Uislamu ni project ya wakatoliki

Uislamu ni project ya wakatoliki

Luka 1:15
Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

Sasa atajazwa roho mtakatifu tangu akiwa tumboni Kwa mama yake Ili iweje kama sio kuzaliwa na dini?

Yani anazaliwa akiwa tayari ameshawekewa muongozo wa kuufata na huo muongozo ndio dini yenyewe
Basi sawa kama hivyo ndo unavyoielewa hiyo Aya. Lakini sijaona kama hayo maneno yanaeleza kuhusu uislam.

Twende unavyotaka, hiyo Aya inamaanisha kila mtu anazaliwa akiwa muislam kama mnavyofundisha?
 
Mm nikimbie mada ? Utakuwa unanifananisha , waislamu ndio hamna elimu kuhusu dini yenu maana mmedanganywa mengi
Nenda kajibu Yale maswali niliyo kuuliza kwenye Ile mada.

Sasa si bora wewe ungekuwa unapatia katika unayo yaandika. Shida unakosea sana, mpaka tunawapa watu uvivu wa kukujibu. Sababu una makosa mengi.
 
Yani wakatoliki waanzishe uislamu alafu badae waangaike kutaka kuufuta kwenye uso wa dunia? Ivi wakatoliki wao walikua na hamasa gani iliyowapelekea kuanzisha project ambayo baadae ikaja ikawaathiri
wao wenyewe? Ivi unajua uislamu ulichangia kuanguka kwa utawala wa Roma uko mashariki ya kati ?
 
Nenda kajibu Yale maswali niliyo kuuliza kwenye Ile mada.

Sasa si bora wewe ungekuwa unapatia katika unayo yaandika. Shida unakosea sana, mpaka tunawapa watu uvivu wa kukujibu. Sababu una makosa mengi.
Sijaona swali lolote ,mada mlijibiwa mkakimbia

Kila siku nawauliza, kwanini Quran ziliharibiwa ,ikakusanywa moja ,nyingine zilikuwa na shida gani?


Je matini au Manuscript ya Uthman ipo wapi
 
Kwa karne nyingi, uhusiano kati ya Ukatoliki na Uislamu umekuwa wa mvutano na wakati mwingine wa ushirikiano wa ajabu. Madai ya aliyekuwa padri wa Kanisa Katoliki, Dr. Alberto Rivera, yameibua mjadala mzito kuhusu chanzo halisi cha Uislamu. Rivera alidai kuwa Vatican ilikuwa na mkono wa moja kwa moja katika kuanzisha dini ya Kiislamu, kama mpango wa kisiasa na kiroho wa muda mrefu wa Kanisa wa kupata udhibiti wa Mashariki ya Kati.

Madai ya Alberto Rivera Kuhusu Chanzo cha Uislamu

Katika mahojiano,Padre Rivera alieleza kuwa alipokuwa ndani ya Vatican, alifunuliwa kuhusu mpango wa siri wa kuunda dini mpya ya Kiarabu ili kuwapa Wakatoliki udhibiti wa Yerusalemu, kuwachochea Waarabu dhidi ya Wayahudi, na baadaye kuwaunganisha Waislamu na Wakatoliki kupitia heshima ya Mariamu. Rivera alisema:

“Vatican created Islam in the 7th century to control the Arab world and to create a military power that could seize Jerusalem for the pope.”

Aliongeza kuwa Muhammad alifunzwa na wakristo wa mashariki waliokuwa na mwelekeo wa Roma, na hakuwa na ufahamu wa kina wa Injili bali alipewa mwelekeo wa kuanzisha dini inayompinga Kristo lakini inayohifadhi baadhi ya mafundisho ya Mariamu.

Historia inaonyesha kuwa Waarabu walikuwa na mahusiano na Wakristo kabla ya Uislamu. Mmoja wa watu waliokutana na Muhammad akiwa kijana ni mmonaki aitwaye Buhaira, ambaye alitambua “alama ya kinabii” kwa Muhammad na kumhimiza alindwe. Baadhi ya wachambuzi wa kihistoria wanasema Buhaira alikuwa na mafungamano na taasisi ya Kikristo ya Kirumi, au angalau alikuwa chini ya ushawishi wa Roma kupitia matawi ya Ukristo wa mashariki.

Katika maandiko ya Patrologia Latina, inaelezwa kuwa Kanisa Katoliki lilikuwa na misheni mbalimbali za siri zilizokuwa zikifanya kazi katika maeneo ya Mashariki, ikiwemo Arabia. Mapadri hawa walihubiri Mungu mmoja lakini waliepuka kulazimisha Injili kikamilifu, jambo ambalo linawiana na madai ya Rivera kwamba

“The Vatican only gave the Arabs partial truth and kept the rest hidden to form a controllable religious bloc.”

Kitabu kitakatifu cha Waislamu, Qur’an, kinamtaja Mariamu kwa heshima ya kipekee, na anatajwa zaidi ya wanawake wote, hata kuliko kwenye Biblia. Muhammad anafundisha kuwa Mariamu alizaliwa bila dhambi, jambo ambalo linashabihiana sana na mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu

“Immaculate Conception”.

“And [mention] when the angels said, ‘O Mary, indeed God has chosen you and purified you and chosen you above the women of the worlds.’” (Qur’an 3:42)

Rivera alitumia hoja hii kama ushahidi wa kuwa Kanisa lilipandikiza ibada ya Mariamu ndani ya Uislamu kama chombo cha baadaye cha kuunganisha dini hizo mbili. Katika moja ya project zake alieleza

“This was the Vatican’s secret weapon: Mary. The Muslims would one day unite with Catholicism under her name.”

Zaidi ya hayo, Fatima mji wa Ureno ambako Bikira Maria aliripotiwa kuwatokea watoto mwaka 1917 umepewa jina sawa na binti wa Muhammad.

Hili linatajwa na wachambuzi wa historia ya dini ya kama hatua ya kimakusudi ya kuunganisha heshima ya Mariamu kati ya Wakatoliki na Waislamu.

Tukio la Fatima linatajwa sana na Wakatoliki, huku pia jina hilo likiwa na nafasi ya kipekee kwa Waislamu, na linazidi kuonesha muktadha wa Mariamu kama daraja la kidini kati ya dini hizo mbili.

Katika kitabu The Prophet cha Catholico Ahmed Zaki Yamani, imeandikwa kuwa maendeleo ya Uislamu katika karne ya 7 yalikuwa ya ajabu na yalikubalika haraka katika maeneo ya ki-Bizanti.

Padre Rivera alidai kuwa hili liliwezekana tu kwa sababu ya mkono wa Kanisa, likitumia Uislamu kama njia ya kudhibiti upanuzi wa Ukristo wa Kiprotestanti na Uyahudi katika Mashariki ya Kati. Anasema...

“The Pope realized he could use Islam as a sword against the Jews and the true Christians.” — Rivera.

Kwa mujibu wa kitabu Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps, hata baada ya kuanzishwa kwa Jesuit karne nyingi baadaye, ushahidi wa ushirikiano wa siri kati ya Vatican na Uislamu uliendelea kuwepo kupitia mikutano ya kisiasa, misimamo ya pamoja dhidi ya Israeli, na ushawishi wa Mariamu.


Alexander Hislop, katika kitabu chake maarufu The Two Babylons, anaeleza kuhusu asili ya mafundisho ya kipagani yaliyofichwa ndani ya Ukatoliki,

inadaiwa kuwa wakati Papa alipokamatwa na maadui wa Kanisa, walikuta maneno ya Kiislamu (Shahada) yakiwa yameandikwa kwenye kiti cha enzi chake

“La ilaha illa Allah, Muhammadur Rasulullah”

maandishi haya yalikuwa sehemu ya usiri wa mafungamano ya kidini yaliyolenga kuunganisha dini kubwa za dunia kwa ajili ya lengo la kisiasa la Kanisa.


Heshima ya Mariamu katika Ukatoliki na Uislamu, na Mji wa Fatima

Uislamu unampa Mariamu (Maryam) heshima kubwa, hata kuliko Biblia yenyewe. Yeye ndiye mwanamke pekee aliyatajwa kwa jina ndani ya Qur’an, na sura nzima (Surah Maryam) imetengwa kwa ajili yake. Qur’an inaeleza:

“Na kumbuka waliposema Malaika: Ewe Mariamu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na amekutakasa, na amekuteua juu ya wanawake wote wa ulimwengu.” (Qur’an 3:42)

Hii inafanana na mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu Immaculate Conception, kwamba Mariamu alizaliwa bila dhambi ya asili na alibeba Yesu kwa usafi kamili wa kiroho.

Mjini Fatima, Ureno, ndiko ilikodaiwa kuwa Bikira Maria alimtokea msichana mmoja mwaka 1917. Tukio hili lilipewa umuhimu mkubwa sana na Vatican. Kinachovutia zaidi ni kwamba jina "Fatima" ni jina la binti wa Mtume Muhammad. Wachambuzi wa kiroho na historia wanaamini kuwa kuchaguliwa kwa mji huo na matokeo yake yalikuwa na lengo la kufanikisha uhusiano wa kihisia kati ya Waislamu na Wakatoliki kupitia Mariamu/Fatima, ikimaanisha kwamba ibada ya Mariamu inaweza kuwa daraja kati ya dini hizo mbili.


Katika karne ya 20 na 21, kumekuwa na matukio kadhaa ya kihistoria ambapo Mapapa wamekutana na viongozi wa Kiislamu, wakashiriki ibada pamoja na hata kuweka mikakati ya ushirikiano wa kidini.

Mwaka 2019, Papa Francis alizuru UAE na kusaini "Document on Human Fraternity" pamoja na Sheikh wa Al-Azhar. Huu ulikuwa mkutano wa kihistoria unaoonyesha jinsi viongozi wa Kidini kutoka Ukatoliki na Uislamu wanavyojenga daraja la ushirikiano, wakiweka mbele maadili ya amani, umoja, na haki za binadamu. Huu ni mfano wa juhudi za kukuza uelewa na mashauriano kati ya dini hizo mbili kubwa, ingawa bado kuna maswali na shaka kuhusu umoja wa kweli wa kidini.
Kitendo Cha wakristo khshusha thread nyingi dhidi ya waislamu Kuna mazingatio kwa mwenye akili

Kiufupi mmeshindwa kuitetea DINI YENU
 
Yani wakatoliki waanzishe uislamu alafu badae waangaike kutaka kuufuta kwenye uso wa dunia? Ivi wakatoliki wao walikua na hamasa gani iliyowapelekea kuanzisha project ambayo baadae ikaja ikawaathiri
wao wenyewe? Ivi unajua uislamu ulichangia kuanguka kwa utawala wa Roma uko mashariki ya kati ?
Ni sababu huna elimu na historia,na hujui kuunganisha dot ,

Uislamu ulikuja kuwageuka Catholic,japokuwa kwasasa umeshasalenda, Pale Saudi Arabia tayari pashawekwa pupet wao na Sasa taratibu Saudia Arabia inaenda kuwa kama Ulaya,


Dola ya Byzantine, kama muendelezo wa Dola ya Roma Mashariki, ilikuwa na mamlaka ya kidini na kisiasa. Baada ya Mfalme Constantine kuhalalisha Ukristo katika karne ya 4, Ukristo ukawa dini rasmi ya dola.

Kwa muktadha huu, Wakristo wa Byzantine walihitaji udhibiti juu ya maeneo matakatifu kama Yerusalemu, ambayo yalikuwa yakisumbuliwa na Wayahudi waliopinga ukristo.

Katika mazingira haya, Waarabu waliokuwa wanaishi kandokando ya Himaya ya Byzantine walikuwa washirika muhimu, kama vile Waarabu wa Ghassanid, ambao walikuwa Wakristo waliowekwa kama ngome ya kinga dhidi ya Waarabu wa kipagani na Wapersia.

“The Ghassanids, a Christian Arab tribe allied with Byzantium, were instrumental in defending the Empire’s southern borders.”
— Irfan Shahîd, Byzantium and the Arabs in the Sixth Century


Hii inathibitisha kuwa kabla ya Uislamu, kulikuwa na ushirikiano wa karibu kati ya Wakristo wa Byzantine na Waarabu wa Mashariki ya Kati.


Wakati Waislamu wa mwanzo walikimbilia Ethiopia (Hijra ya Kwanza), walipewa hifadhi na Negus (al-Najāshī), Mfalme Mkristo wa Dola ya Aksum. Hili linaonyesha kwamba Uislamu haukuonekana kama tishio la moja kwa moja kwa Wakristo wa wakati huo, bali kama harakati ya karibu na Ukristo.

