Ujasusi - Umoja namba 97

Ujasusi - Umoja namba 97

Tuendelee mkuu, naona Zakayo atajikuta anaonja joto la jiwe, Merina na Janeth watakutana,, tuendelee tuendelee mkuu
 
ILIPOISHIA
Basi turudi kwenye mika mitano nyuma siku hio ndio siku ambayo bwana Bruno anatumiwa picha na mtu asiemjua ikionesha kidani hicho ,huku chini ikiambatana na maelezo
“ ukitaka ukweli juu ya mahali alipo mtoto wako fika new Africa hoteli chumba namba 108 siku ya ijumaa saa nne kamili usiku hakikisha jambo hili linakuwa siri yako kosa moja tu utampoteza mtoto wako” huku video ya mtoto wake ikimuonesha katekwa .

UNAENDELEA SEHEMU YA NANE .
Siku hio bwana Bruno aliopokea ujumbe ilikuwa ni siku ya jumanne usiku kwenda jumatano , kwa hio alikuwa na siku mbili za kujiandaa , hakujua watu hao walikuwa ni watu gani na walikuwa wakihitaji nini.

Alitamani kumtafuta wema japo amuulize juu ya swala hilo lakini aliogopa kwani aliona watu hao ni watu waliokuwa wakimjua nje ndani , lakini alijiuliza inakuwaje watu hao wakajua kuhusu mtoto wake , je ni wema anamchezea mchezo , au ni mtu gani , hayo yalikuwa ni maswali mengi ambayo yalieongeza shauku ya kutaka kujua na siku hio ifike .

Hatimae siku iliwadia siku ambayo kwa Bruno aliisubiri sana kwa hamu , ilikuwa muda wa saa tatu kama na nusu hivi ndio aliokuwa akiingia ndani ya hoteli ya new Africa .

Aliingia ndani ya hoteli hio huku akiangalia saa yake , moja kwa moja alielekea kwenye bar ilokuwemo humo ndani na kuagiza kinywaji ,, kilichomshangaza ni kwamba siku hio ndani ya bar hio kulikuwa na ulinzi mkubwa sana ambao mpaka yeye ulishangaza ila hakutaka kujali sana .

Alivuta muda mpaka ilipofika saa nne kamili ndipo alienda mpaka kwenye lift na kuelekea sehemu alipoambiwa sekunde kadhaa tu alikuwa nje ya chumba namba 108 , aligonga mlango na ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrembo hivi mrefu alievalia suti nyeusi , aliingia na kisha alikaguliwa na mashine kisha alionyeswa kukaa kwenye moja ya sofa lililopo humo ndani huku akiambiwa subiri na muda mfupi baadae ndipo alipopigwa na mshituko baada ya kumuona mtu alieoko mbele yake .
“ mheshimiwa raisi “
“ ndio bwana Bruno karibu sana “ aliongea raisi na kwenda kukaa na baada ya hapo kuliletwa vinywaji aina ya cocktail(mvinyo) na akakaribishwa huku wengine wakiwapisha kwa maongezi
“nadhani upo kwenye mshituko bwana Bruno mkubwa sana , lakini nitangulie kwa kusema kuwa nakujua nje ndani , najua historia yako nzima ya maisha yako kwa ujumla , na hata simu na ujumbe uliopokea juzi unatoka kwangu”
“nimekusikia muheshimiwa , lakini ni nini dhumuni ya haya yote na unamjuaje mwanangu ?”
“safi sana Bruno najua mahusiano yako ya nyuma na wema , lakini pia namjua mtoto uliezaa na wema , nadhani uthibitisho niliokutumia umeuona , hapa nizungumzapo , mtoto wako yupo mikononi mwangu “
“Bruno lamberk alijikuta akipandwa na hasira na uchungu wa ajabu maana kila akimkumbuka mtoto wake huyo na jinsi alivyohangaika japo kuijua sura yake, jambo hilo lilimuuma lakini pia lilimpa shauku na furaha ya kujua kuwa mtoto wake yupo hai “
“ ni kweli mheshimiwa unachozungumza , lakini sijajua sababu ya haya yote “
“ kama nilivyotangulia kusema nakujua nje ndani , ndio kitu kinachonipa sababu ya kuwepo mahali hapa kuzungumza , najua kwamba wewe ndio kiongozi wa genge la uuzaji wa madawa ya kulevya afrika mashariki yote huku ukijificha kwa kujifnya kutoa misaada huku ukiharibu vijana wataifa hili ambao ndio nguzo ya nchi hii” aliongea raisi na wakati huo alikuwa siriasi kweli na alimfanya Bruno ashituke .
“unataka nini kwangu muheshimiwa ?”
“ nadhani mpaka sasa ushajua ninacho hitaji , nataka kuondoa biashara yote ya madawa ya kulevya nchini na wewe utanisaidia katika hilo “.
“hahahha.. mheshimiwa hilo ni jambo ambalo haliwezekani kabisa , na ni bora ukaendelea kuongoza kwa utulivu huku ukichana na swala hili kabisa litakuletea matatizo mbeleni “
“ nadhani bwana Bruno unanichukulia kirahisi , nimetoka mbali na kuyaweka rehani maisha yangu mpaka kufikia hatua hii na usitake kunitishia kwamba haliwezekani , linawezekana kabisa na wewe utakuwa mmoja ya watu ambao utasaidia katika hilo vinginevyo utaletewa zawadi ya mtoto wako akiwa maiti “.
