'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Nataka akimaliza shule binafsi sasa ageukie vyuo na hospitali binafsi.
 
Ujinga ni kuanzisha mada ya jambo usilo na weledi nalo. Hakuna taifa lisilo na mfumo wa Bei elekezi kwa kuwa wafanyabiashara by nature ni Profit maximizer. lengo la serikali ni kulinda na kutetea maslahi ya Raia na ndio sababu utakuta wakati mwingine inatoa ruzuku mpaka kwa taasisi binafsi kama shule na hospital ili kuboresha huduma zao, Hutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo n.k ndio sababu kwny uchumi unaambiwa hakuna pure capitalist state or pure socialist state kazi ya serikal ni kuingilia ili kulinda maslahi ya Raia wakati wowote. Mbona hulalamiki wakipanga bei elekezi ya Fuel, nauli n.k Ile tabia yenu ya kujipandishia ada kama vile Nchi haina serikal ilifika mwishi siku jk alipokabidhi madaraka nov 5. mnawatoza wazazi na walezi ada halafu ikitokea mnataka kuongez Madarasa mnaitisha michango ya ujenzi kama vile ni shule ya serikal mbona Bakhresa au Mengi akitaka kutanua biashara zao wanaenda benk au ku issue share badala ya kutembeza bakuli kwa wateja? mnataka mruhusiwe mcharge gharama kibiashara lakin hamuendeshi kazi zenu kibiashara kutwa mko wizarani kuomba ruzuku na misamaha ya kodi, wazazi wanalipa kodi lakin kila mpango wa kuendeleza shule lazima mkamue wazazi nje ya ada wanayolipa. Hili jipu lishatumbuliwa kazi iliyobaki ni kusafisha tu kidonda. Jk alipelekewa hiyo sera muda mrefu akawa anawaonea aibu sasa kazi kapewa Kauzu zaidi ya Dagaa mwendo wa sura ya mbuzi hakuna kuchekeana
Sijui ni. Nchi zipi zenye kufuata market evonomy unazoziongelea aambazo zinapanga bei? Kwa nini tusirudishe Tume ya bei? Tatizo ni kuchanganya mifumo...kisha tunachanganyikiwa. Hivi kweli hiyo bei elekezi ya mafuta inafanya kazi itakiwavyo na kutoa ushindani kwa watoa huduma na nafuu kwa walaji? Binafsi nafikiri bei elekezi ni kushindwa kwa mdhibiti na mfumo wenyewe - mifano uliyotoa ya kuchangisha watumiaji katika uwekezaji kwenye taasisi binafsi inaelekeza au ni ushaidi tosha kuthibitisha udhaifu huo wa kimfumo na kiudhibiti.
 
Watanzania tumeshaumiza na viongozi wezi na wajinga kiasi ambacho hatujui hata haki zetu za msingi. Kila mtoto aliyezaliwa Tanzania ana haki ya kusomeswa na serikali yake hadi walau kidato cha nne. Kama atasomeshwa shule binafsi au ya umma sii tatizo. Mzazi au mlezi ndiye mwenye wajibu wa kuamua mwanae aelimishwe wapi. Serikali ina wajibu wa kmfwatilia huyu mtoto alipo na kuhakikisha anapata kile kinachotakiwa kwa kuongezea malipo ya msingi kulingana na kipato cha mzazi au mlezi. Ndiyo maana nchi za wenzetu wanatoa vocha kwa wale wazazi wenye kipato cha chini walioamua kuwapeleka watoto wao shule za binafsi.
Nchi yetu imepoteza utawala wa sheria siku nyingi. Viongozi wanawaonea wanyonge kwa kuwasukuma pembeni ili wasijue haki zao za msingi. Shule za binafsi zitakuwepo na zitaendeshwa kwa gharama kubwa ili kutoa elimu bora. Cha maana serikali isimamie na kutoa miongozo kulingana na sheria na hata kubsidize kwa wale wanaosomesha huko kwa sababu mbalimbali pasiko kuwa na kiwango kinachotakiwa. Serikali isaidie kuwalipa waalimu na wafanyakazi ili sda ishuke kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na sheria. Serikali isiingilie tu kwa maneno, bali kwa vitendo. Yaani kwa kutoa fungu litokanalo na kodi ili kila mtoto apate elimu bora pale wazazi na walezi walipochagua. Hatuhitaji matabaka ya Kikwete, wauza madawa ya kulevya, wahujumu uchumi, na watawala wasioheshimu sheria za nchi yetu. Tunahitaji Tanzania inayosheheni Amani, Upendo, na Mshikamano. Tanzania inayotoa haki kwa wanyonge na walio nacho. Serikali inayosimamia sheria na mapato ya nchi kwa usawa. Tunahitaji serikali yenye heshima na utu. Serikali itakayosimamia elimu bora na yenye tija kwa wote. Tunayo mali asili kibao. Tujipange, tusonge mbele katika sekta zote hasa elimu hapa nchini. Tuna ukosefu mkubwa sana wa elimu ndiyo maana tuliridhishwa na ujinga wa kechekewa na kasi mpya, nguvu, mpya, na ari mpwa ktk wizi, udanganyifu, unyang'anyi, uzinzi, ulaghai, mauwaji, na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu. Zama hizi tuangalie elimu yetu, tuifanyie kazi na kulikomboa taifa letu.
 
Ccm ndio wanalalamika sana sasa maana walijua wataendelea kula kupitia system
 
Ndugu Mbogo, mbona upo Mbogo hivyo, au mwenzetu una kashule Kako ka private, lakini sivyo utakuwa mwalimu ambaye mnadanganywa na eti mishahara haiwezekani kupande bila kuongeza ADA kila mwaka.
 
Wamiliki wa shule za private wanajinasibu kutoa huduma na kuisaidia serikali, kama mnaona mnayemsaidia hataki si mzifunge ili msiendelee kupata hasara kwa mnayemsaidia? Kama wananchi wanazihitaji sana hizi shule basi subirien reaction kwa serikali yao pendwa watakapoanza kudai elimu bora hapo ndo mtakumbukwa kwa wema wenu(kama mnavyodai)
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

umeongea kama mdau wa shule binafsi kwa njia moja ama nyingine. Lakini pia umechanganya mambo mengi katika hoja yako ambayo kila moja linahitaji maelezo yanayojitegemea. Pana dalili ya hasira na jazba katika maneno yako. Haya maneno nakuandikia ni dibaji tu. Nitakurudia na maneno ya nyongeza kupinga fikra zako zilizo nyingi katika huu uzi. Ila kwa sasa niseme haya machache:

Hakuna mfumo wa uchumi katika taifa lolote duniani unaotoa uhuru usiokuwa na mipaka kwa sababu kufanya hivyo ni wendawazimu. Pili, kilichofeli duniani ni Ukomunisti wa Ki-Marxist, sio ujamaa! I shall return!
 
Huu uzi ndio picha halisi ya wanyonge huko mitaani ...raia wamechachamaa ...safi ...tumechoka elimu kugeuzwa biashara ....
 
Wala haitatekelezwa...ukitaka kuamini mtume mwanao na sh 320000 shule afu uone tutavyomrudisha...longolongo likija tunawarudishia watoto wenu tunaanza biashara nyingine..msituzingue tuwalishie watoto wenu kwani tuliwazalia?
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!
Nina mashaka na akili yako kama inatumika vizuri
 
Kwani wazazi wa watoto wanaosoma hizi private wamelalamikia ada kuwa ndefu.??

Maana naona mapovu tu. No logic.
 
Siyo jambo jipya hili bali serikali dhaifu iliyopita haikusimamia. Acha kusema sana sisi wenye watoto tunaijua adha na taabu tunayopata kusomesha watoto. Magufuli oyeee..
 
mbona watoto wa magufuli wanasoma shule za serikali na mkewe ni mwalimu wa shule ya serikali.

Sio wote, wa mama huyu hawasomi serikalini, lkn wengine yes, namfahamu mmoja ht Shule yenyewee alikuwa anazingua
 
Unakashule kako ulipanga kupandisha ada sio:what: hiyo hakuna na hakutakuwa na tabia ya kupandisha ada hovyo kama mlivyozoea:what:
 
Back
Top Bottom