Ijue siri ya boyfriend na girlfriend

Cataliyya

Cataliyya

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Messages
664
Likes
238
Points
60
Age
32
Cataliyya

Cataliyya

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2015
664 238 60
KARIBU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU PAMOJA

Sunday, August 10, 2008

IJUE SIRI YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND -5

IMEKUWAJE KUKAWA NA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND ?

Shetani mara zote huwa ni muharibifu, huwa analivunja pendo la Agape ndani ya mioyo ya watu, yaani FAMILY LOVE. Kitu cha ajabu kabisa wazazi na watoto ghafla wanakuwa maadui. Na hii mara nyingi ilitokea kutokana na wazazi kufanya maagano na miungu au mizimu (mizimu ni mapepo au roho za Ibilisi zilizovaa sura za watu waliokwisha kufa) au kwa maneno mabaya ambayo huondoa pendo la kweli ndani ya familia. Hii ni ngumu kidogo kwa mtu kuelewa kwa wepesi, ngoja nikuvunjie vipande vidogo vidogo;

Watu walimwacha Mungu na kuzisikiliza roho zidanganyazo, yaani uchawi, mapepo, na mizimu halafu uadui na chuki ikajengeka katika familia. Kwa mfano; Mtu anapiga ramli, mchawi au mganga anamwambia umelogwa na dada yako au mama au baba yako. Wakati mwingine mapepo husema uongo kupitia mtu mmojawapo katika familia hiyo akionekana ni mzima tu au wakati mtu huyo akiombewa na hivyo kuibua uadui, chuki na mafarakano katika familia hiyo. Wakati mwingine Shetani huwafunga watu kwa ulevi na hivyo kupelekea kuvunjika kwa family love. Maana ulevi ni kinyume na agizo la BWANA. Efeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”

Kutokana na uadui ulioibuka ndani ya familia, kulikosababishwa na watu kufuata njia zao na si njia ya Bwana, matokeo yake ni wazazi na watoto kuwa maadui. Baba anarudi nyumbani amelewa, binti yake anakimbilia jikoni, watoto wa kiume hawakai nyumbani wanazurura tu, kisa mama makali. Wazazi wakakosa busara, hekima na maarifa ya kuwaelekeza watoto wao mambo mema, kwa kuwa wamemwacha Mungu. Na hivyo watoto wao hawakufundishwa na Bwana, Isaya 54:13 “Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi” Zile sehemu au nafasi za wazazi ndani ya mioyo ya watoto wao zikapotea, zikawa tupu. Maana yake upendo, amani na furaha ndani ya watoto zikapotea. Ndiyo maana nilikwambia kuwa, vitendo vya kukumbatiana, kutomasana, kupakatana, kupigana busu na kuambiana maneno fulani kati ya girlfriend na boyfriend, ni kutafuta amani, furaha na upendo uliopotea. Maana nafasi za wazazi wao ndani ya mioyo yao zipo wazi. Hivyo vijana wakaanza kutafuta namna ya kuzijaza nafasi hizo. Ghafla (special relationship with opposite sex) girlfriend na boyfriend zikaanza. Na vijana wengi wakaingia katika uhusiano wa namna hiyo bila kujua ni nini hasa maana yake na mwisho wake ni nini au ni wapi. Na haikuwezekana kuwa mke kwa sababu umri wao ni mdogo bado na pia haukuwa wakati wa Bwana aliopanga kwa mapenzi kuamka; hivyo vijana wengi baada ya kuingia kwenye mahusiano hayo wakayachochea na kuyaamsha mapenzi, wakajikuta wakifanya zinaa. Hii ikawa kama sehemu ya starehe kujaribu kuiridhisha au kuifurahisha nafsi. Ndiyo maana hakuna uhusiano wa boyfriend na girlfriend kwa watu wazima, ni kwa vijana. Maana sijawahi kuona wazee eti ni boyfriend na girlfriend wake (hata kama hawajawahi kuzaa), kama wapo basi ni mbinu za Shetani kutetea zinaa na hao watakuwa ni watumishi wa Ibilisi.Sikiliza mpendwa, kubwa analolifanya Shetani ni kuvuruga au kuvunja upendo wa familia. Naye hutumia njia za namna mbalimbali. Njia nyingine anayoitumia Shetani ipo sana katika nchi au mataifa tajiri dunia na sasa njia hii inakuwa kwa kasi sana katika nchi zetu za dunia ya tatu. Anawasogeza wazazi mbali na watoto wao kwa kuwafanya wazazi wajishughulishe sana na pesa na kazi na kusahau wajibu wao kwa watoto wao kama Bwana alivyotuagiza, Wapo BUSY. Waefeso 6:4 “Nanyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana” Mith 19:18 “Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia wake” Na ndiyo maana kwa wenzetu (wazungu) mtoto kuwa na girlfriend au boyfriend sio tatizo. Ooh! Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa, maana Shetani anatumia nguvu nyingi sana katika kuutetea uovu dunuani.

Inawezekana hunielewi ninaposema ‘anatumia nguvu nyingi’ ninamaanisha nini. Hivi sasa anawatumia watawala, mataifa makubwa na sheria za kimataifa. Ngoja nikupe vitu;

Zipo baadhi ya nchi, mzazi kumwadhibu mtoto ni kosa kisheria, na unaweza hata kufungwa jela. Mnaigeria fulani alikuwa akiishi nchi mojawapo ya Ulaya. Siku moja binti yake alifika nyumbani akiwa na boyfriend wake. Akamtaka baba yake aondoke nyumbani ili yeye apate nafasi ya kustarehe na huyo boyfriend wake. Jambo hilo lilimuudhi sana Baba yake, hivyo alimchapa kofi sawia. Binti yake alipiga simu polisi na baba yake akakamatwa, na akaamriwa kutoonekana mazingira ya nyumbani kwake kwa siku tatu asimsumbue binti yake na kumlipa binti yake kwa kumsumbua na kumzalilisha mbele ya boyfriend wake. Baada ya kesi kwisha akaichukua familia yote na kuirudisha Nigeria .

MATOKEO YA MAMBO YA MWILINI

Baada ya kujua maana ya girlfriend na boyfriend kama jinsi anavyoitumia Shetani, mwanzo wake na lengo la Shetani la kusababisha kuwapo kwa boyfriend na girlfriend, nimeona ni vema pia nikujulishe jinsi mfumo wa mashambulizi ya Ibilisi ulivyo kwa undani zaidi.

Ninataka wazazi na vijana waelewe mbinu hii mbaya mno ya Shetani ambayo huathiri vizazi vingi. Na hata sasa tunahitaji neema ya Mungu na kanisa kusimama katika nafasi yake ili kuokoa vizazi vijavyo kutoka katika hali hii ya zinaa.

Mungu alipomuumba mwanadamu ndani yake aliweka hali ya uungu na akampa mwanadamu jukumu la kuendeleza uumbaji wake, katika mwili na Roho. Mwanadamu huzaliwa katika mwili na pia mtu huzaliwa katika Roho. Yoh 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa na Roho ni Roho”

Mungu ameagiza mwanadamu amwabudu, amsujudie, amheshimu na kumtumikia yeye peke yake. Wazazi wanalo jukumu kubwa la kuwalea watoto wao katika maadili mema sawasawa na mpango wa Bwana. Na hii ni ili watoto wakue wakimfahamu Mungu, wamtii na kumtumikia.