“ huna huo ujasiri bendera wa kuuwa watu , na nikutahadharishe tu kwamba usije ukathubutu kumgusa mtoto wangu , utakiona kiti chako cha uraisi cha moto sana “
“kwa hio unataka kusema kwamba humtaki tena mtoto wako , au unanipima kama naweza kuua au siwezi sasa subiri uone “ aliongea na kisha alibofya simu akaongea kwa lugha ya kifaransa ambayo kwa Bruno ilisikika vyema baada ya sekunde bwana Bruno alipewa simu na hapo ndipo alipo sikia sauti mwanadada akilalamika kwa maumivu ya mateso .

Raisi aliichukua kisha akaiweka sikioni “ you can kill her now “ aliongea na kisha alimpa bodigdi wake simu huku akinyanyuka akiondoka .
“ wait bendera “
“ unataka nini kutoka kwangu “
“ are you ready to talk?? “ aliuliza raisi akimwangalia Bruno alietingisha kichwa kuwa yuko tayari na raisi alirudi na kukaa .
“ nahitaji kujua mtandao wa madawa ya kulevya unavyofanyika hapa nchini ,watu wote waliopo chini yako majina yao na mahali wanapo patikana “
“ unaloongea ni gumu kutendeka maana nitakuwa na wasaliti wenzangu na nitakapo sema tu jua na mimi nitakuwa mfu “
“ unamaanisha nini kuwa mfu ?”
“ kwasababu mimi sio mwanzilishi wa mtandao huo hapa Tanzania kuna waanzilishi , mimi nilipewa uongozi tu “
“tutakupa ulinzi na hakuna baya lolote litakalokukuta “
“ huna ulinzi wa kunipa mimi , mtandao una mizizi mirefu mno kuanzia ikulu mpaka idara za usalama kote huko kuna washirika na inawezekana hata huyo utakae nipa anilinde akawa mshirika , sasa niambie ni ulinzi gani ambao unataka kunipa ?”
“Bruno I am not asking you here , mtoto wako maisha yake umeyabeba wewe , na hapa huna choice ni wewe kukubaliana na mimi au mtoto wako afe , pili nakuambia nitakupa ulinzi so you have nothing to fear “
“ okey let do it , lakini nayafanya haya kwa ajili ya mtoto wangu sio vinginevyo na nataka unihakikishie ulinzi wa mtoto wangu “ aliongea Bruno na raisi alikubali hilo na muda mfupi baadae mwanadada mmoja aliingia akiwa na karatasi mkononi ulikuwa ni mkataba ambao ulipaswa Bruno asaini , ulikuwa na vipengele ambavyo bruno baada ya kumaliza kusoma alijikuta akitoa jasho .
“ alishika karamu huku akitetemeka na kumfanya raisi atabasamu , lakini Bruno aliishia kusaidi mkataba huo .
“ hongera sana na nikuambie hakuna baya lolote litakalo kukuta na kwanzia sasa na nataka nikutambulishe kwa walinzi wako wapya .” alitoa ishara na kisha waliingia watu wawili ,waliovalia suti alikuwa ni msichana mdada mrembo kweli mrefu wa rangi ya chocholate , mwingine alikuwa ni mwanaume kwa haraka haraka umri wakeulioonesha sio chini ya miaka 25.
“ huyu ni danieli na huyu ni suzzane . ni wana usalama , kuwanzia sasa ndio watakuwa walinzi wako ni makomandoo wako vizuri , na kesho suzzane utaniletea ripoti kutoka kwa Bruno . aliongea raisi na kisha aliagana na Bruno na kisha kuondoka .
*****
Wakati hayo yanaendelea ndani ya jumba la kifahari la mheshimiwa raisi mstaafu ndani ya sable hio kubwa , alionekana mheshimiwa mwenyewe akiwa sebleni na mvinyo wake akiangalia runinga , muda huo ilikuwa ni saa nne na nusu hivi usiku , alionekna kunogewa na kipindi kilichokuwa kikioneshwa kiasi kwamba hata simu yake ilivyo ingia uumbe wa maandishi alijikuta akihituka .
“mheshimiwa kakutana na Bruno saa nne kamili new Africa hoteli “ ulikuwa ni ujumbe mfupi lakini uliobeba taarifa iliomshitua sana mstaafu .
“ kwanini Bruno akutane na bendera ?”” ni swali la kwanza alilojiuliza huku akisimama akizunguka zunguka hapo sebleni .
“ lazima kuna kitu kinacho endelea sio bure , na kama itakuwa ni jinsi ninavyo hisi basi tumekwisha “ aliongea huku akichukua simu yake na kutafuta namba Fulani kwenye simu yake , na baada ya sekunde kadhaa alikuwa amekwisha kuipata na alipiga na ikapokelewa upande wa pili .
“sam Bruno kakutana na bendera “ aliongea mstaafu na kusababisha kimya kifupi .
“ ni kweli muheshimiwa ??“
“ ndio ni kweli nimepokea ujumbe mfupi kutoka ikulu sasa hivi “
‘ unahisi ni kipi wameongea ?”
“ siwezi kujua , lakini nina hisia mbaya juu ya hili na kama hisia zangu zinanimbia kweli basi itakuwa hatari kwetu .”
“ naelewa lakini Bruno hawezi kufanya hivyo kabisa , naelewa msimammo wake na anakotoka yule ila inabidi kesho tukutane tulijadili hili kwa mapana ili tujue ni kipi Bruno aliongea na muheshimiwa “ aliongea sam na mstaafu alikubali .
Siku ya pili yake asubuhi matajiri hawa walifika ndani ya hoteli ya serena walipo kubaliana , kila mmoja alionakena kuwa na dukuduku la kujua ni kipi Bruno aliongea na raisi.
“ jamani nina hisia mbaya sana juu ya hili , tunaitaji kulitafutia ufumbuzi mapema kabla hata bruno hajajua tulichokifahamu “
“ ni kweli sam na hili tokea jana nalifatilia kwa umakini mkubwa sana , lakini mpaka sasa sijajua wameongea nini , kwani muheshimiwa inaonekana anafanya mambo yake kwa siri sana “
“ sasa tunafanyaje ?”
“ mimi naona tusubiri , ila inabidi Bruno awe kwenye uchunguzi “
“ nina shushu wangu kwenye moja ya walinzi wa Bruno nadhani anaweza kufatilia hilo na akatupa majawabu , nishampa kazi hio tokea jana “ aliongea sam lakini kabla hajamaliza sentesi yake alipokea simu kutoka kwa mtu aliempa kazi .
“ ingia watsapp mkuu “ ilikuwa ni kauli moja tu . na sam aliingia watsapp , zilikuwa ni picha za danny na suzzane walinzi wapya wa Bruno . kwani caption ilisomeka hivyo .
“ Bruno kaongeza walinzi wapya picha zao hizi hapa “ aliongea sam na kisha zilipitiswa kwa kila mmoja ,
“ wanaonekana kama wanausalama “ aliongea mstaafu huku mkuu wa TISS mstaafu akichukua simu ile .
“ unawajua ??”
“hapana , ila kama sura zao zinakuja kuja nitumie hizo picha kuna mtu anisaidie kuzitambua , aliongea mkuu wa mstaafu TISS huku akimkabidhi simu rich sam , na alimfowadia , huku mkuu wa TISS akipiga simu .
“ Michael upo ofisini ?”” ilikuw swali la kwanza
“ ndio mkuu “
“ kuna picha nahitaji kuzitambua nakutumia sasa hivi “
“ sawa “ aliongea na kuzituma huku wote wakisubiria kwa hamu jibu na baada ya dakika kadhaa kulitumwa faili kwa njia ya watsapp .
““Danieli mtalemwa mwenye namba ya utambulisho N00D)( huyu ni komandoo daraja la kwanza amepata mafunzo yake nchini CUBA , china na Thailand , huku elimu yake ya kipelelezi na ujasusi akiichukua nchini Israeli , mafanikio yake ni makubwa sana katika operesheni alizo fanya hapa nchini ikiwemo ya amboni tanga , kibiti na rusumo ni mhitimu wa chuo kikuu UDSM ngazi ya shahada ,na uzamivu monash nchni Australia akisomea maswala ya uinjinia .
Suzzane rashidi ( aka miss k) namba za utambulisho N02S huyu ni komandoo daraja la kwanza , lakini pia amafudhu mafunzo ya kipelezi alikuwa nchini urusi kama undercover agent katika misheni ya umoja wa taifa , mafunzo yake kachukua CUBA na thailland huyu ni hatari Zaidi katika udunguaji , lakini pia ni mbobezi katika maswala ya computer (IT).”

Mkuu wa TISS alitoa jasho , hakutaka hata kuongea kitu aliwapa wenzake taarifa ile na kila mtu alishangaa.
“ nadhani sasa tunapata picha ya kinacho endelea kwasasa , nanusa harufu ya usaliti “. Aliongea sam .
“ sio harufu , Bruno keshatusaliti mpaka sasa na adhabu ya Bruno ni kifo kama sheria ya kundi inavyosema “ aliongea mstaafu raisi .
“ nadhani kwa upande wetu ni swala la kuchukua tahadhari kwa sasa , japo nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Bruno kahadaika mpaka kukubali kushirikiana na raisi “ aliongea mkuu wa majeshi .
“ mimi naitoa familia yangu mapema bongo huku tukiendelea , ila mheshimmiwa inabidi uandae ripoti ili iende makao makuu tuone wanatoa majibu gani “ aliongea rich sam.
“ ni kweli ila haina haja ya kupaniki kwa sasa , swala hili nitalishughulikia mwenyewe na nawahakikishia hakuna atakaepata madhara .’”
“ ni sawa lakini mimi familia yangu ni muhimu Zaidi “ aliongea sam na kisha kila mtu akinyanyuka . lakini hapo hapo kuliingia msaidizi wa raisi na kumpa kimemo .
“Mheshimiwa raisi bendera yupo mlangoni anataka kuingia “ .
Nzuri sana
 
SEHEMU YA 70
Ilikuwa ni muda wa saa mbili kamili za jioni ndani ya hoteli ya Krebb`ys iliokuwa ikipatikana ndani ya Mwenge jijini Dar , ndani ya chumba cha mikutano walionekana watu sita wakiwa wameketi kwenye viti katika chumba ambacho kilikuwa ni cha mikutano , moja ya watu waliokuwep ndani ya eneo hilo alikuwa ni mheshimiwa mstaafu Matinde na bwana Kizito kabwela , Abdallah khalifa , Merina sosteness , ICP wa arusha , bwana Hamduni , huyu alikuwa ni waziri mstaafu na Zakayo .
“Jamani nadhan tushasalimiana vya kutosha na kwasasa hatuna budi ya kwenda moja kwa moja kati a ajenda yetu iliotuletea mahali hapa ., jambo kubwa lililotukutanisha leo ni kupokea ripoti ya mwisho kutoka kwa Zakayo juu ya uchunguzi ambao tulimpatia aufanyie kazi hivyo moja kwa moja nitamkaribisha ili atupe ripoti hio na baada ya hapo mengine yatendelea “ aliongea Matinde na Zakayo alikaribishwa .
“ Naomba niende moja kwa moja kwenye uchunguzi wangu , kazi mlionipa ilikuwa ni kujua ni wapi Damiani alipo na hilo nimefanikiwa kwa asilimia mia moja na ninavyozungumza sasa , Damiani yupo ndani ya nchi hii akifahamika kwa jina la Stephano lamberk “ aliongea zakayo na kuwafanya wote waliokuwa hapo ndani kushangaa na kati ya walioshangaa Zaidi alikuwa ni Merina.
“ Unahakika na hilo bwana Zakayo , linawezakana vipi ?” aliuliza waziri mkuu bwana Hamduni.
“ Hivi ni vipimo vya urefu upana na unene wa bwana Damiani na hivi ni vipimo hivyo hivyo vya bwana Stephano lamberk kila kitu kinaendana , hio ni moja pili kwasasa sehemu ambayo anaishi Damiani ndio sehemu ambayo anaishi Stephano lamberk , katika uchunguzi wangu nilifanikiwa kumkamata kwa siku nzima bwana damiani ili kunipa nafasi ya kufanya uchunguzi wa hisia zangu na imegeuka ni kweli , kwani wakati wote ambao nilikuwa nimemshikilia damiani , bwana stephano lamberk hakuonekana mahali popote pale mpaka nyumbani kwake “
“ lakini hata hivyo bwana zakayo swala hilo bado linakuwa gumu kuaminika kwetu hapa , inawezakanaje Damiani akawa na sura mbili tofauti “
“ waheshimiwa swala hilo linawezakana kabisa kwa asilimia mia moja , huu ni ushahidi wa leo mchana stephano lamberk alipo nitembelea ofisini kwangu “ alionyesha video ilikuwa ikimuonyesha stephano lamberk akiwa ofisini kwa zakayo akiwa na janeth wakiwa wamekuja kuchukukua flash yao .
****
MASAA MATANO NYUMA
Damiani na janeth walikubaliana moja kwa moja kwenda ofisini kwa zakayo kwa ajili yakufatilia kile ambacho wamekipoteza , walichagua njia hio kwani waliamini kama wangeenda kwa namna ya kishari basi wasingeweza kumhimili zakayo hvyo wakashindwa kupata kile walichokuwa wakikihitaji na ndio maana waliamua moja kwamoja kwenda ofisini kwa zakayo .
Muda ambao walikuwa wakifika ndani ya jengo hilo ndio muda ambao na zakayo alikuwa akitokea ubalozi wa kenya kwenye miadi yake na bwana njoroge .
“ karibu sana janeth “
“ asante sana Agent zakayo“ aliongea janeth na kumfanya zakayo atabasamu na mpaka hatua hio aliamini janeth alikuwa akijua kila kitu kuhusu yeye .
“ karibu sana bwana stephano lamberk au damiani rabani “ aliongea zakayo na janeth alijikuta akimwangalia damiani na kisha walipeana ishara na wote kwa pamoja waliketi .
“Hakika wewe ni agent zakayo ,, sikutegemea kabisa , umefuzu kwenye swala zima la undercover “
“ hahahah.. asante kwa sifa hizo janeth , hizi ndio kazi zetu tunasomea kabisa ndio maana , lakini pia na mimi napenda nimsifie bwana damiani kwa kuendelea kujificha kwenye kivuli cha stephano lamberk “
“ unataka kumaanisha nini zakayo “
“ haina haja ya kunificha mpaka sasa hivi bwana damiani , nilikuwa nikikufatilia kwa muda mrefu sana kutoka maagizoya watu tofauti tofauti , naweza kusema kwamba wewe ni mtu mmoja unaetafutwa sana “
“mimi sio damiani ni stephano lamberk “
“sina haja ya kukufosi kuwa damiani au stephano lamberk , lakini naamini ujio wenu unamuhusu Zaidi damiani na kama ni hivyo sitotaka kuzungumza na wawakilishi nitaongea na damiani mwenyewe “ aliongea zakayo na hapo ni kama alikuwa akiwatega , kwani janeth na damiani waliangaliana na kisha walipeana ishara , na kwa sekunde chache tu damiani aliweza kiujifungua sura yake upande wa usoni na kubakia na sura yake halisi na jambo hilo lilimshangaza sana zakayo .
“ zakayo mpaka hapo ushajua stephano lamberk ni damiani na nakusifia juu ya hilo , lakini tunaomba jambo hilo libakie kuwa siri “
“ hilo swala mpaka sasa naweza kusema haliwezekani , lakini niseme kwamba nimestaajabishwa na teknolojia iliotumika kumbadilisha damiani , naweza kuijua teknolojia hio ?”
“ hilo linawezakana tu iwapo utakubaliana na sisi kwamba nitakachokueleza mahali hapa kuhusu hio teknolojia kitabaki kuwa siri “.
“hilo siwezi kuwahakikishia , na niseme ni swala gumu kwangu kulifanya , kwani kuna watu wanahitaji kujua uwepo wa damiani hapa nchini na endapo nita waambia kwamba damiani ni stephano lamberk hakuna hata mmoja ambaeye anaweza kuniamini .
“ kwa hio unataka nini bwana zakayo “ aliuliza damiani .
“nina mambo makuu mawili ambayo nahitaji , lakini kabla ya kuweka kile ambacho ninahitaji nadhani niwasikilize nyie kilichowaleta mahali hapa maana si jambo dogo kuweka wazi siri zenu zote “
Tumeweka siri zetu wazi kwani tunaamini kwamba tunaweza tukakulipa ukatutunzia siri , kwani kwa taarifa tulizo nazo juu yako ni kwamba kwako hakuna linaloshindikana juu ya pesa “
“ hahahahaha..janeth naona umenipa cheo kikubwa lakini naweza kusema kwamba umepatia , lakini hata hivyo ili kuwatunzia siri yenu haina budi kunilipa pesa nyingi sana “.
“hilo tutalizungumza , nataka vitu vyangu , flashi na simu yangu “ aliongea damiani na kumfanya zakayo amwangalie .
“ hilo ndio hitaji pekee ulilolijia mahali hapa ?”
“ ndio hilo tu hakuna lingine ,, unatupatia vitu vyetu sisi tunaondoka na tunakuacha na ukweli unaweza ukauuza mahali popote pale kujipatia pesa kama ilivokuwa desturi yako kama sio tabia “.
“ vitu nitawapatia “ na niseme mpaka sasa sina hitaji lingine kutoka kwenu kwani ujio wenu umekamilisha kazi yangu ya muda mrefu niliokuwa nikiifatilia “ aliongea zakayo na kisha aliwaonesha kamera upande wa juu .
“inaonekana ni kweli umefanikiwa , ila tulijipanga kwa ajili ya hilo hivyo ni sahihi kwa wewe sasa kutupatia kile tunachokihitaji “ aliongea janeth kwa sura ya mbuzi na zakayo hakutaka kuongea nao sana , alitoa flash na simu na kisha alimkabidhi damiani .
“ tutakutafuta zakayo , lakini mpaka sasa kuwa makini na watu unaowaambia kuhusu jambo hili , linaweza lisiwe jema kwetu na kwako pia , hivyo naamini utafanya maamuzi ya busara “.
“ hilo ni juu yangu janeth “ aliongea zakayo huku akitabasamu .
*******
Wazee walijikuta wakipagawa mara baada ya kuangalia vido nzima ya bwana stephanno lamberk kujivua sura , hakuna alieamini , ni neno moja tu miongoni mwao ndio lilikuwa ndani ya vichwa vyao ‘ogopa sana teknolojia na Mungu ‘.
“ nadhani mpaka hapo waheshimiwa mshajua kwamba damiani na stephano lamberk ni mtu mmoja “ aliuliza zakayo na hakuna aliepinga Zaidi ya kumsifia katika gunduzi yake hio , kwani wazee hao mpaka kwa wakati huo wote walikuwa kwenye mshangao , kuna ,muda waliona labda video aliwaonyesha zakayo ilikuwa ya kutengenezwa lakini ilikuwa na ukweli ,tena ule ukweli wenyewe wa mambo .
“ hio ni ripoti yangu ya kwanza kuhusu damiani , ripoti ya pili inayomuhusu mzalendo .. hii hapa ni ripoti yake “
“ Mpaka sasa nimegundua kwamba mtu aliekuwa anajiita mzalendo sio mtu mmoja “
“ inamaanisha nini kuhusu swala hilo bwana zakayo?”
“ kutokana na matukio mbali mbali yaliotokana na mtu aliejiita mzalendo kwa uchunguzi wangu nimebaini moja ya matukio hayo yalifanyika na watu wenye haiba tofauti tofauti , kwa maana hio nimekuja na suruhisho la kwamba mzalendo ni sawa na kikundi cha watu wanao fanya matukio kwa malengo maalumu huku malengo hayo mpaka sasa sijayajua bado “
“ basi mpaka hapo bwana zakayo inabidi swala hilo ulifanyie uchunguzi Zaidi ili tupate kujua, kama kweli hawa wanaojiita wazalendo ni kikundi cha watu tujue moja kwa moja ni watu wa aina gani “ aliongea bwana matinde “
Wakati kikao hiko kinaendelea upande wa Merina yeye mawazo alikuwa yamemjaa , hakujua kabisa ni swala gani lililokuwa linaendelea hapo kwani akili yake yote ilikuwa kwa damiani tu , hakujua mtu ambae alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote alikuwa naye muda wote hapa nchini pasipo kujua , lakini pia roho ilimuuma , aliona huenda damiani hakuwa akimpenda kama yeye alivyokuwa akimpenda swala hilo lilimfikirisha sana .
“ nadhani mpaka sasa naweza kupokea malipo yangu ya awali ya juu ya kazi inayohusiana na damiani “ aliongea zakayo .
“ miss merina ?” aliita kizito na kumshuta merina aliekuwa kwenye mawazo na kizito alielewa ni jambo gani lilokuwa likiendelea katika kichwa cha mwanadada huyo .
“tumehitimisha kikao na kwasasa malipo ya awali yanatakiwa kufanyika “ aliongea matinde na baada ya hapo merina alitoa simu yake na kutachi na baada ya muda mfupi .. alimpa simu ile zakayo aliingiza namba yake ya benki na hela iliruhusiwa kuingia kwenye akaunti yake , jambo lililomfanya kijana huyu atabasamu .
*****
Upande wa ikulu , ikiwa ni siku nyingine , aliingia kijana mmoja aliekuwa amevalia suruali yake ya kijivu pamoja na koti lakie huku akiwa na miwani ya jua , bwana huyu mwenye rangi nyupe alienyoa mtindo wa pank mara baada ya kukutana na katibu muhtasi ,,aliomba moja kwa moja kuonana na raisi , na baada ya dakika kadhaa kijana huyu aliruhusiwa .
“ karibu pancho “ alingea mheshimiwa raisi huku akimkaribisha kijana ambae sasa tunamtambua kwa jina la pancho .
“ leta taarifa pancho “aliongea raisi na kijana yule pasipo ya kuongea alingiza mkono wake kwenye koti na kutoa simu na kwenda upande wa ‘gallery ‘ na kuweka picha na kumpa raisi .
“mheshimiwa akama unavyo ona hizo picha nimezichukua jana , nimewafatilia kwa muda sasa na nimegundua wakuu hawa wastaafu wanafanya vikao kwa siri sana ,, huku kiongozi wao mkuu akiwa ni mstaafu matinde “.
“shit !, huyu mstaafu matinde ni moja ya watu ambao walikuwa wakinipinga vibaya sana tokea kipindi cha raisi bendera , unaweza kuniambia wanaongea nini , au uliweza kulijua hilo “
“ hapana mheshimiwa sijaweza kugundua lolote , lakini kama unavyo ona katika hio picha yupo agent Z”
“ ndio nimemuona zakayo huyu , unataka kusema nini ?”
“angalia mbele Zaidi ya hizo picha “ aliongea pancho
“hii ni ofisi ya kimbona si ndio “
“ ndio muheshimiwa , kwa uchunguzi niliofanya nimegundua zakayo moja ya watu aliokuwa anawasiliana nao ni huyu bwana kimbona “.
“pancho najua kwanini zakayo anawasiliana na kimbona , kazi ninayotaka hapa iwe kipaumbele uifanyie kazi nikujua watu hawa wastaafu vikao vyao vinahusu nini , nataka uniambie kila kitu na baada ya hapo nitajua cha kufanya na hawa watu , lazima kuna jambo wanalipanga kimya kimya na linaweza kuwa na hatari kwangu “
“ sawa muheshimiwa “ aliongea pancho .
“ kuna jingine ?”
“ ndio muheshimiwa “
“ lipi ?”
“ni juu ya madam “
“ kipi kingine kimetokea “
“ nimegundua anamahusiano ya karibu na professa janeth “
“ unamaanisha huyu professa anaejiita janeth bendera ?”.
“ ndio muheshiwa “
Raisi alijikuta akijifikiria kwa muda , hili swala la janeth lilikuwa pia likimtekenya akili yake kwa muda mrefu ila hakulifatilia na hapo aliona ni kwakati sahihi wa kumjua janeth .
“ noamba taarifa zote zinazomuhusu huyu mwanadada pancho , fanya swala hili kimya kimya “
“ sawa muheshimiwa “

Pancho ni moja ya wapelelezi binafsi wa raisi bendera , na moja ya kazi kubwa ya pancho ilikuwa ni kumfatilia mke wa rais yaani madam wema na wastaafu wote waliokuwa ndani ya uongozi wa bendera , haikujulikana ni kwanini raisi bendera , alikuwa ameweka watu kuwafatilia wastaafu hawa , lakini ilionekana kabisa kuna jamnbo alikuwa anaogopa lilikitokea .
ITAENDELEA
SEHEMU YA 71
THE OLD FRIEND(RAFIKI WA KITAMBO)
Wakati pancho anatoka ndani ya ofisi ya raisi ndio sabi na yeye alikuwa akiingia mahali hapo , jambo ambalo lilimpa mashaka Zaidi ni baada ya sabi kukutanisha macho na bwana pancho , kuna hsisa mbaya zilimcheza , ila hakutaka kulipa kipaumbele swala hilo .
“ mheshimiwa nimetika wito wako “ aliongea sabi mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ya raisi .
“ nataka kuonana na watu wafautao kwa muda tofauti tofauti “
“ hakuna shaka muheshiwa naweza kuwapelekea taarifa mara nitakapo jua taarifa zao “
“ mtu wa kwanza ninaetaka kuoanana nae ni mkurugezi wa kampuni ya Z stylish wear , wapili nataka kuonana na merina sosteness wa kampuni ya STL wa tatu ni stephano lamberk wa kampuni ya NLT aliongea mheshimiwa na kumfanya sabi kushituka lakini alijaribu kujiweka sawa ili asishutikiwe .
“ hakuna shaka muheshimiwa nitaandaa miadi na hawa watu kwa siku ya kesho “
“ hakuna shaka , unaweza kwenda sasa ni hayo tu “ aliongea raisi na sabi alitoka .
“ stephano lamberk “ alijjisemea sabi na hapo hapo jambo aliloambiwa na suzzane usiku wa jana yake lilimfikirisha .
*****
Ni baada ya sabi kurudi nyumbani kwake .muda wa saa nne kama dakika arobaini na tano hivi ndipo alipo pokea simu ya suzzane , kwanza alishangaa mrembo huyo kumpigia simu muda huo , ni kweli kijana sabi alikuwa akimfukuzia suzzane ili kupata penzi lake , lakini kutokana na ubize aliokuwa nao suzzane hakuweza kufanikiwa , umri wa sabi na suzzane ulikuwa na utofauti mkubwa sana , kwani suzzane alikuwa mkubwa kwa sabi , lakini jambo hilo halikumzuia sabi kumpenda suzzane , mwanzoni kijana sabi alimpendea mwanadada huyo kimapenzi tu , lakini pia kumtumia katika kazi zake , lakini kadiri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo alivyozidi kuvutiwa na mwanadada huyo , japo aliijua historia nzima ya damiani na sabi hata pamoja ya agent danny , lakini moyo wake hakuacha kumpenda mwanamke huyo .
Hivyo kupokea kwake simu ya mwanadada huyo ndani ya muda huo lilimshangaza kwani ni mara ya kwanza kwake kupigiwa na suzzane ndani ya muda huo .
“nipo na hali mbaya sabi , nifate kisemvule “ aliongea suzzane na hapo hapo simu ilikata
Sabi hakuchelewa , aliwasha gari yake kuelekea maeneo ya kisemvule huku akijaribu kuitrak simu ya suzzane na katika hilo alifanikiwa kwani ndani ya kama nusu saa alikuwa mbele ya gari la suzzane , alishuka haraka haraka na kwenda kufungua mlango na hapo ndipo alipopigwa na butwaa , kwani suzzane alikuwa ametapakaa damu kwenye paja na alilofunga na kitambaa huku akiwa hana fahamu , sabi hakujiuliza mara mbili mbili alimchukua na kumuingiza kwenye gari na kisha akalitoa , spidi huku wazo la kwanza n kuelelekea hospitalini .
Lakini ile anakaribia kongowe ndipo suzzane alishituka .
“ nipeleke moja kwa moja kwako sabi “ aliongea suzzane na kusmshangaza sabi
“ nakupeleka hospital “
“ hapana nipeleke kwako “.
Sabi hakuwa na ujanja , kwani aliendesha gari moja kwa moja na kwenda mpaka kwenye nyumba yake iliokuwa ikipatikana maeneo ya kawe.
Zikiwa zimepita siku mbili za suzzane kuendelea na matibabu ndan iya nyumba ya sabi , ndipo suzzane alipomuambia kuhusu damiani .
“ hivi abasi unaweza kuamini kwamba stephano lamberk , ile sio sura yake halali ni mtu mwingine “ aliongea suzzane huku hata yeye akiwa kama mtu ambae haamini maneno yake , kwani aliona yataonekana kichekesho mbele ya sabi .
“ inawezekana vipi suzzane “
“ mtu alinipa hili jeraha anaitwa damiani “
“ damiani ?”
“ ndio damian , na kuna hisia zinaniambia kabisa damiani ni stephano lamberk “
“ huyu damiani ni nani na anawezaje kuwa mtu mwingine kwa wakati mmoja “
“ hilo sijui “ aliongea suzzane siku hio wakiwa wameketi kwenye sofa , wakiwa wamelaliana na walionekana walitoka kufanya mapenzi muda mfupi uliopita .
***
Sabi alijikuta akiyakumbuka maneno hayo ya suzzane .
“ kuna haja ya kuonana na stephano lamberk kabla hajaonana na raisi , nimjue mtu huyu kwa undani “.
Aliongea sabi na kisha akatoka eneo hlo na kwenda kuendelea na kazi zake , lakini ile anaingia kwenye ofisi yake , kuna jambo lingine lilimvutia macho .
“ rich sam “ aliongea kwa sauti ya chini na hio ni mara baada ya kumuona tajili samwli akiwa amongozana na katibu muhtasi .
“ karibu sana bwana sam “ aliongea raisi henry mara baada ya kuingia ofisini kwa raisi .
“ nashukuru sana muheshimiwa , na pole na majukumu “
“ asante sana sam , ndio kazi yangu hio , lazima nitumikie wananchi kwa weledi mkubwa “
“ ni kweli kabisa “
“ nadhani unajambo la muhimu lililokuleta mahali hapa “
“ ndio muheshimiwa nina jambo la muhimu nililokuja kukuuliza , kwani nilitaka nikuulize kwa simu lakini nimeona itakuwa vyema sana kama nitaongea na wewe ana kwa ana .”
“ ni jambo gani hilo sam “
“ ni juu ya damiani “
“ damiani ?”
“ ndio muheshimiwa , tulikuwa na operesheni ya kumkamata kijana huyu , mara baada ya kujua kaingia nchini , lakini operesheni hio iliiingia doa mara baada ya mtu kuingilia kazi ya vjana wetu , na kutokana na maelezo ya vijana wanasema mtu huyo aliengilia anaweza akawa ni suzzane “
“ suzzane ?”
“ ndio ,uheshimiwa , na ndio ,maana nipo mahali hapa kuuliza kama ulifanikiwa kumpata damini , nadhani unaelekwa kwamba swala la damiani limekuwa kubwa ndani ya umoja wetu “.
“ naweza kusema ndio alikuwa ni suzzane , lakini katika hio operesheni nadhani kulikosekena mawasiliano , kati yangu na nyie , kwani suzzane hakujua kwamba walikuwa ni vijana wako , na kuhusu damiani hatukufanikiwa kumpata , kwani kuna Zaidi ya watu waliofika na kumuokoa ndani ya tukio “ aliongea muheshimiwa na kumfanya sam ashangae .
“ unamaanisha na suzzane hakumpata damiani ?“
“ ndio bwana sam sina haja ya kudanganya juu ya hilo , na mpaka hatua ya sasa bad tunawafatilia vijana waliousika kumuokoa damani katika mikono ya suzzane “
Sam lilolomleta mahali hapo ikulu ni kutaka kujua kama raisi alikuwa amkamata damiani au lah , na ndio maana baada ya kumuliza mheshimiwa juu ya swala la damiani aliaga na kuondoka , huku akiwa na uhakika kwamba kuna uhakika au ukweli kwenye maneno ya mheshimiwa , na hilo lilimpa tumaini la kumkamata damiani akiwa wakwanza .
Na swala hilo hakutaka kulichelewesha , kwani mara baada ya kuingia kwenye gari lake tu alimpigia kimbona simu .
“ vipi “
“ henry hajamkamata damiani bado , nasikia suzzane alipokea kichapo na damiani akasepa “
“hio ni taarifa nzuri kwetu sabi , nadhani mpango upo pale pale “
“ ndio , wapange vijana waingie kazini , inabidi tumkamate sisi wa kwanza “ aliongea sam
“ hakuna shaka sam “
“ hakikisha unawaonya vijana juu ya kutofanya uzembe “ aliongea sam na kisha alikata simu na kuegeamia siti ya gari na kufumba machozi huku akionesha kupata Amani ya moyo wake .
*****
Stephano lamberk , au damiani , hakwenda kazini siku iliofata , alikuwa na mambo mengi kichwani mwake aliokuwa akiyafkiria , moja ya jambo kubwa kwake lililokuwa likimuumiza kichwa ni juu ya kulipiza kisasi juu yale waliohusika na kifo cha mama yake .
Mpaka wakati huo aliamiani wabaya wake washamjua tayri yupo nchini , na alikuwa makini sana , kwani kitendo cha kujidhirisha sura yake mbele ya zakayo aliamini kwamba jasusi yule hawezi kuacha kutowaeleza wanaompa pesa , kwani alijua ni kwa namna gani zakayo alikuwa akipenda pesa , hivyo aliona namna moja iliobaki kwa muda huo ni kuanza kudili na maadui zake moja kwa moja pasipo kuogopa .
Lakini kabla yajambo hilo kuanza , yapo mambo ,mengi katika kichwa chake yaliokuwa yakizunguka na swala kubwa lilokuwa likimzunguka katika kichwa chake ni swala la ‘MZALENDO ‘ kundi hilo la mzalendo lililokuwa limeanzishwa na mheshimiwa bendera pia lenyewe lilikuwa likimfikirisha mno , bado alikuwa hajafanya maamuzi ya moja kwa moja kujiunga na kundi hilo ama asijiunge ,japo nafasi kubwa ya yeye ya kujiunga ilikuwa kubwa , lakini bado kuna nafsi ilikuwa ikimwambia kwamba asijiunge .
Swala la pili lililokuwa likimzungusha kichwa chake ni swala la mtu ambae alikuwa akimpa maelekezo tokea akiwa hatarini miaka kadhaa nyuma mpaka kwenda Thailland , kwenda China na hatimae kurudi nchini , alikuwa akipokea maelekezo kwa mtu ambae hakuwahi kujitambulisha kwake , swala hilo pia aliona ni muhimu sana ya kulifanyia kazi .
Wakati akiwa ndani ya nyumba yake akiwaza hili Na lile ndipo alipokuja kushituliwa na kengele ya getini , alinyanyuka na kuangalia ni nani aliekuwa akigonga na hapo ndipo alipokuja kupigwa na mshangao , kwani mtu aliekuwa mbele ya geti kwakutumia kamera alikuwa ni sabi mboneche , rafiki yake wa Thaiilland .
“ Sabi “ alitamka maneno hayo huku akiwa ni mwenye kujishauri afungue ama asifungue .
*****
Merina tokea ajue kuwa damiani ndio stephano lamberk , kwake swala hilo lilimpa wakat mgumu sana , alikuwa ni mwingi wa mawazo tokea usiku aliujua ukweli huo , aliwaza mambo kadha wa kadha, jambo kubwa alilolokuwa akiliwaza katika kichwa chake ni mapenzi aliokuwa nayo juu ya damiani , lakini mapenzi hayo kwake yalimtia shaka kwani hakujua kama damiani alikuwa akimpenda yeye kama anavyo mpenda , jambo hilo lilimtia mashaka mno .
Mrembo huyu mwenye pesa zake mjini hakustahili kabisa kuwazia penzi , kwani kila kitu alikuwa amejaaliwa na sidhani kama kuna mwanaume ambae ni rijali angemkataa mwanamke huyu pindi atakapojilengesha kwake .
Kwani ni mwanamke aliekuwa akifatiliwa na wanaume wengi mno ikiwemo vigogo wa serikalini lakini wote walipigwa za mbavu na kujikatia tamaa , merina alikuwa ni moja ya wanawake waliokuwa na msimamo mno , na alikuwa anajua kile alichokuwa akikihitaji kwenye maisha yake .
Ikiwa ni siku nyingine siku iliopambazuka , siku ambayo damiani anakutaka na sabi ndio merina na yeye alikuwa akitoka nyumbani kwake kuelekea kwenye kampuni ya damiani NLT .
Siku hio kwakuwa ilikuwa ni siku ya kazi , na yeye hakwenda kazini na vle vile damiani basi mara baada ya kufika ndani ya jengo hilo la kampuni ya NLT alikaribishwa kwenda kuonana na mwanadada janeth .
“ karibu “ ilikuwa ni sauti kavu ya janeth akimkaribisha merina .
“ where is damiani ?”
“ lilikuwa ni swali la kwanza kutka kwa Merina kwenda kwa janeth , swala ambalo lilinfanya janeth ashangae , kwani usiriasi aliokuwa nao mwanadada huyu , ulimfanya ajiulize uhusiano uliopo kati ya Damiani na Merina , lakini pia ajiulize imekuwaje mwanadada huyu akajua Stephano lamberk ni damiani .
“unamaanisha nini , who is damiani ?”
“stephano lamberk , where is he , najua kila kitu ni damiani so stop pretending I need to meet him please “ aliongea merina huku akipunguza hasira zake na hapo janeth alijikuta akivuta pumzi , kwani mpaka hatua hio alijua kwa vyovyote vile zakayo ashamwaga siri zote za stephano lamberk .
“ kaa kwanza mpenzi “ aliongea janeth kwa sauti ya upole na merina alikaa chini .
“una mahusiano gani na damiani ?”
“ ni mpenzi wangu “ alijibu merina na kumfanya janeth atoe macho .
ITAENDELEA WIKIEND

Nicheki watsapp : 0687151346
Pia unaweza changia 3000 kumsapoti mwandishi then nitakutumia yote mpaka mwisho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom