'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Kumbuka hapa hakuna hata sheria moja iliyotungwa ndani ya awamu ya Magufuli, zote ni zaawamu zilizopita kwa hili laumu awamu zilizotunga sheria hii.
 
wewe ndio pumbavu kabisa usiyejielewa, kale makapi ulale shenzi wewe
 
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni... Sasa wamefungua na maduka ya dawa eti wale 'watu binafsi hawana issue'... Lets see how far they go...
 
Mtoa mada umeyataka mwenyewe watu wana hasira na ugumu wa maisha yamepata mkombozi nawe wamwita huyu mkombozi yeye na serikali yake ni wajinga. Sasa nani mjinga hapa?? Lugha uliyotumia unawapa watu nafasi ya kukuchambua wewe badala ya hoja. Umeandika kwa hasira matokeo yake ni haya. Shule binafsi zinatoza ada kiholela fuateni utaratibu. Mnatoza ada kushinda hata shule za wenzetu ng'ambo.
 
Magufuli aliwa beep wabongo kwa kulipangia bunge bajeti ya kufanya tafrija, kitu ambacho katika checks and balances hana mamlaka nacho.

Alipoona wabongo wanamshangikia, akajua hapa nafanya lolote ninalotaka.

Wengine tulioona makosa tume peotest udikteta huu, lakini nchi ipo katika euphoria, watu hawaelewi.

Sasa hivi hayo mengine hata sishangai.

Serikali ingepaswa kuziboresha shule zake na kutoza ada zilizo za chini kuliko zile zinazotozwa na shule binafsi.

Hivyo ndivyo inavyopaswa kushindana.

Lakini siyo mambo ya ada elekezi wala kupangiana ada.

Katika uchumi wa soko nguvu ya soko ingeachwa kupanga hizo bei.

Sasa sina hakika hapa serikali ya Magufuli inataka kufanya nini - to set a mandatory maximum fee?
 
Kuwa na ada elekezi siyo mbaya. Ila mbaya ni kupanga ada. Huduma na miundo mbinu kwenye hizi shule inatofautiana sana. Hapo ndipo ninapoona ugumu wa zoezi hili. Ni lazima kazi ya ziada ifanyike ili kuweza kutengeneza bei elekezi zinazo cover shule za maeneo yote.

serikali imefnya jambo zuri sana tatizo nloona hapa ni kukurupuka,hizi shule kubwa kubwa zina mambo mengi sana,tangu chkula,malazi,vitendea kazi etc mfano unakuta shule zina maabara mwanzo mwisho wakati shule za serikali ni magofu tu,unakuta wanafunzi tangu form 1 mpaka form 4 hata hajawahi kuiona bansen burner,sasa hapo unataka shule kama feza itoe huduma zote hizo kwa laki 3?hiwezekani.au tuseme tu tumerudi kwenye ujamaa,watu wote wasome shule za serikali japokuwa hazina kitu.
nadhani hii itashusha sana elimu.
kitu kingine ambacho nimekiona kwa watanzania ni kutokujitambua kwa kiasi kikubwa sana,yaani hawatambui kuwa huduma inazotoa hizi shule private ndizo huduma ambazo shule za kawaida kabisa zinapaswa kutoa,shule zetu za serikali ni kiini macho tu.mh rais angeanza kwanza kuboresha shule zetu hizi halafu ndo tuzishushe hizi zingine.unanilazimisha nitoe huduma kubwa kwa bei ndogo wakati hata wewe mwenyewe unayenilazimisha hufikii kiwango changu?
hii ni tatizo
 
da elekezi mnalia ina nauli elekezi mnataka,bei elekezi ya mafuta mnataka. JPM hajaleta sheria wala kanuni mpya. Anaamsha waliolala. Ni mwendo wa Karumekenge kwenda shule. Atake asitake Karumekenge atakwenda shule. Shikamoo rais wangu John Pombe Joseph Magufuri. Hapa kazi tu.
 
Mwenye uzi vipi bhana. Hii ni nchi, sio shimo la taka kwamba kila mtu anatupa kadri anavyojisikia. Hivi kila mtu akifanya atakavyo utajisikiaje. Vyakula, mafuta, kampuni za cm, dala dala, mabasi, umeme nk kila mtu apandishe anavyotaka kwa kuwa hakusaidiwa kujenga itakuwaje? Tuliza msuka, elimu yote ipo chini ya wizara. Wizara na serikal ndo vyapanga jinsi ya kuendeasha shule, mitaala, ada za mitihani na vyeti pia. Na wakiona haufai wanakufungia. So kama unamiliki shule kuwa mpole kwa kufuata maelekezo.
 
Hivi watanzania mnataka nn jamani? Mbebwe migongoni na raisi ndo muone serikali inafanya kazi, mshatunyonya sana na upandishaji wenu wa ada kiholela mmefanya shule kuwa biashara, hizo ada elekezi zitasaidia sana, tulipokuwa tunaelekea ada za nursery tu zingefika 5ml

mellisatz;
Nnilidhani umesoma kumbe div 5? Huyo atakaye mtoa mtoto wake shule ya kata inayo toa elim Bora na si Bora elim ampeleke St au Seminari fulani ni nani??
Huko nursery ulikosema, ni shule ngapi zina hiyo huduma ya nursery? Je huyo mwalim analipwa na Halmashauri gani? Jamani msijitoe ufaham.
Ikulu imeamua kuurudisha ujinga kwa kasi iso kifani. Elim si darasa la wanafunzi bila mwalim. Ijipange tu taratibu. Watoto huzaliwa kila siku, ndo maana wanaandikisha darasa la kwanza kila mwaka mpya wa masomo.
Hata akianza na hili darasa la kwanza leo, huku akijenga darasa la 8 kila shule mwakani hatutahitaji shule ya kata kwani tiyari tutakuwa na wanao ingia darasa la 8 la bureeee bwerereee. Lakini waliokwisha ingia sekondari hizo, waendelee wasibughudhiwe masomo yao. Ndio mantiki ya mleta thread
 
Serikali ni refarii mkuu kuhakikisha fair business, mbona inafanya hivyo kwenye mafuta na umeme kupitia EWURA.

Serikali zote sikivu duniani zinafanya hivyo, sema hii kitu ilikuwa ngeni hapa kwetu ndo maana wenye shule binafsi mnalalamika
 
Umeguswa wewe kwenye ilo ndo maana unakuwa mkali kasome masharti ya uanzishwaji wa shule ndo urudi apa.Policy ipo watu walikuwa wakiiby pass.
Kila sector ina bei elekeZi mbona hulalamiki mafuta kupewa bei elekeZi au bse hauko uko?
Basi acha na wenye mafuta wajipangir bei watakavyo tuone kama patakalika apa

Jipu linapotumbuliwa, damu kutoka ni sehemu ya tiba, tulia mwanawane dawa ipite.
 
Serikali ni refarii mkuu kuhakikisha fair business, mbona inafanya hivyo kwenye mafuta na umeme kupitia EWURA.

Serikali zote sikivu duniani zinafanya hivyo, sema hii kitu ilikuwa ngeni hapa kwetu ndo maana wenye shule binafsi mnalalamika

Fedha walizokuwa zinatosha, sasa #Hapakazitu.
 
Leo Wamarekani waliokwambia hivyo wanakopa kwa wajamaa hao hao huko China !!!

1. Hii si habari ya Wamarekani wala Wachina, ni habari ya kanuni za uchumi huria.
2. China si Wajamaa, ni Wakomunisti, kwenye vitabu tu. Na hata wao wenyewe wanakubali kwamba a market economy is the way to go, sasa hivi wana manage transition tu.
3. Government price setting is bad for the economy. Moreover, it is lazy.There is a myriad ways in which a government can institute a framework that would ensure a fair, sound and quality education system. Price setting is not one of those measures.
 
Acha tu turudi zama za mwalimu, let us experience the difference.

Ambao hatukuzaliwa enzi za mwalimu tunataka kurudishwa huko na mjamaa magufuri.

Kama ulimpigia kura mjamaa magufuri huna haja ya kulalamika, kubaliana na kila kitu.
 
Ndio uelewe kuwa jamaa anataka kufuta matabaka kwenye shule zetu. Ayo mazingira yafanane, pasiwepo na high class na lower classed citizens

Kama lengo ni hilo afute mfumo wa English medium na Swahili medium. Huu uamuzi ni wa hovyoo na bure kabisaaa......
 
Acha tu turudi zama za mwalimu, let us experience the difference.

Ambao hatukuzaliwa enzi za mwalimu tunataka kurudishwa huko na mjamaa magufuri.

Kama ulimpigia kura mjamaa magufuri huna haja ya kulalamika, kubaliana na kila kitu.

Demokrasia inakubali kukataa mambo ya mtu uliyempigia kura.

Si lazima kukualiana naye kwa sababu tu umempigia kura.
 
Back
Top Bottom