TCleverly
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 1,921
- 866
Nafikiri kwa ujumla tayari unaelewa vizuri Nikupateje kama Kiswahili changu kinafika kuelewa yote uliyoyaandika! Mimi ni mwingereza anayeishi hapa Uingereza na ninafundisha lugha ya Kiingereza kwa wageni katika shule ya kimataifa. Baadhi ya wanafunzi wangu (wanaotoka nchi mbalimbali) wanashangaa kabisa ninapowaambia kwamba England siyo nchi ya kujitegemea (it is not an independent country). England ni sehemu mmoja ya United Kingdom kama unavyojua. Sasa tatizo silo tatizo la geografia bali ya matumizi! Watu wengi ulimwenguni wanatumia neno England lakini wanafikiri lina maana ya nchi nzima (UK). Kosa hili ni kwa kawaida siku hizi kosa hili lilikua kwa miaka mingi na sasa inakaribia siyo kosa ni jambo la matumizi ya watu tu imekuwa desturi. Hata hapo Uingereza (England, siyo sehemu nyingine ya United Kingdom) watu wengi wanatumia neno England kumaanisha nchi nzima (United Kingdom)! Imekuwa lugha ya kila siku ya watu ulimwenguni! Lakini ni hatari kufanya kosa hili katika Scotland watu wa Scotland watakasirika kama ukifanya hivyo, yaani kusema England lakini unamaanisha nchi nzima (the UK)! Basi watu wengi ulimwenguni (hata katika Tanzania) wanatumia neno England (Uingereza) lakini wanamaanisha the United Kingdom, yaani, nchi nzima! Lakini kwa rasmi au kama unataka kusema vizuri juu ya nchi ya kujitegemea, correct ni the United Kingdom au Great Britain (United Kingdom = Great Britain + Northern Ireland). Naamini tatizo hili ya machanganyiko ya maneno inahusu nchi yetu tu. (Nafikiri ulitoa mfano nzuri sana ulipotaja jambo la English League football!)
Sasa, natumaini niliweza kwa kiasi kukusaidia na swali hili, licha ya upungufu wa Kiswahili changu! Samahani kama sikuelewa vizuri!
are you ENGLISH or BRITISH???