Msingi mzuri wa utumishi na nafasi ya kijana katika kanisa na jamii kwa ujumla huanza kuundwa tangu tumboni (utunzaji wa mimba), anapozaliwa na katika ukuaji wa mtoto (namna mtoto anavyolelewa). Utunzaji wa mimba unahitaji ushirikiano wa wazazi wote wawili, baba na mama pamoja na jamii nzima inayowazunguka. Wazazi walio na hofu ya Mungu na wanaomtii Mungu katika maisha yao, huwa na hekima na ufahamu wa Rohoni, na hivyo huwa na uwezo mkubwa wa kuwalea watoto wao katika misingi mizuri ya Kikristo na maadili mazuri katika jamii nzima. Mungu naye huwa akiwafundisha watoto wa watumishi wake. Isaya 54:13 “Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi” Watoto wakifundishwa na Mungu huwa watumishi wazuri wa Mungu, huwa waadilifu na wenye manufaa makubwa hasa katika jamii yao . Shetani analifahamu hili, na ndiyo maana huanza kwa kuharibu misingi ya vijana tangu utotoni, maana anajua watamshinda. 1 Yoh 1:14 “Nimewaandikia ninyi,… vijana kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu” Ukisoma maneno haya kwa kutafakari utaona wazi kabisa kuwa hali ilivyo sasa ni kama kinyume. Ooh! Mungu tusaidie vijana. Biblia inasema ‘vijana wana nguvu’ na ndivyo inavyopaswa kuwa. Lakini vijana wengi siku hizi ni dhaifu mno, maana wanamtumikia Shetani. Sasa hivi wengi ndiyo wadhaifu kiroho, afadhali wazee wana nguvu. Biblia inasema ‘neno la Mungu linakaa ndani ya vijana’ lakini vijana wengi wa sasa hawana neno ndani yao . Kinachosikitisha sana ni hiki, ‘vijana wanaambiwa wamemshinda Shetani’ hapa mimi sisemi, jaribu kufikiri kwa makini na kutafakari maisha yako wewe kijana au vijana wengine unaowafahamu. Je wamemshinda Shetani?

Ili familia iwe bora na yenye ufahamu wa Ki-Mungu ni lazima au inahitajika iundwe na Mungu mwenyewe. Uhusiano wa girlfriend na boyfriend mara nyingi umepelekea mimba zisizotarajiwa, mimba nyingine zimetolewa, na zilizobahatika kufikia mwisho hazikupata matunzo mazuri na hata watoto hao mara nyingi hukosa malezi bora. Wakati mwingine mahusiano haya yamesababisha kuwepo kwa ndoa zisizo na hofu ya Mungu kwa kuwa zilianza kimwili hivyo mara nyingi huvuna matendo ya mwili, kama hawakutubu na kumpa Yesu maisha yao .

Kwa kuwa ndoa nyingi zilizoanza kwa namna hiyo, huwa na mafarakano, na mara nyingi huwa na maisha yaliyojaa misongo ya mawazo (stress) kwa sababu ya kuvurugika kwa mipango mbalimbali. Na pengine hutengana na hivyo watoto hukosa malezi bora na mara nyingi huathirika kiafya na kisaikolojia. Na haya yote huchangiwa na ama malezi duni ya mimba ama wakati wa ukuaji ama mazingira magumu au yasiyo na utulivu (family disharmony) au kukosa malezi ya mzazi mmojawapo.

Ngoja nikupe mifano kidogo; Watoto wengi ambao walikuwa na utapia mlo (kwashiorkor) hupata matatizo ya uwezo wa kufikiri wanapokuwa watu wazima, maana utapia mlo huathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto. Tatizo hili huwa kubwa pia kwa watoto ambao mama zao walikosa lishe bora wakati wa ujauzito. Na utafiti wa kisaikolojia unaonesha kuwa watoto ambao wamekulia katika familia zilizokuwa na mafarakano au magomvi, wengi wao huathirika kisaikolojia na pia huchangia kusababisha magonjwa ya akili. Watoto au kizazi kilichokulia katika mazingira ya vita, huweza kuongeza idadi ya watu wenye magonjwa ya akili au kuwa na taifa lililo na watu wasio na utu (cruelity) au vijana wasio na uwezo mzuri wa kuwa na mahusiano mazuri na jamii nyingine.
Mpendwa hili si suala dogo kama watu wengi wanavyofikiri. Maendeleo ya sayansi na teknolojia, utandawazi uliopo sasa, upatikanaji wa madawa ya kulevya umekuwa rahisi, sasa ukiyaweka mambo yote haya mbele ya kijana ambaye hakupata msingi mzuri wa maisha toka utotoni, kiafya na kiimani na asiye na neno la Mungu ndani yake kwa hakika ni rahisi sana jamii kumpoteza kijana huyu. Ila ninafurahi maana Mungu wetu kwa kweli ni mwema, maana yeye hutupa akili njema, hutupa ufahamu wa rohoni, hekima na busara hata kama tulikulia kwenye mazingira magumu. Hii ni kwa sababu Mungu hutuwazia mawazo ya amani na pia hutuinua uli tumtumikie yeye. Hivyo haijalishi kwamba ulizaliwa mazingira ya namna gani, Yesu anapokuwa upande wetu hufanya yote kuwa mazuri. Ukiwa kwa Yesu historia ya maisha yako haiwezi kuathiri maisha yako kamwe.

Ooh! Haleliya! Sikiliza, lengo la Ibilisi ni kuwafanya vijana wafanye dhambi na pia kuangamiza au kuteka vizazi vingi vijavyo. Vijana ni kundi kubwa na lina nguvu ya kufanya mabadiliko makubwa kiimani, kiuchumi, kisiasa na kijamii katika jamii yetu ya sasa, ikiwa vijana wataamua kubadilika na kumtafuta Mungu kwa bidii.

Haijalishi kuwa wewe ni mtoto, kijana au mzee kumbuka unayo nafasi yako muhimu unayopaswa kutumika kikamilifu sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ninayo furaha kubwa sana ndani yangu kwa maana Mungu wetu yu mwema na hutupasha watumishi wake habari za mambo yajayo. Kwa hiyo ninaamini kuwa lipo kusudi kubwa tena maalum kwa Mungu kutufunulia siri hii kubwa.

Watumishi wa Mungu tuwe macho maana ipo kazi kubwa iliyopo mbele yetu kwa ajili ya utukufu wa Mungu, nayo ni kung’oa na kubomoa, na kuharibu ngome na kupanda.

JE YESU ANAIFAHAMU SIRI HII YA BOYFRIEND NA GIRLFRIEND?

Yesu aliuona uharibifu ambao Shetani aliufanya, wa kuharibu au kuvunja pendo la familia. Na ndiyo maana alipokuwa msalabani alisema hivi; ‘Mama tazama mwanao’ halafu akamwambia yule mwanafunzi, ‘Tazama mama yako’ Yoh 19;26-27 “Basi Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, mama tazama mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, tazama mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake” Yesu alipomwambia mama tazama mwanao na mtoto amtazame mama yake, maana yake, upendo wa ndani ya moyo (family love) ambao Ibilisi aliuharibu, uundwe, uumbike upya, uhuishwe tena. Biblia inaniambia yule mwanafunzi akamchukua mama yake nyumbani kwake. Maana yake ni hii; Ile nafasi ya moyo wa yule mwanafunzi, aliingia mama yake, na hii iliwezekana kwa neno la Yesu. Usiniulize kama yule mwanafunzi alikuwa ameoa au la, ninachojua ni kwamba Yesu alikuwa anahuisha upendo wa familia (family love)
Ndiyo maana wapendwa walio ndani ya Kristo kweli, na neno lake ndani yao , hawababaishwi na boyfriend au girlfriend maana ndani ya mioyo yao wamekamilishwa kwa neno la Kristo. Wengine watafikiri kwa kuwa wazazi wake au mzazi wake amefariki basi ni sawa kuwa na boyfriend au girlfriend, sivyo hata kidogo. Biblia inasema, Mungu wetu yeye ni Baba wa yatima. Maana yake nafasi za wazazi wako au mzazi wako inachukuliwa na Mungu mwenyewe.
Wengine wataniuliza, mbona nafasi ndani ya moyo wa Isaka haikuchukuliwa na Mungu? Kumbuka Isaka aliishi katika kipindi cha Agano la Kale na sisi tupo katika Agano Jipya, Mungu ametusogeza karibu sana na yeye katika Agano Jipya kuliko katika Agano la Kale. Kristo mwenyewe yupo ndani yetu tuaminio na kutii Yoh 15:4. Sikiliza; Hata kama family love itaharibiwa na Shetani, na wazazi kutowapenda watoto wao, amani, furaha na upendo wa Kristo huwahifadhi waliomwamini Yesu. Na hivyo hawatafuti amani au furaha au upendo kutoka kwa girlfriend au boyfriend bali kwa Yesu.
Hivyo ni dhahiri kabisa kuwa na (special relationship with opposite sex) girlfriend au boyfriend ni chukizo kwa Bwana. Soma maandiko vizuri, muombe Mungu akupe Roho ya mafunuo, akupe kujua na maandiko na macho ya moyo wako yatiwe nuru, ili uone njia ya Bwana ifaayo. Rumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na ukamilifu” Hebu jiulize, hivi nikweli huwa unafahamu ukweli halisi au ni kwa sababu umekuta uhusiano wa namna hii upo na wewe ukaiga? Jiulize tena, hivi ni kweli Mungu ndiye anayekuongoza kuwa na special relationship with opposite sex? Kumbuka Biblia inakuambia, usifuatishe tu mambo ya dunia hii maana yake unapaswa kuyaelewa, nia yako igeuzwe, ifanywe upya ili usiyatamani mambo ya dunia bali uyatamani mambo ya Mbinguni. Pia ujue hakika mapenzi ya Mungu sio unabahatisha tu. Hivyo mpendwa usiige tu vitu mwombe Mungu akupe kujua.

