Ujasusi - Umoja namba 97

Ujasusi - Umoja namba 97

SEHEMU YA 66

THE TRICK WHICH BROUGHT RELIEF
(HILA ILIOLETA AHUWENI )

TUENDELEEE
Ilikuwa ni siku nyingine tulivu kabisa na hii ni kutokana na kashikashi zote zilizotokea siku iliopita , siku ambayo wale wakubwa wa maadui wa Damiani , watu ambao walikuwa wakimtafuta kijana huyu kwa udi na uvumba walikuja kupata taarifa za uwepo wake nchini .
Moja ya watu hao alikuwa ni bidada Suzzane , dada huyu ambae roho yake kadiri siku zilivyokuwa zikisonga ilizidi kubadilika na kuzidi kuwa nyeusi , kwenye akili yake alikuwa akumuwazia Damiani Tu , kwani katika maisha yake ya kijasusi hakuwahi kumfatilia mtu kwa muda mrefu sana kama alivyokuwa akimfatilia Damiani , kwake swala hilo lilikuwa ni dharau ikilinganisha na historia yake ya kazi lakini pia mtu ambae alikuwa akimtafuta hakuwa na mafunzo yoyote kama aliokuwa nayo yeye , halafu akamzidi akili , kwake jambo hilo lilimkera na kila alipokuwa akimka asubuhi mtu wa kwanza kumfikiria katika kichwa chake ni Damiani tu.
Siku hio alipo amka alikumbuka miadi yake na mheshimiwa raisi kwani alikuwa amepokea simu ya kumtaka siku inayofatia kwenda kuonana na mheshimiwa ikulu magogoni , alijiandaa vyema kwa siku hio huku akiwaza mambo kadhaa ya kuripoti kwa muheshimiwa , kwani kichwa chake kilikuwa na mambo mengi sana ya kumueleza mheshimiwa , lakini alidhamiria kwamba mambo ambayo atamueleza ni yale ambayo alikuwa na uhakika nayo.
Lisaa limoja alikuwa ndani ya eneo la ikulu , moja kwa moja alipita hatua zote za usalama ikulu na kisha alipita moja kwa moja mpaka ofisini , muda hio ilikuwa ni saa nne asubuhi , hivyo mheshimiwa raisi alikuwa tayari yupo ofisini , baada ya kufika kabisa kwenye mlango , aliambiwa asubiri kwani mheshimiwa alikuwa na mazungumzo na mkurugenzi wa ikulu mawasiliano bwana Sabi mboneche , hivyo Suzzane alisubiri kwenye masofa , na hata dakika moja haikuisha Sabi alitoka , walionyeshana tabasamu na kisha Suzzane akaingia ndani .
“ Karibu sana Suzzane “ Aliongea mheshimiwa mara baada ya Suzzane kuingia ndani hapo , kiufupi mheshimiwa raisi kwenye watu aliokuwa akiwaamini sana na kuwapenda na kuwaheshimu alikuwa ni Suzzane na hio ni kutokana na ufanisi wa kazi Suzzane aliokuwa nao , lakini pili siri nyingi za mheshimiwa raisi Suzzane alikuwa akizijua .
“ Asante sana mheshimiwa pole sana na safari “
“ Nashukuru sana Suzzane , safari yangu ilienda salama kabisa na mambo mengi nimefanikisha , vipi hali ya nchi kiusalama na mipango yetu kwa ujumla ?”
“ Kwanza mheshimiwa naweza kusema kwa sasa hali sio shwari sana , kwani mtu tuliekuwa tukimtafua tayari yupo nchini “
“ Unamaanisha Damiani is confirmed to be in Tanzania “
“ Yess , mheshimiwa na swala ambalo linanipa mashaka na nione kwamba hatupo salama ni kwasababu na Kimbona na wenzake naamini mpaka sasa wanayo taarifa kamili ya uwepo wa damiani nchini , na kama unavyojua Damiani tunaamini ana nyaraka ambazo tunaamini ndio mheshimiwa raisi kaziacha “
Mheshimiwa raisi alijikuta jasho likimtoka , aliamini swala hilo ni hatari sana kwake kama Kimbona watapata nyaraka hizo kabla ya yeye , kwani aliamini huenda raisi Bendera aliandika vitu vingi vya kumuhusu na endapo watu hao watavipata ingekuwa hatari kwake na mipango yake .
“ Suzzane hakikisha unampata damiani wewe kwanza kabla ya wakina kimbona na uzichukue hizo nyaraka “
“ Sawa mheshimiwa hilo nalifanyia kazi mpaka sasa na baadhi ya vijana wangu wapo kazini wakifatilia mahali ambapo damiani yupo “
“ Good kuna lingine , vipi kuhusu huyu mzalendo , je ndio huyo huyo Damiani anatuchezea au kuna mwingine ?”
” Mheshimiwa kuhusu swala la mzalendo bado sijajua Zaidi , lakini naamini kwa kujua siku ambayo Damiani ameingia nchini ndio nitajua kupambanua kama mzalendo ni huyo huyo Damiani au ni mtu mwingine “
“ Kama ni hivyo Suzzane naamini kumpata Damiani kwa sasa iwe kipaumbele , ili tuweze kujipatia majibu ya maswali yetu haraka sana “
“Sawa muheshimiwa “
Suzzane baada ya mazungumzo na raisi , alitoka ndani ya ofisi hio na ile anatoka tu mtu wa kwanza kukutana nae nje tena alikuwa ni Sabi , na Sabi alimsimamisha .
“ Vipi Suzzane , unaonekana unaharaka?”
“ Ndio Sabi kwasasa nina haraka Zaidi ya neno lenyewe “
“ Okey kama unaharaka basi nisikucheleweshe , nilitaka kujua kama lini unanafasi tutoke tukapate chakula cha jioni sehemu tulivu nina mambo kadhaa ya kuongea na wewe “.
Suzzane alimwangalia Sabi usoni na kisha aliachia tabasamu la kinyonge ni kama ni mtu aliekuwa akimthaminisha kijana huyo na kuridhishwa na jambo Fulani .
“Nitakwambia Sabi siku ambayo nitakuwa free “. Aliongea Suzzane na kisha alitoka eneo hilo na kuliendea gari lake na kuwasha na kutoka kabisa eneo la ikulu .
Wakati akikunja upande wa kuingia benki kuu ya Tanzania , simu yake iliita , aliweka kijiearphone sikioni na kisha alibonyeza kitufe cha kupokelea
“ Yess Festo ,, umefanikiwa ?“
“ Ndio Suzzane nimefanikiwa kupata namba za gari lile pale mgahawani na nimezifatilia namba hizo usajili wake , mmiliki wa gari ni Merina sosteness “
“ Merina Sosteness ?”
“ Ndio kwa taarifa zake ni mmiliki wa kampuni ya STL ni mwanadaa mwenye pesa zake mjini”
“Okey Festo asante kwa kazi nzuri , nipatie adress eneo analoishi huyu mwanadada”
“ Okey”
Suzzane alikuwa akimjua vyema Merina sosteness , kwani mwanadada huyu alikuwa ni moja ya wanawake ambao walikuwa na mafanikio makubwa ndani ya taifa la Tanzania wakiwa na umri mdogo , japo hakujua sana undani wa mwanadada huyu , lakini kitendo cha kutoka pale mgahawani huku akiamini kwenye gari lake Damiani alikuwepo aliamini kuna mengi Zaidi ya kujua kuhusu mwanadada huyu .
Hivyo mara baada ya kupata taarifa hio kutoka kwa Festo kijana aliemwachia kazi ya kufatilia kamera zilizokuwepo kwenye mgahawa wa Mama Afrika,aliona jambo la maana kwake kwa wakati huo ni kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Merina .
*******
Merina siku hio hakuwa hata na hamu ya kwenda kazini kabisa , kwake mawazo yake yalikuwa yakimuwaza Damiani tu muda wote , aliamini Damiani muda wowote anaweza akaja hapo nyumbani kwake na kumletea gari lake , hivyo aliamini kwenda kazini anaweza akaikosa nafasi ya kutokuonana na Damiani kwa mara nyingine .
Siku hio alikuwa ni mwenye furaha sana kiasi kwamba hata mdogo wake Mage alimshangaa dada yake na aliishia kutabasamu tu huku akijisemea mapenzi nyoso.
Muda ulikuwa unaenda pasipo dalili ya Damiani kuoneakana kurudisha gari jambo ambalo lilikuwa likimpa sana wasiwasi sana Merina, aliogopa huenda Damiani jana yake alipata matatizo, roho yake haikutulia kabisa , muda huo ilikuwa inaenda saa sita kamili za mchana ndipo waliposikia honi ya gari nje , mtu wa kwanza kunyanyuka kwenye sofa alikuwa ni Merina , alikimbilia nje na alikuwa amesahau kama hakuwa akihusika na kufungua geti kwani kulikuwa na mlinzi siku hio .
Mlinzi alifungua geti na hapo hapo moyo wa Merina ulipiga kite baada ya kushudia gari yake , hakumuona dereva aliekuwa ndani lakini kwake aliamiani mtu aliekuwa ndani ya gari hilo alikuwa ni Damiani , hivyo alijikuta akiachia tabasamu mara baada ya gari hilo kuingia taratibu na kwenda kupark , lakini wakati huo huo , wakati mlinzi anataka kufunga geti , mwanadaa Suzzzane alitinga ndani hapo .
Jambo ambalo lilimshangaza sana Merina , hakujua mwanadada huyo ni nani .
******
Kitendo cha Zakayo kumwambia kwamba kazi tayari , kilimfurahisha sana Kimbona , hakuamini kwamba kazi yake imekwenda haraka haraka hivyo pasipo kutarajia , moja kwa moja alimwambia Zakayo aende kesho ofisini kwake kwa ajili ya kumpa maendeleo ya kazi.
“Vipi tena huyo ?” Aliuliza sam
“ Zakayo huyu jasusi wa kimataifa , huamini nimempa kazi masaa machache na sasa ananirudishia majibu kwamba kazi tayari “
“ Unaniambia ile kazi ya kumfatilia damiani ?”
“ Ndio nimemwambia kesho anileteee taarifa hio ofisini nadhani itakuwa moja ya hatua kubwa sana kama tutampata huyu kijana mapema”
“ ni kweli kabisa Kimbona , huyu Damiani kuna mambo mengi sana tutayafahamu kutoka kwake kama tutampata “
“Ndio na swala hili lazima tulifanye kwa ufanisi mkubwa na sisi tuwe wa kwanza kumtia mikononi kwani naamini kuna uwezekano mkubwa sio sisi tu tunaomfatilia kijana huyu “ Aliongea Kimbona .
Siku iliofata kimbona alikuwa ofisini akiwa na hamu kubwa ya kuonana na bwana Zakayo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya kazi yake aliompatia kijana huyo , na kweli baada ya lisaa limoja zakayo alitia timu ndani ya ofisi ya Kimbona , na mara baada ya kuingia walisalimiana na kuketi na Kimbona hakutaka kuchelewa alimwambia Zakayo amwambie kazi yake imefanikiwa kwa kiasi gani .
“Nadhani unakumbuka makubaliano yetu mpaka sasa ni kumkamata Damiani na ndipo hela yako nakumalizia ?”
“ Nakumbuka sana na mpaka sasa nishamkamata yupo kambi yangu ya siri ni swala la wewe tu kwenda kumuona “
“Unauhakika Zakayo ?”
“ Nishawahi kuleta mzaha katika kazi , nadhani unajua fika historia yangu mimi sio mbabaishaji katika kazi yangu “
“Kwa hio Damiani yupo wapi ?”.
“Nishasema yupo kambini kwangu ni swala la muda kupanga kwenda kumchukua , ila kwasasa nahitaji malipo yangu , kuhusu alipo Damiani utawatuma vijana wako kwenda kufatilia mahali nitakapo waelekeza .
“Nitaaminije kama ni kweli ?”
“Hii hapa ni video inayomwonesha Damiani akiwa kambini kwangu “ Aliongea zakayo huku akimkabidhi kimbona video inayomwonyesha Damiani , ni kweli kabisa alikuwa ni Damiani akiwa amefungwa Kamba na plasta mdomoni .
“ Hahahahaha… hahahaha ,, safi Sanaa , nimekukubali bwana Zakayo , nitawaagiza vijana wangu waende wakamchukue , ni wewe tu kutuelekeza mahali alipo “
“ Hakuna shaka muda ukifika nitawapa eneo husika , mimi sitokuwepo eneo hilo ila kuna mtu wangu wa karibu atawapokea , mkifika mtapata mtu wenu “ aliongea Zakayo na baada ya hapo malipo yalifanyika na Kimbona aliaga huku akimwahidi muda wa saa nne usiku ndio utakuwa muda mzuri wa kwenda kuonana na Damiani na vijana wake kumchukua .
******
Huku nyumbani kwa Merina alijikuta akiwa katika mshangao wa uwepo wa Suzzane hapo ndani , lakini alimpa ishara mlinzi na mlinzi alimfata Suzzane , na Suzzane alitoa kitambulisho na kujitambulisha kama polisi … wakati huo huo alitoka Mage ndani akiwa ameshikilia simu na kumpelekea dada yake ambae muda wote alikuwa akimsubiria Damiani kushuka kwenye gari , alichukua simu ile lakini ile anaweka sikioni , mlango wa gari ulifunguliwa na alitoka mwanaume mmoja hivi makamo , hakuwa Damiani , ni mwanaume mwenye muonekano kama wa Damiani kimwili na kirangi , alikuwa amevalia jeans na tisheti ya Timberland , wakati huo huo Merina akiwa katika mshangao ndipo alipojikuta akisikia sauti ikimpa maelekezo kwenye simu sauti asio ifahamu , na hapo hapo ikakatika jambo ambalo hakuelewa mara moja …. Na wakati huo na Suzzane alikuwa yupo ashamsogelea karibu Merina , na yeye alikuwa akimwamngalia mwanaume alietoka kwenye gari hio .
“Miss Merina asante sana kwa msaada wako wa jana .., ndio nimefika hapa kurudisha gari “ Aliongea mwanaume huyo kwa sauti ya kikakamavu na kumfanya Merina ashangae na hata Suzzane na hivyo hivyo kwa Mage , lakini Merina akili yake mara moja ilifunguka na akili yake ilirudi kwenye simu .
“ ATAKACHO ONGEA MWANAUME ATAKAEKULETEA GARI HAKIKISHA UNAMJIBU KIUSAHIHI KWA USALAMA WA DAMIANI “ hayo ndio maneno alioyasikia kwenye namba mpya aliopokea .
Merina na yeye akili yake ilicheza hapo hapo na kwakuwa mwanamke huyu alikuwa amejaaliwa akili nyingi alijikuta akijaribu kuweka tabasamu usoni mwake .
“Nashukuru sana kwa kurudisha gari langu salama , jana nilikukabidhi nikiwa sikuamini kabisa , lakini umeonyesha uaminifu wako “
“Ni kweli dharula ya jana ilikuwa ya aina yake , nashukuru sana kwa msaada wako Merina “
“Samahani kabla hamjaendelea , mimi ni polisi na nimefika hapa kuna mtu namtafuta na jana alionekana akiingia kwenye gari yako maeneo ya mgahawa wa Mama Afrika “ Aliongea Suzzane na kumfanya Merina hapo amgeukie Suzzane na kumwangalia lakini kabla hajajibu mwanaume aliengia na gari hapo alijibu swali hilo .
“ Yeah ndio mimi , kwanini unaniulizia ?” Jibu hilo lilimfanya Suzzane atoe picha na kumuonesha merina na merina aliipokea , na aliona picha hio ilikuwa ni ya Damiani , japo alishituka lakini aliweka uso wa kawaida ili asishitukiwe .
“Sijawahi kuonana nae huyu mtu na wala simtambui , mtu niliekuja nae hapa nyumbani alikuwa ni huyo mbele yako na ndie alieo ondoka na gari yangu “
“Unauhakika ?”
“ Kwani kuna nini afande “ aliuliza yule mwanaume .
“Wewe huyu ni nani yako ?”
“Mimi naitwa Fredi uhusiano wangu na Merina ni wakibiashara Zaidi , mimi ni meneja masoko kutoka kampiuni ya Z-stylishi wear “ Alijjitambulisha mwanaume huyo na hapo hapo Suzzane alijihisi amepigwa na kitu kizito kichwani, kwani mpaka hapo aliamini kampuni ya bwana huyu aliye mbele yake ndio kampuni ambayo mmiliki wake ni Zakayo .
Suzzane hakutaka kusema Zaidi neno , hapo hapo aliona tayari ashafanyiwa mchezo na Zakayo na huenda Zakayo tayari ashampata damiani , na yote haya anayo yashuhudia ni janja yake .
“Okey nashukuru kwa ushirikiano wenu , lakini Merina niambie ukweli una uhakika hujamuona mtu huyu “ Alionyesha picha ile ya Damiani na Merina alitingisha kichwa kusema kwamba hajamuona .
Suzzane hakutaka kupoteza muda pale pale alimpigia simu Festo amtumie video Za kamera za pale mgahawani na Festo naye hakuchelewa aliweza kuzituma pale pale na hapo ndipo Suzzane nusu tusi limtoke , kwani mwanaume aliengia kwenye gari na mwanaume aliesimama mbele yake walikuwa wanafanana , kwa maana hio sio Damiani alieingia kwenye gari la Merina .
“This was all trick ( huu wote ni mtego ) aliongea Suzzane aking`ata meno yake kwa hasira , kwani video ile kwa jinsi ilivyoonesha pale aliamini kuna mchezo unachezwa ,.. hivyo hakutaka kubaki hapo ndani bali aliaga na kuondoka zake.
“Enhe kaka samahani , Damiani yuko wapi ?”
“Unamzungumzia Damiani gani huyo mbona hata mimi simfahamu “
“Inamaana aliekupa gari ulilete hapa humjui jina kama anaitwa Damianni ?”
“ Hapana dada yangu mtu alienipa gari hili ni boss wangu wa kampuni na ndie alienipa maelekezo yote ya kipi natakiwa kuongea pindi nifikapo “
“ Boss wako ni nani ?”
“ Ni zakayo ,, mmiliki wa Z stylish wear”
Hapo hapo Merina alijikuta akimkumbuka Zakayo na mpaka hapo alijua kwa vyovyote vile lazima Damiani atakuwa kwenye mikono ya Zakayo .
Wakati akiagana na Bwana Fredi pale pale simu yake aliokuwa ameshikilia mkononi ilitoa mlio kuashiria ilikuwa inaita , na kuangalia jina ni Matinde mkuu wa TISS mstaafu . alipokea na kuweka sikioni .
“Miss Merina nimekupigia kukutaarifu kuwa ile hela tuliokubaliana kumlipa mpelelezi wetu iandae mapema kwani kazi ishakamilika , na Damiani kapatikana hivyo kama kawaida tutakutana sehemu ambayo tutakuelekeza baadae kwa ajili ya makabidhiano.
“Kwa hio mheshimiwa damiani yupo na zakayo kwa sasa ?”
“ Ndio merina , Rest Assured, lakini kumbuka sana hio hela usisahau “
“ Sawa muheshimiwa “ aliongea Merina na alijikuta pumzi yake ikishuka kwani ile hofu aliokuwa nayo ilipotea na sasa alikuwa amejawa na furaha anakwenda kumuona Damiani kwa mara nyingine , kwake pesa sio kitu kabisa.
“If it was zakayo it must be very good relief “
“Kama ni Zakayo itakuwa ni ahueni”
KIPI KITAENDELEA STAY TUNED
Wasiliana na mimi kwa namba 0687151346 watsapp only .
Or WhatsApp öffnen
 
Natamani nisiifungue wala kuisoma walau ifike hata page 3,4 hv ndio nizifaidi kwa pamoja.
 
Aiseee hatari sana, naye Damiani amatekwa kizembe zembe ana mafunzo kabisa, naona Patrick anataka kujiingiza kwenye moto Kwa ajili ya mbususu, Merine na Janeth ni mtu na mdogo wake Ila watakikuta wanatwangana makonde Kwa ajili ya Damiani, Kazi nzuri sana mkuu endeleeaaa
 
Aiseee hatari sana, naye Damiani amatekwa kizembe zembe ana mafunzo kabisa, naona Patrick anataka kujiingiza kwenye moto Kwa ajili ya mbususu, Merine na Janeth ni mtu na mdogo wake Ila watakikuta wanatwangana makonde Kwa ajili ya Damiani, Kazi nzuri sana mkuu endeleeaaa
KESHO WAKUU TUTAENDELEA
Hivi Kesho haijafika mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom