Uingereza ni nchi gani? Je, ni Britain au England?

Scotland kwa Kiswahili ni Uskoti.

Wales kwa Kiswahili ni Welisi (Kenya)/ Wailesi (Tanzania).
 
Mkuu Nikupateje kwa kuzingatia swali lako, Uingereza ni tafsiri ya neno England na wala sio UK.

Ili kuweza kujiridhisha na jibu hili ni vyema ukazingatia historia kwa ufupi.

Mosi, lazima tutambue kwamba kuna kisiwa cha Britania(Britain au Great Britain) kinachojumuisha tawala tatu tofauti nazo ni Uingereza (England), Uskoti(Scotland) na Welisi (Wales).
Mwaka 1707 Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliungana kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania (The Kingdom of Great Britain).

Pili, mnamo mwaka 1801, Ufalme wa Muungano wa Britania ukaungana na Eire (Ireland) na kutengeneza muungano mpya uliotambulika kwa jina la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland).

Tatu, mwaka 1916 utawala wa Eire ukaleta kashkash na sehemu ya ardhi ikajimegua kutoka United Kingdom of Great Britain and Ireland na baadaye mwaka 1922 kutengeneza taifa jipya lililojipa jina la Jamhuri ya Eire.

Nne, kutokana na kumeguka kwa Eire, mwaka 1927 ukazaliwa muungano mpya wa tatu ambao upo hata sasa ukiwa na jina la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Naamini utakuwa umenielewa na hatimaye umepata kilichokutatiza.

Mkuu,

Hivi hujawahi kusikia waandishi wa vitabu na magazeti wakisema MALKIA WA UINGEREZA, wakati hiyo UINGEREZA unayoiita ENGLAND ni moja tu ya kisehemu anachotawala?

Mimi nilidhani jina rahisi tungetumia neno BRITANIA na hivyo malkia yule tumwite MALKIA WA BRITANIA, Waziri Mkuu yule yule tumwite WAZIRI MKUU WA BRITANIA, BUnge lile tuliite BUNGE LA BRITANIA. Na ubalozi ule tuuite UBALOZI WA BRITANIA ingawa hata neno UBALOZI tunatakiwa kulijadili maana kwenye Commonwelath tuna HIGH COMMISSION na siyo AMBASSADOR.
 
Mkuu,

Hivi hujawahi kusikia waandishi wa vitabu na magazeti wakisema MALKIA WA UINGEREZA? Sasa utasemaje kuwa.

Mimi nilidhani jina rahisi tungetumia neno BRITANIA na hivyo malkia yule tumwite MALKIA WA BRITANIA. Na ubalozi ule tuuite UBALOZI WA BRITANIA ingawa hata neno UBALOZI tunatakiwa kulijadili maana kwenye Commonwelath tuna HIGH COMMISSION na siyo AMBASSADOR.

Mkuu makosa ya waandishi au ukosefu wa neno mahsusi hautoi uhalali wa kutaka kuita ambavyo tunataka kuita.

Mathalani, Malkia Elizabeth wa kwanza alikuwa akitambuliwa kwa cheo cha Malkia wa Uingereza (Queen of England).

Malkia wa sasa ambaye ni Elizabeth wa pili anatambuliwa kwa cheo cha Malkia wa UK na baadhi ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Hivyo utumikaji wa neno Malkia wa Uingereza labda watu hufupishwa tu au hutumika kimazoea kama ilivyokuwa kwa Elizabeth I.

Hii naifananisha na uitwaji wa Rais wetu kwa jina lililozoeleka la Rais wa Tanzania, wakati katiba inamuita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mkuu makosa ya waandishi au ukosefu wa neno mahsusi hautoi uhalali wa kutaka kuita ambavyo tunataka kuita.

Mathalani, Malkia Elizabeth wa kwanza alikuwa akitambuliwa kwa cheo cha Malkia wa Uingereza (Queen of England).

Malkia wa sasa ambaye ni Elizabeth wa pili anatambuliwa kwa cheo cha Malkia wa UK na baadhi ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Hivyo utumikaji wa neno Malkia wa Uingereza labda watu hufupishwa tu au hutumika kimazoea kama ilivyokuwa kwa Elizabeth I.

Mkuu naomba usiniangushe.
Unajua maelezo yako ya mwanzo niliona unaijua vizuri history na nikakujibu kuwa sihitaji kwa sababu kama kuna history ninayoijua basi ni ya UK.

Na kwa kuijua inabidi nikijibu harakaharaka kisa cha Queen Elizabeth I kuitwa Queen of England na huyu wa sasa kuitwa kama ulivyosema wa UK.

Queen Elizabeth I hadi anafariki England ilikuwa iko na jina lilelile kwani hata Wales ilipokuwa incorporated legally haikubadili jina. Yaani kuingia kwa Wales hakukuifanya England ibadili jina, kwani muungano wa Wales na England huwezi kuuita Union kwani in fact Wales ilivamiwa tunakoita anexation, tena tangu enzi za Edward I.

Taabu ikaja kwa Scotland. England ilijaribu mara kadhaa kuivamia Scotland lakini Scotts walikuwa very organised na walikuwa wanawatwanga kisawasawa.

Na kuna wakati England ilitaka kushindwa yaani Mary, Queen of Scots alitaka kumpindua dada yake huyo Elizabeth I atoke pale ili atawale kote Scotalnd na England. Ikashindikana na story ni ndefu lakini kwa kifupi akakamatwa na akauawa na dada yake for teason.

Muungano wa England na Scotland ulianza dalili za kuonekana alipofariki huyo Elizabeth I na akarithiwa na King James I mwaka 1663 yaani alitawala kama King James VI katika Scotland na hapohapo King James I katika England.

Kitendo cha James kutawala kote England na Scotaland hakiitwi Union bali kiliitwa PERSONAL UNION. Lakini kilikuwa ni dalili nzuri za kuungana baadaye kwani hakukuwa tena na tatizo la nani apoteze ufalme kati ya Scotland na England, jambo linalotutaabisha hapa kwani Rais wa Zanzibar hakupoteza urais wake.

Mwanzo huo ulizaa matunda mwaka 1707 ambapo ndipo England ilipoungana rasmi na Scotland, yaani sheria za nchi zikaungana na bunge pia.

Ndipo hapo jina GREAT BRITAIN likapatikana kwa nchi mpya.

Hivyo, kabla ya 1663, pale England alijulikana kama MONARCHY OF ENGLAND. Kuanzia 1663 hadi 1707 alijulikana kama MONARCHY OF ENGLAND hapohapo apia alijulikana kama MONARCHY OF SCOTLAND.

Kuanzia 1707 alijulikana kama MONARCHY OF BRITAIN. Ireland ilipokuja kujiunga ikajulikana kama MONARCHY OF UK. Na kwa sababu neno UK ni refu, basi UK ikatosha lakini inaeleweka ukisema MONARCHY OF BRITAIN unaeleweka.

Natumaini nineeleweka.
 
UK=UMOJA WA KIFALME hii hujumuisha visiwa vitano vinavyopatikana pale kaskazini mwa atlantiki vikitawaliwa na wafalme au malkia eg wales,north ireland,south ireland,scotland & britain au england kiswahili uingereza
ENGLAND=UINGEREZA ndo pia inaitwa britain hizi nchi huitwa united kingdoms coz mfumo wake wa utawala ni wa kifalme na hata mfumo wao wa maisha unafanana mm nimekuwa uskochi miaka mitatu napafahamu kiasi fulani
 
Mkuu nimekuelewa sana pia maelezo yako umeyaweka kwa ufasaha katika lugha ya kiswahili kwani nilizoea kusoma au kuangalia historia hii kwenye filamu zenye umombo hivyo kwa kiasi fulani hiyo historia ya tawala za kifalme ninaielewa na usione kama nakuangusha.

Unajua kiini cha habari hii nzima kama ulivyoiibua ni namna ya utumiaji au utumika wa neno Uingereza, je ni nchi ipi haswa yenye umiliki wa jina hilo (kwa lugha ya kiswahili)?

Labda tuwapishewaungwana wengine wataoweza kutuondolea hiki kisebusebu cha matumizi ya jina Malkia wa Uingereza.

Binafsi naamini ni namna tu ya utohoaji ndiyo inayoleta mushkeli hapa, maana ukiangalia anavyoitwa kwa lugha za kigeni au hata katika mtiririko ule wa vyeo vya kifalme utaona hakuna utata kabisa.

Mkuu naomba usiniangushe.
Unajua maelezo yako ya mwanzo niliona unaijua vizuri history na nikakujibu kuwa sihitaji kwa sababu kama kuna history ninayoijua basi ni ya UK.

Na kwa kuijua inabidi nikijibu harakaharaka kisa cha Queen Elizabeth I kuitwa Queen of England na huyu wa sasa kuitwa kama ulivyosema wa UK.

Queen Elizabeth I hadi anafariki England ilikuwa iko na jina lilelile kwani hata Wales ilipokuwa incorporated legally haikubadili jina. Yaani kuingia kwa Wales hakukuifanya England ibadili jina, kwani muungano wa Wales na England huwezi kuuita Union kwani in fact Wales ilivamiwa tunakoita anexation, tena tangu enzi za Edward I.

Taabu ikaja kwa Scotland. England ilijaribu mara kadhaa kuivamia Scotland lakini Scotts walikuwa very organised na walikuwa wanawatwanga kisawasawa.

Na kuna wakati England ilitaka kushindwa yaani Mary, Queen of Scots alitaka kumpindua dada yake huyo Elizabeth I atoke pale ili atawale kote Scotalnd na England. Ikashindikana na story ni ndefu lakini kwa kifupi akakamatwa na akauawa na dada yake for teason.

Muungano wa England na Scotland ulianza dalili za kuonekana alipofariki huyo Elizabeth I na akarithiwa na King James I mwaka 1663 yaani alitawala kama King James VI katika Scotland na hapohapo King James I katika England.

Kitendo cha James kutawala kote England na Scotaland hakiitwi Union bali kiliitwa PERSONAL UNION. Lakini kilikuwa ni dalili nzuri za kuungana baadaye kwani hakukuwa tena na tatizo la nani apoteze ufalme kati ya Scotland na England, jambo linalotutaabisha hapa kwani Rais wa Zanzibar hakupoteza urais wake.

Mwanzo huo ulizaa matunda mwaka 1707 ambapo ndipo England ilipoungana rasmi na Scotland, yaani sheria za nchi zikaungana na bunge pia.

Ndipo hapo jina GREAT BRITAIN likapatikana kwa nchi mpya.

Hivyo, kabla ya 1663, pale England alijulikana kama MONARCHY OF ENGLAND. Kuanzia 1663 hadi 1707 alijulikana kama MONARCHY OF ENGLAND hapohapo apia alijulikana kama MONARCHY OF SCOTLAND.

Kuanzia 1707 alijulikana kama MONARCHY OF BRITAIN. Ireland ilipokuja kujiunga ikajulikana kama MONARCHY OF UK. Na kwa sababu neno UK ni refu, basi UK ikatosha lakini inaeleweka ukisema MONARCHY OF BRITAIN unaeleweka.

Natumaini nineeleweka.
 
UK=UMOJA WA KIFALME hii hujumuisha visiwa vitano vinavyopatikana pale kaskazini mwa atlantiki vikitawaliwa na wafalme au malkia eg wales,north ireland,south ireland,scotland & britain au england kiswahili uingereza
ENGLAND=UINGEREZA ndo pia inaitwa britain hizi nchi huitwa united kingdoms coz mfumo wake wa utawala ni wa kifalme na hata mfumo wao wa maisha unafanana mm nimekuwa uskochi miaka mitatu napafahamu kiasi fulani

South Ireland(Republic of Ireland) haimo kwa UK. Ndio maana utakutaga zikuhusishwa zinaanisemwa UK and Ireland. Ni nchi inajitegemea na raisi yupo sema wao kama sie tulitawaliwa na watu hao hao pia.

Ila wanajua kugezana mambo ya mengine mengine na zaidi na ilivyo kwa EU. Bali kuna ile freedom ya kusafiri katika nchi hizo za uk na rep iitwayo common travel area... Hii hawaitaji passport ila tangu dunia imekuwa hatari basi mtu inabidi ajibebee tu kusafiria. Ukisafiri ukishuka hauulizwi(labda ushtukiwe)yaani hakuna passport unatoka tu kama local flight.
I guess bado watakuwa wanaendelea tangu nitembelee mitaa hiyo.
 
Na hawa wote UK na Ireland wanatumia Kiingereza (English)?
 
Pole sana, Hasason, lakini inaonekana kwa kweli umekosa! Ndiyo, naitwa David nami nakuja Tanzania kila mwaka kwa wiki kadhaa lakini siyo mimi aliyekuwepo TBC 1 au pale ubalozi. (Sijui TBC ni nini lakini kwa uhakika sijawahi kuhojiwa na Shaaban Kisu.)
 
Shukran somo zuri hili mkuu nimekudondoshea like
Mkuu Nikupateje kwa kuzingatia swali lako, Uingereza ni tafsiri ya neno England na wala sio UK.

Ili kuweza kujiridhisha na jibu hili ni vyema ukazingatia historia kwa ufupi.

Mosi, lazima tutambue kwamba kuna kisiwa cha Britania(Britain au Great Britain) kinachojumuisha tawala tatu tofauti nazo ni Uingereza (England), Uskoti(Scotland) na Welisi (Wales).
Mwaka 1707 Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliungana kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania (The Kingdom of Great Britain).

Pili, mnamo mwaka 1801, Ufalme wa Muungano wa Britania ukaungana na Eire (Ireland) na kutengeneza muungano mpya uliotambulika kwa jina la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland).

Tatu, mwaka 1916 utawala wa Eire ukaleta kashkash na sehemu ya ardhi ikajimegua kutoka United Kingdom of Great Britain and Ireland na baadaye mwaka 1922 kutengeneza taifa jipya lililojipa jina la Jamhuri ya Eire.

Nne, kutokana na kumeguka kwa Eire, mwaka 1927 ukazaliwa muungano mpya wa tatu ambao upo hata sasa ukiwa na jina la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Naamini utakuwa umenielewa na hatimaye umepata kilichokutatiza.
 
Pole sana, Hasason, lakini kwa kweli nafikiri umekosa! Naitwa David lakini sijawahi kuwepo TBC1 (pia sijui hii ni nini) na kwa uhakika sikuhojiwa na Shaaban Kisu kwenye kipindi cha lulu (tena sijui hii ni ya nini) za kiswahili! Pia Sijawahi kuwepo pale ubalozi uliotaja. Best wishes,
David
 
Uingereza ni england, linatokana na neno waingereza.
English people ni watu kutoka england tu. Kuna Scottish, na welsh people. Hivyo waingereza= english people. na uingereza ni sehemu wanapotoka waingereza which is england.
 
Back
Top Bottom