My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,333
- Thread starter
- #61
Mkuu Umesema kweli kabisa ila Engine hata ikinunuliwa haiwezi kufungwa kwenye ndege bila Boeing kuihakiki, hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho wanunue Engine kisha waifunge kimya kimya bila kuifanyia check up yoyote.Brother, naomba twende step kwa step kuna vitu nimenote hapa haviko sawa ama vimekuzwa ama vimewekwa kwa namna ya ushabiki wa kitaarifa/habari (sensationalized), tuanzie hapa
1. Engine ya ndege lazima ifanyiwe check up kabla ya kuwa verified sokoni ila kama ni mfuatiliaji wa maswala ya aviation asilimia kubwa ya vifaa unavyoviona ni baada ya ajali kisha wataalamu wanaamua kudesign solution, mfano tu sababu ya madirisha ya ndege kuwa oval ni baada ya ajali ya ndege huko miaka ya 60-70 na kugundua square windows zinagerate pressure jaribu kumsiliza huyu rubani kwenye link nimeiweka chini kbs ya post hii, kwenye engine hapa bado nakukatalia Boeing hawatengenezi engine na malfuction za ndege hizo sio engine kufeli ni system ya kucontrol pitch ya ndege inayoitwa Maneuvering Characteristics Augmentation System (MCAS), ingia hapa usome kinachoendelea https://interestingengineering.com/...-update-other-changes-for-embattled-737-max-8 na link ingine iko chini kbs inayoeleza kinachoendelea.
2. hapa unaposema ndege ZOTE zilizoruka zimeanguka kwa tatizo hilo hilo naomba tujikumbushe kwamba mpaka sasa aina ya ndege hizo zilizo kwenye order ni ndege 4987 na zilizotengenezwa na kukabidhiwa na kuanza kuruka ni ndege 381 na zilizopata ajali ni ndege 2 sasa unaposema ndege zote zilizoruka naona umekuza mno taarifa, angalia hapa idadi ya ndege za aina hiyo zilizokuwa delivered https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Boeing_737_MAX_orders_and_deliveries na pia ajali za ndege za aina hiyo angalia link hii hapa inalist ya ajali zoote za boeing mwishoni kabisa utaona ndege ya Lion na Ethiopian Air, link hii hapa isome https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_accidents_and_incidents_involving_the_Boeing_737 .
3. FAA wanahoja za kujibu maana walipaswa kuangalia system zote na kujihakikisha kuwa ziko sawa, kilichogundulika ni kuwa sensor inayocontrol MCAS system haikuwa inasoma sawasawa sababu ya bugs za software iliyotumika, jana wametoa update ya hiyo software, hii ndiyo iliyosababisha ndege zote za aina hiyo kuw agrounded mpaka solution inayoeleweka itakapopatikana na kikubwa walichokosea Boeing ni kutoitolea taarifa hiyo system mpya kwenye manual book yao haipo kabisa
4. Tatizo la ajali linafanana sababu ni system ile ile moja
Mkuu ukiwa unajipanga kuendelea na part two au three au four jaribu kuchuja kwanza taarifa zako na data zako ili twende sambamba, hizo zingine za kijasusi tunajua ni theory na maoni yako binafsi kwa mtazamo wako kama watu wataona kuna ukweli ni sawa au ni story tu kama zingine pia ni sahihi maana kuna dalili za kutaka kuongelea ujasusi zaidi kuliko tatizo la awali lililogundulika (sikatai kuwa ujasusi 'unaweza' kuwepo pia)
* Link hapo chini kabisa ni ya mfano niliouelezea hapo juu wa oval window hiyo ya juu yake ni kinachoendelea sasa hivi, najaribu kuweka links ili tuwe na ushahidi na hoja zetu sio kwamba naspeculate tu from no where mtoa mada
Pia report ya kweli kabisa Boeing hawawezi kuitoa, wanachofanya ni kuhakikisha kuwa hawakimbiwi na wateja, tazama Trump alivyochanganyikiwa na kuanza kulaumu ma pilot wa Africa.
Kutengeneza madirisha ya Oval shape hayo ni maboresho Kwa ndege na si kwamba hadi litokee tatizo ndo Wanafanya check up ,check up ni lazima mkuu kwa kila kifaa cha Aviation.
Sent using Jamii Forums mobile app
