Ujasusi - Umoja namba 97

Ujasusi - Umoja namba 97

SEHEMU YA 72
MZALENDO
Damiani hakuwa na haja ya kumzuia sabi asiingie , kwani japo alikuwa hamuamini bwana huyu kwa asilimia mia moja , lakini jina lake kuwepo katika orodha ya wazalendo , lilimfanya amfungulie na hakuvaa tena ile sura ya Stephano lamberk bali alikuwa ni damiani mwenyewe .
“ Damiani!!!! ulikuwa ni mshangao kutoka kwa sabi mara baada ya kufunguliwa geti na mtu ambaye alikuwa akimjua , rafiki yake wa kitambo kutoka nchini Thailland ,.
“ sabi , karibu sana “ aliongea damiani huku akiwa ameweka tabasamu usoni mwake waliongozana wote kwa pamoja mpaka ndani na damiani alimkaribisha kwa hug rafiki yake sabi huku wote wakionekana kukumbukia kipindi walichokuwa pamoja wakiwa nchini Thailland .
“ ni muda mrefu sabi “
“ ni kweli damiani “.
“uliingia lini nchini Tanzania? “ aliuliza damiani .
“ mara baada tu ya kumaliza masomo yangu ya kipepelezi ndio nilirudi rasmi “
“ni kitambo kumbe , na ndio maana ulipata nafasi nzito serikalini “
“ ndio lakini nadhani mpaka sasa unajua kwanini nipo pale ikulu “.
“ hapana sijui “
“ utashindwaje kujua wakati wewe ndio mkuu wetu wa kitengo “
“ unamaannisha nini kuhusu hilo “
“ namaasha ‘ MZALENDO’
“mzalendo !?”
“ ndio damiani , najua mpaka sasa unataarifa kamili ya nini kinaendelea hapa nchini , na nafikiri ushajua machache juu ya mzalendo “
“ ni kweli , lakini hlo swala la kuwa mkuu wa kitengo limenichanganya “
“ utaelewa damiani , ilimradi nipo hapa nitakueleza kila kitu kilichotokea, natoka nchini Thailland na kurejea Tanzania , mpaka kuingia ikulu naamini pia utanieleza safari yako ya China mpaka kurudi nchini “ aliongea sabi na kisha alianza kumuhadithia damiani .
*****
Moja ya mambo yalionitia nguvu katika harakati zangu za kusomea maswala ya upelelezi ni swala la kifo cha baba yangu mzee mboneche , swala hili kwangu lilikuwa kama ni motisha , na ndio maana sikukata tamaa kabisa , nilikuwa na nia moja tu ya kuhakikisha nawapata waliohusika na mauaji ya baba yangu , japo jambo lililokua mbele yangu lilionekana kuwa gumu sana , lakini kwangu niliamiani kwa namna moja ama nyingine lazima nifanye kitu .
Mara baada ya mimi kuagana na damian , sikutaka kubweteka kwani nilitumia muda mwingi katika kujifua kimapigano ,lakini pia katika mafunzo ya kipelelezi , nilitumia Zaidi ya miezi kadhaa mbele ndio nilirudi rasmi ndani ya taifa la Tanzania .
Ilikuwa ni siku ya jumamosi ndio siku niliotua ndani ya uwanja wa ndege wa Julias Kamabarage Nyerere, mara baada ya kutua ndani ya uwanja huu kutokea terminal namba tatu nilisogea mpaka upande wa taksi , lakini ile nazikaribia tu kuna jamaa mmoja aliekuwa amevalia kofia ya NIKE alinisogelea na kama unavyojua maneno ya watu wa taksi , bwana yule ambae alikuwa na mwonekano wa kiutu uzima lakini sio sana , alikuwa ni makadirio ya miaka kuanzia therethini kwenda mbele , alinichangamkia huku akiipigia debe taksi yake , na mimi kwakua ndio ilikuwa shida yangu basi sikua na haja ya kuchukua taksi nyingine , niliingia ndani ya taksi hio na moja kwa moja tulitoka ndani ya eneo hilo , gari zilisonga, mita kadhaa wakati tukiwa tunaingia kwenye flyover , ndio nilisikia sauti ya bwana huyu ikiwa imebadilika .
“ Karibu sana Tanzania Sabi Mboneche” ndio mtu huyu ambae nilimjua kama dereva taksi ndivyo alivynikaribisha tena sauti yake ikiwa imebadilika haikuwa ile ya mwendesha taksi tena hii ilisikika ikiwa na usiriasi ndani yake .
“Umelifahamuje jina langu ?”
“ Nakufahamu vyema Sabi , tulikuwa tukikufatlia kwa muda mrefu tokea kifo cha baba yako brigedia Mboneche “
” Mlikuwa mkinifatilia nyie ni nani “
“ utajua kila kitu sabi, na nimekuja hapa kukupokea nikupeleke sehemu husika ili kupata majibu ya maswali yako yote “
“ sihitaji majibu naomba unishushe nitapanda teksi nyingne “.
“hutaki kujua chanzo cha kifo cha baba yako? , au hilo sio jambo lililokurudisha nchini “
“umejuaje yote hayo , wewe ni nani ?”
“MZALENDO “
“ mzalendo ?“
“ ndio mimi ni moja ya mwanachama wa mzalendo na wewe pia ni moja ya wanachamam wa wazalendo na ulikuwa ukisubiriwa tu “
“ sijakuelewa bado “
“ utanielewa tutakapo fika sehemu husika “
Aliongea dereva yule wa taksi na baada ya muda mfupi tulikuwa tukipita maeno ya Ubungo , sikujua ni sehemu gani bwana huyu alikuwa akinipeleka , sikuwa nikimuamini mtu , kwani moja ya kauli ya baba alioniacha nayo ni kutokumuamini mtu , na mimi sikuwa nikimuamini mtu kabisa , nilijua swala lililomuua baba lilikuwa ni swala nyeti mnoo na na mimi ilipaswa kuwa makini na kila hatua ninayo piga , lakini swala la mtu huyu kujitambulisha kwangu , lakini sio kujitambulisha kwangu tu ,alionekana akijua mambo yangu mengi , alinifanya nizidi kushangaa sana , sikutarajia kama mambo yangu niliokuwa nikiyafanya kimya kimya yalikuwa yakijulikana, nilijiua kila kitu nilichokuwa nikikifanya nilikifanya kwa siri kubwa mnno , lakini mtu huyu alikuwa akinijua vyema ,swala hilo kwangu lilinishangaza , na ndio sababu ya mimi kutulia tu kwenye gari hio ili kuona mwisho wake , nilikuwa nipo tayari kwa lolote , kwani tokea naingia nchini nilikuwa nmejipanga kwa hali yoyote nitakayo kutana nayo na swala hili kwangu niliona ni moja ya sehemu tu ya hali ambazo nilikuwa nimekwisha kuzitarajia .
Ni ndani ya kama dakika arobaini na tano hivi tulikua ndani ya eneo la kibaha , kwakweli japo nilikuwam nimeamua kila kitu kufatishana na mtu huyu ambaye nilikuwa simjui bado , lakini wasiwasi ulinizidia , kwani eneo tulilokuwepo lilinishangaza pia .
“ tunakwenda wapi ?”
“ kambini “ aliongea mwanuame huyu aliekuwa akijiita mzalendo .
“ huku ndio kambini ?”.
“ ndio , hupaswi kuwa na wasiwasi sabi , upo mikononi salama , nakuona jinsi ulivyo nawasiwsi”
“ wasiwasi ni lazima , ndio kwanza nmeingia nchini , na jambo la kwanza kukutana nalo ni swala hilo , unafikiri nitaachaje kuwa nawasiwasi”.
“unacho ongea ni sawa kabisa , na mimi nataka utoe hofu , kwani sehemu tunayo enda ni sehemu salama Zaidi , lakini wewe pia ni moja ya watu tuliokuwa tukiwasubiria “.
Baada ya kufika kwa Mathiasi tuliingia barabara ya vumbi upande wa kushoto , na gari ilipiga mwendo na ndani ya madakika kadhaaa tulikuwa mbele ya jumba moja lililozungushiwa ukuta , lililokuwa na alama juu kabisa ya ‘N’ .
Baada ya kufika mbele ya jengo hili hatimae geti lilifunguliwa na sisi tuliingia ndani , na hapo ndipo niliposhangazwa zaidi na mandhari ya eneo hilo .
Mtu alienipokea ndani ya eno hilo alikuwa ni Master P , nakumbuka wakati naingia ndani ya eneo hilo , ilikuwa ni saa tisa hivi mchana jua likiwa linawaka kali .
“karibu bwana sabi mboneche , kwenye kambi ya ‘ MZALENDO’” aliongea bwana huyu na kuzidi kunichanganya .
“hapa panahusika na nini , na kwanini nipo hapa “
“hilo sio swali la wewe kuuliza , umekuja mwenyewe kwa hiali yako hapa “ aliongea master p na kunifanya nipandwe na hasira , maana sio kweli kwamba nimekuja mwenyewe ndani ya eneo hilo , kwani mwendesha taksi ndio alienileta .
“ najua unamaswali mengi sana yakuuliza , na nikuhakikishie kwamba ndani ya muda mfupi maswali yako yatajibiwa , kwasasa unatakiwa kukutana na makamu wetu wa ‘MZALENDO’.
Sikutaka kuongea sana mara baada , kwani nilifatisha kila kitu nilichokuwa nikiambiwa kwa wakati huo , na ni kweli nilikuwa nina maswali mengi , na nilishangaa pia mpangilio wa hapo ndani ,ilionekana kama kambi ya jeshi .
Baada ya kutembea mita kadhaa ndani ya vyumba ndani jumba hilo , hatimae niliingizwa kwenye ofisi ambayo niliambiwa ndio makamu alipo na hapo ndipo nilipo pigwwa na butwaa .
Aliekuwa mbele yangu alikuwa ni Madam Wema, mke wa raisi wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
“ karibu sana Sabi Mboneche “
“asante sana madam “ nilijibu kwa wasiwasi huku nikikaa .
“ ni mara yangu ya kwanza kuonana na wewe ana kwa ana “
“ ndio madam , hata mimi sikutegemea kama nitaonana na wewe eneo hili “
“ huna haja ya kunishangaa sabi , nikupe pole na safari “
“ asante sana “
“nipo hapa kwa ajili ya kukujibu maswali yako “.
“nitakushuru sana madam “
“naomba nikuulize swali kabla sijaendelea ?”
“ hakuna shaka madam unaweza kuuliza “
“ je unaamini baba yako alikufa kifo cha kawaida “nilishagnaa lakini sikuwa na budi kujibu .
“ hapana , baba yangu ameuliwa “
“ unajua aliemuua baba yako ?”
“ hapana , na nipo hapa nchini kwa ajili ya kujua ni nani aliehusika kumuua baba yangu “
“walio husika kumuua baba yako ni U-97”
“U-97?”
“ ndio Ni ufupisho wa unity 97 au UMOJA NAMBA TISINI NA SABA “
“ ndio nini madam ?”
“hii ni taarifa fupi ya UMOJA NAMBA TISINI NA SABA ,” alinipa flash
“ kwa muda wako utapitia na utaelewa nusu ya umoja huo”
‘ lakini niseme kwamba sababu ya baba yako kufariki kwasababu alijua mambo ambayo hakutakiwa ajue , kiufupi alikuwa amejua karibia nusu ya umoja namba tisini na saba na hio ndio iliompelekea kuchomwa sindano ya sumu “
“ ilikuwaje baba yangu akajua yote hayo ?”.
“hio ni taarifa utakayo ipata kwenye mafaili utakayokuta kwenye hio flashi , inahusu mchakato mzima wa umoja huo hapa nchini , lakini jambo lilolofanya baba yako kufatilia umoja huo ni kutokana na amri kutoka kwa raisi bendera , kwani mheshimiwa alijua kuwa taarifa ya awali aliokuwa nayo juu ya umoja NAMBA TISINI NA SABA ilikuwa sio sahihi , kulikuwa na mambo ya ziada na ndio yaliompelekea baba yako kuanza kufatilia na pale alipokuwa akiukaribia ukweli ndipo alipo uwawa “
“ madam kwakweli ndio naanza kujua , na jambo hili limenishangaza mno , lakini linaonekana kuwa kubwa mno “
“ sio jambo dogo sabi na ndio maana upo hapa , sisi unaotuona hapa tupo hapa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujua ni nini maana ya umoja huu ndani ya nchi yetu lakini pia kuundoa kabisa , na hilo ndio jukumu la MZALENDO .
“hili nifaili lenye taarifa zote zinazohusiana na mzalendo “ alinipatia flashi nyingine .
“ mwisho , nadhani umepokea mafunzo ya kutosha hivyo jiandae kwa mapambano ya kuendeleza kile ambacho baba yako hakukimaliza “
“ nina swali madam “
“ mh”
“wakati baba yupo hatua za mwisho za uhai wake alinipa namba ambazo nilipiga simu , na kupitia namba hizo nilipata kupokea maelekezo ya kwenda nchini Thailand , nataka kujua kama na nyie mnahusika juu ya namba hizo ?”
“ hizo namba hazipo chini ya mpango wa MZALENDO bali zipo chini ya mpango X(tunauita mpango x kwasababu hatuujui jina ,, rejea ripoti Ajenti zakayo ).
“mpango x ?”
“ ndio , kwa taarifa za awali mpango huu ulikuwa ukiratibiwa na Daniel mtalemwa na marehemu bruno lamberk , na mpaka sasa hatujui juu ya mpango huu mpaka mtu ambae tunatarajia atakuja kuendeleza “
“ kuna mtu ambae ameandaliwa juu ya mpango x?”
“ Damiani Rabani “.
“Damiani Rabani ?”
“ unamfahamu ?”
“ ndio nimekutana nae nchini Thailland akiwa na historia inayofanana kiasi kama yangu , lakini kuna mambo ambayo tulikuwa tunatofatiana , tulikuwa marafiki , lakini kwasasa yupo nchini China “.
“ni vyema kama mlionana , huyo ndie mtu tunaemtegemea ili sisi kama wana umoja huu wa MZALENDO tuanze kazi na mimi nipo kama kivuli tu kwani kazi yangu itakamilika pale damiani atakapo kidhi vigezo vya kuwa kiongozi wa MZALENDO , lakini wakati tunamsubiria damiani kuna misheni yako ya kwanza ambayo unapaswa kuifanya “
“ misheni gani hio madam ?”
“ unapaswa kuingia ikulu ili iwe rahisi ya kuwasiliana na mimi “.
“ kuingia ikulu ?”
“ndio , unapaswa ufanye juu chini mheshimiwa raisi akuamini na hatimae kukupa uongozi ndani ya ikulu hio itafanya kazi yetu kuwa rahisi “
.”litawezanaje hilo ?”
“ mpango wa misheni hio ushaandaliwa , na maelekezo yote utapewa na mpaka sasa nikwambie sina la ziada la kuongea na wewe kila kitu utakielewa kupitia hizo faili ,”
Madam wema baada ya kuongea maneno hayo aliondoka , na mimi nilizungushwa ndani ya kambi hio ya MZALENDO na kuangalia kila kitu kilichokuwa kikipatikana humo , kiufupi ni sehemu ambayo ilikuwa ikijjitegemea sana , kwani ilikuwa na kila kitu kwanzia maswala ya kiteknolojia , siraha , mpaka sehemu za kufanyia mazoezi .
Baada ya hapo nilirudishwa mjini huku nikiambiwa eneo hilo nitafika kwa mwaliko maalumu .
ITAENDELEA
SEHEMU YA 73
THE LIST(ORODHA )
Baada ya kutoka hapo nilielekea moja kwa moja hotelini ,sikutaka kufika nyumbani moja kwa moja , nilienda hotelini , nilikuwa na hamu kubwa ya kujua nini kipo ndani ya hizo faili ambazo madam wema alinipatia , nilitaka kujua Zaidi kuhusu huu UMOJA NAMBA TISINI NA SABA ,.umoja ambao umehusika na kifo cha baba yangu .
Baada ya kufika hoteli ya Landmark niliweka makazi hapo kwa siku moja ili kufatilia swala hilo , baada ya kukaa nilitoa laptop yangu ya kampuni ya apple na kisha nilichomeka flash ile na kufungua , na ni kweli nilikutana na faili la U-97 katika faili hili kulikuwa na mambo kadha wa kadha yaliofanywa na raisi bendera katika kutokomeza umoja huu , huku jambo kubwa la umoja huu lililokuwa likijulikana ni swala la madawa ya kulevya , kwani umoja huu ulihusishwa na madawa ya kulevya , jambo ambalo lilinishangaza ,.
Nilishangaa Zaidi baada ya kuona moja ya watu ambao walikuwa wapo kwenye umoja huu akiwemo raisi mstaafu Athumani Ndalu , lakini pia na viongozi wengine pamoja na matajiri .
Lakini pia ripori ilionesha iliishia kutoa hitimisho kwamba umoja huu sio kama Tanzania tunavyoufahamu , Brigedia Mboneche na mheshimiwa bendera ndio wanaujua undani wa umoja huu kwani wao ndio waliokua na ripoti kamili ya umoja huu . lakini ukweli huo umeambatanishwa kwenye nyaraka ambazo haijulikani ni nani amekabidhiwa nyaraka hizo ambazo zimepewa jina kama KAULI YA MWISHO YA RAISI KABLA YA KIFO.
Hio ndio ripoti iliokuwa kwenye flash , baada ya kumaliza kusoma ripoti hio huku moyo wangu ukienda mbio , kwani japo nilitarajia jambo ambalo naenda kukumbana nao lilikuwa jambo kubwa , lakni sikuwa nikidhania kuwa jambo hilo litakuwa kubwa namna hio .
Niligeuka kwenye faili la MZALENDO
Taarifa iliopo kwenye faili hili ilikuwa ni siku kamili ya kuanzishwa kwa umoja huu ambapo ilikuwa ni mwaka wa nne wa awamu ya kwanza wa utawala wa raisi bendera , huku mwanzilishaji akiwa yeye mwenyewe ,sababu za kuanzishwa kwa umoja huo ni kutokana na kwamba ndani ya usalama wa taifa(TSS) kulikuwa na mashushu wengi wa U-97 hivyo jaribio lolote la kuondosha umoja huo lisingefanikiwa hio ilikuwa sababu kuu , lakini kigezo cha kuwa MZALENDO kilikuwa ni watu ambao hawajawahi kuhudumu katika fani ya usalama wa taifa, yaani vijana wapya , huku sababu ya kuhusisha vijana hao ni ili kuhakikisha kuondosha umoja huu unafakikiwa pasipo ya maadui kujua mienendo yao .
Pia kulikuwa na orodha ya watu kumi ambao ndio agent wa MZALENDO watakao husika katika kuiondosha U-97 ndani ya taifa la Tanzania , huku katika orodha hio jina langu lilikuwepo , na la damiani , Janeth , Merina sosteness , Patrick henry mushi , Abasi shayo , Zakayo , Elvice benard , Pancho na Karim .
Hayo ndio majina ya watu wanaohusika na orodha ya MZALENDO na kiongozi katika orodha hio alikuwa ni damiani rabani(akikidhi vigezo) .
Hakukuwa na kingine cha ziada .
Basi baada ya siku kadhaa kupita ndio nilipatiwa mpango wa misheni ya kuingia ikulu , tukio la misheni hii lilikuwa likifanyika siku ambayo ni maazimisho ya miaka hamsini ya ndoa ya mheshimiwa raisi na madam wema , na ndani ya tukio hili nilihitajika kupigwa risasi kumlinda raisi , na mtu atakae tekeleza tukio hilo alikuwa ni bwana karim , mtaalamu wa maswala ya kuendesha drone.
