Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.
Magazeti ya Tanzania hovyo kabisa maana watu wanahangaika sana habari za zitto na CDM wakati nchi inakufa bandari mambo hayaendi sawa kenya, uganda na rwanda wanasonga
 
Ndo maana unaona wewe binafsi hakuna anguko,lakini wenye upeo mpana wameshaona tatizo la chadema.
Kama chama kinazidi kuimarika,kuna wanachama wangapi wameingia nakutoka baada ya ZZK kuvuliwa madara?

Jipe moyo wa plastiki joto likipanda utayeyuka tu, CHADEMA ni taasisi is more than a mere person, kwa huu usaliti bye bye..
waende kwa wneye mahaba nao, watanzania wa leo hatudanganyiki!
 
CHADEMA.jpg WALEVI.jpg
 
mnapika kazi au mnapiga picha??kumbe akili za oral stage still zinafanya kazi hadi kwenye stage hii uliyonayo?ajabu

Wanafiki watupu hao! Kazi alipga Nyerere hao wanapiga kazi ya ufisadi. Si uanaona vuvuzela tumbo limeanza kuvimba kama la Chaijuisi?
 
Mleta mada, soma hapa kwa makini:

Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) CHADEMA said arf

Salaam,

Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.

Said A Arfi (mb)

Nakala Vyombo vya Habari
Huyu mzee ni wa kumsikitikia alikurupuka kuruka kwenye ndege ya Chadema akidhani kabeba parachuti kumbe kakwapua koti la mzungu.
 
Rest in peace chadema
...yap tumepumzisha timu zetu za m4c kwa muda na soon tutaanza kukandamiza mpaka mlete polisi,...piiiipooooooozzzzzzzzzz poweeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr..!!!! kamanda lema ndani, kikosi cha anga kama kawa , mzee wa gwanda mstari wa mbele 2015, lazima msahau mlango,walizimia wengi 2010 sasa wengi watakufa kwa mshtuko 2015....
 
Ndo maana unaona wewe binafsi hakuna anguko,lakini wenye upeo mpana wameshaona tatizo la chadema.
Kama chama kinazidi kuimarika,kuna wanachama wangapi wameingia nakutoka baada ya ZZK kuvuliwa madara?

Chama hakijapasuka na wala hakitapasuka, ila wale wa upande ule wa pili ndio wanamaumivu baada ya mbinu zao chafu kugundulika, chama sio mtu mmoja chama ni wanachama na si viongozi! tunahitaji viongozi wanaoweza kuongoza kwa kufuata taratibi na kanuni za chama, sio wanowaza umimi kila kukicha, sio wanaoweza kununuliwa kwa manufaa ya watawala.
 
Nimekuwa nafuatilia sana siasa za mageuzi ya nchi yetu!

SImfahamu sana Godbless Lema, lakini nilikiwa Arusha uchaguzi wa 2005, alishindwa kwa kura kadhaa,inaaminika kulikuwa na "zengwe", Mrema (kama sikosei, wa CCM akapita)....Hapo ndipo alipoibuka Godbless Lema! Kipindi kile hakuwa mtu mwenye vurugu kama nimjuaye leo.....

Tundu Lissu, nilikuwa namfahamu akiwa anatetea haki za watanganyika, mambo ya ardhi n.k, amekuwa mwanaharakati makini, amehudhuria na kutoa mada mbalimbali katika majukwaa ya kuelimisha umma n.k Kiukweli nilikuwa namuona ni msomi makini na mwerevu1

Hawa wanasiasa wawili wanafanana sana namna walivyoingia na kupat aumaarufu kwenye siasa...Tundu Lissu, na Godbless Lema wote wakaibuk atena 2010 kwa kushinda viti vya ubunge...wot ekwa mbinde!

Hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia sana yanayotokea CDM, hawa jamaa wawili wapo katika usukani wa sakata lilnaloendelea CDM; Tundu Lissu (eti mwanasheria wa CDM) ametangaza kuwa "ZITO KABWE, MKUMBO NA M.KITI ARUSHA" eti "WAMEFUKUZWA"???

Godbless Lema ndiye mpika majungu wa M1, M2, M3 etc...waraka ambao hata uongozi wa CDM umesema hautambui!!

Sasa kama uongozi hauutambui huo waraka kina ZZK wamefukuzwaje?

Je CC ina mamlaka ya "kumfukuza" mwanachama? ama ni Baraza Kuu?

Mimi naona, CDM inakwisha, INAKUFA! WHY? Kwa sababu wanatumia siasa za majitaka za Lissu na Lema...na wengine wachache! Hata watu makini kama Mnyika na Kamanda Mbowe wanashawishika na siasa hizi?

CDM 2015 itrapoteza sana voti Bungeni, na what I see MBOWE, LEMA, LISSU, MNYIKA na MDEE watapoteza nafasi zao Bungeni.

CDM inapoteza muelekeo kwa kuwa imealika watu kwenye madaraka AMBAO SIYO WANASIASA!
Bado sijaona point za kufa Chadema huo ni mawazo finyu tena ya kitoto,kwa upeo wangu mimi kama mtu mzima ukitoa kitu kibaya ndani ya nyumba sio kosa,kwa hiyo Chadema wao wasonge mbele kufanya mikakati ya kujenga chama,unaona ccm wanavyo zunguka nchi nzima kumwaga sera Chadema wanadangawa na magazeti na malumbano yasiona tija,kama wameshawamwaga waendelee na mikutano yao kama zamani.
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

Magazeti yanayoandika hivyo ni uhuru, mzalendo, jambo leo, habari leo, rai...unategemea nini hapo?
 
Sakata la CHADEMA kuwavua uongozi viongozi wake limechukua nafas sana katika maeneo mbalimbal,.jambo ambalo pia limechangia kulipa umaarufu suala hilo ni kitendo wanachama wa chama pinzani cha CHADEMA yaan CCM kuonesha kusikitika kwa tukio hilo wakat CHADEMA na CCM ni vyama pinzani. Kitendo cha wanachama wa CCM kuumia,kusikitika na kutounga mkono kuondolewa kwa viongozi hao wa CHADEMA kimeipa nguvu CHADEMA na kuona kuwa wapo sahihi maana adui yako anaposiktika na kuonesha kukerwa kwa ulichokifanya hapo ujue umemshinda na lengo la kumuumiza na kumdhoofisha limetimia..wanachama wa CCM badiliken na muje kivingine ili kutolipa umaarufu na uhalali kitendo hiki cha CHADEMA.. .....NIONAVYO MIMI.!!
 
Bravo mkuu!
Bahati mbaya sana kuna wapuuzi wanaokataa kuukubali ukweli kuwa Zito ni MSALITI na hana thamani mbele ya jamii kwa kununuliwa na afanye kazi ya CCM Kuondoka kwake Chadema ni njia ya kuimarisha chama na kulinda misingi ya upinzani wa kweli kwa manufaa ya WaTanzania....Walidhani kuwa angweza kufanya kama alivyofanya Mrema huko nyuma kwa kuibomoa NCCR Mageuzi.. Kasi ya Chadema iko palepale na hao Zito sympathisers waondoke naye tu!

ni nan mwenye uwezo wakufany mambo makubwa na mazur aliyokifanyia chama ZZK tangu aanze ubunge, pamoja na mapungufu yake? kwamm sioni mbadala mana babu(dr. slaa) ndo huyo anaelekea kufa kisiasa
 
mkuu umesahau na magazeti ya ccm yanatetea kweli.
 
Sakata la CHADEMA kuwavua uongozi viongozi wake limechukua nafas sana katika maeneo mbalimbal,.jambo ambalo pia limechangia kulipa umaarufu suala hilo ni kitendo wanachama wa chama pinzani cha CHADEMA yaan CCM kuonesha kusikitika kwa tukio hilo wakat CHADEMA na CCM ni vyama pinzani. Kitendo cha wanachama wa CCM kuumia,kusikitika na kutounga mkono kuondolewa kwa viongozi hao wa CHADEMA kimeipa nguvu CHADEMA na kuona kuwa wapo sahihi maana adui yako anaposiktika na kuonesha kukerwa kwa ulichokifanya hapo ujue umemshinda na lengo la kumuumiza na kumdhoofisha limetimia..wanachama wa CCM badiliken na muje kivingine ili kutolipa umaarufu na uhalali kitendo hiki cha CHADEMA.. .....NIONAVYO MIMI.!!

Nakubaliana na wewe 100%> Chadema imechukua umamuzi sahihi wa kudhibiti mamluki ndani ya chama lakini sisi wananchi tunashangawa na kelele zinazopigwa na CCM hapo ujue wamebanwa mbavu. mipango yao imefichuka.

Go on Chadema... vita ni kali ni mpango wa kurusha mawe gizani...ukisikia yowe ujue jiwe limempata adui.
 
Sakata la CHADEMA kuwavua uongozi viongozi wake limechukua nafas sana katika maeneo mbalimbal,.jambo ambalo pia limechangia kulipa umaarufu suala hilo ni kitendo wanachama wa chama pinzani cha CHADEMA yaan CCM kuonesha kusikitika kwa tukio hilo

Wanakoleza tu hao hawana lolote unafiki mtupu!
 
Tafuta historia ya CHADEMA,wewe mleta uzi utaanza kujihurumia mwenyewe kabla haujahurumiwa.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

Kweli, hata mimi naona hivyo. bahati mbaya ccm kambi zote zinamsapoti zitto kwa sababu ndiye anapunguza kasi ya chadema 2015. pia sijaona wanachadema wenyewe wakimuunga mkono zitto, zaidi ya waccm na mapandikizi yao.
 
Back
Top Bottom