Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

image.jpg Huyu kuitwa kuhojiwa au .........
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.
Kuzuia mazishi ya chadema ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mikono
 
hii ni vita kati ya wapenda demokrasia na wahafidhina.
mkuu hata kama kusoma hujui basi huwezi hata kuona picha ukutani?
 
Ndo maana unaona wewe binafsi hakuna anguko,lakini wenye upeo mpana wameshaona tatizo la chadema.
Kama chama kinazidi kuimarika,kuna wanachama wangapi wameingia nakutoka baada ya ZZK kuvuliwa madara?

Siku zote tawi la mti huanguka na majani yake. Wanaoondoka ni majani ya zitto.
 
Chadema kinaongozwa kwa misingi ya kilaghai

Walaghai kati ya CCM na CHADEMA ni wapi wakati CCM kuanzia Mwenyekiti haruhusiwi kupingwa, makamu mwenyekiti huteuliwa , katibu mkuu huteuliwa , manaibu katibu wakuu huteuliwa na sekretelieti yote huteuliwa, ambavyo ni vyombo vya juu kabisa vya Chama . JE HAPA MWANACHAMA ANA CHAKE AU CHAMA NI CHA MWENYEKITI WA TAIFA ANAETEUA VIONGOZI WOTE HAO WA NGAZI YA JUU KABISA v/S CHADEMA ambao kiongozi wa kwanza mtei alipambana kwa kura kuupata umwenyekiti na mwenyekiti wa pili Bob Makani alipambana kuupata umwenyekiti vivyo hivyo kwa mwenyekiti wa sasa, Tuje kwenye uongozi wa viongozi wakuu wa vyama.Tangu mwaka 1954 mpaka leo 2013 ni takribani miaka 60 lakini CCM imekuwa na wenyeviti waNNE tu na hakuna aliyewahi kupambana kwa kura na mpinzani wake na kura zote huamuliwa kwa ndiyo na hapana V/S CHADEMA ambayo tangu uindwe ina miaka 20 lakini ina wenyeviti watatu na wanaopambana kwa kura kuupata uwenyekiti. Kama kuna mwana CCM YEYOTE ANAPINGA AWEKE USHAHIDI WAKE HAPA
 
wewe hata ukipewa tochi hutaona huo mpasuko kwa sababu unafikiria ki mamluki!!
 
Ndo maana unaona wewe binafsi hakuna anguko,lakini wenye upeo mpana wameshaona tatizo la chadema.
Kama chama kinazidi kuimarika,kuna wanachama wangapi wameingia nakutoka baada ya ZZK kuvuliwa madara?
Kwa hiyo unadhani bila Zitto hakuna CHADEMA? Pole sana. Tofautisha mwanachama halisi na mfuasi wa mtu ndani ya chama.
 
kwa mtu yeyote , mwenye akili timamu na asiyesukumwa na utashi wa tumbo lake amekuelewa kamanda , mungu akulinde sana , nakala ya uzi huu nawapelekea wale wote wenye visokolokwinyo , wanaofanya mambo yao mchana na usiku kuhakikisha kwamba cdm inakufa .
 
Mleta mada, soma hapa kwa makini:

Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) CHADEMA said arf


Salaam,


Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.


Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.


Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi


Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu


Nawasilisha.


Said A Arfi (mb)


Nakala Vyombo vya Habari
 
Nakubaliana nawe mkuu. Tatizo la sisi Watanzania hatupendi kufikiri ila tunapenda kufuata mikumbo, wakati mwigine kwa kutofahamu au kwa kujaribu kupunguza shida zetu za kila siku za njaa au kwa kutafuta umaarufu. Ndiyo maana nchi inadidimia kimaendeleo kila siku kwa sababu hiyo. Chama tawala kinajua udhaifu huo wa watu kufuata ya mikumbo kwa sababu ya njaa yao kali waliyowasababishia kwa makusudi ili waweze kuwamudu, ndiyo maana jambo lisilo na kichwa wala miguu CCM wanaliavalia njuga wanajua tu kuna malimbukeni kibaao watawafuata.Lakini masuala nyeti yanayohusu maendeleo yetu sisi tunayapuuza na kuwakabidhi wafadhiri wayatatue. Kwa mwendo huu tutafika !!!? Hapa kufika katika safari ya maisha bora kwa kila mtanzania mpaka aondolewe msababishaji CCM madarakani.

umenena ukweli mkuu. tatizo na kikwazo cha maendeleo katika nchi hii ni CCM ila wananchi wengi bado wapo gizani na hawajagundua hilo.
 
CHADEMA = SACCOS
Sasa inakufa kikondoo.
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

Sakata la zitto na dkt. Kitila mjumbe wa baraza kuu chadema ailipua kamati kuu:


natanguliza maombi ya usikivu mwema:


ama kweli sasa CHADEMA NI PIGA NIKUPIGE.


TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .


UTANGULIZI.


Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.


MIGOGORO NDANI YA CHAMA


Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.


Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.


Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.


Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.


Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.


Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.


KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU


Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)


Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.


Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.


Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.


Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.


Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.


Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.


Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.


MSIMAMO WANGU.


Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.


Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.


(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .


(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.


Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.


Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.


Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.


Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.


Nawashukuru sana.


Imetolewa na ;-


Joseph Y. Patrick


+255713802226


Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa
 
Back
Top Bottom