HENRY14
JF-Expert Member
- May 13, 2021
- 2,340
- 4,386
Habari zenu wanaJF na wadau wa jukwaa la ujenzi.
Nimesoma mada nyingi humu kuhusu ujenzi wa makazi. Makazi yakizidi tunajikuta na miji na hatimaye majiji. Kama ilivyo kwa nyumba abayo ikipangiliwa vibaya 'livability' yake inakuwa ngumu, basi miji na majiji ni hivyo hivyo.
Kama mkazi wa Dar na mdau/mpenzi wa ujenzi na tasnia ya ubunifu/usanifu majengo, nimekuwa nikiangalia jinsi miji yetu ya Tanzania inavyokua, kwa fano Dar lenyewe. Siwezi kusema nimeitazama kitaalam sana ila naweza kusema nimejifunza machache, likiwemo suala la kwamba maendeleo ya maeneo yanayofanywa na wananchi ni kwa kasi kubwa kuliko wataalam wa mipango miji na huduma za jiji zinavyopangwa au kupatikana. Kwa maana vijiji na miji vinaanzishwa na wananchi na baadae huduma na miundombinu inapelekwa na serikali. Nazungumzia barabara bora, maji, umeme, shule, hospitali, nyumba za ibada, viwanja vya wazi vya starehe na michezo, n.k. Kwa mfano huu nimeona kuwa mwishowe tunajikuta tunajenga jiji lisilo bora kwa vigezo kadhaa.
Nimeona mada hii inaweza kuchambuliwa kwa namna tofaut, ila nimeona nianze na 'livability'(urahisi au ubora wa kuishi jiji husika), kwa maana naamini hili huenda ndilo jambo kuu la ujenzi wa miji. Hii ni 'big picture' na swali langu litakuwa ni "je, jiji letu liko 'livable'?" na "je, tunaweza kuliboreshaje?" na ni wapi tumepatia vema na kustahili kuwa mfano kwa majiji mengine?
Kama tutaweza kujadili suala hili, ningependa pia kuwashirikisha video chache za 'inspiration' kutoka kwenye miji mingine. Nianze na hii survey ya Most Livable cities ya 2014 iliyofanywa na shirika la habari la Monocle. Tumaini langu ni kuwa tutajifunza na kulinganisha na sisi tulipo na kujiuliza ni nini tufanye tubereshe majiji yetu.
NB: Nimeandika summary ila ya sec. 20 za hii video ila mimi mbovu wa kutafsiri kiingereza hivyo nitaweka kama ilivyo, baadae nitajitahidi kuiweka kwa kiswahili.
Summary
The most livable cities in the world get the essentials right:
Reliable public transport
Good Schools
Low crime
But they attain a more subjective excellence too. They must be cities which people would want to live and work. Cities that not only make it easy to get to the office, but have life in them too. These are steered by individuals who constantly look at other cities to improve, and they change and adapt, as any great city must, without losing sight of their strengths.
Karibuni.

Quality of Life Cities: Vancouver, Tokyo & Copenhagen: