Ujasusi - Umoja namba 97

SEHEMU YA 78
LIVE OR DIE MISSION (MISHENI YA KUFA NA KUPONA )
Kijana Damiani anaendelea kuwa na wasiwasi juu ya mtu ambae anamsaidia katika misheni zake , Nara roboti ambalo limetengenezwa linaendelea kumpa maelekezo ambayo yanakuwa ni fikirishi katika kichwa cha Damiani , lakini licha ya yote hayo Damiani dhamira yake ya kulipiza kisasi kwa wale waliohusika na kifo cha mama yake inaendelea kubaki vile vile .
Suzzane alikuwa ndani ya nyumba yake akiwa ni mtu ambae anawaza hili na lile hususanni katika misheni zake zote alizofanya , alikuwa akiangalia picha ya kila mtu ambae alikuwa akmfatilia kwa muda mrefu , Damiani, japo ameshapewa maagizo ya kuacha kumfatilia kijana huyu mdogo , lakini bado alikuwa na shauku ya kutaka kujua ni nani yupo nyuma ya damiani , kwani aliamini nguvu ilioko nyuma yake ilikuwa ni kubwa mno , licha ya kwamba aliona kuna uhusiano uliokuwepo kati yake na madam Wema mke wa raisi , lakini bado kuna kitu kwake aliona hakipo Sawa kabisa , kuanzia siku anaanza kumfukuza Damiani miaka ya nyuma mpaka sasa aliona kuna jambo kubwa liko nyuma ya kijana damiani , aliendelea kuwaza hili na lile katika kazi yake hio ya kipelelezi .
Aligeukia upande wa mtu anaejiita mzalendo , moja ya jambo kubwa analojua ndani ya huu umoja ni kwamba Damiani alikuwa hahusiki kabisa , alikuwa akilijua hilo vyema kwani alishafatilia sana juu ya jambo hili kwanzia siku ambayo damiani anaingia nchini mpaka siku hio pamoja na mengine mengi
Swala lingine alilokuwa analiwazia kwa muda huo ni juu ya janeth , alikuwa akijua fika kuhusu janeth kwani alikuwa na taarifa zote kamili juu ya Janeth , lakini pia aliamini kwa namna moja ama nyingine Janeth anaweza akawa ni mmoja ya watu wanao jiita wazalendo , na kama hilo sio, basi moja kwa moja kuna muunganiko mkubwa wa mwanadada huyo na mzalendo , alifikiria tukio la mwanadada huyo Kuchoma madawa ya Kimbona , siku aliopambana nae na siku alio tekwa na Carlos mpaka ,Damiani kuja na kumuokoa swala na kumuua Carlos, kwake swala hilo aliliona lina umuhimu wake pia , alijua kwa yote hayo yaliotokea kuna muunganiko ulioko kati ya Mzalendo na Damiani , alikuwa na uhakika juu ya hilo , hakika jasusi huyu alikuwa kwenye wakati wa tafakuri nzito na yote hayo yalijiri kwenye kichwa chake mara baada ya kuambiwa na mheshimiwa kuwa aache kumfatilia Damiani .
Wakati akiwa kwenye tafakuri hio ndipo alipokuja kushitushwa na mwito wa simu yake , alichukua simu y ake na kisha aliiweka sikioni , na aliekuwa akipiga alikuwa ni Patrick .
“ Yess Suzzane najua kwa sasa unaweza ukawa kwenye wakati mgumu , kwani kazi uliokuwa unaifanya kwa muda mrefu hatimae leo umeambiwa uichee “
“ Nenda kwenye point ya msingi ulionipigia Patrick “
“ Nimeingia dili la ndoa na Merina kwa shart la kumlinda Damiani asipatwe na madhara ya aina yoyote ile “
“ hahahaha .. nadhani unakichaa Patrick , umekosa wanawake “
“sijakosa wanawake Suzzane , binadamu hatufanani katika maswala ya kimaamuzi , mimi nampenda Merina na nitafanya lolote kwa ajili yake ilimradi niwe nae , akini licha ya yote hayo nina mipango yangu kichwani , na mipango yangu hio siku ikiwa ni wakati wa kuianzisha naomba uwe mtu wa kunisaidia katika hilo “
“ Naomba unitoe katika mipango yako mimi Patrick “
“ Think about it Suzzane “ aliongea kisha akakata simu na kumfanya Suzzane asonye lakini wakati huo akiwa ni kama mtu ambae amepata kujua kwanini mheshimiwa amemtaka kuacha kumfatilia Damiani , lakini licha ya hayo , hakutaka kuamini kabisa kwamba Henry mtu anaemjua tokea akiwa makamu wa raisi anaweza akafanya maamuzi ya aina hio kisa kulinda penzi la mwanae , kwake hilo lilikuwa ni kama kichekesho .
*******
Ilikuwa ni siku ya jumatano asubuhi , siku ambayo kwa kijana Damiani hakuwa na mpango wa kwenda kazini na vile vile kwa mwanadada Janeth ambae alikuwa akipenda kulala nyumbani hapo kwa damiani japo vyumba tofauti na yeye alikuwa yupo hapo nyumbani na muda huo ilikuwa ni asubuhi angavu muda wa saa tatu za asubuhi .
Wakati damiani akiwa anaendelea kuangalia CNN habari za kiabiashara ndipo Janeth alitoka na kumuendea Damiani sehemu ambayo amekaa , kwenye sofa akitokea ndani .
“Damiani angalia “
Damiani alichukua simu ya mwanadada huyo aina ya Samsung fold na kisha aliangalia , na alijikuta macho yake yakimtoka .
Ilikuwa ni taarifa ya inayo muhusu mrembo Merina na Patrick wakitarajia kufunga ndoa huku kichwa cha habari kikisomeka .
“HATIMAE KILE KILICHOKUWA KIKISUBIRIWA NA WATU WENGI SASA KIPO WAZI , MREMBO TAJIRI MERINA KUONA NA KIJANA MTANASHATI TAJIRI PATRICK HENRY MUSHI , HUKU NDOA YAO IKITARAJIWA KUFUNGWA SIKU MOJA NA NDOA YA JANE NA MTOTO WA TAJIRI KUTOKA DUBAI “
Taarifa hio ilisomeka hivyo kwenye huku ikiambatana na video iliokuwa ikimuonesha kijana Paatrick akilitolea swala hilo ufafanuzi .
Upande wa Janeth alijikuta jambo hilo likimpa furaha ya aina yake , kwani aliamini kwa kuolewa kwa Merina basi atakuwa na nafasi pekee ya kupendwa na kijana Damiani , japo umri wake na wa Damiani ulikuwa tofauti lakini alitamani sana jambo hilo litokee .
Damiani alikuwa kwenye mshituko mkubwa japo alijikaza mbele ya janeth lakini swala hlo kidogo halikuwa jema kwake , alikuwa akimpenda mwanadada huyo , lakini jambo la kutangaza ndoa na kijana Patrick kwake liliuma .
“Hata hivyo wanapendezana” aliongea Janeth na kumfanya Damiani atingishe kichwa kuashiria kuwa na yeye akubaliane na maneno yake , lakini haikuwa hivyo kwani ndani ya moyo wake alikuwa akiungua .
“Naomba tusiongelee mambo hayo kwa sasa “
“ Okey love “ aliongea Janeth huku akijibebisha kwenye bega la kijana Damiani
Kwa damiani hata kile alichokuwa akikiangalia kwa muda huo hakikuwa na maana kabisa ,, alitoka hapo na kwenda chumbani kwake huku akijikuta kupata safari ya ghafra jambo ambalo kwa janeth aligundua kuwa mwanaume huyo hakuwa sawa na hakutaka kumbughuzi .
“ shi*t inamaana kalikuwa kanajifanya kunipenda “ alijikuta akiongea huku akipiga kioo cha chumbani kwake kofi akiwa ametuna kwa hasira na wivu .
Wakati akijiangalia kwa hasira kwenye kioo , simu yake ndio ilimshitua , aliichukua na kuangalia namba ilikuwa ni ngeni ila hakujiuliza mara mbili mbili kwani alipokea na kuweka sikioni .
“ Tukutane nyumbani kwa Bruno “ ilikuwa ni sauti ya kike ilioamrisha hivyo na kukatwa , na hapo ndipo damiani alipokumbuka kuwa siku hio alikuwa akihitajika kuonana na mtu ambae atakuwa anamsaidia katika misheni yake inayotarajiwa kufanyika .
Damiani alijiandaa vizuri na kisha alitoka na kuelekea sehemu ambayo alikuwa na miadi na mtu ambae alikuwa akihitaji kuonana nae kwa siku hio , kutoka hapo alipo kuwa akiishi na nyumbani kwa Bruno palikuwa ni umbali mfupi sana kwani ndani ya dakika kumi tu alikuwa mbele kabisa ya jengo hilo la kifahari , na nje ya jengo hilo kulikuwa na gari ya Vanguard nyeusi iikiwa imesimamishwa na baada ya Damiani kukaribia hapo gari ile illitoa mwanga kwenye taa za mbele ( headlights) na hapo damiani alitambua kuwa mtu aliekuwa anatakiwa kuonana nae muda huo ni huyo aliekuwa kwenye gari , basi wote kwa pamoja walifunguliwa geti na kisha waliingia ndani .
Alikuwa ni mwanadada mrembo haswa , aliejazia na kwa mwanaume yoyote ambae angemuona angemtamani hususani kufanya nae mapenzi , alikuwa na rangi flani hivi ya Kinyarwanda
“ Naitwa Seline Amber au unaweza kuniita Akaliza ni mwenyeji wa Rwanda”
“Seline Amber !”
“ yes , I see your complexion say everything “( naona muonekano wako unasema kila kitu )
“ yes I know your name “( ndio najua jina lako )
“should we sit first ??“ Aliongea mwanadada huyu huku akitabasamu na kufanya vishimo vya mashavu yake vionekane .
“Tafadhari naomba ujitambulishe vizuri , Bruno kila siku ni mtu wa kunishangaza sana “
“Mimi ni mpelelezi wa kujitegemea , lakini pia nilikuwa nikifanya kazi chini ya Bruno na naendelea kufanya kazi chini yake “
“ unamaanisha nini kuendelea kufanya kazi”
“Nafikiri wote tunafanya kazi Chini ya Bruno mister Stephano naweza kukuita hivyo au damiani “ aliongea mwanadada huyo kwani kwa wakati huo Damiani alikuwa kwenye sura ya Stephano yaani mzungu feki .
“ vyovyote vile , lakini mimi simfanyii kazi Bruno , ila Nafuata nyayo za Bruno kukamilisha kisasi changu “
“There is no need to say all that mister D”( hakuna haja ya kuongea yote hayo )
“Sawa , lakini kabla ya kuendelea nataka kujua Mahusiano yako na Bruno , umeanza kumfanyia kazi lini na Mengineyo , kumbuka mimi ndio Mrithi wako kwa hio ni kama Boss wako “
“ hahahahah.. you are so funy Mister Damiani , Anyway I do respect you but kama nilivyosema mimi ni mpelelezi wa kujitegemea na pia wewe sio boss wangu bali nipo katika kutimiza majukumu yangu katika kuhakikisha unakamilisha misheni zako zote kwa kukupa mbinu na maelekezo sahihi , isitoshe mimi nina mtu ananilipa kwa ajili ya kazi hii “
Damiani alijikuta akizidi kumshangaa mwanadada huyu , japo ya uzuri wake lakini alikuwa akijiaminii mno , jambo hili kidogo lilimfanya Damiani kuwa na hali ya kutojiamini .
“Sawa ila nataka kujua , ili kama nafanya kazi nawewe niweze kukuamini “
“Nimeanza kufanya kazi na Bruno kwa Miaka ishirini sasa “
“ Miaka ishirini !”
“ Unashangaa , au muonekano wangu unakufanya kushangaa ?”
“ Ndio unaonekana kuwa mdogo kimuonekano , kwa hio kama ulifanya kazi na Bruno kwa sasa una miaka mingapi ?”
“Nina miaka 35 sasa , so kimahesanu nimeanza kufanya kazi nikiwa na miaka kumi na tano , sitaki swali lingine bwana Damiani “.
“Okey , Shikamoo “
“Haha .. come on .. naomba niende moja kwa moja kwenye misheni “
“ okey “
“Tajiri Mahmood ataingia Tanzania tarehe kumi siku tatu kwanzia leo , na hio ndio siku yako ya kukamilisha mauji ,Utamuua kwa njia ya kisu “
“Kisu ! , kwanini iwe kisu “
“ Ndjo mpango ulivyopangwa , lazima auwawe kwa kisu tena kichomwe moyoni , lakini kisu hiko sio kisu cha kawaida , ni kisu ambacho utapewa siku hio ya mauaji , naomba nikukumbushe tu kwamba mtu unaeenda kumuua ni mtu ambae atakupeleka moja kwa moja kwa mtu ambae amehusika na kifo cha mama yako , kwa hio misheni hii ikifeli utapoteza maisha , lakini pia hutoweza kulipiza kisasi kwa wale waliomuua mama yako .”