SASA NIFANYE NINI?
Ndugu mpendwa ni vema ufahamu jambo hili ya kuwa pasipo Yesu huwezi kufanya neno lolote. Yoh 15:4b “…maana pasipo mimi (Yesu) ninyi hamwezi hufanya neno lolote” Maana yake ni hii; Hata sasa huwezi kufanya uamuzi ulio bora na sahihi katika kuwa na mahusiano kama hujajikabidhi kwa Yesu na kumruhusu aingie ndani ya moyo wako ili akuwezeshe kuwa na maisha yenye maamuzi sahihi na kufanya yampendezayo Mungu. Inawezekana upo katika uhusiano wa aina hiyo au ndiyo unaanza uhusiano huo. Najua unahisi kama utakosa vitu fulani vitamu na utakosa furaha, sikiliza furaha hiyo si ya kutoka kwa Bwana, hivyo ni vema utafute furaha kwa Yesu. Ikiwa wewe ni kijana mdogo acha kuyaamsha na kuyachochea mapenzi maana utavuna uharibifu kwa kuwa unapanda kwa mwili na sio kwa roho. Inawezekana pia wewe ni mzazi, kumbuka hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Hata kama umechangia sana kuharibika kwa watoto au mtoto wako, ni vema ujinyenyekeze chini ya mkono wa Yesu, ulio hodari yeye atafanya sawasawa na haja ya moyo wako. Hakikisha unakuwa muda mzuri wa kuzungumza na familia yako.
Kabla ya kuendelea kukisoma kitabu hiki, ikiwa upo tayari kumpa Yesu nafasi ya kwanza katika maisha yako, na unasikia ipo hali ya kutaka kufanya yaliyo mema machoni pa Mungu, basi acha kujiuliza maswali ya upingamizi, acha kutazama au kufikiri juu ya huyo rafiki yako bali fikiri juu ya uhusiano wako na Mungu, omba sala hii kwa sauti ukimaanisha.
Bwana Yesu nakuja mbele zako, unitazame mwanao. Nimekutenda dhambi wewe. Ninatubu mbele zako, unisamehe na kuniosha dhambi zangu zote kwa damu yako. Ninavunja maagano yote niliyoyafanya na Shetani. Ninakuruhusu Roho Mtakattifu uingie ndani ya moyo wangu sasa. Uniongoze katika kweli yako. Ninaahidi kukutegemea wewe Yesu, na kukutumikia kwa uaminifu hata nitakapokufa. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa, niwezeshe kukufuata hata milele. Amina.
Ikiwa umeomba sala hii, dhambi zako zote zimefutwa, na Kristo yupo ndani ya moyo wako sasa, wala usitie shaka. Tangu sasa ni vema ushirikiane na wapendwa waliookoka na uwe ukisoma Biblia ili ukue kiroho. Usiache kumuomba Mungu maana sasa wewe ni mwanaye hivyo anakusikiliza kila umwitapo. Yoh 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa” Siku zote utaendelea kuwa rafiki wa Mungu ikiwa utafuata maagizo ya Bwana na kuacha dhambi. Yoh 15:14 “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruvyo”
Jipe moyo utashinda maana Yesu naye alishinda. Ufunuo 3:11,21 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyotayari kuujia ulimwengu wote kuwaharibu wakaao juu ya nchi. Naja upesi shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”
Ole wake apingaye neno la Mungu, maana hasira ya BWANA itakuwa juu yake

Posted by Adriano at 5:56 AM No comments:

IJUE SIRI YA BOYFRIEND NA GIRLFRIEND 4

MAANA ILIYOFICHIKA YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND

Nataka ujue maana ya girlfriend na boyfriend, kama jinsi Shetani anavyoitumia, na jinsi anavyochochea tafsiri yake ndani ya watu wengi na kuwaangusha katika zinaa (dhambi)

Kwa maana ya ndani iliyofichwa na kufunikwa kwa maneno mazuri yaani girlfriend na boyfriend, ni hii; Ni uhusiano wakaribu sana kati ya watu wa jinsi tofauti na mara nyingi huambatana na kufanya ngono (zinaa)

Vijana wengi hawaukubali ukweli huu, na ndiyo maana nikakuuliza unapata hisia gani unaposema girlfriend au boyfriend wangu, tofauti na uposema rafiki yangu kwa hali ya kawaida? Kama na wewe unaipinga maana hiyo niliyokuambia fanya hivi; Jaribu kumuuliza msichana mwenye akili timamu kama anaye girlfriend, au muulize mvulana ambaye ni rafiki yako akuambie kama anaye boyfriend. Nina uhakika hatakupa jibu la moja kwa moja na ukipigwa usishangae, na usiseme Adriano amenituma.

Vijana wengi hupenda kuwa na girlfriend au boyfriend wakiwa na maana ya urafiki wa kawaida, wakipendana, wakisaidiana na kushirikiana mambo mbalimbali mazuri. Sikiliza uhusiano huu hauna asili ya Afrika na asili yake ni nchi za magharibi (western countries) na kwao huu hi uhusiano wenye lengo la kufanya ngono na hutoa nafasi ya wazi kabisa ya kufanya zinaa. Girlfriend au boyfriend si mchumba na wala si mke.

Ooh! Haleluya! Inawezekana hata maana ya mchumba hufahamu. Sikiliza mpendwa; Mchumba ni mtu wa jinsia tofauti na wewe ambaye umemposa au umeposwa naye na tena umefanya naye shauri au patano au mkataba au agano kuwa utaoana naye. Na baadaye patano hilo hufanyika mbele ya mashahidi (wazazi, jamaa, marafiki na kanisa) Na huyo huwa ni matunda ya maombi yako kwa BWANA akupatie. Maana yake ni kwamba, unakuwa umefunga mlango wa watu kukuchumbia au wewe kumchumbia mtu mwingine. Biblia inamwita mtu aliyeposwa mke na yule aliyeposa Biblia inamwita mume. Usifikiri ni jambo la kujiamulia tu utakavyo wewe, upo utaratibu wa Mungu. Urafiki wa uchumba haufanani na urafiki wa girlfriend na boyfriend, hivyo mchumba si girlfriend au boyfriend. Na pia girlfriend au boyfriend si machumba. Wengi wenye girlfriend au boyfriend ukiwauliza, kama wana mpango wa kuoana wanajibu Mungu akipenda. Sikiliza, utaratibu wa Mungu juu ya ndoa sio wa kubahatisha.

Natamani sana utambue kuwa Shetani ndiye mwanzilishi wa girlfriend na boyfriend. Na kwa kupitia maneno hayo au uhusiano huo hupenyeza hisia na misisimko ya dhambi ndani ya mioyo ya watu, ambayo hupingana na neno la Mungu; msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi. Maana girlfriend na boyfriend ya kawaida huwa haina ubaguzi, kwamba huyu ni girlfriend au boyfriend wangu na huyu sio.

Hivyo kutokana na mahusiano haya automatically mapenzi huchochewa na kuamshwa. Hali ya kuwa na boyfriend au girlfriend humpa Ibilisi nafasi ya kupenyeza tamaa za mwili. Maana kila mmoja hutamani kuwa karibu sana na mwenzake. Na mara nyingi hupenda kufanyiana mambo mazuri wakimaanisha upendo. Likini ukweli ni kwamba, Shetani hufunga ufahamu wao rohoni na macho yao ya kiroho hutiwa giza na hujikuta wakiivunja amri ya sita. (usizini) Asilimia kubwa ya vijana walio na magirlfriend au maboyfriend wamekwisha fanya uzinzi na kama bado hawajafanya ndani ya mioyo yao hivi sasa kuna shauku kubwa ya kutaka kufanya hivyo na huanza kushindwa kujizuia wanapokuwa pamoja. Ooh, Roho Mtakatifu akusaidie! Na kama hawatamruhusu Yesu aingie ndani ya mioyo yao , wataanguka katika zinaa iwapo uhusiano huo utaendelea.Jiulize Biblia inaeleza wapi uwe na girlfriend au boyfriend? Biblia inasema “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” Ebrania 12:14 Maana yake uwe rafiki wa watu wote, na sio kuwa na special friend yaani girlfriend au boyfriend, na kama ni special basi awe ndiyo ambaye Mungu amekupa kuwa mke au mume na uwe na uhakika. Hata hivyo ukaribu wenu una mipaka yake.

Mtume Paulo aliandika hivyo akimaanisha urafiki hasa kati ya wavulana na wasichana. Kama huamini soma misitari unaofuata baada ya huo Ebr 12:15-16 anasema hivi; “mtu asiipungukie neema ya Mungu” maana yake mtu asitoke katika mpango ambao Mungu amempangia, ambao ni kwa neema tu mtu hupewa. Halafu anasema, “shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua” maana yake hisia za ndani ambazo mwisho wake ni uchungu (jehanamu) zisiwasumbue. Sikiliza; mahusiano haya mara nyingi husababisha chuki, mafarakano, vijana wengi wana uchungu mioyoni mwao na wakati mwingine hupelekea baadhi ya vijana kujiua. Wapo vijana ambao wamejeruhiwa mno, na ukimwambia suala la kuoa au kuolewa anatamani akumalize kabisa, maana hataki kusikia, na hiyo ndiyo furaha ya Shetani unapokuwa katika hali ya namna hiyo. Ndiyo maana Paulo anaendelea kusema; “asiwepo mwasherati…” Maana girlfriend na boyfriend huchipusha shina la uchungu, husumbua na mwisho wake ni uasherati. Shina la uchungu linapochipuka humtia mtu unajisi (humchafua kiroho), Ebr 12:15. Kumbuka girlfriend au boyfriend sio mchumba, sio mke ana jinsia tofauti na wewe na ana hisia za mwili kama kawaida.

Vijana wengi wanajua kuwa uhusiano huu huchochea kufanyiana mambo ambayo Mungu hakuruhusu kufanyika kwa wakati huo, na hii ni kwa sababu Shetani hupata nafasi. Haijalishi unataka au hutaki, unapokuwa na girlfriend au boyfriend, Ibilisi hutumia nafasi hiyo kuingiza hisia za dhambi ndani ya moyo wako na kutia giza macho yako ya kiroho ili usiione njia ya Bwana. Mithali 16:2 “njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe, bali Bwana huzipima roho za watu” Hivyo ni lazima uwe na uhakika kuwa unaongozwa na Roho Mtakatifu. Rumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndiyo wana wa Mungu”

Mwanzoni vijana wengi walipokuwa na girl/boyfriend zao, hawakupenda sana kuonekana na watu (maana matendo ya giza hayafanyiki nuruni), lakini siku hizi wapo wengi ambao hupenda kuonekana kuwa wana girlfriend au boyfriend. Na lengo ni kuonekana kuwa wao ni wa kisasa sana au ni kuonesha kuwa ana handsome mzuri na kama ni kaka basi anataka watu wamuone beauty girl wake, siku hizi wanawaita sex lady. Hii ni roho ya Shetani ya kiburi na kwa tafsiri nyingine moyo wake umekuwa mgumu. Mara nyingi hupenda kukaa aidha gizani, uchochoroni kwenye kona au chumbani wao wawili. Hii ni kujitafutia mazingira ya kufanya zinaa, maana ndio mpango wa Shetani kusababisha kuwapo kwa uhusino wa namna hii. Maana yeye hupinga neno la Mungu, 1 Kor 6:18 “Ikimbieni zinaa” Biblia haisemi kemea zinaa bali inasema kimbia, maana yake uondoke kabisa karibu na zinaa.

Mkumbuke Yusufu alivyofanya kule misri kwa mke wa Potifa. Mwanzo 39:5-12 “…nitafanye ubaya huu mkubwa nimkose Mungu…, Yusufu akaiacha nguo yake mikononi mwake akakimbia akatoka nje”

Wengine hupenda kubusiana 2 Kor 13:12, “Salimianeni kwa busu takatifu” Hili si busu kwa boyfriend au girlfriend maana huwa linaambatana na hisia ya dhambi (ngono). Na huwezi kusalimia kwa busu takatifu kama wewe si mtakatifu.Wengine hupeana zawadi. Kupeana zawadi si tatizo ila tatizo ni aina ya zawadi wanazopeana na malengo hasa ya kutoa zawadi hizo. Kwa mfano mtu anakupa zawadi ya nguo ya ndani (underwear) au picha za uchi, hii ni ishara ya kukutaka ngono. Kwa hiyo kupeana zawadi ni vema iwapo zawadi hiyo inatolewa katika mpango wa Mungu na sio kwa ajili ya kupata kitu fulani au kwa ajili ya anasa. 2 Timotheo 3:4b “Wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu”

Wengine hujiwekea maagano kwa matendo au maneno yao wenyewe. Sikiliza; mtu anasema bila wewe sina raha, ni wewe tu unayenifurahisha au siwezi kuishi bila wewe n.k. Maneno haya hufanyika kuwa agano au mkataba katika roho na hupelekea kukosa amani, kukosa furaha na wakati mwingine hupelekea kifo pale urafiki unapokwisha. Hii ni kwa sababu maneno hayo hutamkwa lakini huwa ni unafiki au ni nje ya mpango wa Mungu. Pia huwa rahisi kwa Shetani kuwaangusha maana huwa hakuna uongozi wa Roho Mtakatifu. Jaribu kujiuliza kwa nini usiseme, bila Yesu sina raha au ni Yesu tu unayenifurahisha au siwezi kuishi bila Yesu? Maana huo ndio ukweli. Mithali 6:2 “Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako” Pia katika maneno ipo nguvu kubwa kiasi cha kuweza kusababisha kifo. Mith 18:21a “mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi”

Kuwa na girlfriend au boyfriend si mpango wa Mungu. Kwa nini uhangaike kuwa na girlfriend na boyfriend wakati watu wote ni rafiki zako? Ndivyo yasemavyo maandiko, “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote” Ikiwa ni wakati wa kuwa na partner, ni vema kupiga magoti na kumwomba Mungu akupe ambaye ni mwenzi wako mtarajiwa.

Wengine huwa na girlfriend au boyfriend kwa malengo ya kuja kuoana baadaye. Na wengine huwa na marafiki wa aina hiyo wengi ili aweze kuchagua mmoja anayefaa. Ooh Skiliza, hakuna kitu cha namna hiyo katika maandiko matakatifu. Mungu humpatia mtu mwenzi mmoja na kamwe Biblia haisemi kuwa Mungu atakuletea wasichana au wavulana wengi ili uchague mmoja, huo ni utaratibu wa Shetani maana yeye ndiye hubahatisha ila Mungu wetu hafanyi mambo kwa kubahatisha. Mith 19:14 “…bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA”

Ngoja nikupe mifano kutoka kwenye Biblia ili unielewe vizuri;

Isaka alipotaka kuoa alitafutiwa mke na sio girlfriend na wala hakuwa na girlfriend hapo mwanzo. Mwanzo 24. Utaratibu wa kwenda kumtafuta mke wa Isaka kutoka kwa jamaa ya Baba yake ni kivuli cha mambo ya sasa. Maana yake ni sawa na kijana kupiga magoti mbele za Mungu kuomba mwenzi wa maisha. Maana Mungu ndiye Baba yetu, ndiyo maana tunaomba mwenzi (mke/mume) kutoka kwa jamaa ya Mungu kama vile Isaka alivyotafutiwa kutoka kwa jamaa ya Baba yake.

Hatupigi magoti mbele za Mungu kuomba girlfriend au boyfriend bali tunaomba Mungu atuwezeshe kuwa na amani na watu wote. Na kama ni kuoa au kuolewa tunaomba mwenzi na si vinginevyo. Kumbuka Biblia yatuagiza kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ni lazima kwanza usome neno la Mungu na umruhusu Kristo akae ndani ya moyo wako ili akupe Roho Mtakatifu ambaye atakuwezesha kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Rumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo...” Ndiyo maana ni lazima kukubali Yesu akuokoe na akupe ufahamu wa rohoni na nguvu ya kuomba ili uelewe undani wa uhusiano wako ulio nao sasa (kama unaye), je watoka kwa Mungu au ni mawazo yako tu.Yakobo alipotaka kuoa, alikwenda kwenye ukoo wa mama yake akajipatia wake na si girlfriend na wala Biblia haituambii kuwa alikuwa na girlfriend hapo mwanzo.

Wengi hujikuta wakifanya ngono aidha kwa kutaka au pasipo kutaka, lakini chanzo halisi ni boyfriend au girlfriend wake. Na vijana wengi hujuta na hulaumiana baada ya kufanya dhambi. Nimewasikia wengine wakisema, “Sikuwa nataka kufanya ngono lakini kila ninapokuwa na girlfriend/ boyfriend wangu najikuta tu nimekwisha fanya hivyo, sijui kwa nini?” Kumbuka nimekuambia kuwa yapo mambo ambayo Biblia hairuhusu kufanyika kwa wakati huo. Lakini mtu anapokuwa na boyfriend au girlfriend wake hufanya hivyo. Na mwili una mihemko yake na pia kwa kuwa hukutii maandiko ( Ikimbieni zinaa) na pengine huna Roho Mtakatifu, hivyo huongozwa na mwili wako na sio Roho wa Mungu.

Wengine kwa kigezo cha kuonesha upendo kwa mwenzake, hupenda kushikana shikana, kutomasana, kukumbatiana, kupigana busu, kupakatana au kusemeana maneno kama niliyokutajia hapo mwanzo. Kwa nini hufanya hivyo? Kwa sababu ni girlfriend au boyfriend wake. Mith 7:10, 13, 21 “Natazama mwanamke akamkuta, ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo. Basi akamshika, akambusu, akamwambia kwa uso usio na haya. Maneno yake mengi na ulaini akamshika kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda” Ndio maana nikakwambia kwamba, hata kama ni mchumba, ukaribu wenu una mipaka yake, na pasipokua na kiasi hupelekea kufanya dhambi na matatizo mengine makubwa katika jamii na hulichafua kanisa (kwa vijana walio makanisani).

BOYFRIEND NA GIRLFRIEND ZILIANZAJE?

Hebu jiulize kwa nini mtu awapo na boyfriend au girlfriend wake hupenda kufanyiana mambo niliyokutajia hapo juu? (kubusiana, kukumbatiana, kutomasana au kusemeana maneno niliyokutajia). Zipo sababu zilizopelekea kufanyiana mambo hayo, nayo ni hii; Ni kutafuta amani, furaha na upendo uliopotea. Inawezekana unajiuliza ulipotea wapi au inakuwaje? Ninachotaka ni wewe ufahamu ni nini chanzo cha kuwepo kwa girlfriend na boyfriend.

Pendo la Mungu ni pendo la AGAPE. Ni pendo ambalo halidai malipo wala halihesabu gharama. Ni upendo ambao hudhihirika wazi kwa matendo yake na sio kwa maneno tu. Ni pendo lililomfanya Mungu kumtoa mwana wake wa pekee Yesu kwa ajili yetu.

Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu, Mwanzo 1 :27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. Kwa hiyo mtu akawa na tabia za uungu ndani yake. Basi ni dhahiri kuwa tabia ya upendo wa Agape ilikuwapo ndani ya mwanadamu. Pendo hili la agape kwa mwanadamu likafanyika PENDO LA FAMILIA (Family love)

Pendo la agape, Mungu akampenda mtu ambaye amemuumba, maana ni mtoto wake. Pendo la familia, wazazi wakawapenda watoto wao na watoto wakawapenda wazazi wao. Ni upendo wa asili (natural love) ambao Mungu aliuweka ndani ya mwanadamu.

Katika familia ambazo upendo wa familia umehuishwa na Kristo, pana tabia za namna hii ; ngoja nikumegee kidogo vitu vitamu ;

Mama huwa karibu au humwangalia sana mtoto wa kiume, japo humwangalia pia mtoto wa kike. Maana yake uhusiano wa kifamilia kati ya mtoto wa kiume na mama huwa wa karibu sana. Ndiyo maana mara nyingi mama huwa wa kwanza kugundua na kumwonya mtoto wa kiume anapoanza tabia zisizofaa. Mara nyingine utamsikia mtoto wa kiume akimsifia mama yake ‘Mama ukivaa kitenge hiki huwa unapendeza sana’ au wakati mwingine akimtengenezea mama yake kilemba kikae sawasawa, fuatilia utayona haya.

Vilevile uhusiano kati ya mtoto wa kike na baba yake huwa wa karibu sana. Baba humwangalia au hushughulika sana kwa ajili ya binti yake kuliko mtoto wa kiume, japo pia humwangalia mtoto wa kiume. Uliza watoto wa kiume watakuambia, wengine husema ‘Baba anampendelea sana dada sijui kwa nini’ ni kwa sababu upo upendo wa ziada. Ndiyo maana Baba huwa wa kwanza kugundua tabia fulani kwa binti yake, na ndiyo maana mara nyingi utawasikia akina baba wakiwauliza wake zao, ‘Binti yetu siku hizi vipi, mbona hivi ?’ Baba hujisikia uchungu sana binti yake anapofanya mambo yasiyofaa kuliko mtoto wakiume anapofanya hivyo. Maana yake ni kwamba kuna upendo wa ziada kati ya baba na binti yake.

Fungua Biblia yako, tazama Mwanzo 27 :46 ‘Rebeka akamwambia Isaka, moyoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi, kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yananifaidia nini ?’ Inaonesha wazi kabisa kuwa Rebeka alikuwa na upendo wa ziada kwa mwanawe Yakobo. Kwa tafsiri nyingine alikuwa akitafakari sana juu ya maisha ya baadaye ya kijana wake, (future ya Yakobo) hata akapata uchungu sana moyoni mwake (anasema, maisha yangu yananifaidia nini)

Angalia upendo wa Hana kwa mwanawe Samweli, 1 Sam 2 :19 ‘tena mama yake humfanyizia kanzu ndogo na kumletea, mwaka kwa mwaka…’ Kumbuka Samweli alikuwa akihudumu Hekaluni, kwa hiyo hakukuwa na haja sana ya mama yake kumfanyizia kanzu, maana Hekaluni mna mavazi.

