Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 2,398
- 3,074
Wadau wa elimu.
Huwa tunaanzia kufundisha watoto a e i o u
Kisha ndio babebi... halafu ndo mambo ya 'Baba anakula nzige, aliyeng'ang'ania jani shambani'.
Nani alisema kuwa ni lazima mambo yaende hivyo?
Mfano tukiamua kuanzia kumfundisha mtoto namna jet engine ya ndege inavyotengenezwa halafu tukamwambia 'Mtoto ukisoma, ukaelewa mambo ya aeiou, ba ebibobu na baadaye ukawa mkubwa mwenye akili, utaweza sasa kutengeneza ndege inapaaa juuuuuu'
Kwa uzoefu wangu sie nyumbani tulianza kusomewa hadithi kwanza. Hadithi taaamu kweli halafu tunaambiwa, mkijifunza mkajua kusoma mtajisomea wenyewe hadithi nzuri kwenye haya mavitabu yoote zimejaa habari za kuvutia sana. Guess what! Nilijikuta nimekuwa msomaji mmoja matata shule ya msingi tu. Kitabu cha kurasa mia tatu sijui mia tisa huko sijui (Eric Shigongo books) nnakikata chini ya wiki.
Mzee mwenyewe huyu hapa๐
View: https://youtu.be/31c1k00hBFM?si=9X97CEMNOa1iHAjH
Sasa ukiachana na kusoma tu, jiulize mwanao ungependa awe nani? Baada ya kusoma. Halafu mfundishe hicho kitu na baada ya hapo mwambie, ajisomee yeye mwenyewe akikazana atafaidi hicho anachopenda.
Itamjengea mtoto udadisi, na msukumo wa kuelewa utatokea ndani yake kabisa hadi utashangaa.
Zama za kulazimisha mambo, ni akili za kitumwa. Hazifai.
Haiya, sasaa kama Taifa:
Tujiulize tunataka wananchi wajao wawe na mtazamo gani? Wa ajira au ujasiriamali? Biashara, uchuuzi, viwanda eeh?
Baada ya hapo tuwekeze kwenye kuwapa picha watoto za hivyo vitu katika hali watakazozipenda. Kisha waambiwe, wasome kwa bidii waje wafanye makubwa katika sekta za ujasiriamali, uongozi, usindikaji wa bidhaa, viwanda nk.
Mfano, tunaenda kindergarten vidudu na mpishi, wanajifunza watoto kupika keki na kupamba. Kisha wanaambiwa mtaweza kujitengenezea keki, biskuti, mtamiliki viwanda vya pipi etc.
Au anaenda mjasiriamali anayetengeneza mafuta ya kupaka, shule ya msingi. Wanakusanywa wanafunzi kama wanavyokusanywa kuoneshwa mazingaombwe....
... By the way tunavoweka maonesho ya mazingaombwe je? Tunathamini zaidi wananchi wa kesho wavutiwe na uchawi au lengo ni nini?๐คซ๐ค
... Turudi kwenye mada. Basi wanakusanyika wanafunzi, na mjasiriamali anaonesha hapo jinsi anachanganya sabuni au mafuta ya kupakaa. Baadhi wanashiriki kuandaa wamevaa kisayansi kabisa. Wanagawiwa zawadi ya mafuta. Mwishoni wanafunzi wanamuungisha bidhaa nyingine kadri inavyofaa.
Mwalimu anawaambia, wakiwa wadadisi, wakiijua sayansi, kemia, na hisabati mbona watamiliki hadi viwanda kabisa.
Mzazi usisubiri shuleni, wewe mwenyewe unaweza kumuanzisha mtoto uelekeo ufaao hapo hapo nyumbani. Muoneshe lengo, halafu kisha kila hatua anayopiga italeta mantiki. Akili tu mtu wangu.
Aliyetembea duniani anisaidie, hivi huko Uchina, Japani, Ujerumani wanafanyeje?
Basi kwa leo ni hayo.