Uislamu ni project ya wakatoliki

Sijaona swali lolote ,mada mlijibiwa mkakimbia

Kila siku nawauliza, kwanini Quran ziliharibiwa ,ikakusanywa moja ,nyingine zilikuwa na shida gani?


Je matini au Manuscript ya Uthman ipo wapi
Huwezi kunikimbiza au hata mada yako hakuna ya kunikimbiza.Hili nilishakujibu na hapa nakujibu tena. Uje tena usema hukujibiwa.

Hapa nakujibu kwa swali, ziliharibiwa na kina nani na ilikuwa lini ?

Kukusanywa kwa Qur'an nilikupa sababu Ile siku na sio sababu ya kuharibiwa kama unavyo sema wewe. Huwa najiuliza habari za Waislamu huwa unazisoma wapi ? Huenda unazisoma kwa wale ambao sio Waislamu au kwa maadui Waislamu.

Ile siku nilikujibu ndio maana ukakimbia, nilikwambia sijui matini Iko wapi. Lakini alichokifanya swahaba Uthman ni kuandika nakala nyingine tano na kuzitawanya katika Ile mini mitano, huku akiwatuma na walio ihifadhi Qur'an Ile, ili wakawafundishe watu husika.

Lakini kwetu sisi hatuna haja tena na Matini hiyo, sababu kuwepo kwake na kutokuwepo kwake ni sawa, tangu Mtume yuko hai Qur'an ilikuwa inahifadhiwa vifuani mwa watu. Ndio maana ukisoma habari za viraa utaona chain inafika mpaka kwa Mtume, na kwa njia nyingi.

Sasa usije tena ukasema hujajibiwa swali au maswali yako. Wewe ndio hujibu maswali ninayo kuuliza.
 
Bado unajichanganya sana na unazalisha maswali zaidi

1. Kama Qur’an ilikuwa vifuani tu, kwa nini Abu Bakr alikusanya maandishi baada ya vita vya Yamama?

2. Kama Qur’an haijawahi haririwa, kwa nini Uthman aliamuru kuandikwa upya na kufuta tofauti za usomaji?

3. Kama nakala zote zilikuwa sawa, kwa nini Uthman azichome?

4. Je, unaweza kutaja msururu wa usomaji (chain of qiraa) unaofika kwa Mtume moja kwa moja bila kupitia kwa sahaba aliyeandika au kusoma?

5. Kama matini ya Uthman haina umuhimu, kwa nini leo Waislamu wote duniani wanasoma Qur’an hiyo hiyo ya Uthman?
 
Kula chuma hicho makerubi wa Mwamposya
 

Attachments

  • Screenshot_20250506-110721.jpg
    346.4 KB · Views: 15

View: https://m.youtube.com/watch?v=UIimWL8wEs8&pp=ygULY3Jvd24gbWVkaWHSBwkJhQkBhyohjO8%3D
Huyu mwamba Chionda nimemvulia kofia kwenye uelewa wake wa maswala ya dini.

Ku-appreciate uelewa wake zaidi inabidi uwe unafuatilia hayo mambo.

Nikiwa kama mfuatiliaji mkubwa wa documentary za ancient civilisation na religious archeology (kwa week lazima niangalie si chini ya documentary tatu).

Chionda nimemvulia kofia, kuangalia documentaries sawa; ila kuweka kichwani info zote alizonazo kama yeye hata kama hana formal qualification jamaa ni serious scholar wa social and religious anthropology anajua mambo mengi mno kushinda hata hao western scholars.

Yaani kuna vitu ameongea inabidi nikipata wasaa nitafutie documentary.

Heshima yako Chionda, ni nadra sana kukutana na mmbongo ambae topic anayoiongelea anaijua in depth. Interview aikuwa fair kwa sababu interviewer hakuwa na uelewa wa mpana wa topić kumchimba Chionda aende deeper naamini ni more knowledgeable kushinda maswali aliyokutana nayo.
 
Tofautisha kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa katoliki la Roma.
Hayo ni Makanisa mawili tofauti.
 
Mudy mwenyewe alizaliwa Pagan, Baba zake Pagan wanaabudu sanamu.
 
. Kama Qur’an ilikuwa vifuani tu, kwa nini Abu Bakr alikusanya maandishi baada ya vita vya Yamama?
Alikusanya kwa ajili ya vizazi vijavyo, na hii sababu ya viongozi wote. Sababu wasomaji walikuwa wanakufa.
2. Kama Qur’an haijawahi haririwa, kwa nini Uthman aliamuru kuandikwa upya na kufuta tofauti za usomaji?

Si kweli habari hizi unazipata wapi ?

Aliamuru kuandikwa baada ya kupewa ushauri na swahaba Hudhaifa bin Al Yamani, kwa kuchelea vifo vya wali hifadhi Qur'an. Na UISLAMU ulikuwa umetangaa mini mingi na mikubwa kwahiyo ikaandikwa kwa ajili ya kutawanya.

Kingine habari za kufutwa ndio nazisikia kwako ndio maana najiuliza hizi habari huwa unazitoa wapi ?

Uthman hakufua bali alizokisanya lahaja zote sehemu Moja, ili isije huko mbele ikaleta shida kwa Waislamu, endapo wakisikia huyu anasoma hivi na yule anasoma vile. Ndio maana vikawepo viraa kumi.

Kingine, nakuomba ujibu maswali ninayo kuuliza, sio unauliza tu maswali na hujibu unayo ulizwa.
3. Kama nakala zote zilikuwa sawa, kwa nini Uthman azichome?
Habari ya kuzichoma hizo nakala umezitoa wapi ? Na ni nakala gani zilizo chomwa ?
4. Je, unaweza kutaja msururu wa usomaji (chain of qiraa) unaofika kwa Mtume moja kwa moja bila kupitia kwa sahaba aliyeandika au kusoma?
Bila shaka kabisa naweza.
5. Kama matini ya Uthman haina umuhimu, kwa nini leo Waislamu wote duniani wanasoma Qur’an hiyo hiyo ya Uthman?

Unaposema kwanza Qur'an ya Uthman unaelewa maana yake ?

Hatusemi Haina umuhimu, bali hiyo ndiyo iliyo tangaa na ndio inayo tumika, japokuwa kipindi inakusanywa haimaanishi maswahaba hawakuwepo Wala hawakuwa na wanafunzi, la hasha Ile iliandikwa kwa ajili ya watu wengine wa mini tofauti.
 
Muhammad mwenyewe alizaliwa akiwa mpagani yeye na familia yake yooote na mababu zake.....mkuu dini tunazikuta Duniani hatuzaliwi nazo.
 
Kijana huu uzushi wenu imebaki kwenu nyie maamuma ,ndio maana ule mjadala wa sheikh Muhammad Hijab na Qadhi ,walisema kwa nyie maamuma inatakiwa mdanganywe kuwa Quran haijawahi kubadilika

Maswali yangu unaruka ruka tu ,NARUDIA Tena

1. Ikiwa Qur'an haijawahi kubadilika, unawezaje kuelezea tofauti za lahaja (qira'at) zilizokuwepo kabla ya kuunganisha msahafu mmoja katika utawala wa Uthman bin Affan?
(Mfano: Kisomo cha Ibn Mas'ud, Ubay bin Ka'b na wengine kilikuwa tofauti katika baadhi ya maneno – je, hizi tofauti zilifutwa vipi?)

2. Je, unafahamu kuwa Uthman aliamuru kuchomwa kwa nakala zote nyingine za Qur’an ili kubaki na msahafu mmoja pekee? Unadhani ni kwa nini alifanya hivyo kama Qur’an zote zilikuwa sawa?

3. Je, una ushahidi kwamba kila aya ya Qur’an ya sasa ilikuwa katika nakala za mwanzo kabisa zilizokusanywa katika zama za Abu Bakr? Au kuna aya ambazo zilijulikana kwa baadhi tu ya maswahaba?

4. Ikiwa Qur'an haijawahi kubadilika hata herufi moja, kwa nini tunakuwa na matoleo tofauti ya qira’at kama Hafs na Warsh? Na je, tofauti hizi zilitoka wapi?

5. Ikiwa Qur’an ni ile ile kutoka kwa Mtume (s.a.w) hadi sasa, una ushahidi gani wa maandiko ya asili (manuscripts) kutoka karne ya 1 au ya 2 Hijri yanayolingana kwa asilimia 100 na Qur’an ya leo?

6. Katika historia ya Usahihi wa maandiko (textual criticism), ni kawaida maandiko ya kale kupitia uhakiki wa mabadiliko madogo madogo. Je, Qur’an imetoka vipi kwenye utaratibu huo wa kihistoria kama maandiko mengine ya kale?
 
mimi nimeisoma hii comment kama ilivo mkuu -- haikumake sense, wewe ni mtaalamu sana emu iangalie ina make sense?
Ina make sense , uislamu kama dini ,ni dini mpya,

Quran hii ya hafs imekusanywa juzi tu hapo misri mwaka 1924

,haya nakaribisha maswali sasa
 
Ina make sense , uislamu kama dini ,ni dini mpya,

Quran hii ya hafs imekusanywa juzi tu hapo misri mwaka 1924

,haya nakaribisha maswali sasa
mtalaamu ile comment stand-alone haiwezi make sense
 
But mimi naona waislamu wengi ndo misukule ya waarabu,
 
Dini sahihi inafundisha chuki? au mungu wenu ndo alisema mchukie watu wengine
 
Kijana huu uzushi wenu imebaki kwenu nyie maamuma ,ndio maana ule mjadala wa sheikh Muhammad Hijab na Qadhi ,walisema kwa nyie maamuma inatakiwa mdanganywe kuwa Quran haijawahi kubadilika
Naendelea kusisitiza ili mjadala uwe na maana. Unatakiwa ujibu maswali ninayo kuuliza.

Huyo Muhammad Hijab sio msomi wa dini zaidi ya kujikita kwenye Falsafa. Ndio maana nakushangaa na hutaki kujibu maswali ninayo kuuliza.

Uzuri dini yetu sio kama yenu, sisi tunahimizwa kusoma dini na kuifatilia na kuuliza.
Maswali yangu unaruka ruka tu ,NARUDIA Tena
Hakuna swali nililo ruka. Ili uonyeshe kama nimeruka swali, usibadilshe swali. Bali onyesha wapi nimeruka.

Hili ni swali lingine ndio maana nakwambia hakuna swali ambalo sijakujibu. Unatakiwa uwe mkweli kweli maneno na unayo yaandika.

Umeuliza swali la kijinga na linaonyesha wazi huna unachokijua katika hili.

Hivyo viraa vyote vikisomwa Mtume yuko hai, ndio maana ya kuwa Qur'an imeshuka kwenye herufi Saba, yaani ndimi Saba tunasema lahaja. Kama hujui maana ya lahaja, ni mfano kwa sisi Waswahili, Kiswahili Cha Kiamu, macho husemwa mato. Matamshi yanakuwa tofauti ila maana ni Moja. Ndio maana ndimi zote hizo zikahifadhiwa kwa maandishi zama za swahaba Uthmani.

Hakuna tofauti zilizo futwa, bali ndio kazi aliyo ifanya swahaba Uthman, kuzikusanya ndimi zote Saba katika nakala Moja, ili isije kuonekana ni jambo gani au likaleta utata kwa vizazi vijavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…