“ Huyu ni tajiri mkubwa na atakuwa na ulinzi mkali , nitawezaje hilo “.
“unaweza ukawa hujafanya mauaji kwenye maisha yako , lakini kumbuka jambo moja tu kwamba kwa sasa huwezi kusema neno siwezi , kuna jambo moja tu kufanya ili ufanikiwe na ulipize kisasi cha mama yako ,ufeli misheni ufe ndani ya mikono ya adui waliohusika na kifo cha mama yako , au usifanye kabisa ,ushindwe kulipiza kisasi cha mama yako , lakini pia upoteze maisha , kwani watu waliohusika na kifo cha mama yako ni watu wanaokutafuta na muda si mrefu watakufikia hvyo uamuzi ni wa kwako “.
“ wapo watu tisini wa kuwaua , hivyo kabla ya kuingia kwenye misheni yoyote lazima nijue uwezekano wa kufanikiwa ni asilimia ngapi “
“ hii ndio misheni yako ya kwanza , lakini itakuwa kama jaribio kwako la kwanza ukifanikiwa kwenye hii misheni zote utafanikiwa , asilimia ya kufaulu katika misheni hii ni hamsini “
“ hamsini !“
“ Ndio kwa maana hio unaweza kufa siku hio au kutoka ukiwa mzima “.
“ kuhusu maelekezo mengine nitakupa siku ya misheni , kwa hio kwanzia sasa Nara atakusadia kukupa maelekezo mengine ya kiufanisi “
“ Unamjua Nara ?”
“Niliambiwa kuna Msadizi wako anaitwa Nara, This is Live Or Die mission hakikisha unajipanga”
Damiani alijikuta akivuta , pumzi kwa nguvu , hofu ilianza kumjaa , aliamini misheni hio ni ngumu sana kwake kufanya na kutoka akiwa hai , hususani kwa tajiri mkubwa kama huyo ambae ni hakika kwamba atakuwa na ulinzi mkali sana .
“Kwaheri mister Damiani , tutawasiliana siku ya tukio “ aliongea mwanadada huyu na kisha kwa mapozi kabisa akaondoka huku akimwacha damiani kwenye mawazo , hata lile swala la Merina lilokuwa likimsumbua kichwa chake lilikuwa lishapotea kwenye nafasi yake ya ubongo ,
ITAENDELEA
SEHEMU YA 79
Ni siku moja mbele siku mbele kala ya siku ambayo tajiri Mahmood kuingia nchini kwa ajili ya mazungumzo ya ndoa ya mtoto wake , siku hii ilikuwa ni siku ya jumapili, na kama ujuavyo siku hii waumini wengi wa dini ya kikristo wanakuwa wanasali siku hii .
Siku hii mojaya waumini waliohudhuria ibada , alikuwa ni mstaafu Matinde , alikuwa ndani ya kanisa la askofu Jembe , kanisa lililokuwa likijulikana kwa jina la UZAO UPYA ni kanisa ambalo lilikuwa limesheheni watu wengi sana ambao walikuwa ni wafuasi wa Askofu Jembe , huku moja ya watu hao wengi ni wanawake .
Mstaafu Matinde alikuwa amekaa siti yake ya mbele kabisa , akiwa amevalia suti yake sagi ya rangi ya kijivujivu , alikuwa hana wasiwasi kabisa akiwa ni moja ya waumini ambao walikuwa wakisikiliza mahubiri ya askofu Jembe .
Baada ya masaa mawili hatimae ibada hio iliisha , na mtu wa kwanza kunyanyuka kwenye kiti hicho kusogea mbele kwa ajili ya kumpa mkono askofu alikuwa ni mstaafu Matinde .
“Mheshimiwa , kumbe na wewe umefika kwenye ibada , karibu sana “.
“ Asante sana , nimekuja na mimi ninayo shida ya kuonana na wewe baba askofu “
“hakuna shaka tunaweza kuongozana kuelekea ofisini “
Baada ya askofu kuongea hivyo aliagana na baadhi ya waumini ambao alikuwa akitaka kuonana nao siku hio kwa ajili ya maombezi , na kuwaambia kuwa maombezi yatafanyika siku inayofatia yaani jumatatu .
“Karibu sana mstaafu “
“ Nashukuru sana “
“Enhe nadhani kuna jambo kubwa lililokuleta , maana kwa ninavyojua wewe sio moja ya waumini wangu “
“Ni kweli , nina jambo ambalo ninataka kuzungumza , lakini nimeona siku ya leo ni nzuri Zaidi kwa ajili kuongea kwani haina macho mengi “
“Nadhani itakuwa vyema tukianza “
“Nitaenda moja kwa moja kwenye point : “ nataka uwe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania “.
“Unatania muheshimiwa , nitakuwaje raisi wakati raisi tunae “.
“Raisi tunae ndio , lakini anaweza kutoka ikulu pale muda wowote “
“Unamaanisha kuna mpango kwa kumtoa Henry ikulu “.
“ Ndio mpango upo na mtu ambae anafaa ndani ya chama kumrithi ni wewe “.
“Kwanini niwe mimi “
“ Sina haja ya kuzungumza mengi bwana Jembe , nataka uniambie kama upo taayari kuwa raisi au hapana ?”
“Sina haja ya kukataa , lakini naataka kwanza kujua kama jambo hili ni la uhakika na sio utani ?”
“ Jambo hili ni uhakika ,hakuna haja ya sisi kukudanganya “
“Kama ni kweli kipi natakiwa kufanya “.
“Tunataka uanze kuhubiria washarika wako juu ya UMOJA NAMBA TISINI NA SABA “
“UMOJA NAMBA TISINI NA SABA ?”