Kibiblia maana yake ni hii ; Mtoto wa kiume anapokuwa bado hajaoa, ndani ya moyo wake, nafasi ambayo itakuwa ya mkewe huwa inashikiliwa na mama yake. Na kabla mtoto wa kike hajaolewa, nafasi ambayo itakuwa ya mume wake hushikiliwa na baba yake. Na jambo hili hushikiliwa na family love. Ndivyo ilivyo usishangae, ngoja nikupe mifano kutoka kwenye biblia ;

Kabla Isaka hajaoa nafasi ya mkewe ndani ya moyo wake ilikuwa inashikiliwa na mamaye Sara. Lakini Sara alifariki kabla Isaka hajaoa. Isaka alihuzunika sana, hakuwa na furaha na mara nyingi alikuwa akitafakari peke yake. Hii inaonesha jinsi upendo kwa mama yake ulivyokuwa wa ziada. Ndipo mtumishi wa Ibrahimu alipotumwa kumtafutia Isaka mke. Mwanzo 24 :24…, ‘…bali nenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu, Isaka mke’ Mara baada ya Isaka kumwona Rebeka, ghafla huzuni ikaisha, furaha ikarejea, akafarijika. Mwanzo 24 :67 ‘Isaka akamuingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka akawa mkewe, akampenda, Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamaye’

Biblia inasema, Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, maana yake, ndani ya moyo wa Isaka palikuwa na nafasi iliyokuwa wazi, ambayo imeachwa na mama yake baada ya kufariki. Sasa Rebeka anaingizwa katika nafasi hiyo. Unaweza kujiuliza kwa nini asimwingize kwenye hema ya baba yake ? Usifikiri alimwingiza kwenye hema ya mama yake eti kwa sababu mama yake alikuwa amefariki, la hasha sivyo. Mambo au desturi nyingi katika Agano la Kale ni kivuli cha mambo ya sasa. Hivyo maana yake ni kumwingiza Rebeka moyoni mwake. Ndivyo ilivyo, maana anachukua nafasi ambayo hapo mwanzo ilishikiliwa na mama. Wimb 3 :4 ‘…nikamwona mpendwa wa nafsi yangu, nikamshika nisimwache tena, hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, chumbani mwake aliyenizaa’ Maana yake, mkewe anaingia kwenye nafasi ambayo hapo mwanzo ilishikiliwa na mamaye Sulemani.

Baada ya kujua upendo uliopo katika familia, uelewe kuwa pendo hilo (family love), ndilo lililoshikilia amani na furaha za watoto kabla hawajaoa au kuolewa. Inawezekana unafikiri mambo haya yalikuwa ni desturi zao tu. Umesahau kuwa mambo ya Agano la Kale ni kivuli cha mabo ya sasa ? Soma kitabu cha Waebrania sura ya kumi, utaelewa.

Posted by Adriano at 5:54 AM 1 comment:

IJUE SIRI YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND-3

MAPENZI

Mapenzi ni kitu kilichowekwa na Mungu ndani ya kila mwanadamu. Mapenzi ni kitu kilicholala na huamka yenyewe kwa wakati ambao Mungu amepanga kwa kila mtu. Hivyo mapenzi yapo ndani ya kila mtu tangu anapozaliwa, ila huwa yamelala, na yana muda wake wa kuamka. Wimbo 2 :7 “Nawasihi enyi binti za Yerusalemu,… msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha, hata yatakapoona vema yenyewe” Utakubaliana nami kuwa huwezi kuamsha kitu ambacho hakijalala, kwa hiyo mapenzi huwa yamelala. Anaposema ‘yatakapoona vema yenyewe’ maana yake Mungu alikwisha yapangia utaratibu na muda wake ili yaamke. Kumbuka kila kitu alichokifanya Mungu ni kizuri na chema hivyo alijua hali halisi ya ujana, hali yetu ya kibayolojia ndiyo maana akaweka muda wa mapenzi kuamka. Biblia inasema mapenzi huweza kuamshwa na mtu mwenyewe. Wimbo 2 :7 “…enyi binti za Yerusalemu,…msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha…” Maana yake wewe mwenyewe unao uwezo wa kuyachochea na kuyaamsha. Inawezekana ukafikiri ni sawa au ni vema tu kuyachochea na kuyaamsha mapenzi wakati wowote, lakini jiulize kwa nini Mungu aliyawekea utaratibu (gerentee) ya muda maalumu wa kuamka ? Sikiliza, Mungu amevipa vitu vyote kufanywa kwa muda aliyepanga yeye kwa sababu vitu hivyo huwa vizuri vinapofanyika kwa muda huo. Ooh ! Haleluya ! Unapofanya kitu chochote hata kama ni kizuri ukikifanya kwa muda usio wa Mungu kitu au jambo hilo linakuwa si jema tena linakuwa dhambi, na haliwi lenye faida. Muhubiri 3 :1,9-11 Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu, …je mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo ? Nimeona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake, ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya tangu mwanzo hata mwisho”

Lazima ujue kuwa Mungu alikwishaandaa mpango na utaratibu mzuri wa maisha yako tangu enzi. Isaya 46 :10 “Kumbuka mambo ya zamani za kale maana mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi, nitangazaye mwisho tangu mwanzo na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado, nikisema shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote” Mungu anaposema nitangazaye mwisho tangu mwanzo, maana yake aliufahamu mwanzo wako hata mwisho wako. Alijua utazaliwa lini, utazaliwa wapi na nani na alijua utaoa au utaolewa lini na nani na utaishi wapi. Na katika yote hayo Mungu anakuwazia mawazo mema na mpango wake juu maisha yako ni mwema. Ni lazima uelewe hili, Mungu anaposema, shauri langu litasimama maana yake anategemea yote aliyokupangia, ukikubali na kutii yote akuagizayo, hataacha kutimiza yote aliyokupangia ambayo ni mema (maana hakukupangia jambo baya), mazuri na mwisho wake ni uzima wa milele.Sikiliza mpendwa, Mungu humaliza kwanza halafu ndipo anaanza. Ooh ! Haleluya ! Maana yake ni hii yeye aliratibu maisha yako na kukupangia matukio yote hata mwisho, akaona ni vema ndipo akaruhusu uwepo duniani. Tatizo kubwa ni watu kutojua na kutotaka kujua kalenda ya Mungu kwao na hivyo hutafuta njia za mkato (shortcut ) na ndipo uangamivu huja juu yao. Yer 29 :11 Maana ninajua mawazo ninayowawazia nnyi asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumiani siku zenu za mwisho »

Kukuwazia amani, maana yake ni kuwa na maisha mazuri ya furaha hapa duniani. Na anaposema ‘kuwapa ninyi tumaini la siku zenu za mwisho’ uwe na uhakika ni uzima wa milele. Hivyo hata utaratibu wa mapenzi upo ndani ya mpango wa Mungu. Watu wengi husumbuka kutafuta utaratibu wao badala ya kumwachia Mungu awaongoze katika utaratibu ulio mzuri na ulio bora.

Vijana wengi hushindwa kuishi sawasawa na mpango wa Mungu aliowapangia, na wengi wao si kwa sababu hawataki ila ni kwa sababu hawaijui siri hii kubwa ambayo Mungu ameiweka ndani yao. Unauliza siri ipi, soma Muh 3 :11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake, tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao ,… Ni vema uitambue siri hii itakusaidia.

Kwa hiyo mapenzi yamewekewa muda wake wa kuamka, kwa hiyo ukiyaamsha kwa muda wako unaotaka wewe, unakuwa umejitoa katika utaratibu au mpango wa Mungu na kuiendea njia yako binafsi, ambayo mwisho wake ni dharau ya milele yaani Jehanamu. Mara nyingi baada ya vijana kutoka katika mpango wa Mungu na kukutana matatizo makubwa na mazito katika maisha yao hujaribu kuyatatua kwa kutumia akilia zao. Na mara nyingi hufanya maamuzi yasiyo sahihi na hivyo hupata matatizo makubwa zaidi na kusahau kumtegemea Yesu aliye mshauri wa ajabu na mfalme wa amani.

Sikiliza, Uhusiano wowote ni lazima uanzishwe na Yesu mwenyewe ili uhusiano uwe bora, unaompa Mungu utukufu na wenye faida katika maisha yako. Biblia inaeleza jambo hili wazi kabisa, Muh 3 :9 Je mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo ? Ahaa ! Kumbe hakuna faida bali ni hasara tupu kujishughulisha upendavyo wewe na sio kama apendavyo Mungu.

Ndugu mpendwa, hupaswi kuyachochea wala kuyaamsha mapenzi. Inawezekana unatenda matendo au unazungumza maneno ambayo hufanya mapenzi ya wengine kuamka, maana yake umeyachochea, na hii ni chukizo kwa Bwana. Pengine hufanyi ngono lakini umekuwa ukiwafanya wengine waendelee kufanya hivyo. Maana yake ni kwamba unatumiwa na Shetani kama ajenti wake. Inawezekana unajiuliza utayachocheaje mapenzi ya wengine kuamka ? Tembea yako, tazama yako, uvaaji wako, maneno yako na matendo yako yanaweza kabisa kuchochea mapenzi ya wengine kuamka. Ooh, hilo ni somo jingine, Mungu akipenda tutajifunza.

MAANA YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND

Kwanza tuangalie maana halisi ya kawaida ya girlfriend na boyfriend, halafu tuangalie maana halisi anayoitumia Shetani, ambayo imefunikwa kwa maneno mazuri yaani girlfriend na boyfriend, kama mtu awekavyo chakula kizuri katika mtego wa panya.

Neno friend lina maana rafiki, girl ni msichana na boy ni mvulana. Sasa ukiyaunganisha maneno hayo, unapata rafiki wa kike au rafiki wa kiume. Hii ni maana ya kawaida ya girlfriend na boyfriend, si mbaya kwa jinsi unvyoyasikia maneno hayo. Kumbuka Shetani hutumia maneno mazuri akiwa na maana au kusudi la kwake tofauti ambalo ni chukizo kwa Mungu. Na huwateka watu wasipofahamu undani halisi na wasio na macho ya kiroho yaani ufahamu wa rohoni wa kutambua mbinu za Ibilisi. Jambo kubwa hapa si kuvijua vitu au kuyaelewa maneno yanayotajwa, ila ni kufahamu maana halisi ya hayo unayoyasikia katika ufahamu wa rohoni. Haleluya! Ndiyo maana ipo karama ya kupambanua roho.

Mpendwa ni vema uwe makini sana na kila unalolifanya. Wapo watu wanaotetea uovu wakidai wana ufahamu wa roho au wamefunuliwa na roho. Sikiliza, kuwa na roho au kufunuliwa mambo fulani na roho si tatizo, ila tatizo ni roho ya namna gani uliyonayo au ni roho wa nani aliyekufunulia unayotuambia. 1 Yohana 4:1 Wapendwa msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Mara nyingi Shetani hutumia maneno mazuri, kumbuka alivyomjaribu Yesu. Mathayo 4:6 Akamwambia, ukiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini, kwa maana imeandikwa atakuagizia malaika zake; na mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Haya ni maneno mazuri na pia ni kweli yameandikwa, soma Zaburi 91:11-12 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake... mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Lakini ulikuwa ni mtego wa kumtaka Yesu awe na kiburi ili ajikweze au ajitukuze kuwa yeye ndiye mwana wa Mungu. Bwana Yesu aliitambua maana halisi au maana ya ndani iliyifichika, kwa kupambwa kwa maneno mazuri aliyoyataja Shetani, na ndiyo maana Yesu alishinda. Kushinda kwa Yesu si kwa sababu ya kuyaelewa maneno ya Shetani bali ni kufahamu maana ya maneno yale kwa tafsiri ya rohoni. Kwa hiyo huwezi kuona ubaya wa kuwa na girlfriend au boyfriend usipokuwa na ufahamu wa rohoni ambao ndiyo unaotuwezesha kutambua maana halisi zilizofichika.

Hebu jiulize mwenyewe; Unaposema girlfriend au boyfriend wangu ndani yako, moyoni mwako huwa unajisikiaje, unapata hisia gani na huwa unafikiri nini hasa akilini mwako unapotamka hivyo?

Posted by Adriano at 5:38 AM No comments:

IJUE SIRI YA GIRLFRIEND NA GIRLFRIEND -2

UPENDO NI NINI?
Mara nyingi vijana hudanganyana kwa kuambiana nakupenda lakini hawajui nini maana halisi ya upendo au wakati mwingine wanakuwa na upendo wa kinafiki. Upendo ni hali ya ndani ya moyo au nafsi na huelezwa kwa maneno na kwa matendo makuu mazuri yafanywayo kutoka ndani ya moyo. Upendo hauangalii gharama za kufanya tendo la upendo. Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”

Kiasi cha upendo uliokuwamo ndani ya Mungu kwa mwanadamu, ndiyo uliomfanya Mungu kuwa tayari kumtoa mwanawe, tena wa pekee, maana yake hakuwa na mwingine lakini alimtoa kwa ajili ya uzima wetu. Kiasi cha upendo uliokuwamo ndani ya moyo wa Ibrahimu, alivyompenda Mungu ndiyo uliomfanya Ibrahimu kuwa tayari kumtolea Mungu mwamawe Isaka awe sadaka ya kuteketezwa, japo alikuwa ni mwana pekee tena aliyempata uzeeni. Si jambo rahisi lakini upendo hauhesabu gharama iliyopo katika kutenda. Maana upendo huambatana na imani ndani ya mtu. 1 Korintho 13:4-8 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu, hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wowote;…”

Kiasi cha upendo uliokuwamo ndani ya Yesu kwa mwanadamu, ulimfanya Yesu kuwa tayari kuutoa uhai wake, akafa msalabani kwa ajili yetu. Sasa mpendwa msomaji unaweza ukaelewa nini maana ya halisi upendo. Wenzetu husema ‘To love is a very great responsibility’ Siku hizi watu wengi hutumia neno nakupenda ili kukidhi haja ya tamaa zao, hawana upendo ila ni unafiki mtupu umejaa ndani mwao. Pendo lisiwe na unafiki….
SHETANI HUTUMIA MANENO MAZURI
Mara nyingi Shetani hutumia maneno mazuri, aidha yameanzishwa na Mungu au ya kibiblia ili apate kuwapoteza watu wengi. Na vijana wengi hawajui jambo hili na hivyo wengi wao hujikuta mikononi mwa Shetani na hawajui cha kufanya na mwishowe huangamizwa kabisa. Tazama mifano ifuatayo;

· Neno mpenzi lina maana nzuri ki-Biblia, 1 Kor 7:1 “Basi wapenzi wangu kwa kuwa tuna ahadi hizo na tujitakase” Maana yake anawapenda mno. Rumi 9:25 “…nitawaita watu wangu wale wasio watu wangu, na mpenzi wangu yeye asiye mpenzi wangu”

Mpenzi ni mtu yule umpendaye sana na sio upendo wa kinafiki. Si rahisi kutambua ukweli wa maneno unayoambiwa na mtu, ni lazima uwe na macho ya rohoni na ufahamu wa rohoni. Maana Roho wa Mungu ndiye ajuaye mambo yaliyo ndani ya moyo wa mtu. Wapo vijana wengi ambao huambiana ‘naomba uwe mpenzi wangu’ ila ndani yao hawana nia nzuri’ Sasa wewe utajuaje kuwa huyo anayekutaka uwe mpenzi wake ana nia mbaya na wewe na ametumia neno zuri, mpenzi au nakupenda? Roho Mtakatifu anahitajika.

· Girlfriend na Boyfriend ni maneno mazuri kabisa, huyatumia kwa maana ya kwake na kuwafanya vijana waingie kwenye mtego wake bila kujua. Ni lazima umuelewe Shetani na mbinu zake ndipo utakapoweza kumshinda kwa kutumia neno la Mungu. Maana Shetani hujigeuza, unashangaa!! Soma 2 Kor 11:14 “Wala si ajabu, maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru”

Tunapotega samaki huwa tunaweka chakula chao kwenye ndoana ili wavutiwe na hatimaye wananaswa na ndoana. Vilevile katika kutega ndege au panya ni lazima uweke chakula kidoga, ambacho kitawavutia na hivyo huweza kunaswa na mtego kirahisi. Sasa na Shetani naye huweka vitu vizuri katika mambo mbalimbali kuwavutia vijana na wengi wao hunaswa na mtego kwa kuona vitu vizuri badala ya kuona mtego, maana macho yao ya rohoni hayaoni yametiwa giza . Na mara nyingi huwa hawana neno la kutosha ndani yao na hivyo hutumia akili zao kujaribu kupambanua kila kitu. Mpendwa naomba ujiulize, hivi kwa akili yako binasi bila msaada wa Mungu unaweza kujua na kutambua kuwa anayekuomba uwe mpenzi wake hakudanganyi au hana pendo la kinafiki?
JE NI VEMA KUWA NA GIRLFRIEND AU BOYFRIEND?
Vijana wengi hujiuliza swali hili. Na wengi wao huona kuwa ni vema tena yafaa, lakini hawajui maana halisi ya girlfriend na boyfriend na wala hawajui zilianzaje. Kama nilivyokueleza hapo mwanzo, Shetani hutumia maneno mazuri akiwa na maana ya kwake tofauti tena mbaya ili awateke watu. Kabla ya kulijibu swali hili na kueleza maana ya girlfriend na boyfriend na chanzo chake kibiblia ni vema ufahamu undani juu ya mapenzi na jinsi Mungu alivyoweka utaratibu wa mapenzi katika maisha ya kila mtu.

Posted by Adriano at 5:33 AM No comments:

IJUE SIRI YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND -1

UTANGULIZI
Mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa injili ya Kristo, Wafilipi 1:27
Na ashukuriwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye aliyeniwezesha kuandika kitabu hiki. Kitabu hiki kitakuwezesha na kukusaidia kuelewa undani wa Girlfriend na Boyfriend na kuona njia ipasayo ya uzima. Vijana wengi siku hizi huambiana nakupenda lakini hawajui nini maana halisi ya UPENDO au huambiana hivyo kiunafiki tu. Ni vema ufahamu utaratibu wa mapenzi jinsi ulivyopangwa na Mungu katika maisha yako. Maana huo utaratibu umewekwa ndani ya moyo wako tangu enzi, na wengi hawafahamu jambo hili. Muhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake tena ameifanya hiyo milele ndani ya mioyo yao , ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya tangu mwanzo hata mwisho.
KWA NINI MUNGU AMEUMBA TOFAUTI ZA JINSIA?

Tendo la kujamiiana au tendo la ndoa limewekwa na Mungu mwenyewe kwa makusudi maalum na kwa utaratibu mzuri kabisa. Mungu hakuweka tofauti za jinsia kwa mwanadamu peke yake, bali pamoja na viumbe wengine. Lakini pana tofauti kubwa ya makusudi halisi ya kuweka tofauti kwa mwanadamu na kuweka tofauti hizo kwa viumbe wengine.

Mwanzo 1:20-25, “Mungu akasema maji nayajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu… na kila ndege arukaye kwa jinsi yake. …Mungu akasema nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake… na wanyama wa mwituni kwa jinsi zake ikawa hivyo”

Mungu anaposema kwa jinsi zake maana yake viumbe vyenye jinsia na namna tofauti. Aliumba namna hizo tofauti kwa NENO tu, lakini mwanadamu aliumbwa kwa neno (na tumfanye mtu kwa mfano wetu…) na kwa vitendo. Maana Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi na akamfanya mwanamke kwa kutumia ubavu wa mwanamume. Uumbaji wa mwanadamu ni tofauti sana na viumbe wengine.

Viumbe wengine wote waliumbwa kwa jinsia na namna tofauti kwa ajili ya kuendeleza uumbaji (recreation) na pia kwa matumizi ya mwanadamu. Mojawapo ya sababu za kuumbwa kwa mwanamke na mwanamume ni;
Kuendeleza uumbaji wa Mungu
Kuvitawala vitu vyote
Kuitiisha nchi
Kusaidiana

Mwanzo 2:18, “Bwana Mungu akasema si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi a kufanana naye” Wanyama hawakuambiwa hivi.

Mungu anapofanya kitu huwa na kusudi na utaratibu maalum wa alichokifanya. Tendo la ndoa liliwekwa na Mungu kwa makusudi maalum na aliweka utaratibu wake na malengo maalaum. Tendo la ndoa limekuwa chanzo cha matatizo mengi makubwa kwa mwanadamu si kwa sababu tendo la ndoa ni baya, ila ni kwa sababu watu wanalifanya nje ya wakati wa Mungu, na wanalifanya isivyotakiwa yaani kinyume na utaratibu na makusudi ya Mungu. Wengi huwa hawajui ya kuwa tendo la ndoa linatakiwa kufanywa kwa utukufu wa Mungu. Kwa mwanadamu tendo la ndoa huwaunganisha watu wawili wa jinsia tofauti kuwa mwili mmoja na huambatana na furaha ya hisia za ndani ambazo hukamilishwa kwa UPENDO. Ndiyo maana wavulana wengi wanapokuwa wakitongoza husema NAKUPENDA, ila siku hizi hata wasichana hutongoza. Hii ni kwa sababu upendo hukamilisha ndoa. Ndoa ni moja ya jambo ambalo Mungu amempa mwanadamu ili limpatie mwanadamu furaha na kamwe sio kwa ajili ya huzuni, hasira au matatizo. Lakini siku hizi ndoa imekuwa kama mwiba; maana watu wengi hudhani ndoa ni kama sehemu ya starehe na hawaichukulii ndoa kama sehemu ya kumtukuza Mungu.

Upendo chanzo chake halisi ni Mungu mwenyewe. Tangu enzo ya uumbaji Mungu alimpenda mwanadamu, na ndiyo maana mwanadamu alipoasi Mungu hakumwangamiza mara, bali alimwokoa na kuurejesha upendo halisi kwa njia ya Yesu Kristo. Katika Biblia Yesu ni Bwana arusi na kanisa ni Bibi arusi, na ndiyo maana kuna upendo wa ajabu wa Yesu kwa kanisa.Jamani hii ni copy na paste kutoka, KARIBU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU PAMOJA nimeona itawasaidia wengi humu.MUNGU AWABARIKI SANA!!
 
M

mtengwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Messages
1,746
Likes
240
Points
160
M

mtengwa

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2011
1,746 240 160
Nimechukua muda mrefu kusoma ba kutafakari. Nimejifunza mengi sana, pia imenitia moyo na kusema na mimi kuhusu ujana wangu. Mungu nisaidie nienende njia unayoitaka
 
Cataliyya

Cataliyya

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Messages
664
Likes
238
Points
60
Age
32
Cataliyya

Cataliyya

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2015
664 238 60
Nimechukua muda mrefu kusoma ba kutafakari. Nimejifunza mengi sana, pia imenitia moyo na kusema na mimi kuhusu ujana wangu. Mungu nisaidie nienende njia unayoitaka
Amina mtumishi ubarikiwe, hili ni somo ndio maana ni refu
 
projectman

projectman

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Messages
313
Likes
113
Points
60
projectman

projectman

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2015
313 113 60

ukweli mtupu!
 
griffin2

griffin2

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
557
Likes
664
Points
180
Age
48
griffin2

griffin2

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
557 664 180
ubarikiwe mtumishi lakini sidhani kama watasoma
 
Illuminata Rodgers

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Messages
2,377
Likes
1,421
Points
280
Illuminata Rodgers

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2015
2,377 1,421 280
Duuh yataka moyo kusoma
 
Forum statistics

Threads 1,237,971
Members 475,809
Posts 29,308,375