“The King of Abyssinia, who was a Christian, granted the Muslims asylum and protection…”
— Ibn Ishaq, Sirat Rasul Allah



Hali hii ya ushirikiano wa awali kati ya Wakristo na Waislamu inaibua maswali: Je, ni kwa nini wakubali dini mpya, kama haikuwa na agenda za pamoja? Je, kulikuwa na mpango mpana wa kisiasa?

Katika nyakati za kisasa, Mapapa kama John Paul II na Francis wamekuwa wakisali katika misikiti kama ishara ya "maelewano ya kidini." Papa John Paul II alisali katika msikiti wa Umayyad mjini Damascus mwaka 2001, na Papa Francis alifanya hivyo Istanbul na Abu Dhabi.

Je, hii ni juhudi za kisasa tu? Au ni mwendelezo wa uhusiano wa kihistoria wa muda mrefu? Je, hii inaashiria kuwa Kanisa Katoliki lina nafasi ya kipekee katika historia ya Uislamu? Nakuachia maswali


Wayahudi walikuwa na historia ndefu ya mvutano na Wakristo wa Byzantine, hasa kuhusu suala la utambulisho wa Yesu. Wakati Wayahudi walikataa Kristo kama Masiya, Wakristo waliona hiyo kama uasi wa kiroho. Inawezekana kabisa kuwa majaribio ya Byzantine kudhibiti Wayahudi yalijumuisha kuunda nguvu mbadala dini ambayo inamtambua Yesu kama nabii, lakini si Mungu jambo ambalo Uislamu unalifanya.

Baada ya Mtume Muhammad, Waislamu walifanikiwa kuvamia na kuchukua maeneo makubwa ya Dola ya Byzantine, kama Syria, Misri, na Palestina.

“The Muslim conquest of the Levant and Egypt dealt a major blow to the Byzantine Empire.”
— Hugh Kennedy, The Great Arab Conquests, 2007

“Project ilipogeuka, ikawa hatari kwa waliyoianzisha.”
 
Ndio nini sasa, umedandia gari kwa mbele hakuna ukijuacho bora ukae kimya.
Nisichokijua nikipi hujui mwanzo wa vitu kabla ya kila kitu hata agano jipya kuwepo uislam ulikuwepo why kwasababu ndio dini ambayo mtoto wa ibrahim wa kwanza aliyetolewa bomani kwa baba yake baada ya Mungu kusema atolewe anatakiwa kuzaliwa mtoto kama mtoto wa ibram kwenye tumbo la sara ndio akafukuzwa akazaliwa issaka.

Hapo sasa huyo mtoto akatafuta Dini ingine ya kumuabudu Mungu sio hiyo ya babae kwa hasira kwa hiyo alipata majini yakamsaidia nakumuongoza katika uandikaji wa kurahani na vingine.

Akaanza kumuabudu Mungu kupitia hiyo dini yake . Akaoa nakuoa zaidi ya mke mmoja akakua katika dini yake mwenyewe alioanzisha yeye namama yake.

Sasa kama unasema eti ni wakatoliki zamani DINI iliyokuwepo ni ya wayaudi tu. Na haikuzaa uislamu ni huyo mwenyewe kupitia nguvu za majini ali tengeneza dini yake. So usijidanganye. Kwa kitu hujui......

Wakatoliki hawakuwepo wakati hii dini imeanzishwa ndio pale GAZA alijenga msikiti mkubwa. Wayahudi wanayo kanisa lao pale GAZA na wajukuu ws nje wa Abrahamu ndio wapalestina.

Sasa Africa kama east western south waliletewa tu hii dini sio kwamba wanaijua . Soma historia wewe kengee na vitabu vingine uelewe .

Warabu ambao wengi ni saudi arabia ,ppalestina,hata misri hao ni wajukuu ,vilembwe wa aibraham kwa mtoto wa kwanzaa
 
Kama sio kuwepo Kwa kanisa katoliki na hayo makanisa mengine yote yasinge kuwepo

Hivyo basi ukristo wote ni mpagani
Hacha uongo! Kanisa limeanza wakati wa mitume wa Bwana Yesu, na Rumi ilihusika kuwaua mitume.
 
Paulo ndio aliyoamzisha ukristo na hiyo kazi alipewa na Dora ya roman empire na yeye Paulo ni mrumi

Matendo ya Mitume 22:28
Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.
Unao ushahidi wa Paulo kuanzisha Ukristo?
 
Back
Top Bottom