“Ndio “
“ kivipi “
“Unaweza ukatafuta namna ya kuelezea huu Umoja kwa mfano unaweza kutumia neno Freemason , huku ukijikita Zaidi katika kuwasema viongozi kwamba wamejiunga ndani ya umoja huu , na pia serikali inaongozwa na umoja huu “
“Hapo nimekuelewa ,lakini vipi kuhusu ulinzi wangu “
“Ulinzi tutakupatia , lakini pia hakuna mtu atakae kugusa kwani wewe ni mtumishi wa Mungu “
“Hapo sawa ,lakini nataka kujua mpango huo “
“Tumetoka mbali sana katika mpango huu ni miaka sasa , hatuwezi kukutambulisha moja kwa moja katika mpango huu , ila tunahitaji ,matookeo kwanza “
“kwa hio nikishafanya kazi hio nakuonekana na manufaa ndio mtanitambulisha rasmi “
“Ndio “
******
Ilikuwa imebaki siku moja kabla ya siku ambayo Damiani alikuwa anaenda kukamilisha misheni yake , siku hio alikuwa na mwanadada Janeth muda wa jioni , wakiwa wameketi .
“ Janeth kuna siri nyingine ndani ya FULL BODY MASK “
“Kwanini unauliza hivyo ?”
“Nataka kujua “.
“ Ndio zipo nyingi tu , lakini siwezi kukuambia zote”
“ Naomba uniambie “
“Nitakuambia moja “
“sawa “
“Inauwezo wa kubadilika sura mara mia moja “
“Ni kweli hilo linawezekana ?”
“Ndio , twende ukaone “
Waliongozana na kuingia ndani ya chumba ambacho Damiani ndio anaihifadhi ile Mask , aliivaa , na baada ya hapo alielekezwa na Janeth afikirie sura ya mtu yoyote yule mwenye asili ya kizungu, huku akiwa amejiangalia kwenye kioo .
Na maajabu yake ndani ya sekunde hio hio sura ilibadilika na kwenda sura ya Trump , jambo ambalo lilimfanya Janeth acheke”
“Mbona unacheka ?”
“ Kwa hio kwenye wazungu wote umemfikiria Trump?”
“Ndio ninaemkubali“
Damiani alijikuta akiwa kwenye mshangao , kwani kila alipo kuwa akifiria sura ya mtu ilikuwa ikibadilika .
“Kuna nyingine “
“Ndio zipo nyingi ila hii ni ya mwisho “
“Nielezee “
“Nina sharti “
“Wewe sema bwana “
“Nakupenda Damiani “
“Hahaha .. kwa hio sharti lako ni kunipenda ?”
“Ndio na ukinikataa hapa sikuambii “.
“Basi na mimi nakupenda “.Damiani alijua yote ni utani ndio maana alikuwa mwepesi kujibu
“Kweli !”
“Niambie sasa “
“ Unamfahamu Muhamad Ali ?”
“Ndio namfahamu “
“Hii FBM inaweza ikakupa uwezo wa kupigana kama Muhammad Ali lakini ili hilo kuwezekana lazima uwe unajua aina ya Mapigo ya Muhammad ali anayopiga , ukishayajua , ukifikiria hilo pigo FBM itakupa uwezo kupitia ubongo wako na utajikuta unaweza mapigo hayo “
“Kweli ?”
“Unajua mapigano ya Muhammad ali ya aina yoyote “
“Ndio na nayafahamu vyema , nilipokuwa Thailland nilijifunza sana maana nilikuwa nampenda sana “
“Basi twende tukajaribu kupigana nje hapo “
Damiani na Janeth walitoka mpaka nje upande wa kushoto sehemu iliokuwa na Swimming pool , ila hapa kulikuwa na uwanja wa basket ball .
Janeth na yeye alijiweka sawa kuanza mapigano .
“Usinionee huruma Damiani , nione kama mtu ambae nimehusika na kifo cha wazazi wako hivyo ndio namna pekee ya FBM kufanya kazi kwenye mwili wako “
Wakati hayo yanaendelea na Abasi aliingia hapo ndani na aliwaona wawili hawa wakiwa upande wa nyuma , na pasipo kuwashitua alianza kuwaangalia .
Damiani hakutaka kuanza na mapigo ya Muhammad Ali , alitaka kuanza na mapigo ya Kithai thai .
Janeth na yeye hakuwa mzembe , alikuwa vizuri kwenye mafunzo ya Kung fu vibaya muno , alimfata damiani kwa kumtaka kumpiga teke la shingo , lakini damiani alihepa kushoto , lakini ile anajiweka sawa Janeth alileta mapigo ya ngumi mfululizo ambazo damiani kadri muda unavyokwenda alikuwa akishindwa kuzipangua .
Janeth hakuwa akimwendea kiutani utani Damiani kwani alijua bila kufanya hivyo Damiani angemdharau , na hilo ni kama kosa namba moja kwa Damiani kwani alijikuta akichotwa mtama na kabla hajatua chini alizuiwa na mguu wa kushoto wa Janeth na kisha alipigwa tikitaka ya kifua na moja kwamoja alizama kwenye swimming pool mzima mzima , jambo ambalo lilimfanya Abasi atoe kicheko kilichosikika na kumfanya Janeth amwangalie na kisha kutabasamu .
Damiani alijikuta akifedheheka mno na hali ile , alitoka kwenye maji akiwa anatweta huku hasira zikianza kumjaa , na jambo hilo Janeth alilishuhudia na kumfanya atabasamu kwani aliona misuli ya uso ya damiani imevimba kiasi cha kuonekana .
Ilikuwa ni kitendo cha kushitukiza Janeth alikuwa amefikiwa na Damiani na ngumi zilianza kutua mfululizo lakni mwanadada huyu alizikwepa kisutadi kabisa huku nyingine alipangua , lakini kila ngumi aliokuwa akipangua ilikuwa nzito kwake kiasi cha kumuumiza na hapo ndipo alipo jua Damiani anatumia sasa uwezo wa Muhammad ali , mwendo ule uliendelea na sasa wakati huu Janeth hakuzipangua alianza kuzikwepa , lakini ni kama Damiani swala hilo aliliona , kwani alijikuta kwa spidi ya ajabu ambayo hakuwahi kuwa nayo hapo kabla alimchapa bonge la guu kwenye ubavu wa Janeth , jambo ambalo lilimfanya janeth apepesuke na kwenda kutua katikati ya Ua , lakini Damiani hakutaka kumuacha kwani wakati huo akili zake hazikiwa hapo kabisa , alimsogeea Janeth na kumtaka kumpiga ngumi za moyo Janeth , lakini ile anaipeleka , alijikuta akipigwa na kitu kama shoti kwenye kichwa chake na kumfanya kichwa kimuume na kudondoka chini .
*****
Kwenye moja ya matajiri wakubwa duniani ambao walikuwa na ulinzi mkali , basi tajiri Mahmood alikuwa na ulinzi , bwana huyu kwanza alikuwa akitembea na walinzi wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume na hawa wote walikuwa ni wanajeshi makomandoo aina ya ‘special force’( hawa ni wale makomandoo ambao wamebobea kwenye mafunzo ya kazi maalumu unaweza pia kuwaita kama special unit lakini hawa kazi yao kubwa ilikuwa ni ulinzi , na wanajeshi hawa walitolewa katika kitengo cha ‘ THE PRESIDENTIAL GUARD SPECIAL FORCES (UAE-PG)
Unaambiwa mpaka sasa haieleweki kwanini tajiri huyu anawalinzi wengi , kwani hii ‘UAE-PG’ ndio ‘unit’ yenye wanajeshi ambao wanauchapa mkono ndani ya ‘Middle East ‘(Mashariki ya kati ) Yote.
Sasa ukiachana na tajiri huyu kua na walinzi hawa wawili ambao wanatoka kwenye ‘PG’ lakini alikuwa na wanausalama waliokuwa Undercover Na ambao pia alikuwa wakifatishana na yeye kila mahali.
Tajiri huyu akitaka kwenda mahali , watu wanaoenda kwanza ni wanausalama , na wanahakikisha mahali atakapo fikia panakuwa salama na ulinzi unaimarishwa , kabla ya kutua na ndege yake binafsi .
Basi siku ambayo Janeth anapimana uwezo na Damiani ndio siku ambayo wanausalama walikuwa washaingia nchini na kuweka makazi yao ndani ya hoteli ya Serena .
ITAENDELEA
TUTAENDLEA ANYTIME SOON UNAWEZA UKATOA MCHANGO WAKO KUNISAPOTI ,NAMBA YA MALIPO 0687151346 ISSAI SINGANO KIWANGO CHA CHINI KABISA UNACHOWEZA KUCHANGIA NI 1000 TU UKISHAFANYA MAIPO NJOO INBOX WATSAPP NIKUSHUKURU KWA KUTUMUA MWENDELEZO MPAKA MWISHO.
By singanoJr.
Let bitu mkuuu

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA 83
Ilikuwa ni siku nyingine kabisa siku ambayo ilikucha kwa mbinde kutokana na mambo yake yaliopita usiku ,taarifa zilizokuwa zimesambaa mitandaoni ni juu ya kifo cha tajiri mkubwa kutoka Canada Trembley .
Huku jeshi la polisi likitoa ripoti ya kwamba kifo hicho kimefanywa na watu wasiojulikana wenye ujuzi kama ilivyokuwa kwa polisi wa Tanzania .
Staili ya kifo hicho ilishangaza polisi na pia makachero waliokuwa wakimlinda tajiri huyo , hawakuweza kuamini kama kuna sniper ndani ya Tanzania ambae anaweza kufanya mauji ya namna hio , kwani mambo kama hayo yalikuwa yakionekana kwenye muvi , lakini ndani ya taifa la Tanzania mdunguaji wa aina hio ndie aliekamilisha mauaji hayo .
Taarifa zilitumwa na Canada jinsi tukio hilo lilivyotokea , uchunguzi nao ulifanyika lakini hakuna alieweza kushukiwa kama mhalifu na ukizingatia muda wa tukio hilo ulikuwa ni usiku , serikali ya Tanzania haikuwa kifungoni kwani tajiri huyo aliingia nchini kimya kimya .
Raisi henry alikuwa kwenye wakati mgumu kwani ni ndani ya siku kadhaa matajiri wakubwa walikuwa wamepoteza maisha ndani ya taifa lake , alikuwa akipokea simu mbali mbali kutoka kwa mataifa makubwa duniani juu ya kile kinachoendelea nchini lakini hakuwa na jibu la moja kwa moja .
Wakati akiendelea kupokea simu aliingia Pancho ndani ya ofisi hio .
“Nipe taarifa pancho “
“Nimemaliza kazi mkuu “Aliongea na kisha alitoa flash na kumkabidhi .
“Hii ina nini ?”
“Ni sauti za kikao cha wastaafu Matinde na washirika wake mambo wanayo ongea .
“Kuhusu janeth hili ni faili lake “alimkabidhi faili na hapo hapo Henry alianza nalo .
“Janeth ni mtoto wa bendera na mke wangu Wema ?”
‘Ndio mheshimiwa “
Raisi alijikuta moyo wake ukitaka kusimama hata ule uwezo wa kupumua ulipotea kwa muda , ni uzuri tu kwamba raisi huyu hakuwa na matatizo ya kiafya .
Alijiona kama ni mtu mwenye mikosi , kwani ni jana tu ndio kagundua Merina ni mtoto wa Bruno na mkewe na leo anagundua Janeth ni mtoto wa Wema Na bendera .
Mbaya Zaidi sio kwamba likuwa ni taarifa tu , lakini pia kulikuwa na Picha za Janeth akiwa na Bendera , lakini pia mke wake akiwa Na janeth kwa maana hio wawili hawa walikuwa wakimficha , alijiona mjinga
“Asante sana pancho nadhani kazi yako imeisha “
“uko sawa muheshimiwa?”
“Niko sawa , unaweza kwenda “.
Naam zilipita siku kumi mbele hali ndani ya Tanzania ilikuwa imetulia , kwani mwili wa tajiri Trembley ulisafirishwa kuelekea nchini kwao kwa ajili ya maziko , moja ya watu waliokuwa wametangulizana na mwili huo alikuwa ni Madam wema , hakutaka kuwa mbali na Merina kabisa muda wote alikuwa karibu yake , japo jambo hilo Merina hakuelezwa bado kwani alikuwa kwenye majonzi ,lakini madam Wema alipanga kuongea na Merina baada kupoa .
*****
“KWA MAJINA NAITWA JOHN ONYANGO BENDERA , NI RAISI WA AWAMU YA NANE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , NAJUA WAKATI HUU MNAONA UJUMBE WANGU HUU HUENDA SIPO TENA DUNIANI , ILA NATAKA KUWAAMBIA WATANZANIA KWAMBA KIPINDI CHA UONGOZI WANGU NI KIPINDI KIGUMU SANA KWANGU KWANI WENGI NILIOKUWA NIKIWAAMINI NDANI YA UONGOZI WANGU WALINIGEUKA .
NAKIRI NILIKUWA NIKISUMBULIWA NA MARADHI YA MOYO NA KUTOKANA NA TAARIFA YA DAKTARI SINA MUDA MREFU WA KUISHI , LAKINI NATAKA NIWAAMBIE WATANZANIA KUWA TAIFA LETU LIPO HATARINI ZAIDI KAMA TU HATUTASIMAMA IMARA KULILINDA ZIDI YA WATU AMBAO WANATAKA KULIANGAMIZA .
SINA MUDA MREFU WA KUISH LAKINI NISEME KWAMBA NAIPENDA SANA NCHI YANGU , NAWAPENDA SANA WANANCHI WANGU NILIOKUWA NNIKIWAONGOZA KATIKA KIPINDI CHOTE .
DHUMUNI LA WARAKA HUU KWA WATANZANIA NI KUTAKA KUWAKUMBUSHA SWALA ZIMA LA UZALENDO KWA NCHI YETU .
NAIACHA NCHI YANGU KWENYE MIKONO YA RAISI HENRY NIKIAMINI ATAWAFANYA WANANCHI WA TANZANIA KUJIVUNIA KUWA NDANI YA NCHI HII .
ASANTENI “
Damiani alijikuta akisikiliza hio video na kujikuta akitokwa na machozi ,allimuona mheshimiwa Bendera kama mmoja ya watu waliokuwa wakiipenda Tanzania kwa dhati kabisa .
Baada ya kuangalia video hio aligeukia karatasi iliokuwa kwenye bahasha hio na kisha aliisoma .
Juu kabisa ya karatasi hio kulikuwa kukisomeka neno MPANGO ZERO-U-97 .
Aliendelea kusoma yalikuwa ni ambatanisho la WARAKA HUO WA RASI KABLA YA KIFO
“ILI KUJUA MAANA YA MPANGO X UNAHUSU NINI MTAFUTE MTOTO WA BRUNO UTAPATA KIDANI , NA HIKO KIDANI KITAKUWA NI UFUNGUO WA KUPATA HAZINA YA BRUNO NA NDANI YA HAZINA HIO UTAPATA KUJUA NINI MAANA YA MPANGO X NA NA PIA UTAPATA KUJUA SIRI AMBAYO AMEIFICHA BWANA BRUNO LAMBERK , LA PILI HAKIKISHA UNAENDELEZA KITENGO CHA MZALENDO ILI KUILINDA NCHI YETU MBALI NA WALE WANAOITAKIA MABAYA , UKISHAFANIKIWA KUIFIKIA HAZINA HIO RUDI KATIKA KARATASI ULIOPEWA NA BRUNO NA ANGALIA MAJINA YA WATANZANIA WALIOPO KATIKA HAYO MAJINA KISHA HIO NDIO ITAKUWA MISHENI YENU NDANI YA KITENGO CHA MZALENDO KUWAONDOA DUNIANI WATU HAO . …” ,
KAZI KWAKO BWANA DAMIANI LAMBERK NI MIMI MZALENDO JOHN BENDERA ONYANGO “
Kulikuwa na maelezo mengi mengi ndani ya karatasi hii , lakini yaliokuwa na umuhmu Zaidi ni hayo nilioonyesha hapo juu.
Damiani mara baada ya kusoma WARAKA WA MWISHO WA RAISI KABLA YA KIFO CHAKE anajikuta akiacha kufanya misheni zote alizopewa na bruno na hio ni mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Zakayo juu ya Merina kuwa ni mtoto wa Bruno .
******
Ndege ya shirika la QATAR AIRWAYS ilitua ndani ya uwanja wa JNIA na baada ya ndege hio kusimama kwa muda wa nusu saa hivi mbele kabisa ya mlango wa ‘Arrival ‘ .
Alitokea madam Wema akiwa ameambatana na mwanae Jenny au Merina , alionekana kuwa ni mwenye furaha kweli na pia kwa Merina vile vile ,kwani alikuwa tayari ashaambiwa ukweli wote juu ya wazazi wake wa damu .
Watu waliokuwepo mahali hapo kwa ajili ya kuwapokea ni watoto wote wa madam Wema yaani kuanzia Janeth mtoto mkubwa na watoto wake wa kike wa mwisho lakini mtaalamu Damiani hakukoseakana ndani ya uwanja huo na mtu wa kwanza kumuona Damiani ni Merina , na Merina alimkimbilia Damiani na kwenda kumkumbatia , hakuamini kwamba Damiani alikuwa hai kwani mara ya mwisho kuonana wote walikuwa wametekwa.
Hatimae familia ya mwanamama Wema ilitimia , kwake ilikuwa ni furaha , hakuamini kwenye maisha yake ataonana na mtoto wake aliepotea , lakini pia hakuamini kwenye maisha y ake kama mme wake atawakubali watoto wake wote kama wanae ,kwake alijikuta akijawa na furaha sana .
Raisi henry hakuwa tena na kinyongo na mke wake ,kwani aliamua kumsamehe na kuendelea na maisha na uongozi .
****
Zikiwa zimepita siku kadhaa taarifa ya kusikitisha ilimfikia msheshimiwa raisi .
Taarifa hio ilikuwa ikihusu kuuwawa kwa Suzzane na mtu asiejulikana akiwa nyumbani kwake , jambo hilo lilo lilimuuma mheshimiwa mno ,kwani alikuwa akimwamini sana mwanausalama huyo.
Siku hio hio anapokea taarifa hio pia alipata taarifa ilio ufurahisha moyo wake , taarifa hio ilikuwa ni kifo cha mstaafu Matinde .
“Kazi nzuri Pancho “ Aliongea raisi na kisha pancho aliagana na raisi.
Sasa wakati zikiwa zimepita siku mbili baada ya kasha kasha za hapa na pale ndani ya ikulu , upande wa Damiani alikuwa anamhadithia Merina kuhusu namna alivyokutana na Bruno ndani ya kijiji cha Lushoto mpaka mama yake kkupoteza maisha , lakini kubwa Zaidi lilikuwa ni juu ya kidani ambacho Merina alikuwa nacho .
Baada ya Merina kuhadithiwa na kuoneshwa kidani hicho Hapo hapo ndipo alipo tambua kidani chake cha utotoni alichokuwa amekitunza miaka na miaka kwa maelekezo ya mlezi wake Bahati kwamba kitamsaidia sana huko mbeleni .
Baada ya kutambua kidani hicho hatimae Merina alimletea Damiani hicho kidani na hapo kisha walikiunganisha na hapo hapo ikatokea alama ya herufi G .
Uzuri ni kwamba yote haya yalikuwa yakiendelea ndani ya nyumba ya Bruno mbezi beach .
Katika kujiuliza uliza Ndipo damiani alipokumbuka kitu LEGACY ROOM .
Waliongozana na mwanadada Merina na kuingia ndani ya chumba cha LEGACY ROOM .
“KARIBU SANA MISTER DAMIANI RABANI NA MERINA SOSTENESS”
“Asante Nara”.
“NAWEZA KUKUSAIDIA NINI DAMIANI “.
Damiani hakueongea neno lolote , alilisogelea lile roboti Nara na kisha alizunguka kwa nyuma , na wakati wote huu Merina alikuwa akishangaa tu mara baada ya kuzunguka nyuma ya sanamu hili ,alikuta alama alioitegemea alama ya herufi G .
Mara baada ya kuona alama hii alipagusa na hapo hapo palitengeneza shimo na hap hapo sauti ya Nara ilisikika.
“UNAWEZA KUINGIZA UFUNGUO KUKUPA TAARIFA ZOTE UNAZOZITAKA MR DAMIANi “Liliongea hili roboti na damiani hakuchelewa aliingiza kile kidani chenye herufi G na hapo hapo ,mwanga ndani ya hiki chumba ulibadilika na kuwa mweupe kabisa .
“HONGERA MISTER DAMIANI RABANI, MPAKA SASA WEWE NDIO MMILIKI HALAI WA LEGACY ROOM “lakini baada ya neno hili mwanga ulibadilika na kuwa wa blue na hapo hapo Skrini kubwa mfuno wa TV iliokuwa ukutani ilionyesha video na mtu aliekuwa kwenye Vidio alikuwa ni Bruno .
*****
MIAKA NANE NYUMA
Ilikuwa ni siku ya jumanne , muda wa saa mbili kamili gari aina ya VX iliingia ndani ya geti la nyumba ya bruno na akashuka mwanaume mmoja hivi mzee wa kizungu , umri wake ulikuwa ni kama wa raisi Biden wa Marekani , mara baada ya bwana huyu kushuka , alipokelewa na Bruno kwabashasha na kisha walikaribishana .
“Nimetumwa na Level 01 “
“Level 01 !”Aliongea Bruno kwa mshangao mkubwa .
“Ndio bwana Bruno “
“Amekutuma nini ?”
“Kakuchagua kuwa mrithi wake “Bruno alijikuta akishangaa Zaidi bwana huyu ambae alifahamika kwa jina la Taylon.
“Umenichanganya “
“Mkuu yupo kwenye hali mbaya ya kiafya na amekuchagua kuwa kiogozi mkuu kabisa wa U-97 lakini kwa masharti”
“Mashart gani ?”
“Ya kutolipiza kisasi dhidi ya watu waliohusika na kifo cha familia yako “
“Unataka kumaanisha nini , inamaana Level 01 ndio aliehusika na kifo cha familia yangu “
“Hapana ila ni viongozi wa juu wa U-97 “
“kama ni viongozi wa juu kwanini hataki nilipize kisasi ,na pili kwanini niwe mkuu wa U-97 ?”
“maswali mazuri bwana Bruno , na nitayajibu yote kwa ufasaha “
“sababu ya kwanza umekuwa mwanachama mtiifu sana ,kwani kitendo cha kumpa taarifa isio sahihi mheshimiwa Bendera ,level 01 amekuona ni mtu mwenye akili nyingi ambae pia haupo tayari kusaliti Umoja wetu , Sababu ya pili moyo wa U-97 upo hapa Tanzania , na wewe umeishi sana ndani ya Taifa hili hivyo unalijua taifa hili vyema “.
“Unamaanisha nini kuhusu moyo wa U-97 upo hapa Tanzania .”
“Mpango zero “
“Ndio mpango gani ?”
“Mimi pia sijui , ila utaelewa nini maana ya mpango Zero pale utakapo apishwa kuwa Level 01.
“Nimekubali lakini kwa sharti moja na mimi “.
“Sharti gani?”
“Kabla ya yote nataka kujua waliohusika na vifo vya familia yangu , nikishawajua nitasamehe “
“Mkuu alilitegemea hili na waliohusika ni wengi , lakini waliotoa watu kuangamiza familia yako ni Mahmood pamoja na Trimbley hawa wote ni viongozi wakubwa kabisa ndani ya U-97 , Mahmood ni level 03 na Trimbley ni level 02”.
“Nipo tayari kuwa kiongozi mkubwa wa U-97 , nipo tayari kuwasamehe “
“Hongera kwa uamuzi wako , lakini baada ya kuapishwa level 03 na 02 lazimwa wafe ili uweze kuteua wawakilishi wako , kwani hakuna mwenye uwezo wa kuwatoa madarakani tofauti na kifo “
“lakini hawa si ndio wamehusika na vifo vya familia yangu “
“Ni kweli ndio maana unatakiwa kuwasamehe , ila wakishakufa ni kwa ajili ya U-97 sio kwa ajili ya kisasi , na hivyo ndivyo Mungu wetu atapokea kafari yao”
“Mungu yupi tena ,anaeruhusu vifo vya watu , unaamanisha huyu ninae mwamini , ambae yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu “
“Huyo sio Mungu wa U-97 ,Mungu wa umoja wetu ni Lucifer , hivyo kitendo kujiunga ndani ya umoja huu inamaana kwamba umemkubali Lucifer kama Mungu wako , na unapaswa kumtii”
ITAENDELEA
SEHEMU YA 84

INAENDELEA NDANI YA LEGACY ROOM-PRESENT
MPAKA KUFIKIA HATUA HII NI DHAHIRI DAMIANI USHAFANIKIWA KUMPATA MWANANGU NA PIA UMEFANIKIWA KUPATA KIDANI , LAKINI PIA UMEFANIKWA KUNISAIDIA KULIPIZA KISASI KWA WALIOIMALIZA FAMILIA YANGU , LAKINI PIA KUANGALIA VIDIO HII INAMAANISHA BENDERA KAFANIKIWA KUNIZUIA KUTIMIZA MALENGO YANGU HIVYO MISHENI NAWEZA KUSEMA KWAMBA IMEFELI .
NINA SIKITIKA KUKUAMBIA KWAMBA MIMI NDIO MTU NILIEHUSIKA KUMUUA MAMA YAKO DAMIANI NA SI MTU MWINGINE , NA YOTE ILILIKUWA NI SABABU YA KUTIMIZA MPANGO X.
MMI NIPO HAI NI MZIMA WA AFYA NA SIKUFA KAMA DUNIA INAVYO FAHAMU PAMOJA NA WEWE PIA , MTU ALIEKUFA SIKU YA TUKIO SIO MIMI BRUNO LAMBERK BALI NI CLONE YANGU .
MIMI BRUNO LAMBERK HALISI SIJAWAHI KUONANA NA WEWE ANA KWA ANA ZAIDI YA KUKUPA MAAGIZO YA KILA HATUA UNAYOPITA KWA MSAADA WA NARA .
HIVYO KUTOKANA NA KIFO CHA MAMA YAKO AMBAE MHUSIKA MKUU NI MIMI NAKUOMBA UNISAMEHE .
LAKINI PIA NATENGUA KAULI YANGU YA KUKUMILIKISHA MALI ZANGU ZOTE KWANZIA SASA NA MMILIKI HALALI ATAKUWA NI MTOTO WANGU .
MWISHO MAMA YAKO HAKUFA BURE ILA KAFA KWA AJLI YA WATANZANIA WOTE HIVYO AHADI NILIOWEKEANA NA BENDERA NI KUKUAMBIA SIRI YA MPANGO ZERO , NA HII NI KAMA ZAWADI KWA BENDERA BAADA YA KUNISHINDA NA KUZUIA MPANGO WANGU WA KUWAANGAMIZA MAADUI TISINI KATIKA KARATASI NILIOKUPATIA .
MPANGO ZERO NI MPANGO AMBAO UNAHISTORIA NDEFU HIVYO KUUJUA KWA UNDANI MPANGO HUU NENDA KASOME KITABU CHA ‘BOOK OF ALL NAMES ‘.
Damiani alijikuta akilia sana juu ya maelezo hayo , hakujua mtu aliehusika na kifo cha mama yake ni huyo ambae alikuwa akimsaidia kulipiza kisasi , sio kwake tu lakini pia kwa Merina .
Baada ya kuomboleza kwa muda, wote walitoka ndani ya chumba hichi huku Damiani ndani ya moyo wake akijiapia atamtafuta Bruno dunia nzima mpaka ampate .
Kilikuwa ni kitendo ambacho hata damiani hakuelewa kimetokeaje , kwani Damiani alijikuta akikumbatiwa kwa mbele na Merina na kisha kutemewa damu usoni ,lakini ile anaangalia mbele anamuona Seline amber akiwa ameshikilia bastora ikiwa inafuka moshi , aligeuza macho kwa Merina na hapo ndipo alipojua kuwa mwanadada seline alitaka kumuua yeye ila Merina alishuhudia hilo na kuikinga risasi hio na mwili wake .
Lakini wakati huo huo na seline alitema damu na kudondoka chini na hapo hapo ndipo Damiani alipomshuhudia Janeth akiwa ameshika bastora inafuka moshi .
“I love you Damiani , hakikisha unalipa kisasi”Hayo ndio maneno ya mwisho ya Merina kwenda kwa Damiani.
Huo ndio ukawa mwisho wa Merina na Seline amber .
Baada ya kifo cha Merina ,Damiani aliapia kumuua Bruno kwa namna yoyote ile hivyo alijikita Zaidi katika kuendeleza kampuni yake huku akifuatilia hstoria iliokuwa ikihusu kitabu kilichokuwa na siri za ulimwengu kitabu ambacho kiliaminika kuwa ndio moyo wa UMOJA NAMBA TISINI NA SABA lakini pia ni kitabu ambacho kiliaminika kuwa na siri kubwa sana ya ulimwengu , huku akishirikiana na mwanadaa Janeth ambae alikuja kuwa mpenzi wake .
Mpango zero chini ya INNOVA katika vichanga hamsini ni mtoto mmoja tu wa johan ndie ambae hakufariki katika majaribio hayo na mara baada ya mtoto huyu kupita katika kajaribio hayo alirudishwa kwa mama yake johan huku hospitali ikitoa sababu ambazo zilimridhisha mwanamama huyu , lakini katika ukuaji wa mtoto Ambrose (jina lake ) alianza kuonyesha matendo ambayo sio yakawaida na kuogopesha .
Raisi henry alifanikiwa kuongoza kipindi cha miaka mitano tu kupitia kitengo cha Mzalendo alitolewa madarakani kwa kutokuruhusiwa kugombea tena .
Mzalendo chini ya Damiani walitimiza waraka wa raisi juu ya kuwaua Kimbona , Rich sam , kizito kabwela na Athumani ndalu .lakini pia kikundi hichi kiliwezakumuachia mwanadada Marie jasusi wa CIA kwa makubaliano maalumu ambayo hayakuwekwa wazi .
Misheni ya Death notice kutoka makao makuu ya U-97 ilighairishwa mara baada ya mpango zero kufanikiwa ndani ya muda mfupi na hio ilikuwa ni oda kutoka kwa Level one. .
Je unadhani ni historia gani ipo nyuma ya Mpango zero
Usikose kufatilia simulizi ya kijasusi ya BOOK OF ALL NAMES , lakini kabla ya kufatilia simulizi hio lazima tujue kipi kimechangia ufanikiwaji wa Mpango Zero je ni kweli mpango huo ulifanikiwa kutokana na utaalamu wa kisayansi , jibu ni HAPANA mapango huu haukufanikiwa kutokana na sababu za kisayansi bali ni athari zilizotokana na MASAA MAWILI YA KUMBU KUMBU pamoja na historia nzima ya BOOK OF ALL NAMES .
NB: Kabla ya kusoma kitabu cha U-97(BOOK OF ALL NAMES) hakikisha unaijua vyema historia ya johani pamoja na Joseph ambao majina yao yalikuwa ni Leah na Peter kutoka katika kitabu cha MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU .
THE END
SHUKRANI SANA KWA KUWA NA MIMI MWANDISHI WENU SINGANO JR .(ISSAI SINGANO) HAKIKISHA UNAACHA MAONI YAKO.
Unaweza pia nichangia kwa chochote ulichobarikiwa nacho kupitia namba 0687151346 jina ISSAI SINGANO
WASILIANA NA MWANDISHI KWA AJILI MWENDELEZO HAPA

Kitabu cha MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU kishatoka tayari bei yake ni shilingi 8000 tu lipa namba 0687151346 jina ISSAI SINGANO ukishalipa njoo Inbox watsapp nikutumie softcopy ujisomee mkasa huo wa kusisimua kabisa Utangulizi Gusa [URL="http://drive.google.com/file/d/1CjcIOeRflP-TOv8st2vWvQsqF6II-Hpt/view?usp=drivesdk]HAPAA[/url]
Asante mkuu
 
singano asante sana kipenzi,nimeenjoy sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom