Ujenzi wa barabara ya Ludewa - Kilosa yenye urefu wa Kilometa 24 umefikia Asilimia 90

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Musa Madirisha Kaswahili, Mhandisi Mwandamizi, Msimamizi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, TANROADS Morogoro anaelezea hatua iliyofikiwa katika Mradi wa Ludewa - Kilosa (Kilometa 24) Mkoani Morogoro umefika katika 90%.

Amesema kazi inayoendelea kwa sasa ni kunyanyua tuta la barabara na kuweka madaraja ya kati, makubwa na maboksi.

Mradi huo ulianza rasmi Mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika Julai 2023, gharama yake ni Tsh. Bilioni 32.9.
Mhandisi Mussa Kaswahili.jpg
Mhandisi Kaswahili anafafanua kuwa sehemu iliyobaki ni madaraja matatu ambayo ni Kobe, Wailonga na Mazinyungu, japokuwa kwa hatua iliyofikiwa barabara imeanza kutumika katika Kilometa 24 isipokuwa sehemu zenye madaraja matatu ambayo hajayakamilika.

Amesema: “Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutenga fedha na kuleta, kazi zilizobaki tunaamini zitaisha ndani ya muda.”

Aidha, ametoa rai kwa Wananchi wa Kilosa na vijiji vyake kulinda mazingira ya miundombinu iliyopo kwa kuwa ni faida kwa watumiaji wote.

Mradi huo unajengwa na Wakandarasi wazawa ambapo ulibuniwa ili kuwajengea uwezo kukiwa na muunganiko wa Wakandarasi 7, lengo ni kuwa miradi inayoendelea baadaye isiwe ya Wageni pekee bali Wazawa waweze kuchukua majukumu hayo.

Ameongeza kuwa “Mwanzoni barabara hiyo ilikuwa na changamoto kwa kuwa ina mito mikubwa na kutoka Dumila hadi Ludewa (Kilometa 40) ilikuwa unaweza kutumia saa tatu hadi nne safarini lakini kwa sasa unaweza kutumia nusu saa.”

Kuhusu umuhimu wa mradi huo, Mhandisi anafafanua: “Mradi huu utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kwa kuwa wakazi wengi wanategemea kutumia njia hii kwa ajili ya kusafirisha mazao na biashara zao.”
 
Milani wanayo jenga wazawa haidumu mfano kuna kipande cha lami ifaka madukani chenye urefu kama mita 200 hakina mwaka kulisha anza kupasuka na mitalo ya hovio tena uswa wa nyumba ya mbunge Asenga Sijua hata huyo mbunga hajayaona haya?
 
Back
Top Bottom