Tunasubir mzgo nduguKabisa mkuu
Lete mzigo mkuuuKesho naleta mkuu ndefu
Merina aliendesha gari huku akiwa kama mtu ambae hakuwa akiamini kile kinacho mtokea katika maisha yake , hakuamini kabisa kwamba mtu ambae alikuwa akimuota usiku na mchana ndio mtu ambae yupo pembeni yake , kwake swala hilo lilikuwa ni kama ndoto , kuna muda alijikuta akigeuza macho upande ambao amekaa damiani kuhakikisha kama kweli ni yeye au ni picha yake , ama kamfananisha na mtu mwingine,,hata uendeshaji wake wa gari ulikuwa haupo katika umakini , mambo mengi yalikuwa yakipita katika kichwa chake .>>>>>