Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Bravo mkuu!
Bahati mbaya sana kuna wapuuzi wanaokataa kuukubali ukweli kuwa Zito ni MSALITI na hana thamani mbele ya jamii kwa kununuliwa na afanye kazi ya CCM Kuondoka kwake Chadema ni njia ya kuimarisha chama na kulinda misingi ya upinzani wa kweli kwa manufaa ya WaTanzania....Walidhani kuwa angweza kufanya kama alivyofanya Mrema huko nyuma kwa kuibomoa NCCR Mageuzi.. Kasi ya Chadema iko palepale na hao Zito sympathisers waondoke naye tu!
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

Hata kichaa anajionaga yuko timamu
 
kwa mtu yeyote , mwenye akili timamu na asiyesukumwa na utashi wa tumbo lake amekuelewa kamanda , mungu akulinde sana , nakala ya uzi huu nawapelekea wale wote wenye visokolokwinyo , wanaofanya mambo yao mchana na usiku kuhakikisha kwamba cdm inakufa .
 
WAHAFIDHINA wa CDM wanamuogopa Zitto hata kivuli chake,eti leo baada ya kumvua vyeo ndio yule Mpare wa Kilimanjaro MNYIKA ndio anataja tarehe ya Uchaguzi!!wanatufanya Watanzania wajiiiiiiiiii nga ! ! ! !
 
[Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.


Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.
Nawashukuru sana.


Imetolewa na ;-


Joseph Y. Patrick

Mburula mwingine! Ulikuwa unasubiri sakata la Zito Kabwe ndio uinue pua yako na kulalamika ya kwako? Huoni hiyo ni psychological impotence?
 
Na CHADEMA wakichemka wakamsamehe Zitto kwasababu ya hizi Propaganda za CCM na wapambe wa Zitto, baasi chama kimekufa maana kutakuwa hakuna woga tena kwamba mtu ukitenda kosa laweza kukughalimu, ilimradi tu una vicent vya kufanya Propaganda kwenye vyombo vya Habari basi. Kuna tetesi pia TISS wametoa fungu kubwa tena kwa ZZK ili aanze kucheza na wajumbe wa kamati kuu kwamba ikitokea inaletwa hoja ya kufukuzwa uanachama waigomee, kweli Chadema safari hii mpo kwenye Mtihani mkubwa sana ambao inatakiwa kuufaulu ili TISS wapate hasara hayo mapesa yao na iwakatishe tamaa kwamba pesa siyo kila kitu
 
Mpaka sasa, CDM wamefanikiwa kuilinda HADHI ya Chama.. Wamafanikiwa MPaka sekunde hii kithubutu Na kutomung'unya maneno.. Embe wanaliuta embe waziwazi Na Chungwa linapewa jina lake halisi-CHUNGWA Na si vinginevyo hii ni Hatua inayostahili kuheshimika.

Maelfu ya vyama Vyeti vya Kiafrika makuzi yake yanabebwa Na kujikombakomba, kufichiana Siri, kuzika utu Wa kibinaadam, mwizi hakemewi Na mbakaji, tapeli, mzushi, mwongomwongo Na ndimimbilimbili wote wanakusanywa Kwenye kapu la Chama ilimradi kionekane Na wanachama wengi.

Nataka nitoe Rai tu kwa watanzania wote wenye Akili sio machizi ambao Akili zao zimejaa madawa ya kulevya Na ubakaji, Kwamba dalili ya mvua ni mawingu, jinsi atendavyo Mtu kabla hajapewa madaraka ndivyo atavyotenda akipewa madaraka. Usilogwe Kwamba limtu kigeugeu ati likipewa madaraka litabadika haiwezekani..! CHADEMA Hawa ambao Leo wanathubutu kuwajibishana Ndani ya Chama chao ni imani yangu wakipewa nchi wembe utakuwa ule ule Wa kuwajibishana bila kuoneana haya au urafikiflan.

Taifa letu linahitaji viongozi wasio igiza, maigizo ya Waziri mzima Mwenye familia yake, kutuna Kwenye media Na kuonyesha wahusika wa biashara ya Madawa ya kulevya, kisha kujiapiza Kwamba atahakikisha anawapeleka panapostahili Na within a week mijitu inadunda tu huku mitaani ikisoganze maisha huku jamii ikiteketea Kwa biashara zao, maigizo sampuli hii tuseme NO..! Tunahitaji viongozi wenye uthubutu.

Taifa limeoza hili nyie hamjui tu, siku hizi kila Mtu anajitendea uhuni wazi wazi. Panahitajika uongozi wenye uthubutu.. CDM for mount2015
 
sina uhakika kama kweli wewe ni 'super thinker' lakini umetoa mfano unaokufanya uwe hivyo. ...yaani unamfumania mke wako wa ndoa lakini unamezea kwa kisingizio eti "ndoa ikivunjika watu watanionaje", je kitendo cha mke kutoka nje si tayari kavunja ahadi ambayo ndio ndoa!?
Wanasema kuwa mzee Mtei ni mkwe wa mwenyekiti na ni mchaga (na mengine mengi) huku wakisahau kuwa huyu ni mwasisi wa chama. Alafu katika wazee wa Kitanzania ambao wana uungwana wa hali ya juu ni Mzee Mtei maana miaka ya 70 kama aliweza kumueleza Mwalimu wazi kile alichokuwa akidhani ni sahihi juu ya uchumi wa nchi hii na kukubali kujiudhuru huku akiwaacha wanafiki wengi ndani ya serikali wakimlaghai Mwl. Nyerere kuwa ni 'wajamaa' wenzake tutamdharau vipi leo!?
 
Back
Top Bottom