Hapa namzungumzia uchambuzi wangu binafsi juu ya uwezekano mkubwa wa kampuni ya Boeing kuhujumiwa na mahasimu wao kibiashara, excuse kwamba eti kupata hitilafu engine ni kitu cha kawaida, haikubaliki Kwa sababu zifuatazo.
1.Engine ya ndege ni lazima ifanyiwe regular check up kabla ya kui verify sokoni
2.Boeing wametengeneza zaidi ya ndege 200 aina ya 737 MAX 8 na kuzipeleka sokoni na zote zilizoruka zimeanguka Kwa tatizo hilo hilo
3.Ni nani aliruhusu na ku verify hizo ndege ziruke na kisha kuuzwa? Hakuona tatizo?
4.Kwanini tatizo la ajali linafanana?
Maswali ni mengi ,Boeing imehuhujumiwa
Sent using
Jamii Forums mobile app
Brother, naomba twende step kwa step kuna vitu nimenote hapa haviko sawa ama vimekuzwa ama vimewekwa kwa namna ya ushabiki wa kitaarifa/habari (sensationalized), tuanzie hapa
1. Engine ya ndege lazima ifanyiwe check up kabla ya kuwa verified sokoni ila kama ni mfuatiliaji wa maswala ya aviation asilimia kubwa ya vifaa unavyoviona ni baada ya ajali kisha wataalamu wanaamua kudesign solution, mfano tu sababu ya madirisha ya ndege kuwa oval ni baada ya ajali ya ndege huko miaka ya 60-70 na kugundua square windows zinagerate pressure jaribu kumsiliza huyu rubani kwenye link nimeiweka chini kbs ya post hii, kwenye engine hapa bado nakukatalia Boeing hawatengenezi engine na malfuction za ndege hizo sio engine kufeli ni system ya kucontrol pitch ya ndege inayoitwa Maneuvering Characteristics Augmentation System (MCAS), ingia hapa usome kinachoendelea
https://interestingengineering.com/...-update-other-changes-for-embattled-737-max-8 na link ingine iko chini kbs inayoeleza kinachoendelea.
2. hapa unaposema ndege ZOTE zilizoruka zimeanguka kwa tatizo hilo hilo naomba tujikumbushe kwamba mpaka sasa aina ya ndege hizo zilizo kwenye order ni ndege 4987 na zilizotengenezwa na kukabidhiwa na kuanza kuruka ni ndege 381 na zilizopata ajali ni ndege 2 sasa unaposema ndege zote zilizoruka naona umekuza mno taarifa, angalia hapa idadi ya ndege za aina hiyo zilizokuwa delivered
https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Boeing_737_MAX_orders_and_deliveries na pia ajali za ndege za aina hiyo angalia link hii hapa inalist ya ajali zoote za boeing mwishoni kabisa utaona ndege ya Lion na Ethiopian Air, link hii hapa isome
https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_accidents_and_incidents_involving_the_Boeing_737 .
3. FAA wanahoja za kujibu maana walipaswa kuangalia system zote na kujihakikisha kuwa ziko sawa, kilichogundulika ni kuwa sensor inayocontrol MCAS system haikuwa inasoma sawasawa sababu ya bugs za software iliyotumika, jana wametoa update ya hiyo software, hii ndiyo iliyosababisha ndege zote za aina hiyo kuw agrounded mpaka solution inayoeleweka itakapopatikana na kikubwa walichokosea Boeing ni kutoitolea taarifa hiyo system mpya kwenye manual book yao haipo kabisa
4. Tatizo la ajali linafanana sababu ni system ile ile moja
Mkuu ukiwa unajipanga kuendelea na part two au three au four jaribu kuchuja kwanza taarifa zako na data zako ili twende sambamba, hizo zingine za kijasusi tunajua ni theory na maoni yako binafsi kwa mtazamo wako kama watu wataona kuna ukweli ni sawa au ni story tu kama zingine pia ni sahihi maana kuna dalili za kutaka kuongelea ujasusi zaidi kuliko tatizo la awali lililogundulika (sikatai kuwa ujasusi 'unaweza' kuwepo pia)
* Link hapo chini kabisa ni ya mfano niliouelezea hapo juu wa oval window hiyo ya juu yake ni kinachoendelea sasa hivi, najaribu kuweka links ili tuwe na ushahidi na hoja zetu sio kwamba naspeculate tu from no where mtoa mada