Hilo ndio tukio lililotokea siku ile sasa kama unakumbuka ,, ilikuwa ni misheni maalumu ya mimi kuingia ikulu .
Kwenye moja ya vitu vilivyonisisimua Zaidi ni teknolojia ambayo ilikuwa ikimilikiwa na MZALENDO teknolojia ya kijivika sura ya mtu mahali popote pale baada ya kufanya tukio na ndio maana hata suzzane alishindwa kujua ni nani haswa muhusika wa matukio yale baadala ya kukamata watu wengine ambao hawakuwa wakihusika , hio yote iliwezeshwa na teknolojia iliokuwa ikijulikana kwa jina la FTP( FACE TEMPO PICKER ).
****
“ nadhani mpaka hapo utakuwa umeelewa sasa nilivyosema , kuwa wewe ndio kiongozi wetu “.
“ ndio sabi”
“ kukutana kwetu kulikuwa kwa bahati sana nchni Thailland , kumbe kuna watu waliokuwa wakituangalia muda wote “
“ ni kweli kabisa sabi , tunakazi kubwa sana ilioko mbele yetu “ .
“tena kubwa sana , umoja huu upo ndani ya serikali hivyo itakuwa ngumu sana lakini inawezekana “
“ nadhani tutaongea siku zijazo , lakini kwa usalama wa kile tunacho kifanya inabidi tusionekane kuwa na ukaribu “.
“ ni kweli kabisa , kwa haya yanayo endelea inabidi tuwe makini sana , huu umoja unaonekana upo kila mahali “
“ nina mambo mawili ambayo yamenifanya kukutafuta damiani “ aliongea sabi , na huo ni muda ambao damiani alinyanyuka kwenda kuchukua chupa yenye mvinyo na kumiminia sabi kwenye glass na yeye kwenye glass .
“ nadhani huu utakuwa wakati mzuri wa sisi kuongea hayo mambo “ aliongea sabi huku akitabasamu , alikuwa akikumbuka mengi waliofanya wakiwa na sabi nchini thailland , japo alikuwa na wasiwsi juu ya sabi , lakini kutokana na hsitoria yake sasa alikuwa akimuamini sana , na damu yake ilikuwa ikitembea kwa kasi kila anapokumbuka collabo watakayo enda kufanya kutokomeza UMOJA NAMBA TISINI NA SABA .
“ la kwanza ni juu ya merina “ aliongea sabi na kumfanya damiani akae vizuri .
“ vipi kuhusu merina , unamfahamu ?”
“ ushasahau kwamba na yeye yupo kwenye orodha ya MZALENDO ?”
“sijasahu , lakini sidhani unachotaka kusema kinahusiana na hilo ?”
“ ni kweli , ni juu yako wewe na merina .. namaanisha uhusiano wenu “.
“ kwanini unauliza hivyo sabi ?”
“yule mwanamke anakupenda damiani na hilo ni jambo ambalo linanitia waswasi mpaka sasa “
“Nalifahamu hilo , lakini kwanini likutie wasiwasi , ni jamnbo la kawaida kumpenda mtu “
“ kumpenda mtu au kupendana ?”
“ unamaanisha nini ?”
“ nataka kujua kama wewe pia unampenda “ aliongea sanbi na hapo alimfanya damiani aanze kujifikiria ,, kiufupi hakutegemea swali kama hilo mapema namna hio , hata yeye alikuwa hana uhakika kwamba alikuwa akimpenda sana merina kama yeye anavyompenda .
“ndio “
“ ndio nini damiani ?”
“ umeuliza kama nampenda .. ndio nampenda “ sabi alijikuta akivuta pumzi .
“ unamfahamu patrick mtoto wa raisi henry “.
“ ndio namfahamu ?”
“ anampenda sana huyo mwanamke , na yupo tayari kufanya lolote lile ili awe na merina , na anajua uwepo wako hapa Tanzania na yupo tayari kukupoteza ili awe na merina ,, hilo ndio swala linalonipa wasiwasi “.
“damiani wewe ni rafiki yangu na Patrick pia ni rafiki yangu , namjua sana Patrick na anachozungumza nina uhakika anamaanisha , hivyo naomba swala hili ulifikirie kwa mapana yake pasipo kuacha kitu chochote kinachohusu maisha yako kwa sasa , maamuzi utakayofanya naamini yatakuwa na tija kwenye mpango wetu , hilo nadhani ndio kipaumbele kwa sasa “ aliongea sabi
“ nitalifanyia hilo kazi sabi , usiwe na shaka “ aliongea damiani na sabi aliitika kwa kichwa .
“ swala la pili ni wewe kuwa stephano lamberk , na damiani kwa wakati mmoja , najua teknolojia imekuwa sana na safari yako ya china nadhani ilikuwa ya mafanikio makubwa sana “
“ China imeendelea sana katika swala zima la teknolojia sabi , mimi mwenyewe sikuamini mara ya kwanza lakini , niseme mpaka sasa naiogopa sana teknolojia , kwani kitendo cha mimi kuja nchini kwa jina la stephano lamberk mwenywe ni swala ambalo linanifanya kila mtu ninaemuona nione ni feki “
“ hahaha.. kwakuwa wewe mwenyewe ulikuwa feki “
“ ndio “
“sina muda sana lakini utanieleza kwa kina juu ya hilo, lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba suzzane mpaka sasa anajua stephano lamberk ni damiani , japo hana uthibtisho lakini ana uhakika “.
“nililitegemea hilo sabi na nimejiandaa vyema “
“ ni vizuri sasa kama utajiweka wazi kama damiani na sio stephano lamberk tena “
“ni kweli kabisa “
“hii ni barua kutoka ikulu , mheshimiwa anahitaji kuonana na wewe siku ya kesho “
“ anahitaji kuonana na mimi ?”
“ ndio sijui ana dhumuni gani , laakini hakikisha unafika “
“ nitafika “
Basi baada ya maongezi hayo sabi aliondoka na kurejea ikulu , kwani kazi iliokuwa imempeleka hapo alikuwa ashaimaliza .
******
“okey merina , unaweza ukaniambia , mahusiano yako na damiani yalianza lini ?” lilikuwa ni swali kutoka kwa janeth kwenda kwa merina , na merina alijikuta akishindwa kujibu swala hilo , kwani ni kweli mpaka wakati huo ni kama yeye ndie aliekuwa akimpenda damiani pasipo kujua kuwa mwanaume huyo alikuwa akimpenda pia , hivyo hata swala la uhusiano , lilikuwa hata halijaanza na hivyo jibu hakuwa nalo .
“hilo swali siwezi kujibu ni maswala yangu binafsi , na nimekuja hapa kuongea na damiani sio wewe professa “ aliongea merina na kumfanya janeth akunje nne na kufanya kijisketi alichovaa kionyeshe mapaja yake yalio nona, na kama wewe ni mwanaume rijali ungewaona warembo hawa , basi ungeishia kusema kwamba kijana damiani ana bahati sana .
“okey merina , ni kweli naweza nisipaswe kujua , mahusiano yako na damiani , lakini mbona damiani hajawahi kukutaja kama ashawahi kuwa na mpenzi anaeitwa merina “ janeth hakutaka kuwa mzembe na yeye alirusha kombora .
“ mpaka akutajie , wewe ni nani yake , hayo ni mambo yake binafsi na wewe ni mfanya kazi wake , kwanini akuambie maswala yake yanayohusu mahusiano “
“ siwezi kuweka mambo yangu binafsi kwako pia , lakini kukuambia tu ni kwamba mimi na damiani mapenzi yetu yalianzia nchini China , na mpaka sasa tunaendelea “.
“unasemaje ?” merina aliuliza hilo swali huku tayari machozi yakiwa yashaanza kumtoka ,moja ya sifa ya mwanadada huyu ni kuwa na machozi ya karibu .
“ndio hivyo merina , nisamehe sijakusudia kukuumiza , lakini naamini wewe na damiani sio wapenzi ,kwani hajawahi kukutaja na isitoshe muda wote alikuwa akikuona hapa kwa sura ya stephano lamberk, unafikri angekuwa anakupenda angejificha kwako “.
Maneno aliongea janeth yalikuwa yamemuingia vyema sana merina , na kila neno alilolizungumza kwake aliona ni ukweli mtupu , hakuwa na lingine la kuongea zaidi ya kunyanyuka nakuondoka huku akijikaza machozi yasimtoke , kwani hakutaka kuonana na wafanya kazi wa kampuni hio akiwa na machozi .
Baada ya merina kutoka hapo alikimbilia gari yake , na baada tu ya kuingia alishindwa kujiuzia kwani alianza kulia kilio cha kwikwi , alikaa hapo kwa muda wa madakika kadhaa huku janeth aliekuwa juu ya goroa akimwangalia .
Baada ya madakika hayo alilitoa gari na kuelekea nyumbani kwake, japo alikuwa na maumivu moyoni lakini alijitahidi kuendesha gari kwa umakini ili asije akasababisha ajali.
****
Damiani mara baada ya kuachana na sabi , jambo moja ambalo alikumbuka kulifanya wakati huo ni swala la kuangalia kilichomo kwenye ile flashi aliokabidhiwa na madam wema , alikuwa na hamu mmno nakujua ni kipi bruno alimuachia , hivyo alitoka hapo sebleni na moja kwa moja alielekea kwenye chumba chake.
Baada ya kufika alitoa flash ile kwani alikuwa ameihifadhi kwenye kabati na kisha akaisogelea tarakishi yake iliokuwa ndani ya chumba chake hicho kwani kuna sehemu aliokuwa ametenga kama kijiofisi.
Baada ya kuichomeka , alienda moja kwa moja kuifungua flashi hio na hapo ndipo alipokutana na faili moja tu lililoko kwenye mfumo wa ‘zip’ yaani limefungwa , alijaribu kufungua faili hilo lakini alishindwa kwani lilikuwa likihitaji password kulifungua.
Alitulia kwa madakika kadhaa akifikiria password gani ya kuingiza hapo , na hapo ndipo alipokumbuka nyaraka alizopewaga na bruno , alizifata kwenye ‘safe box’ na kuzitoa kisha kaingiza password ambayo ilikuwa ikitumika kwenye kadi ya benki ya CRDB bank na ni kama aliotea vile kwani faili lile lilifunguka.
Kwa hamu kama zote za kutaka kujua nini kipo kwenye faili hilo aliangalia , na kitu alichokuta ilikuwa ni file kwanza lilikuwa na jina lililokuwa limeandikwa SELLINE AMBER , jina ambalo mara baada ya kulisoma tu alikumbuka aliliona kwenye nyaraka za mwanzo kabisa alizokuwa amepwa na bruno.
Alifungua faili hilo ambalo lilikuwa kwenye mfumo wa ‘Document ’ na kitu ambacho kilimshangaza ni kwamba faili hili lilikuwa na KB moja tu ukubwa wake , lilifunguka na ndani ya faili hilo kulikuwa na neno moja tu lilikuwa limeandikwa kwa herufi kubwa .’DANTE – CHEST CARD ( TANZANIA SWISS BANK BRANCH )’
Hayo ndio maneno pekee yalioandikwa kwenye faili hilo ,kwa mara ya kwanza alianza kujiuliza maneno hayo yalikuwa yakihusu nini , lakini hakuelewa kwa mara moja ,alikaa na kuanza kufikiria na nikama kuna kitu alikuwa akikimbuka lakini kilikuwa kinakuja na kupotea , kila alipo jaribu kukumbuka , alishindwa kabisa .
“ huenda kuna ‘clue’ kwenye hizi nyaraka za bruno “ aliongea na kisha alitoa kila kitu akaangalia kimoja kimoja kwenye zile karatasi alipita lakini hakupata jibu , na wakati akiendelea kusoma zile karatasi kuna jambo alilikumbuka na kujiona ni kama mjinga , alikumbuka kadi ya uswisi ilikuwa kwenye nyaraka hizo , haraka haraka aliangalia kadi hio na neno la kwanza kuliona lilikuwa ni ‘ DANTE’.
“ Yess ni hii “ aliongea
“chest card kadi ya kuhifadhia vitu vyenye thamani benki, hii sio kadi ya ATM ni chest card” alijiongelesha .
Baada ya kuvumbua fumbo hilo hap hapo aiingia , mtandaoni na kutafuta neno DANTE SWISS BANK IN TANZANIA na ndani ya muda mfupi alikuwa amepata kila kitu mpaka eneo husika .
Sehemu yenyewe ilikuwa ni ndani ya jengo la TPA sokoine , hakutaka kuchelewa alijiandaa dakika chache na kisha aliingia kwenye gari lake akiwa na sura ya stephano lamberk na moja kwa moja alielekea posta , ndani ya madakika kadhaa alikuwa nje kabisa ya jengo hilo akiegesha gari , alienda floor ya chini na kuangalia sehemu bank hio inapatikana floor ipi na aliona ipo floor namba saba , aliingia kwenye lift na kuja kutokezea kwenye floor hio , na kulikuwa na wafanyakazi wachache na baadhi ya watu ambao walionekana wapo mahali hapo kwa ajili ya huduma , hakujihangaisha nao , kwani alienda moja kwa moja mapokezi na kuulizia utaratibu huku akitoa ile kadi na mwanadada yule alievalia sare zake , huku akipendezeshwa na miwani , aliiangalia na kisha alimpa maelekezo ya kwenda upande wa kulia , sehemu ambayo kulikuwa na mhudumu mwingine ambae alikuwa na tarakishi kubwa akionekana kuwa bize , baada ya kufika alitoa ile kadi na kisha alimpatia na bwana yule wa kiume alivalia tisheti ambayo ilikuwa na nembo ya benki hio , aliafanya yake na ndani ya muda mfupi alikuwa ashamaliza .
“ nifate tafadhari , aliongea bwana yule kwa heshima kabisa kwani alkuwa akimjua bwana stephano lamberk kwa pesa zake , hivyo alikuwa akimnyenyekea .
“ ni hapa boss wangu ,, namba za boksi ni hizo mbili za mwisho kwenye kadi yako , utaingiza hio kadi na boksi itafunguka “
“ nashukuru “
Damiani baada ya maelekezoo hayo aliingia na kweli alipata boksi ile na aliingiza kadi kwa maelekezo yale na ndani ya dakika aliambiwa aingize namba ya siri na hapo ndipo alipo babaika kwani alikuwa hajui , ila aliona aingize namba ile ile ya mwanzo ya CRDB na ikakubali .
Baada ya kukubali tu boksi ile ilifunguka na ndani kulikuwa na bahasha moja tu ya khaki , alichukua bahasha ile na kisha akatoka nayo na moja kwa moja alienda mpaka kwenye gari yake , na baada ya kuingia tu alitoa vitu vilivuyomo mle ndani .
Ilikuwa ni hati ya nyumba iliokuwa inajina la bruno lamberk nyumba iliokuwa ikipatikana eneo la mbezi beach , lakini pia kulikuwa na picha kama picha ya mlima Kilimanjaro halafu chini yake kulikuwa na maandishi kama tarehe lakini sio tarehe , zilikuwa ni herufi ukiangalia kwa umakini na damian kwa akili yake haraka haraka aligundua ni passcode .
“aliwasha gari na hapo nia yake kubwa ilikuwa ni kwenda moja kwa moja eneo la mbezi beach , aliendesha gari yake kwa spidi kidogo na ndani ya madakika kadhaa alikuwa eneo hilo , na kwakua hakua mzoefu sana alienda moja kwa moja mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa , na akamuonesha hio hati , mwenyekiti wa mtaa huyo alikuwa ni bwana mmoja mfupi mwenye kitambi .
“karibu sana , tulikuwa tukikusubiri “ aliongea bwana huyo na kumfanya damiani ashangae , lakini hakutaka kuongea mengi , kwani bwana yule aliinuka na kuongozana na mzee yule alietembea kwa shida na kitambi chake , na kama dakika tano walikuwa kwenye jumba moja kubwa sana lilokuwa upande wa kulia upande wa kaskazini kutoka baharini .
“ni hapa mheshimiwa “ aliongea mzee yule
“ na damiani aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti kumi na kumpatia mzee yule , na mzee alikenua hadi jino la mwisho .
Damiani aliingia kwenye nyumba hii ambayo ilikuwa kabisa na mlinzi , na ndani ya nyumba hii ilikuwa na mandhari nzuri kabisa , akifatana na yule mzee .
“kuna mtu anakaa hapa ?”
“ hapana , ila tulikuwa tukiifanyia usafi mara kwa mara kwani ndio maelekezo kutoka kwa mwenye nyumba aliotuachia “
“kuna maelekezo mengine ?”
“ hakuna ni , wewe ndio mwenye nyumba yako na kwasasa tunakukabidhi kila kitu na mkataba wetu wa kuiangalia nyumba hii umeisha leo “
“ basi nashukuru “
Basi mzee yule aliondoka na kumuacha damiani akianza kuangalia mle ndani , ilikuwa ni moja ya nyumba nzuri sana ,na kubwa ya kisasa , yenye gorofa tatu kwenda juu , mwenyewe aliisifia hio nyumba , ile ya kwake ya makongo juu haikuwa nzuri kama hii .
Aliingia ndani huku akipokelewa na fanicha(samani) , kuna kitu alikiona chini , yalikuwa ni maganda ya kondomu pamoja na chupa za bia , na moja kwa moja alijjua lazima yule mzee kama sio yeye basi kuna watu aliokuwa akiwapa waje kufanya yao humo ndani , kwani nyumba ilionekana kabisa ilikuwa inakaliwa na mtu , lakini hakutaka kujisumbua Zaidi juu ya hilo .
Kwani kwa siku hio jambo lililompeleka hapo lilikuwa ni jambo moja tu , kujua picha ile inamaanisha nini , aliingia kwenye vyumba baadhi , na chumba cha tatu kuingia ndio chumba alichokutana na picha ile ya mlima Kilimanjaro , hiki kilikuwa ni chumba ambacho alikuwa akilala bruno , ni chumba kikubwa kweli na cha kisasa mno .
Alitoa ile picha ya ukutani , na hapo nipo alipokutana na sehemu ya kuingiza namba , aliingiza namba zilizokuwa kwenye ile picha na ndani ya dakika kadhaa tu sehemu ile ilijitenga na kutengeneza mlango kama wa lift , jambo ambalo lilimshangaza damiani , kwani muda huo alikuwa yupo gorofa ya mwisho juu .
Aliingia ndani na lift ile ilianza kushuka taratibu na ni sekunde kadhaa ilisimama na kufunguka na mbele yake kulikuwa na mlango ambao haukua na komeo wala ila pembeni yake ulikuwa na sehemu ya kuweka kidole yaani fingerprint damiani alijaribu kuweka .
“ACCESS DENIED PLEASE ENTER SECURITY BY PASS CODE “ maandishi yalisomeka na hapo damiani ndipo alipojua kuwa zile password zilikuwa ni za kubypass hio system .
Aliingiza na hapo hapo mlango ule ulifunguka .
“WECOME IN LEGACY ROOM DAMIANI RABANI
ITAENDELEA JUMAPILI MCHANA NICE WIKIEND
NO: 0687151346 Watsapp
 
mnamlipa ?? au unafikir rahis ti kuweka hapa? tulia ataieka tu
Shukrani mkuu .. hawaelewi niliahidi simulizi inaendelea wikiend na nimetimiza ahadi kabla hata ya wikiend kuanza
 
SEHEMU YA 74
DAMIANI MISSIONS( MISHENI ZA DAMIANI )
Upande mwingine , alionekana bwana sam au rich sam akiingia ndan ya jengo la LAPF jengo lililkuwa likipatikana ndani ya eneo la Makumbusho sayansi , bwana huyu mara baada ya kuingia ndani ya jengo hili akiwa na gari yake aina ya Prado, baada ya kupaki moja kwa moja alielekea ndani nya jengo hili .
Ndani ya sekunde kadhaa tu alikuwa ndani ya floor ya kampuni ya KILAC , kampuni iliokuwa ikimilikiwa na bwana kimbona .
Baada ya kufika mapokezi aliruhusiwa moja kwa moja na kwenda kuonana na kimbona kwani alikuwa na miadi naye .
“ karibu sana sam “
“ shukrani ndugu yangu “
“tokea siku ile tuachane hatujaonana Zaidi ya kuwasiliana kwenye simu “
“ ndio ni kweli , na ndio maana nimekuja hapa , japo kuna mambo ambayo nataka kujadiliana na wewe , lakini ni vyema pia tumepata nafasi ya kuonana “
“ jambo gani hilo , nadhani sio jambo dogo “
“ si kubwa sana lakini pia sio dogo sana “
“ nakusikiliza ndugu yangu “
“ ni juu ya mpango zero “
“ mpango zero , kuna shida gani si upo chini ya INNOVA?”
“ ni kweli mpango huu upo chini ya INNOVA , lakini wasimamizi wakuu ni sisi tuliopo ndani ya Tanzania”
“ kuna nini juu ya huo mpango ?”.
“ nilikuwa na kikao na wahandisi wa mpango huu , na ili jambo hili kufanikiwa lazima kuwe na majaribio , na majaribio hayo hayawezi kufanyika tu mahali popote “
“ majaribio hayo ni majaribio gani umeniacha mbali mpaka hapo ?”
“ sijajua kwa kina majaribio hayo ni ya aina gani , ila kampuni inahitaji watu wa majaribio “
“ watu wa majaribio ?”
“ ndio , inahitaj watu wa majaribio , lakini watu hao wanaweza kufariki wakati majarbio hayo yakiendelea “.
“ kwa hapo swala hilo ni gumu kwani hatuwezi kuwapeleka watu katika kifo kwa hiari “.
“ndio maana niko hapa , nadhan mpaka hapo umenielewa “
“kwa hio kipi kifanyike , na ni watu wa aina gani wanahitajika ?”
“ wanasema wanahitaji kwanza vichanga kwa awamu ya kwanza kati ya umri wa miezi sia kuendelea mpaka mwaka mmoja , wanahitaji watoto jumla hamsini “
“ hamsini ?”
Kimbona alijikita akitoa macho , watoto wachanga hamsini ni wengi mno , watatoka wapi watoto hao , hilo ndio swali la kwanza lililoingia kwenye kichwa chake .
“ ni wengi mno , tutawapataje sam ?”
“swali hilo ni zuri kimbona “
“ kuna karatasi kutoka makao makuu ya U-97 imekuja , na imeeleza namna ya kuwapata watoto hao ndani ya Tanzania , lakini karatasi hio lazima isainiwe na Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania na pale itakapo sainiwa moja kwa moja zoezi hilo litaanza “
“ sasa hio karatasi inaeleza nini jinsi ya kuwapata?”.
“bado sijaisoma , lakini muda si mrefu fomu hio italetwa kwenye kikao kitakachofanyika siku chache zijazo , na hio ni baada ya raisi kusaini na kutia muhuri wa barua hio “
“ raisi atasaini kweli , maana hilo swala la vichanga kufanyiwa majaribio ni gumu mno , maana watapatikana wapi?”
“ linaweza kuwa gumu , lakini lazima asaini kwani na yeye yupo ndani ya umoja , na akikiuka maagizo inamaana anakitafuta kifo , na kwa ninavyomjua henry hawezi kukubali kifo “.
“hapo ni kweli , lakini swala hili hata kwa mimi mwenyewe linanipa ugumu sana , huu mpango unaohitaji vichanga ni mpango gani kwanza ?”.
“hilo siwezi kujua kimbona , na nipo hapa kwasababu katika kikao hicho sisi tunaowakilisha wenzetu lazima tutie na sisi sahihi katika karatasi hio ya mkataba “
“ kutia saini tena “.
“ ndio , na hio ndio kazi niliopewa , kuwashawishi wana umoja wote asitokee hata mmoja wa kupinga jmbo hilo , kwa hio kimbona jiandae kwa siku hio “
“mmi nitasaini “ aliongea kimbona na kumfanya sam atabasamu .
“ nilijua utasaini “
“ hahahaha.. unaonekana kunifahamu vyema “
“ ndio maana sisi ni marafiki “
“ ni kweli “.
*****
Damiani alijikuta akipigwa na butwaa , baada ya kuingia ndani ya chumba hiki , hakikuwa chumba , kwani kilionekana kama maabara Fulani hivi yenye teknolojia ya hali ya juu mno ,, mwonekano wa chumba hiki ulikuwa ni wa kipekee ,uliopendezeshwa na tarakishi zilizokuwa zimpangiliwa kwa mpangilio mzuri huku zikiwa zinawaka , lilikuwa ni jambo la kushangaza mno kwa kijana damiani , kwani hakutegemea kama kuna sehemu ndani ya Tanzania yenye chumba kama hicho, chumba hiki kilikuwa kipo chini kabisa ya ardhi kwani hakukuonekana na dirisha lolote Zaidi ya mwanga flani wa rangi ya blue ( ultravilot light ) uliokuwa ukikimulika chumba hiki .
Lakini kilichomshangaza Zaidi , kulikuwa na roboti lililokalishwa kwenye kiti , likiwa na muonekano flani hivi wa kama sanamu zile za budha , lakini lilikuwa na macho flani yanawaka taa , huku likiwa na uwezo wa kuzungusha kichwa , lilikuwa likitoa sauti lakini midomo haikucheza , lakini cha kushangaza Zaidi ni kwamba roboti hili lilikuwa na uwezo wa kuzikotrol tarakishi zote zilizokuwa ndani ya chumba hiko ( LEGACY ROOM )
“Mister Damiani Rabani you can ask me anything
( Unaweza kuniuliza jambo lolote Damiani Rabani)
“wewe ni nani ?”.(Who are you)
“I am designed to assist you in all plan X missions you can call me Miss Nara
Nimetengenezwa ili kukusaidia kukamilisha misheni zote za mpango X unaweza kuniita Miss Nara )
“Nani aliekutengeneza ?”(Who created you)
“Bruno lamberk “.
“What is all about Plan X missions(Mpango X ni mpango gani?)
“Once you reach your final mission you will be informed , remember this is plan X , all deatails is concealed”(Utafahamu mpaka pale utakapofikia misheni ya mwisho ya mpango x , kwasasa ni mpango usiofahamika , na ndio maana unaitwa mpango x)
“ Why am I chosen to do those missions ?”(Na kwanini nifanye hizo misheni? ).
“Because without doing so , you won`t achieve your goals (Kwasababu pasipo kufanya hivyo hutoweza kukamilisha malengo yako)
“What do you know about my goals”(Unafahamu nini kuhusu malengo yangu?”)
“Taking revenge against peaple who involved with your mother`s death”(Kulipiza kisasi dhidi ya watu waliohusika na kifo cha mama yako).
“How did you know about death of my mother when the one created you died the same day and time wth her.( Wewe umejuaje mama yangu amekufa wakati , aliekutengeneza hajakupa hizo taarifa kwani alifariki siku aliokufa mama yangu ?”)
“I am created to have all informations about you Mister Damiani Rabani, I am the one who was instructing through all your steps Damiani (nimetengenezwa kujua vitu kuhusu wewe Mister Damiani , na mimi ndio niliokuwa nakupa maelekezo muda wote”
“Which instructions?”(Maelekezo gani)
“Ask yourself about that Damiani , To give you the hint: This is all of your calling logs, See if I am wrong”(Jiulize kuhusu hilo Mister Damiani , hizi ni taarifa zako zote siku , saa na sehemu uliopiga simu)
Damiani alijikuta akiangalia zile ‘calling logs’ na alijikuta akijua mtu aliekuwa akiwasiliana nae na kumpa maelekezo ni hili roboti linalojiita NARA.
“Vipi kuhusu mwanaume aliekuwa akinipa maelekezo”
“Those are real people staged to help you to accomplish the missions”( hao ni watu halisi , na wapo kukusaidia kukamilisha misheni zako)
“Can i identify them ??”(Naweza kuwajua ?)
“That is beyond informations available, but you will know them with plan X missions accompishiment” (Lipo nje ya uwezo wangu , lakini utawajua baada ya kumamilisha mpango x)
“How can I work with unknown people?(Nitafanyaje kazi na watu ambazo siwafahamu)
“With my help everything is possible Damiani( inawezekana kwani nipo mimi nitakaekusaidia)
“How about Sabi Mboneche (Vipi kuhusu Sabi mboneche?”)
“He is part of Plan X (sehemu ya mpango x)
“Unajua nini kuhusu Mzalendo ?”
“That info ..is unavallable”( Hio taarifa haipo )
Damiani baada ya kupokea hilo jibu alijikuta akishangaa , kwani alichokuwa akijua ni kwamba mzalendo ulikuwa pia unahusiano na mpango x , kwani kwenye maelezo ya sabi , |Madam wema alimwambia kuwa mpango x unamuunganiko na mzalendo , iweje taarifa muhimu kama hio haikuwepo , alijikuta akishangaa mno , lakini alijiambia huenda kuna sabau ya taarifa hio kutokuwepo hapo ndani.
“When am I to get started with those missions) ( ni wakati gani natakiwa kuanza hizo misheni)
“Within those document your are provided with Bruno, there ninety names in order you have to identify the frst name so as I can help you with killing map(Katika nyaraka ulizopewa na Bruno kuna karatasi moja ina majina tisini unatakiwa kutambua jina la kwanza ili nikupe ramani ya kufanya mauji)
Damiani alijaribu kukumbuka juu ya hii nyaraka , na ni kweli aliikumbuka vyema , kuna nyaraka ilikuwa na majina karibia tisini lakini hakuwahi kuyasoma na leo ndio anakumbuka kuwa majina hayo hakuwahi kuyasoma .
“How about those names”( nini kuhusu hayo majina ?)
“Those are what is missions of plan X , you have to kill those people as they are listed in Ascending order” (Ndio misheni zako ndani ya mpango X , watu walioko kwenye yale majiina wanatakiwa kuuwawa kwa mtiririko wa namba kama ilivyopangiliwa)
“Do you mean I have to kill all those people ?(Unamaanisha misheni yangu ni kuwaua hao watu)
“Yes” (Ndio )
“ And why do I have to kill them ??”(Na kwanini ni wauwe kuna sababu gani?)
“By not doing so you won`t be able to trace people who killed your mother” (pasipo kufanya hivyo huwezi kumpata mtu aliehusika na kifo cha mama yako)
Damiani alijikuta akipagawa mno , hakutaka kabisa kukaa tena ndani ya eneo hilo , kwani akili ilikuwa imetibuka Zaidi , alichojua tu ni kwamba hawezi kubishana na roboti hilo kwani sio mtu kwamba litabadili mawazo na ndio maana alitoka kwanza ili arudi kwake akaangalie yale majina , alitaka kujua kwanza watu hao ni wakina nani kabla ya kufanya maamuzi .
*******
Upande mwingine , suzzane alikuwa ashatoka nyumbani kwa sabi mbneche na sasa alikuwa nyumbani kwake , akiwa ndani ya chumba alichokitenga kwa ajili ya kazi zake za kipelelezi , mbele kabisa ya ukuta kulikuwa na picha za watu kadhaa aliokuwa akiwaaangalia huku akiwa amewawekea alama , na moja ya picha iliokuwa imewekewa alama ilikuwa ni ya damiani huku pembeni ikiwa imezungushiwa baadhi ya picha zingine na moja ya picha hizo kulikuwa na picha ya mwanadada janeth , kulikuwa na picha ya merina , kulikuwa pia na picha ya agent z (zakayo ) ,ya stephano lamberk ,kulikuwa pia na picha ya kimbona huku juu kabisa kulikuwa na picha mbili , ilikuwa moja ni ya mheshimia raisi john bendera onyango , na pembeni yake kulikuwa na picha ya bruno lamberk .
Chini kabisa ukitoka picha zilizokuwa zimemzunguka damiani kulikuwa na duara kubwa lilokuwa na x katikati na jina kwa chini yake ‘MZALENDO’.
Miss k (suzzane) alionekana kutafuta koneksheni iliopo katika picha hizo .
“Stephano lamberk ni damiani , nina uhakika na hili kwa asilimia mia moja , hawa wanaomzunguka damiani nina wasiwasi nao , mahusiano yao huenda sio ya kikazi tu , huenda kuna jambo la ziada , huyu merina anaonekana kufahamiana na zakayo , lakini pia zakayo anaonekana kufahamiani na janeth , janeth ni mtoto wa raisi bendera , najua hili sijamwambia mheshimiwa lakini huu sio muda muafaka wa kumwambia , nataka kwanza nijue anaejiita mzalendo ni nani , je kuna uhusiano wowte kati ya damiani na mzalendo , lakini bado kuna ugumu matukio wakati yanafanyika stephano lamberk hakuwa bado nchini kwa maana hio mzalendo ni mtu mwingine , mtu huyu ni nani ?, kama mtu huyu atakuwa anauhusiano na damiani basi uchunguzi wangu lazima uanzie wakati damiani anatoka nje ya nchi hii , nadhani kupitia hapo nitajua kila kitu … lakini janeth anahusikaje na Mzalendo ,kwanini achome madawa ya kimbona “.
Alifikiria agent huyu wakati huo akiwa amesimama ,alionekana kuwa na hasira kweli kila akiangalia paja lake lilikokuwa linamsumbua , alikumbuka vyema tukio la kupigwa risasi na damiani , alijua kumkamata damiani ni swala rahisi mno kwake kwani mpaka hapo alikuwa akijua damiani alikuwa akijificha kwenye kivuli cha stephano lamberk .
Wakati akifikiria hayo simu yake ilitoa mlio , ulikuwa ni ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa mtu wake anampatia taarifa kutoka ikulu , na ujumbe huo ulikuwa ukimwambia kuwa kesho kuna watu wanaenda kuonana na raisi lakini moja ya watu hao alikuwa ni bwana stephano lamberk , jambo hilo lilimfurahisha sana kwani alitabasamu.
*****
Huku upande wa ikulu raisi Henry alionekana kuwa katika wakati mgumu mno kimaamuzi , kwani muda mfupi uliopita barua kutoka makao makuu ya U-97 ilimfiikia barua ambayo ilimhitaji kutia sahihi na kufanikisha majaribio ambayo yanahitajika kufanyika chini ya mpango zero .
Kulikuwa na vipengele vya aina mbili ndani ya mkataba huo m, kipengele cha kwanza kilikuwa ni kipengele cha hiari , kipengele hichi kilikuwa kinatoa hiari kwa mwanamke yoyote kubeba ujauzito kwa njia ya kupandikizwa mbegu za kiume . lakini swala hilo lilikuwa halifanyiki bure kwa wale ambao walikuwa wakijitolea, kunakuwa na malipo ya milioni kumi kwa kila mwanadada atakae jitolea .
Kipengele za pili kilikuwa si cha hiari , kipengele hiki kilihitaji watoto wachanga ambao ni mapacha wakufanana kwa ajili ya majaribio , hii ndio sehemu iliokuwa ngumu sana na iliompa Zaidi mawazo mheshimiwa , kwani kipendele hiki kilikuwa kikimtaka atie saini ya kuibiwa kwa siri kwa watoto pacha katika hospitali kuu , yaani kama watoto hao watabainika kupotea uchunguzi wote wa kipolisi usilenge kukamata wahusika , bali ulenge kuwaridhisha wananchi kwamba uchunguzi huo unafanyika.
Swala hili lilikuwa gumu kwake ukizingatia kwamba, watoto hao wanaoenda kufanyiwa majaribio kuna mawili wanaweza wakafariki kwenye mchakato wa majaribio au wakapona.
Alisoma makataba huu, Na kisha hakuwa na sababu ya kuusaini kwa siku hio kwani aliiweka pemben huku akifikiria cha kufanya.
****
Wakati hayo yanaendelea ikulu , upande wa Damiani alikuwa yupo ndani ya nyumba yake maeneo ya Makongo juu, alikuwa ameketi kwenye sofa huku akiangalia karatasi ile iliokuwa ni sehemu za nyaraka alizoacha Bruno.
Alikuwa akiangalia majina ambayo ni wakati mfupi tu kaambiwa kwamba watu waliokuwa kwenye majina hayo wanatakiwa kuuwawa, kwake swala hilolilikuwa ni swala gumu ukizingatia na majina yenyewe.
Moja ya majina yaliomshangaza Zaidi ni uwepo wa jina la waziri mkuu mstaafu , bwana Hamduni , kulikuwa pia na jina la raisi mstaafu bwana Athumani ndalu , kulikuwa na jina la mkuu mstaafu wa polisi , bwana Kizito kabwela , kulikuwa pia na jina la kimbona , kulikuwa na jina la Sam ,Damiani aliangalia majina haya yaliokuwa yamepangiliwa katika mtiririko wa kinamba
“Hawa wanahusikaje na kifo cha mama yangu?” lilikuwa ni swali la kwanza kuingia kwenye kichwa cha kijana huyu.
“Kimbona , kimbona “ Alijikuta akitamka hili jina mara mbili , mara picha ya mama yake kupigwa risasi inaanza kumjia kichwani chake , anakumbuka maneno ya ya Marie wakati akiwa Thailland , anakumbuka moja ya watu waliokuwa wakizitaka nyaraka alizokuwa nazo , mmoja wa alikuwa ni mtu aliejiita Sam .
“Kimbona na Sam “Hawa watu inabidi niwe na taarifa zao.
Damiani aliangalia upya ile karatasi kwa mara nyingine , aliangalia majina hayo yote tisini , na katika majina hayo ni machachee sana alikuwa akiyajua , mengi yalionekana yalikuwa majina ambayo sio ya nchi ya Tanzania , kwani kuna yaliokuwa yakisomeka kwa kifaransa , kuna yaliokuwa yakisomeka kwa kichina , lakini kuna pia yaliokuwa yakisomeka kwa kijerumani .
Jina la juu kabisa ndani ya karatasi hio ambalo kwa maelezo ya NARA ni kwamba hio ndio misheni yake ya kwanza , jina hili lilikuwa likisomeka ‘ Mahmood seid ‘..
******
Ni siku nyingine kabisa , siku ambayo raisi henry alikuwa akitegema kuoanana na wageni ambao amewaalika siku hio ndani ya ikulu yake , wageni hao walikua ni stephano lamberk ambaye rasi Henry alikuwa akimjuua kama mfanya biashara ,Merina sosteness , Zakayo na proffessa Janeth .
Kama sabi alivyokuwa amepewa maagizo na raisi ndivyo alivyofanya , kwani wageni hao mheshimiwa huyo alihitaji kuonana nao kila mtu kwa wakati wao , na ndio maana kila mtu alikuwa na ratiba yake ya kuingia hapo ikulu .
Mtu wa kwanza kuonana na mheshimiwa siku hio alikuwa ni Merina , japo mwanadada huyu alikuwa kwenye mawazo juu ya |Damiani kuhusiana na maneno alio yasikia kwa Janeth , lakini hakuacha kufika ndani ya ikulu kwa ajili ya kutii wito wa mheshimiwa , kwake swala hilo lilikuwa muhimu mno kwani ni swala lililokuwa likizihusisha biashara zake kwa ujumla .
Mtu wa pili kufika alikuwa ni Stephano lamberk, haikuleweka sabi alifanya makusudi, lakini muda ambao merina alikuwa akiingia ikulu ndio muda ambao stephano lamberk alikuwa akiingia ikulu.
Katika sehemu ya kuegesha magari mtu wa kwanza kutoka kwenye gari yake ya kifahali alikuwa ni Stephano lamberk , na wakati anatoka tu na gari ya merina ilifika maeneo hayo na kusimama na akatoka mlimbwende huyo ambae siku hio alikuwa amependeza vyema , merina alijikuta akibung`aa mara baada ya kukutanisha macho yake na macho ya stephano lamberk .
Wakati wanaendelea kushangaa iliingia gari nyngine aina ya roll Royce , gari hii ilikuwa ni ya mtaalamu Patrick , na yeye alishuka kwenye gari yake na hata yeye hakutegemea kuonana na Merina eneo hilo .

INAENDELEA

SEHEMU YA 75
THE FIRST MISSION (MISHENI YA KWANZA)

Patrick alimwangalia merina ,na damiani alimwangalia Patrick huku mrembo Merina akiwa ameyapeleka macho yake kwa Steohanoo lamberk , wakati hayo yakiendelea jasusi mwenye roho yake mbaya Miss K au Suzzane , alikuwa na yeye ndani ya hayo maeneo , haikujulikna alifka muda gani ndani ya eneo hilo la kupaki magari ndani ya ikulu , sehemu ambayo magari pekee yanayo ingia hapo ndipo yanappaki , kwani kulikuwa na ‘parking’ nyingi ndani ya ikulu , kuna sehemu ambayo ilikuwa ikitumika kuegesha magari kwa muda mfupi . lakini kuna maegesho ambayo yalikuwa yakitumika kuegesha magari kwa muda mrefu.
Hivyo eneo walilokuwepo watu hawa , ni eneo linalohusika kuegesha magari kwa muda mfupi ( temporary parking for the guest)..
Mtu wa kwanza kutoka ndani ya eneo hilo alikuwa ni Merina , wakati Merina anatoka hapo ndipo Patrick na yeye alimsogelea Merina .
“Vipi Merina ,uko poa?”Aliuliza Patrick .
“ Niko poa” Lilikuwa ni jibu moja tu kutoka kwa Merina na aliongeza mwendo , hakutaka kuongea kabisa na Patrick , ni kama mtu aliekuwa akimuepuka .
“ Karibu sana Miss Merina “ aliongea katibu muhtasi wa ikulu akimkaribisha Merina na kisha akamkaribisha tena Patrick .
“ Karibu sana stephano lamberk “ Aliongea mwanadada Suzzane huku akinyoosha mkono kumpa Stephano lamberk , na bwana huyu aliuangalia ule mkono na kisha akaachia tabasamu na kisha alimpa mkono pia suzzane , lakini wakati wanapeana mkono Suzzane alifanya tukio ambalo lilimfanya Damiani ashituke.
Alimsogelea Damiani Kwa kujivuta kwake Kama mtu anaetaka kumkumbatia, lakini haikuwa hivyo kwani alimsogelea sikioni.
“Karibu sana Damiani rabani “ Aliongea suzzane , na kwa Damiani wala hakushituka , alitabasamu kisha akamwangalia usoni Suzzane kwa kujitoa kwake na kisha akatabasamu , huku akiangalia paja la Suzzane “
“Asante sana Suzzane “ aliongea Damiani na kisha alimpita Suzzane aliekuwa amesimama huku akionekana kukasirishwa na kitendo cha Damiani kutabasamu , kwani alichokuwa akitaka yeye ni kumuona Damiani kupatwa na mshituko , lakini hakuwa hivyo bali mwanaume alitabasamu na kupita , hapo moja kwa moja Suzzane aliona kabisa Adui yake kashamzidi kete , kwani tabasamu lile lilimaanisha kwamba Damiania amekubali kudhihirika mbele yake na kama ni hivyo basi hakuja hapo ikulu kizembe , yaani atakuwa kajipanga na hilo lilimfanya Suzzane moja kwa moja apatwe na mashaka , n ahata jambo lake alillokuwa amelipania kulifanya kughairisha .
Sabi ndio aliekuwa ameandaa mtiririko mzima wa wageni wa raisi kuonana nae mmoja mmoja kama mheshimiwa alivyokuwa akhitaji , kuonana alikuwa ni Merina.
“ Karibu sana Merina “ aliongea mheshimiwa Henry kwa tabasamu kumpa mkono Merina na kisha alimuonesha nafasi ya kukaa , na wakati huo huo aliingia Patrick na baba yake alimsabahi na kisha alikaa kwenye sofa upande aliokuwa amekaa mrembo Merina .
“Merina na Patrick nimewaita hapa kuongea kama familia , mpaka sasa natambua mahusiano yenu na ni muda mrefu sasa tokea muanzishe mahusiano hivyo nataka kuwaona ninyi wawili mkiona , mnaweza kushangaa kwanini nimewaita tofauti tofauti , sababu ni kwamba nimewaita hapa kama wafanya biashara , na ninajua kila mtu anaendesha biashara zake, hivyo nataka mniambie ni lini mnaoana “ Aliongea mheshimiwa raisi na kumfanya Patrick amwangalie Merina na Merina amwangaliae Patrick …….
Nje nako Janeth na Zakayo ndio walikuwa wanafika.
“ Karibu sana Stephano “ aliongea mheshimiwa na kisha Stephano alikaa kwenye masofa , na huku mheshimiwa na yeye akikaa .
“ Nashukuru sana mheshimiwa “.Aliongea huku akipeana mkono wakati huo na Patrick .
“Nikupe hongera bwana Stephano lamberk kwa kuendelea kufanya vizuri kibishara ndani ya Tanzania , hii ni mara yetu ya pili kuoanana “.
“ Ni kweli muheshimiwa na mimi nashukuru sana kuonana na wewe kwa mara hiii ya pili , ni heshima sana kwangu “.
“Nadhani ushawawi kuonana na Patrick “.
“ Ndio , ni moja ya wanahisa katika kampuni yangu , nilikutana nae kwa muda mfupi sana”.
“Unatarajia lini kufungua kampuni yako Rasmi “.
“ Natarajia kuifungua mapema kabla ya mwaka kuisha , lakini lengo kuu la kampuni tutafanya siku ambayo tutazindua bidhaa yetu ya kwanza “
“ Hongera sana , wewe ni kijana mdogo lakni unaonekana kuwa na ndoto kubwa za kuifkisha kampuni yako mbali , naweza kusema kwamba umerithi mbinu zote za kibiahsra kutoka kwa baba yako “ aliongea bwana Henry huku akitabasamu kama mtu.
“ Nashukuru sana mheshimiwa kwa kuutambua uwezo wangu , na mimi naahidi kufanya kazi kwa bidi ili niweze kulinufaisha taifa hili , hususani katika maswala ya ajira “.
“Ni vyema sana kuskia hivyo , ila kwa siku ya leo nimekuitia mahali hapa kwa jambo moja , nadhani unafahamu na sisi pia tunamiliki kampuni ya maswala ya kiteknolojia , hivyo tumeona jambo hili litakuwa jema kama tutashirikiana kwa ukaribu Zaidi “.
“ Unamaanisha partnership ?”
“ Nadhani mpaka hapo umenielewa , na nataka jambo hilo uongee na Ptrick kwani yeye ndio muhudika mkuu na msimamizi wa kampuni zangu zote “.
“ Mheshmiwa hakuna shaka juu ya jambo hilo tunaweza kukaa chini na kuongea , lakini pia swala hli pia siwezi kulitolea maaamuzi peke yangu kwani kuna wana hisa pia , tukifanya makubaliano ya pamoja tunaweza kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kuunganisha nguvu “ Aliongea Stephano na kumfanya mheshimiwa atabasamu , kisha walipeana mikono .
Baada ya mazungumzo ya Stephano kuisha , raisi alizungumza na Janeth bendera , na hakuwa na kubwa Zaidi ya kumpongeza kwa kuwa proffesa wa kwanza mwenye umri mdogo ndani ya taifa la Tanzania .
Baada ya madakika kadhaa mazungumzo yao yaliisha , na ikawa ni zamu ya Zakayo kuonana na mheshimiwa .
“Kuna kazi nataka unifanyie ?”
“kazi gani mheshmiwa ?”
“Kuna jambo ambalo linafanyika pasipo mimi ya kujua na baadhi ya wastaafu waliokuwa ndani ya serikali ya raisi bendera .na moja ya watu hao ni Mstaafu matinde “ Aliongea mheshimiwa na kumfanya Zakayo kidogo ashituke , lakini hakutaka kulidhirisha hilo mbele ya raisi .
“Kazi yako ni kuhakikisha unajua ni kipi kinaendelea , ni mara kwa mara nilikuwa nikipokea ripoti wanafanya vikao vya siri , hivyo hio ndio itakuwa kazi yako , kuhusu malipo kwanzia hapa ninap zungumza utakuwa unapata mshahara kama wafanyakazi wengine ndani ya TISS”
“ Sawa muheshimiwa “.
Henry baada ya kumaliza mazungumzo yake na Zakayo alivuta droo ya mtoto wa meza na kisha alitoa picha , picha hio ilikuwa ikimuonesha Zakayo akiwa na Matinge mstaafu wa kitengo cha usalama wa Taifa , aliingalia kwa sekunde kadhaa na kisha aliirudisha huku akionekana kama ni mwenye kulidhishwa na jambo Fulani .
Wageni wote wa mheshimiwa Henry hawakuondoka, kwani mara baada ya kufanya mazungumzo walialikwa kwa ajili ya chakula cha mchana na familia nzima ya mheshimiwa Henry, jambo ambalo hakuna ambae alikataa.
Kulionekana kama kulikuwa na katafrija kwani kuna pia wageni wengi ambao walialikwa siku hio hapo ikulu , moja ya wageni hao alikuwepo bwana Sam , Kimbona , wastaafu wote waliokuwa ndani ya serikali ya mheshimiwa bendera , akiwemo mstaafu Matinde .
Basi wote walijumuika , huku meza aliokaa Stephano lamberk , alikuwepon Merina , Patrick , Janeth pamoja na Damiani wakati wote huo hafla hio unaendelea ,, hafla mabyo hata kwa Patrick hakuwa akijua ilikuwa inahusu nini , basi waliendelea kunywa na kula lakini wakat wpte huo Merina macho yake yalikuwa kwa Sephano lamberk , jambo ambalo kwa Patrick aliliona , hakuelewa kwanini Merina alikuwa akimwangalia sana Stephano , lakini kuna kitu alikiona kwenye macho ya Merina , kitu ambacho alijiambia lazima akifanyie kazi .
Baada ya madakika kadhaa kupita ndipo mheshimiwa Henry na mke wake wema walismama mbele ya Wageni na hio ni mara baada ya chakula na kutoa shukrani , lakini jambo kubwa lililokuwa likihusu tafrija hio ni pongezi kwa mtoto wake wa kike kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu , katika kitivyo cha sheria ‘ Harvard law school ‘ mwanadada huyu aliekuwa akifahamika kwa jina la jane , alikuwa mrembo haswa kama mama yake , lakini licha ya pongezi hizo mheshimiwa aliendelea ..
“Licha ya mwanangu kumaliza salama masomo yake kwa ufaulu mkubwa , lakini pia siku ya leo nataka nimpongeze kwa kupata mchumba , kwangu ni jambo la furaha sana lakini pia uchumba huu ni fursa kwa watanzania kwani mchumba mwenyewe ni mtoto wa Mahmood seid kutoka Dubai kijana wake anaifahamika kwa jina la kareem Mahmood seid .” Aliongea mheshimiwa kwa hali ya furaha mnoo , huku familia nzima ikionekana kufurahia uchumba huo na hata waliokuwepo kwenye tafrija hio walifurahia , na hio yote ni kutokana na wengi kumjua bwana huyu anaefahamika kwa jina la Mahmood seidi , alikuwa ni tajiri mkubwa ndani ya Dubai lakini pia duniani akiwa tajiri namba ishirini akiwa na utajiri wa dollar bilioni 46 .
Watu walimpongeza Zaidi jane kwa kuwa na bahati ya kuolewa na mtoto wa kwanza wa tajiri Mahmood , lakini hayo yakiwa yanaendelea kwa upande wa Damiani mambo yalikuwa ni tofauti kabisa .
Jina la Mahmood ni kama lilikuwa likijirudia rudia kwenye ngoma za masikio yake , moja kwa moja akili yake ilimrejesha katika misheni aliopewa na Bruno misheni ambayo hakuwa akijua ilikuwa inahusu nini , ila alichokuwa akijua ni kwamba ndio misheni ambayo ingempelekea kulipiza kisasi kifo cha mama yake .
Licha ya yote hayo hakujipa uhakika moja kwa moja kama mtu ambae anapaswa kumuua ndio huyo anaetajwa kwa jina la Mahmood , na hilo alipanga kwenda kulifatilia , kwani tokea aangalie majna hayo hakuwahi kufanyia uchunguzi wa jina hata moja kwa yale ambayo hakuwa akiyajua .
Ukweli ni kwamba Damiani alikuwa akimjua vyema Zaidi bwana huyu aliokuwa akijulikana kwa jina la Mahmood , na alimjuua kama mfanya biashara kama wengine walivyokuwa wakimjua , lakini akili yake hapo ndio ilianza kufunguka na kuanza kufikiria kuhusu misheni yake , aliomba jina lile lisiwe linamhusu tajiri huyo .
Licha ya kwamba Jane alichumbiwa , lakini waliomchumbia hawakuwepo nchini , na walikuwa wakitarajiwa kuingia nchini wakati wowote kwa tarehe watakayo ipanga kwa hio siku hio ilikuwa ni utambulisho wa uchumba huo ambao uliambatana na barua .
Partick alijikuta akimfata mdogo wake baada ya utambulisho na kisha kumpa hongera , lakini wakati huo alikuwa ameongozana na Merina .
“Broo ..” aliita Jane na kisha walikumbatiana
“kwanini tusifunge ndoa siku moja , kwani mchumba upo nae na ni mrembo na pia unampenda ?” aliongea Jane
“Ndio kwanza nilitoka kuongea na baba juu ya swala hilo , ila mimi na Merina tutalifikiria hilo , ila ni kupongeze sana Jane kwa kutuletea chuma “ Aliongea Patrick na kumfanya Jane atabasamu .
“ Usichezee Fursa sasa broo .. ushindwe wewe tu “ aliongea kiutani na wote wakacheka .
“ Hongera sana “
“ Asante sana shem wangu “.Alijibu oingezi hio kutoka kwa Merina .
Basi baada ya muda sherehe iliisha na kila mtu alitawanyika , baada ya kutka pale Stephano hakiuelekea moja kwa moja nyumbani kwake bali alienda kwenye Nyumba ya Bruno kwa ajili kuingia kwenye LEGACY ROOM ili kujihakikishia kama kweli mtu ambae anatakiwa kumuua katika misheni yake ya kwanza alikuwa ndio huyo Tajiri mkubwa duniani .
“Welcome back Mister damiani in Legacy room”(karibu sana bwana damiani kwenye chumba cha legacy “
“NARA nataka kumjua Mahmood seid kwenye misheni yangu ya kwanza ni nani?”
“Mahmood Seid is an Emirati billionare, a businessman, the founder of MR Group, an Emirati real estate and retail conglomerate with projects in Asia and Africa, His networth is estimated to be 46B USD ... (Mahmood seid ni tajiri na mfanya biashara kutoka Emirate, Mwenye utajiri wa dola bilioni 46 za kimarekani)
“Kwa hio huyu ndio misheni yangu ya kwanza kuifanya ?”
“Ndio mister Damiani, Una siku kumi na tano kukamilisha misheni hio, kuhusu namna ya kufanya mauaji hayo kila kitu kimepangiliwa “
“unamaanisha nini kuhusu kupangiliwa”
“Mpango wa kukamilisha misheni hio ushapangwa na mtu pekee wa kuukamilisha ni wewe , isku ya jumatano asubuhi utapokea mgeni ambae atakupa ramani nzima ya misheni hio “Aliongea Nara na kumfanya Damiani achanganikiwe Zaidi .
“Ni nani aliendaa mpango huo Nara “
“Bruno lamberk “.
“Anaandaaje misheni wakati amekufa “.
“ Hilo sitambui Mister Damiani “.
Damiani alijikuta akiondoka bila ya kusema jambo lolote , huku akiwa na mawazo mengi , hakuweza kumtafisiri Bruno , swali moja kwake tu ni kwamba anaandaaje mauaji huku akiwa amekufa .
******
“ Patrick nahitaji tuonane tuongee “ ilikuwa nisauti ya merina kutoka kwenye simu , wakati huo anapokea simu Patrick alikuwa anaingia ndani ya nyumba anayoishi suzzane na wakati anaongea na simu alikuwa kwenye gari akiwa sehemu ya maegesho .
“Nimefurahi unataka kuonana na mimi , unaonaje kesho “
“ Sawa , tutaonana peacock hoteli “ Aliongea Merina .
“Okey jioni njema ” Alijibu Patrick , na muda huo ilikuwa ni kama saa moja kasoro za jioni , baada ya kukata simu moja kwa moja alitembea na kuingia ndani ya nyumba hio baada ya kukaribishwa na mlinzi .
“Karibu Patrick “ Aliongea suzzane kwa bashasha akimakribisha .
“Asante Suzzane “
Basi baada ya kukaribishana Suzzane alimkaribisha Mvinyo na kisha walianza kuongea .
“Enhe , nlishangaa leo ulivyonipigia simu ukitaka kuonana na mimi “.
“Ni kweli : Aliongea na kisha akanywa funda moja ya wine kisha akaiweka chini huku akikunja nne na kuendelea: “ Nimekuja hapa kuna jambo moja nataka unisaidie .”
“Jambo gani “
“ Ni kuhusu Damiani rabani “
“ Damiani rabani!”Alionyesha ishara ya mshangao
“Ndio , najua wewe ni moja ya wanausalama na unaweza kunisaidia katika hili , nataka kumjua Damiani rabani ni nani na ana uhusiano gani na Stephano lamberk “.
“ kabla hatujaendelea , nataka kujua dhamira yako kwanza “
“Merina anampenda Damiani rabani “
“Ila yeye hakupendi si ndio , na unadhani akishatoweka Merina hatokuwa na jinsi Zaidi ya kukupenda wewe “
“Asante kwa kunielewa “
“Mimi namjua Damiani “.Aliongea Suzzane kwa kujiamini kabisa .
“Ni nani ?”
“Stephano Lamberk “
“Unamaanisha nini ?”
“ Namaanisha , Stephano lamberk ndio Damiani mwenyewe unayemtafuta na kama huamini hilo unaweza ukamuuliza Merina , na yeye analitambua hilo “ aliongea Suzzane huku akinyanyuka .
“Are you sure Suzzane ?”.
“Unaweza kwenda kujihakikishia mbele ya Merina “
Patrick hakutaki kibaki alitoka na moja kwa moja alielekea nyumbani kwake , huku akiwaza siku ya kesho ndio siku ambayo anakwenda kuonana na Merina , na ndio sku ata
kayo jihakikishia Zaidi , lakini wakati akiwa anawaza hayo , alianza kukumbuka matukio yote yaliotokea ikulu , jinsi Merina alivyokuwa akimwangalia Stephano .., akliona jambo lililozungumzwa na suzzane lina ukweli wake .
ITAENDELEA JUMATANO STAY TUNED

HAYA TUMA HIO 2000 NIKUTUMIE MWENDELEZO MPAKA MWISHO NAMBA NI 0687151346 JINA ISSAI SINGANO HAKA KA OFA KANAISHA SAA NNE YA USIKU UKILIPA NI CHEKI WATSAPP
 
bora nikutumie hyo 2000 unitumie story yote tu maana me ni mrinzi mda mwingi niko mwenyewe lindo nakuwa mpweke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom