi zilizofanya vizuri, walikuwa wanafurahia shule yao kufanya vizuri. Ile video ukiiangalia tu kabla hujajua mengi sana kuhusu hiyo shule unaaanza kuelewa kwa nini shule imefanya vizuri. Watu wamefurahi, walimu wanaonekana wanaipenda kazi yao na bila shaka wanalipwa vizuri. Walimu wanaonekana wako karibu na wanafunzi. Hata mimi nikafurahi kwamba tuna shule kama hii Tanzania.

Sasa huyu Magufuli wenu akianza kutia mkono katika vitu ambavyo hajavijenga ataharibu.
 
hizi shule zinachangia mawazo ya kifisadi hasa kwa waajiriwa wapya serikalini

watoto wanabaguana hata mitaani kipindi cha likizo kisa shule zao.Ziletewe mizengwe zife ili wote turudi kwenye shule za umma, watoto wapate malezi yanayofanana

Hahaha, inaonekana watu wa dizaini hii ndio wale wale wenye mentality ya kumloga mtu atakayeanza kujenga nyumba ya tofali na kuezeka kwa bati kwa sababu atabagua wanavijiji wote wenye nyumba za udongo zilizoezekwa kwa nyasi.

Mawazo ya "heri wote tuwe masikini" ni chuki inayoota kutoka kutojiamini.

You got it all wrong.

Solution si kufuta shule za private, solution ni kuongeza ubora wa shule za serikali kiasi hizo za private msizione za hatari.

Ubaguzi ni hulka ya mtu. Hata kwenye shule za serikali unaweza kuwa na ubaguzi.

Halafu mara nyingine ni inferiority complex tu. Unaweza kukita watu wanajifunza kiingereza kwa kuongea wewe ukaona wanaringa na kubagua.
 
Wewe ndiye una shida ya kuelewa, hata huelewi kwamba si kila mtu anaona rangi kama unabyoona wewe. Una assume tu. Hilo moja.

Pili, bado hujajibu uliyoulizwa, iliyojibu hujaulizwa.

Tatu, inawezekana unaona sijui ninachokisema kwa sababu una comprehension ndogo, huna uwezo wa kuelewa nuance.

Wewe uliyeelewa chochote mbona hujajibu maswali yangu?

Mkuu mi narudisha majeshi nyuma kila mtu abaki na anachokielewa, ila kumbuka kukubali kusahihishwa ni ushindi mkubwa sana
 
Mkuu mi narudisha majeshi nyuma kila mtu abaki na anachokielewa, ila kumbuka kukubali kusahihishwa ni ushindi mkubwa sana

Ukishaanza kuongelea mjadala kwa metaphors za kivita, hutaelewa hata hicho unachojaribu kuhubiri.
 
Subiri hayo maelekezi ndo ujue una hoja ya kuanzisha Uzi au la. Ewura na Sumatra hulalamiki. Hapa umeguswa nini ?
Haja kujivua kuwa mchizi mafuta yanaagizwa ktk mfumo wa pamoja(bulk procorement) ndo maana h?ta sumatra anaweza panga bei kila kitu kipo wazi.watu wamekopa mabank wamejenga shule muwapangie ada bada la ya kuboresha tenu kila kitu serikali imeshindwa na private sectors angalia hospitali angalia shirika la ndege angalia shule huko nako katoeni bei elekezi
 
Ukishaanza kuongelea mjadala kwa metaphors za kivita, hutaelewa hata hicho unachojaribu kuhubiri.

Ebhu tuachane na hizo habari za injili kuna habari

Mesikia nchini Mexico watumishi kuanzia mosi January mishahara itapanda kwa 50% hivi ni kweli?? Kama ndio je ipo siku itawezekana hapa tz? Na Itakuwa chini ya huyu huyu magufuli au mpaka upinzani wachukue nchi???

Hlf duuu jana ratiba ya uefa last 16 imetoka kweli huu sio uonevu arsenal kupangwa na barca au ndo njama za kuitoa arsenal kwa nguvu??

Hlf Chelsea wanarudiana na PSG hii ni haki kweli au ni kumchomea tuu mourinho maana lazima wafungwe hlf vipi Man u Europa watacheza na nani??

Hivi case ya Zanzibar imefikia wapi?? Hlf Bado najiuliza lini magufuli atapewa uenyekiti wa chama au mpaka mwakani hlf hivi unategemea nn ktk bunge la awamu ya 5?

#Jibukwanza
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Sasa kwa nini wasilipe kodi kama ni hivyo? Wanaingiliwa kwa sababu hawalipi kodi.
 
Ebhu tuachane na hizo habari za injili kuna habari

Mesikia nchini Mexico watumishi kuanzia mosi January mishahara itapanda kwa 50% hivi ni kweli?? Kama ndio je ipo siku itawezekana hapa tz? Na Itakuwa chini ya huyu huyu magufuli au mpaka upinzani wachukue nchi???

Hlf duuu jana ratiba ya uefa last 16 imetoka kweli huu sio uonevu arsenal kupangwa na barca au ndo njama za kuitoa arsenal kwa nguvu??

Hlf Chelsea wanarudiana na PSG hii ni haki kweli au ni kumchomea tuu mourinho maana lazima wafungwe hlf vipi Man u Europa watacheza na nani??

Hivi case ya Zanzibar imefikia wapi?? Hlf Bado najiuliza lini magufuli atapewa uenyekiti wa chama au mpaka mwakani hlf hivi unategemea nn ktk bunge la awamu ya 5?

#Jibukwanza

Maswali yako tu yanaonyesha tofauti yangu na wewe.
 
Back
Top Bottom