Ujasusi - Umoja namba 97

Ujasusi - Umoja namba 97

Wasomaji tupo Mkuu. Story murua kabisa
 
singanojr usitufanyie hivyo ndugu zako, ngoma imefikia patamu sana alafu muendelezo unachelewa!
 
SEHEMU YA 63

THE NEW ME ( UPYA WANGU )

TUNAENDELEA.........
Mkusanyiko ulikuwa ni wa siku saba mpaka kumalizika kwake na mpaka wakati huo zilikuwa zimepita siku nne , katika siku hizo zote nne nilikuwa nimepiga hatua kubwa sana , kwani nilikuwa nimekutana na wafanya biashara wengi wakubwa wakiwemo wa Taiwan , Hongkong , USA na Canada na hao nilifanikiwa kuingia nao mikataba ya kibiashara , kusema kweli kwangu niliona kikao hicho kilikuwa na manufaa makubwa sana , na ndio maana niligundua wafanya biashaara wakubwa duniani walikuwa wakipenda sana kuchaguliwa kuhudhuria katika kikao hicho .

Muda wangu wote niliokuwa ndani ya hoteli hio nilikuwa bega kwa bega na mwanadada Lesitha na hata wafanya biashara hao yeye ndio alieniunganisha nao na niliona umuhimu wa uwepo wake ndani ya mkusanyiko huo , lakini pia nilikuja kugundua kwamba ndani ya mkusanyiko huo kama nilivyosema awali kwamba kulikuwa na wafanya biashara wakubwa , wanasiasa na watumishi wa Mungu nilikuja kugundua kwamba jambo la mimi kukutana na wafanya biashara hao lilikuwa lakupangwa kabisa , yaani kati ya wahudhuriaji wote wa mkutano huo walikuwa wamepangiwa watu wa kukutana nao , lakini pia nilikuja kugundua kwamba katika mkusanyiko huo kuna ngazi ( 3 level class) tatu yaani ngazi ya daraja A , ngazi ya daraja B , ngazi ya daraja C daraja la kwanza lilikuwa ni daraja la wafanya biashara wakubwa yaani top 50 na awa utajiri wao ulikuwa si chini ya dollar bilioni kumi kupanda lakini pia kundi hili pia limesheheni wanasiasa wa mataifa kumi na tano yenye uchumi mkubwa duniani na mataifa hayo ni kama marekani (USA), China , Japan , Germany ,United kingdom (UK) , India ,France , Italy , Canada , South korea ,Russia , Brazil , Australia , Spain na Indonesia , lakini pia kundi hili lilikuwa na watumishi wakubwa wawakilishi katika dini zote hapa namaannisha wale viongozi wakubwa wa dini kwa mfano katika ukristo ndani ya mkutano huu kuna kiongozi mkubwa tu aliekuwa akimwakilisha papa , lakini pia upande wa waislamu kulikuwa na kiongozi mkubwa wa dini ambae alikuwa akitokea ndani ya nchi ya brunei alikuwa amepewa cheo cha ‘grand mufti’ kuna viongozi wa ‘ Hinduism ‘ Judaism . Budhism , Atheist( wasio na dini ) , Taoism , Shinto ,Jainism ,Confuniabism , Bahai faith na Zoroastrianism sasa dini zote hizi zina mwakilishi wao katika kundi hili A , tukija upande wa kundi B kundi hili limesheheni matajiri wakubwa mabilionea kuanzia dolla bilioni moja mpaka tisa na kundi hili halikuwa na kiongozi wa dini hata mmoja lilikuwa na matajiri tu lakini pia lilikuwa na wanasiasa wakubwa wa mataifa ya ‘First and Second world countries (Mataifa ya ulimwengu wa kwanza na wa pili ..Kwa kujifunza zaidi unaweza kugoogle ) hapa viongozi hawa walikua ni wale wa chini ya raisi Au kiongozi mkuu kabisa wa Taifa ukimtoa waziri mkuu wa India ambae ameenda kama mwakilishi wa taifa la india ambaye yeye anaingia katika kundi A , kundi la mwisho hili lilikuwa na mtajiri mamilionea lakini kundi hili lilikuwa limegawiwa kwenye ‘level 1 class’ na ‘level 2 class ‘ level one class ndio imejaa mamilionea wote na pia wachungaji wakubwa wa madhehebu mbali mbali walioalikwa hususani wale wenye utajiri mkubwa lakini pia wenye ushawishi mkubwa kwa waumini wao kwa mfano TB Joshua na wengineo , pia kwenye kundi hili pia kuna wanasiasa wa kundi la Third world countries ( hizi ni nchi ambazo kupitia umoja wa mataifa zinaonekana kuwa na kipato cha chini kabisa na Afrika ndio zimejaa ukitoa misri na Afrika ya kusini ambazo zimewekwa kwenye second ) , kwa upande wangu nilikuwa kwenye kundi C level class two kwa hio kisheria ndani ya BIBTWAG huwezi kukaa kikao na mtu wa kundi B wala A lakini kwa upande wetu ulikuwa unauwezo wa kuomba kukutana na mfanya biashara au mwanasiasa wa level class B , sisi wa level class B tulikuwa ni wale wafanya biashara chipukizi au kwa maneno mengine tunao kuja kwa kasi , lakini pia kulikuwa na viongozi wa dini pia waliokuwa wanaushawishi mkubwa wenye ushawishi lakini pia wanasiasa wenye ushawishi pia walikuwa ndani ya kundi letu .

Hivyo nilifanikiwa kufanya vikao na wafanyabishara wa kundi letu lakini pia na wa kundi letiu level one na wote hao niliweza kuingia nao mikataba mbali mbali ya kimaendeleo na kibiahsara kwa ujumla wake , kama nilivyosema kwamba yote hayo niliyafanya ndani ya siku nne hivyo zilikuwa zimebaki siku tatu tu mkutano huo kuisha kwani ulikuwa ni wa siku saba , siku iliofuata ndio siku kwangu ambayo ilibadilisha mtazamo wangu na kila kitu nilichokua nikikiamini na hata ile roho yangu ya upole na ucha Mungu ilinipotea siku hio .

Ilikuwa ni siku ya asubuhi alikuja Lesitha akiwa na tabasamu pana kama kawaida yake na siku hio hakulala na mimi kwani siku zote alikuwa akilala na mimi lakini siku hio hakulala hapo , basi asubuhi hio aliniambia nijiandae kuna kikao kikubwa cha watu wakubwa sana ambao ninahitajika kukutana nao kutoka kundi B na kundi A kwanza nilishangaa sana kwani kama nilivyokwisha kueleza kwamba makundi haya hayaingiliani vikao vyake , hivyo kwangu nilishangaa mno .
“ Are sure lesitha It is me? “
“ unauhakika lesitha ni mimi ?” nilimuuliza nikiwa nimehamanika kweli
“ yes its you , Henry you have something big in you that you may not know yet so be yourself , This is card of invitation “
“ ni wewe ndio , Henry unakitu kikubwa ndani yako ambacho huenda haukitambbuai bado hivyo kuwa wewe , hii ni kadi ya mwaliko “ nilichukua kadi ile na kuisoma na kweli lilikuwa jina langu juu ya kadi ile tena limeandikwa kwa mbwembwe zote kiasi cha kuniaminisha kwamba halijakosewa hata kidogo .
Kikao hicho kilikuwa kinafanyika siku hio hio muda wa jioni kabisa saa mbili za usiku kwa muda wa Singapore kwa hio asubuhi yake hio tulijiandaa kwa ajili ya kuelekea kula bata maana siku hio ilikuwa ni ya mapumziko , sasa kilichonishangaza ni kwamba siku hio lestiha baada ya kujiandaa aliniambia kwamba kwanzia muda huo sitokuwa nae tena na akaniambia kwamba kila maelekezo nitapewa wala nisiwaze na huo ndio mwisho wangu wa kuonana nae , nilishangaa sana lakini pia nilikumbwa na huzuni kwani nilikuwa nimemzoea sana lakini pia alikuwa ndie aliekuwa akiniambai kila kitu kilichokuwa kinahusu ndani ya mkutano huo wa BIBTWAG .

Nilimuuliza kwanini anaondoka hakunipa sababu iliokamili ila alinniambia kwamba zamu yake ilikuwa imekwisha na anaingia hatua inayofata , sikumuelewa kabisa lakini hakuongea sana kwani alitoka ndani ya chumba hicho na kuondoka na huo ndio ukawa mwisho wa kuonana na lesitha , moyonuliuma na hata sijui kwanini , ila nilijikuta kujua baadae kwamba nilikuwa nikimpenda sana mwanadada huyo japo nilikaa siku tatu nne nae lakini kwangu ilikuwa ni kama mwaka .

Basi baada ya lesitha kuondoka alikuja mwanaume mmoja black huyu alikuwa ni mwafrika kabisa , na ana rafudhi flani kupitia kingereza chake ya kinigeria basi baada ya bwana huyu aliekuja alijitambulishwa kwangu kama Rickson Okonkwo tulitangulizana na kwenda nje kabisa ya hall na huko niliingia kwenye chumba moja tulivu ndani ya hoteli hio hio , chumba hiki hakikuwa na mtu kabisa bwana huyu rick aliniambia niketi hapo kuna mtu anakuja kuonana na mimi asubuhi hio huku nikipata kifungua kinywa , na mimi nilikubaliana nae kwani ilikuwa ni kawaida hata kipindi nilichokuwa na lesitha nilikuwa nikikutanishwa na watu wakati wa chakula ama wa chai asubuhi , basi mara baada ya kukaa kwa dakika kama mbili aliingia kijana mmoja wa makamo , sio mkubwa sana mzungu akiwa ametangulizana na bidada mmoja wa kiarabu alievalia hijabu yake na suti ya zambarau iliomkaa vyema .

Nilisalimiana na mzungu yule na alijitambulisha kwangu kama Peterson schwan ni mfanya bishara kutoka Ukraine katika maswala ya teknolojia na alivutiwa na mimi kuwa kama mwenza wake katika swala zima la uwekezaji nchini , kwangu niliona kama fursa nyingine kwani nilikuwa nikipenda sana maendeleao na ukizingatia mimi ni mchaga basi mazungumzo yangu na bwana schwani yalienda vizuri sana , lakini aliniambia kwamba kuna ushindani mkubwa ambao tunakwenda kukutana nao nikamwambia hilo ni swala la kawaida la kibiashara , basi stafutahi yetu ilienda vyma kabisa baada ya mazungumzo hayo tuliagana na Rick alinichukua na kunipa maelekezo kwamba siku hio ilikuwa ni ya bata hivyo napaswa kujiandaa kibata bata , na mimi pia zilikuwa mambo zangu hizo za kupenda bata hivyo haikuwa na tatizo , nililetewa nguo zangu na kila kitu changu nilichokuja nacho nchini hapa na bwana Rick , jambo ambalo lilinifurahisha sana kwani nilikuwa sijawasiliana muda mrefu na familia yangu na nilijiua pia wamenitafuta , japo mara kwa mara nilikuwa nikifikiria usaliti aliokuwa ameufanya mke wangu au huenda anaendelea kuufanya roho iliniuma lakini haikuwa kizuizi changu mimi kutowasiliana na familia yangu .

Siku hio tuliingia kwenye yatcht moja ya kifahari sana ambayo kwenye maisha yangu sijawahi kuota kama nitakuja kuingia kwenye yatcht kama hii , ilikuwa ni ndogo ya kawaida ila ilikuwa ni ya kifahari mno , na ndani kama alivyo sema siku hio ni ya kibata basi ndani ya yatcht hio kulikuwa na warembo mbali mbali wengi wao wakiwa wamevalia nusu uchi , na ile naingia tu walinikimbilia , ilikuw ani mwendo wa Cocktail tu ndani hapo na wine , kiufupi mambo yalikuwa ni ya kufurahisha na kuburudisha na nilikumbuka mbali kweli enzi za ujana wangu .

Kilichovutia zaidia ndani ya yatcht hii kulikuwa na wafanya biashara wakubwa sana lakini wengi wao ni wale ambao nilikuwa nimeingia nao madili ya kibiashara kwa hio siku hio ni kama vile tulikuwa tukisherehekea na kweli tulisheherekea kweli kweli, kula kunywa, fanya uzinzi na warembo hawa mambo mengi ya kumkarahisha Mungu yalifanyika , na hata muda sikuona jinsi ulivyo kuwa ukisonga , kwani mpaka giza linaingia tulikuwa katikati kabisa ya bahari huko na nilichokuja kugundua ni kwamba hakukuwa na kurudi tena hoteli siku hio Zaidi ya kula bata tu .

Basi ilitimia saa moja kamili , ni kama akili yangu ilirudi sasa kwenye mwaliko wa kuonana na wale viongozi wakubwa kutoka kundi B na A sasa kilichonishangaza na kunitia hofu muda wote huo tulikuwa katikati huko ya bahari na mwaliko ule ulikuwa ukinitaka kukutana na wale watu saa mbili kamili juu ya alama na Rickson sikuwa nikimuona .

Basi niliendelea na bata langu kiwasiwasi na warembo muda huo tulikuwa kwenye swimming pool ndani ya hio yatcht ndipo alipokuja bwana mmoja alievalia suti , bwana huyu alikuwa ni mthailland alinisogelea na kuniambia kuna sehemu napaswa kuongozana nae na mimi nilisimama na kumfata na kuelekea upande wa kushoto wa boti na kuingia kwenye boti nyingine wanaziitaga ‘runabaout ‘ ni zile ambazo zinakimbiaga kwa kasi na aliniambia nipande , kwanza nilipatwa na wasiwasi wakupanda huku nikimwangalia na yeye aliniangalia na akanioneshea kidole kuelekeza upande wa juu ya boti na ndipo nilipomuona Rickson na alinitingishia kichwa kuniashiria kuwa niingie kwenye boti zile basi sikuwa na ajizi niliingia kwenye ile boti na kisha iliondolewa kwa kasi mno na tulitumia muda wa kama dakika tano kwa mbele kabisa ndipo nilipo ona meli kubwa mmno ikiwa mbele yetu , tulizidi kuisogelea na nikaosma maandishi yake , ilikuwa ikijulikana kwa jina ‘SUPER B MEGA CFUISE SHIP ‘.
Baada ya kuifikia ilisimama ubavuni kabisa na zikashushwa ngazi nikapanda ndani ya ile meli na kuingia ndani.
Aisee kuna sehemu ambazo nimeshuhudia katika maisha yangu ni nzuri na za kifahari, lakini ndani ya hii meli ni babu kubwa , nakosa hata maneno sahihi ya kuielezea , lakini kiufupi kila kitu ndani ya meli hii kilikuwa ni cha kifahari mno , nilipitishwa katika vyumba kadhaa na kuja kutokea kwenye casino kubwa ndani ya meli hii na hapo nilikutana na watu wakubwa tu ambao sijawahi kuwahuhudia katika maisha yangu laivu wengi wao wakiwa wafanya biahsara wakubwa mno na wanasiasa wakubwa sana .
“ karibu sana bwana Henry , kwa kuvuka ngazi na kuingia kwenye kundi B” ilikuwa ni sauti ya mwanadada mrembo kabisa wa kizungu akinifungulia mlango wa kuingia kwenye mlanogo wa chumba kilichokuwa kimeandikwa kwa maandishi makubwa VIP na mimi niliingia na hapo ndipo nilipo pigwa na mshangao baada ya kuingia ndani hapo na kukutana na sura ninazozifahamu .
ITAENDELEA WAKUU TUVUMILIANE
 
Naash nash
Hii nishamalizana nayo let's hiyo ifuatavyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom