Ujana Wako Ulikula Na Nani?

Ujana Wako Ulikula Na Nani?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,787
Nimesikia wimbo wa Kizazi kipya leo redioni, sijajua ni nani mtunzi na mwimbaji, lakini kijana huyo amefanikiwa kunitisha sana kwa maneno yake mazito.

Baadhi ya maneno ya wimbo wake yanasema:

"Ujana wako ulikula na nani?....Usije ukasumbua watu"
"Pesa zako ulikula na nani.......Usije ukasumbua watu"

Huo wimbo tokea nimeusikiliza alfajiri nikiamka, hadi saa hii nashitukia unanijia, naimba sehemu hiyo hapo juu tu...sijui mwendelezo wake unasemaje!

Wazee wenzangu nisaidieni, huyu kijana aliyeimba wimbo huu mbona anatutisha wazee namna hii!
Atakuwa hana malezi mazuri huyu kijana!
cc: Asprin, DARKCITY, Mtambuzi, Kaizer
 
Bahati mbaya wengine hatuujui huo wimbo pengine tungeliweza kujua maudhui yake...
 
ha!ha!haaa nyongeza tu model avae na nani bwanga nifue mie!!!
 
Hahaha sass mkuun@pakajimmy ukisikia na ule wa kuchapiwa ni siri ya ndani si unaweza kuchanganyikiwa? Jawilat hebu come zis way
Hawa vijana wa kizazi hiki mi nakwambia hawajatulia...yaani ukichapiwa ukauke, wakati mi najua nikichapiwa-.....NI TIKETI YA SAFARI KWAO...:wave::wave::wave::A S 13::A S 13::A S-frusty::A S-frusty::A S-frusty::A S 114::A S 114:
 
Aisee huo wa kuchapiwa siri ya ndani huwa simwelewi, najiuliza huyu anajua manna yake au?

nasikia wazee wa zaman ndio walisema hayo asa cjui ni kweli

humu kama kuna wazee wa zaman watupe maana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom