Uingereza ni nchi gani? Je, ni Britain au England?

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,327
2,000
Mambo mengi humu duniani nayasoma katika English zaidi kuliko kiswahili. Lakini nimekutana na tatizo moja nimeshindwa kulivumilia, wale wenye uwezo nisaidieni.

Ninaposoma katika English, najua kwamba United Kingdom huitwa kwa kifupi UK au Great Britain (GB) na ndimo humo kuna England, Scotland, Wales na Northen-Ireland.

Lakini hiyo UK au Great Britain inapoandikwa kwa kiswahili panaandikwa Uingereza. Lakini wakati huohuo eneo mojawapo la UK liitwalo England utakuta nalo kwenye kiswahili panaandikwa Uingereza!

Ukitazama hata kwenye michezo, utakuta wanasema LIGI YA UINGEREZA, wakati ukweli si ligi ya UK kote, bali ni ile sehemu iitwayo England ambako Scotland kwao na Ferguson hakuguswi.

Hapa mnisaidie. Ukitaja neno Uingereza unakuwa una-refer ni hasa? Je, ni ile England au UK yote?

Je, au haya ndiyo yale ya kumezwa kwenye miungano ambapo unaweza kusema England imewameza akina Scotland na wenzake kiasi kwamba ikitamkwa England basi bila kujali utamaduni wa zingine inamaanisha UK yote.

Kama ni hivyo, basi nchi kama Zanzibar zilikuwa na haki ya kuwa na hofu kama hiyo, maana hata timu ya taifa ya ikiwa haina mzanzibar hata mmoja bado tunaiita TIMU YA TAIFA YA TANZANIA.

Saidia kutafakari?
 
jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,937
2,000
Ukweli wa mambo umeshauleleza hapo juu. England imekuwa maarufu na kuzimeza nchi nyingine za Scotland, Wales na North Ireland.

Hivyo mara nyingi watu wakifanya reference kwa England wanakuta wanatamka UK ama Great Britain hata kwa issue inayohusu England pekee.

Tofauti na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwa Tanganyika haipo na Zanzibar ipo kama kivuli tu hivyo hata jambo linalowahusu Watanganyika pekee bado litasemwa kuwa ni la watanzania, kiasiasa na kijiografia hakuna Tanganyika kwa sasa lakini kwa UK bado Kijiografia Scotland, Wales, North Ireland na England zinatambulika kijiografia.

Na kama umesikia Scotland wapo kwenye mchakato wa kura ya maoni kuona kama waendelee kwenye Muungano ama wajitoe.

Tofauti na malalamishi ya Zanzibar kuwa wanaonewa kwenye Muungano njia sahihi ni kuwa na kura ya maoni na kuamua kama wanataka kuendelea ama la na sio Slogan za ''Mtuache Tupumue''
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,298
2,000
The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland,commonly known as the United Kingdom (UK) or Britain , is a sovereign state located off the north-western coast of continental Europe. The country includes the island of Great Britain (a term sometimes loosely applied to the whole state), the north-eastern part of the island of Ireland, and many smaller islands. Northern Ireland is the only part of the UK that shares a land border with another state: the Republic of Ireland.Apart from this land border, the UK is surrounded by the Atlantic Ocean, with the North Sea in the east, the English Channel in the south and the Irish Sea in the west.
 
Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,952
2,000
Naungana na maelezo ya wachangiaji walionitangulia hapo juu, Jerrytz na Safari ni Safari; kwa kifupi:

United Kingdom = England, Wales, Scotland na Northern Ireland

Great Britain = England, Wales, na Scotland

UK.jpg
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,327
2,000
Sijui kwa nini mmeeleza tofauti na ninavyotaka kujua on contrary mnanieleza ninayoyajua miaka mingi.

Kama ni mifano yenu katika kiswahili basi hata hapa nchini kuna maneno mawili yaani TANZANIA na ZANZIBAR.

Hata kwa kiswahili nikisema USA sipati shida ninaposema Texas, Florida nk ambako ni states ndani ya USA.

Hivi hakuna humu wataalamu wa Kiswahili kuja kunitofautishia UK na England kwa kiswahili, maana hapo mimi ninaona neno moja UINGEREZA.

Msione nimekuja hadi hapa, nimepitia kamusi bado hazinisaidii.
 
Nikupateje, shida yako ni England kwa Kiswahili au?!

Nadhani kuna changamoto hapo maana hata U.S.A tunaita Marekani lakini ukichunguza kwa makini si sahihi kuita hivyo, kama ilivyokuwa kwa USSR ambapo tulikuwa tunaita URUSI na hiyo haikuwa sahihi pia, maana Urusi ilikuwa ni nchi moja wapo tu katika shirikisho la USSR...

Umenifumbua macho katika hili... Ngoja tuone
 
Rolandi

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
900
500
Kama nimekuelewa unataka kujua great britain kiswahili chake ni nini, england kiswahili chake ni nini na united kingdom kiswahili ni nini, au sio?
Ngoja wajuzi watufafanulie
 
mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,994

mbona hapo hamna changamoto yeyote .. mtoa U.S.A ni United states of America.. na AMERICA ni Ameica ka ilivyo ..

Changamoto ipo hapo kwa mtoa Mada na mpaka sasa hamjamjibu swali lake .
 
jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,937
2,000
mbona hapo hamna changamoto yeyote .. mtoa U.S.A ni United states of America.. na AMERICA ni Ameica ka ilivyo ..

Changamoto ipo hapo kwa mtoa Mada na mpaka sasa hamjamjibu swali lake .

Kwahiyo ukisema Marekani= United States of America?!

What about U.A.E - United Arab Emirates = Himalati?! Mbona mnasema Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu

Wewe ni sehemu ya jibu pia katika changamoto iliyopo hapo
 
Soma vizuri ...sijasema Marekani = United state of America ww ndio unalazimisha .
 
mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,994
2,000
Mambo mengi humu duniani nayasoma katika English zaidi kuliko kiswahili. Lakini nimekutana na tatizo moja nimeshindwa kulivumilia, wale wenye uwezo nisaidieni.

Ninaposoma katika English, najua kwamba United Kingdom huitwa kwa kifupi UK au Great Britain (GB) na ndimo humo kuna England, Scotland, Wales na Northen-Ireland.

Lakini hiyo UK au Great Britain inapoandikwa kwa kiswahili panaandikwa Uingereza. Lakini wakati huohuo eneo mojawapo la UK liitwalo England utakuta nalo kwenye kiswahili panaandikwa Uingereza!

Ukitazama hata kwenye michezo, utakuta wanasema LIGI YA UINGEREZA, wakati ukweli si ligi ya UK kote, bali ni ile sehemu iitwayo England ambako Scotland kwao na Ferguson hakuguswi.

Hapa mnisaidie. Ukitaja neno Uingereza unakuwa una-refer ni hasa? Je, ni ile England au UK yote?

Je, au haya ndiyo yale ya kumezwa kwenye miungano ambapo unaweza kusema England imewameza akina Scotland na wenzake kiasi kwamba ikitamkwa England basi bila kujali utamaduni wa zingine inamaanisha UK yote.

Kama ni hivyo, basi nchi kama Zanzibar zilikuwa na haki ya kuwa na hofu kama hiyo, maana hata timu ya taifa ya ikiwa haina mzanzibar hata mmoja bado tunaiita TIMU YA TAIFA YA TANZANIA.

Saidia kutafakari?

nadhani waliokujibu wote hawajakulewa unachokiulizia ..
ila kwa upande wangu nimekuelewa.. na mm nahitaji kujua ..
inshort swali liko hivi..
UKISEMA UINGEREZA UNAMANISHI NN KATI YA HIVI ...
1. UINGEREZA = UNITED KINGDOM (UK)
2. UINGEREZA = ENGLAND .

AU UKISEMA UINGEREZA NI NINI MAANA YAKE
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,327
2,000
Kama nimekuelewa unataka kujua great britain kiswahili chake ni nini, england kiswahili chake ni nini na united kingdom kiswahili ni nini, au sio?
Ngoja wajuzi watufafanulie

Mkuu Row,

Yaani umenielewa vilivyo. Ingawa jamaa yetu naye hapa chini kanikumbusha kwamba hata iliyokuwa USSR tulikuwa tunaita Urusi na wakati huo nikiwa mtoto sikuwa najua ndani ya USSR kuna Urusi ya kikwelikweli.

Nikupateje, shida yako ni England kwa Kiswahili au?!

Nadhani kuna changamoto hapo maana hata U.S.A tunaita Marekani lakini ukichunguza kwa makini si sahihi kuita hivyo, kama ilivyokuwa kwa USSR ambapo tulikuwa tunaita URUSI na hiyo haikuwa sahihi pia, maana Urusi ilikuwa ni nchi moja wapo tu katika shirikisho la USSR...

Umenifumbua macho katika hili... Ngoja tuone

Lakini afadhali hiyo Urusi ndani ya Muungano wa USSR ilikuwa ikimalizwa utata wa kutamka Soviet.

mbona hapo hamna changamoto yeyote .. mtoa U.S.A ni United states of America.. na AMERICA ni Ameica ka ilivyo ..

Changamoto ipo hapo kwa mtoa Mada na mpaka sasa hamjamjibu swali lake .

Ni kweli Mkuu nimehangaika sana kuitafuta hii. Kwa kifupi nataka strict limitation kwamba England kwa Kiswahili ni nini, na UK kwa Kiswahili ni nini. Siyo tu uje useme England kwa kiswahili ni Uingereza bila kusema UK kwa kiswahili nini.

Siyo kila nikisoma gazeti la Kiswahili nikaona neno Uingereza ninaanza kusugua kichwa kujua ina maana gani.
 
ISSA SHARAFI

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
407
0
Mambo mengi humu duniani nayasoma katika English zaidi kuliko kiswahili. Lakini nimekutana na tatizo moja nimeshindwa kulivumilia, wale wenye uwezo nisaidieni.

Ninaposoma katika English, najua kwamba United Kingdom huitwa kwa kifupi UK au Great Britain (GB) na ndimo humo kuna England, Scotland, Wales na Northen-Ireland.

Lakini hiyo UK au Great Britain inapoandikwa kwa kiswahili panaandikwa Uingereza. Lakini wakati huohuo eneo mojawapo la UK liitwalo England utakuta nalo kwenye kiswahili panaandikwa Uingereza!

Ukitazama hata kwenye michezo, utakuta wanasema LIGI YA UINGEREZA, wakati ukweli si ligi ya UK kote, bali ni ile sehemu iitwayo England ambako Scotland kwao na Ferguson hakuguswi.

Hapa mnisaidie. Ukitaja neno Uingereza unakuwa una-refer ni hasa? Je, ni ile England au UK yote?

Je, au haya ndiyo yale ya kumezwa kwenye miungano ambapo unaweza kusema England imewameza akina Scotland na wenzake kiasi kwamba ikitamkwa England basi bila kujali utamaduni wa zingine inamaanisha UK yote.

Kama ni hivyo, basi nchi kama Zanzibar zilikuwa na haki ya kuwa na hofu kama hiyo, maana hata timu ya taifa ya ikiwa haina mzanzibar hata mmoja bado tunaiita TIMU YA TAIFA YA TANZANIA.

Saidia kutafakari?

England amejipa hadhi sababu ndiye mkubwa wa huo muungana (kawameza wenzake)
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Nafikiri kwa ujumla tayari unaelewa vizuri Nikupateje – kama Kiswahili changu kinafika kuelewa yote uliyoyaandika! Mimi ni mwingereza anayeishi hapa Uingereza na ninafundisha lugha ya Kiingereza kwa wageni katika shule ya kimataifa. Baadhi ya wanafunzi wangu (wanaotoka nchi mbalimbali) wanashangaa kabisa ninapowaambia kwamba England siyo nchi ya kujitegemea (it is not an independent country). England ni sehemu mmoja ya United Kingdom – kama unavyojua. Sasa tatizo silo tatizo la geografia bali ya matumizi! Watu wengi ulimwenguni wanatumia neno ‘England' lakini wanafikiri lina maana ya nchi nzima (UK). Kosa hili ni kwa kawaida siku hizi – kosa hili lilikua kwa miaka mingi na sasa inakaribia siyo ‘kosa' – ni jambo la matumizi ya watu tu – imekuwa ‘desturi'. Hata hapo Uingereza (England, siyo sehemu nyingine ya United Kingdom) watu wengi wanatumia neno ''England kumaanisha nchi nzima (United Kingdom)! Imekuwa lugha ya kila siku ya watu ulimwenguni! Lakini ni hatari kufanya ‘kosa' hili katika Scotland – watu wa Scotland watakasirika kama ukifanya hivyo, yaani kusema ‘England lakini unamaanisha nchi nzima (the UK)! Basi watu wengi ulimwenguni (hata katika Tanzania) wanatumia neno England (Uingereza) lakini wanamaanisha the United Kingdom, yaani, nchi nzima! Lakini kwa rasmi au kama unataka kusema vizuri juu ya nchi ya kujitegemea, correct ni ‘the United Kingdom' au ‘Great Britain' (United Kingdom = Great Britain + Northern Ireland). Naamini tatizo hili ya machanganyiko ya maneno inahusu nchi yetu tu. (Nafikiri ulitoa mfano nzuri sana ulipotaja jambo la English League football!)
Sasa, natumaini niliweza kwa kiasi kukusaidia na swali hili, licha ya upungufu wa Kiswahili changu! Samahani kama sikuelewa vizuri!
 
Thanks Sir for enlighten me that the term is a worldwide confusion, but a confusion not pardoned in Scotland. Your post is a rich contribution to my long sought knowledge and I can say I've at least finally found what I have been looking for.

Say hallo to all colleagues in UK.

Cheers
 
Gillah A Maggh

Senior Member
Nov 4, 2013
134
0
Hiyo inatokana na ufinyu wa maneno katika lugha yetu ya kiswahili
Si hilo tu mtoa mada kuna maneno mengi kiswahili hakina hiyo changamoto kwa BAKITA
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Haya asante! Nafurahi saaana kwamba ilikusaidia! Nafurahi pia kama ukijibu kwa Kiswahili - isipokuwa wewe pia unapenda kujizoeza lugha geni!!!
Warmest regards,
David
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom