Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Uimara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Challenge Accepted?? Why did you run away?

Nliwajibika baada ya kushindwa kudeliver ndani ya hiko chama. Infact mimi ndie niliejitoa bada ya kuona napingana na chama hasa katika mitizamo na maono. I ve bn there as one of party think tank
 
ni nan mwenye uwezo wakufany mambo makubwa na mazur aliyokifanyia chama ZZK tangu aanze ubunge, pamoja na mapungufu yake? kwamm sioni mbadala mana babu(dr. slaa) ndo huyo anaelekea kufa kisiasa

Kabwe amekuwa mjanja sana katika kufanya mambo yake....ya kujijenga kisiasa na ameweza kuipa wakati mgumu serikali na CCM - ingawa huo ndio ulikuwa mkakati wake. Lakini tamaa yake ya kufikia kileleni mwa siasa kwa njia za undumila kuwili ndizo zimeleta anguko lake. Na mazuri yote aliyofanya hayaondoi uzito wa kosa la uhaini na ni vema wameligundua mapema. Aidha wapo wengine wengi tu wanaoweza na watakaofanya makubwa kuliko ya Zito Kabwe. The issue hapa ni Chadema kuwapa fursa ...kumbuka huyo unayesema anaelekea kufa kisisasa alippoewa fursa alifanya mambo mazito na mazuri sana wakati wake!
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

mkuu mbinu zilizotumika zilishapitwa na wakati hizohizo zimetumika nccr,tlp na cuf hawajagundua tu kuwa kwa sasa zimechina mbinu zao,ccm muda umefika tua
 
wee tulia tu anafukuzwa waende naye huku kwa maCCM, kuna kijama cha temeke nacho jana kimetoa tamko, nakione huruma kinapotezwa sasa hivi

Hii ndio saa ya kujua mchele na pumba chama kilikokota kenge wengi katika kusaka wanachama sasa kinapita katika tanuru la moto. Hata cdm wakibaki wawili tu ni bora kuliko kubakia katikati ya tope kama watani wao wanaotafuta suluhu na majambazi ilimradi chama kiendelee kudunda
 
Sakata la CHADEMA kuwavua uongozi viongozi wake limechukua nafas sana katika maeneo mbalimbal,.jambo ambalo pia limechangia kulipa umaarufu suala hilo ni kitendo wanachama wa chama pinzani cha CHADEMA yaan CCM kuonesha kusikitika kwa tukio hilo wakat CHADEMA na CCM ni vyama pinzani. Kitendo cha wanachama wa CCM kuumia,kusikitika na kutounga mkono kuondolewa kwa viongozi hao wa CHADEMA kimeipa nguvu CHADEMA na kuona kuwa wapo sahihi maana adui yako anaposiktika na kuonesha kukerwa kwa ulichokifanya hapo ujue umemshinda na lengo la kumuumiza na kumdhoofisha limetimia..wanachama wa CCM badiliken na muje kivingine ili kutolipa umaarufu na uhalali kitendo hiki cha CHADEMA.. .....NIONAVYO MIMI.!!
Kweli mkuu mchawi ukimgundua mbinu zake huwa anachukia haswaaa!! ona akina Mwigu sangoma na wakaanga sumu wengine wa magamba wanavyojamba jamba!! Ritz1 amechukia eti dadake ataukosa ufirst lady!!! tehe tehe tehe!!
 
Mleta mada, soma hapa kwa makini:

Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) CHADEMA said arf

Salaam,

Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.

Said A Arfi (mb)

Nakala Vyombo vya Habari

Kama una akili timamu hutapata taabu kutambua kwamba huyo alikuwa team Zitto na Kitila. Angalia timing ya maamuzi yake. Siku zote alikuwa wapi kuyaweka wazi hayo aliyoyasema?
 
Kabwe amekuwa mjanja sana katika kufanya mambo yake....ya kujijenga kisiasa na ameweza kuipa wakati mgumu serikali na CCM - ingawa huo ndio ulikuwa mkakati wake. Lakini tamaa yake ya kufikia kileleni mwa siasa kwa njia za undumila kuwili ndizo zimeleta anguko lake. Na mazuri yote aliyofanya hayaondoi uzito wa kosa la uhaini na ni vema wameligundua mapema. Aidha wapo wengine wengi tu wanaoweza na watakaofanya makubwa kuliko ya Zito Kabwe. The issue hapa ni Chadema kuwapa fursa ...kumbuka huyo unayesema anaelekea kufa kisisasa alippoewa fursa alifanya mambo mazito na mazuri sana wakati wake!
Yapi hayo makubwa aliyoyafanya ZZK zaidi ya kelele zinazotokana na njaa yake akikatiwa kidogodogo ananyamaza. Angekifanyia chama makubwa si kingekuwa maarufu kuliko yeye? mbona sasa yeye amekuwa maarufu kuliko chama? hapo alikuwa anajenga chama au anajijenga mwenyewe? tafakari
 
Sakata la zitto na dkt. Kitila mjumbe wa baraza kuu chadema ailipua kamati kuu:

natanguliza maombi ya usikivu mwema:

ama kweli sasa CHADEMA NI PIGA NIKUPIGE.

TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .

UTANGULIZI.

Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.

MIGOGORO NDANI YA CHAMA

Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.

Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.

Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.

Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.

Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.

KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU

Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)

Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.

Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.

Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.

Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.

Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.

Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.

MSIMAMO WANGU.

Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.

Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.

(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .

(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.

Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.

Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.

Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.

Nawashukuru sana.

Imetolewa na ;-

Joseph Y. Patrick

+255713802226

Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa

Duh watu wengine mna roho ngumu au akili ndogo na uwezo wa kufikiri kutokuwapo!
mtu mzima [kama kweli] unalalamika na umeona makosa hayo bado unaendelea kubaki kuwa mwanachama mtiifu kwa hao hao unaowatuhumu????

ukiitwa mburula utakataaa? njoo huku kwetu uone na kwenyewe pakoje!
 
Wadau na wapenda Demokrasia hebu sasa tujitkite katika kuangalia upande wa pili wa shilingi juu ya sakata la Zito na wenzake.Ninaleta uzi huu si kwa nia mbaya bali kuona tunazungumzia pia upande wa pili maana tangu swala hili liibuliwe week iliyopita watu wamejikita kuangalia "NINI KITATOKEA" na wengi wamejikita hasa kwenye Postive outcomes ya jambo hili pasipo kuangalia pia "NINI NINGETOKEA"hasa postive outcome ya jambo hili kubwa la Kisiasa katika chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA. Maoni yangu kwa ufupi naona kama jambo hili lisingeibuliwa basi tungeshuudua malumbano pengine zaidi ya haya na hasa jambo hili labda lingekuja kujulikana tayari uchaguzi umeshafanyika kwani mimi naamini chadema kina watu makini ambao wangehoji uhalali wa Zitto Kabwe kama angekuwa mwenyekiti kama mkakati ulivyojionyesha na ni kitu hatari sana kuanza kuhoji uhalali wa Kiongozi wako hili lingezua mengi zidi ya haya na kuwa kete turufu kwa wapinzani wa Chadema.Na hapo pia tungeona baadhi ya viongozi wa Chadema wakija na mkakati huu kama evidence ya kuonyesha namna Zito alivyopata uenyekiti kwa kuvunja sio tu katiba ya chama bali hata kanuni za chama.

My take is "Hafadhali jambo hili limekuja kabla ya Uchaguzi liwe chachu si kwa Chadema tu bali kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini"
 
Na CHADEMA wakichemka wakamsamehe Zitto kwasababu ya hizi Propaganda za CCM na wapambe wa Zitto, baasi chama kimekufa maana kutakuwa hakuna woga tena kwamba mtu ukitenda kosa laweza kukughalimu, ilimradi tu una vicent vya kufanya Propaganda kwenye vyombo vya Habari basi. Kuna tetesi pia TISS wametoa fungu kubwa tena kwa ZZK ili aanze kucheza na wajumbe wa kamati kuu kwamba ikitokea inaletwa hoja ya kufukuzwa uanachama waigomee, kweli Chadema safari hii mpo kwenye Mtihani mkubwa sana ambao inatakiwa kuufaulu ili TISS wapate hasara hayo mapesa yao na iwakatishe tamaa kwamba pesa siyo kila kitu

Usituletee tetesi hapa tupe facts, zitto hahitaji msamaha wala kuonewa huruma na yeyote CDM, isitoshe hakuna direct allegations zinazomlenga zitto mana usaliti unaosemwa kupitia waraka ameshakujibu haujui na aliyeuandaa huo waraka kathibitisha zitto alikua hajui lolote. Wengi wenu ni comment za chuki binafsi na kufata mkumbo. History ya CDM wote tunaijua so haya yanayotokea c jambo geni kwny hiki chama, ni maamuzi ya wachache wenye ulafi na uchu wa pesa na madaraka. Mtu umegombea urais umecheka, umekuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama for several years still bado unang'ang'ania uwe juu tuuu. Huu ni ubinafsi na uroho wa madaraka na pesa. Wakinyanyuka wengine mnawapiga nyundo kichwani warudi chini. Mnaboa bana na mnajifanya hamjui kama mmepoteza mvuto ndani na nje ya chama mnang'ang'ana tuuu pisheni watu wenye mawazo na mtazamo mpya nao wajaribu kama kweli CDM kuna demokrasia ya kweli. Mbona wakina MCcain na Romney wanagombea once kwani wao hawahitaji fame+authority? Watu wakisema kuna ukanda + udini mnawashambulia kua niwabaguzi. Tulianza na NCCR, tukaja CUF na sasa CDM ndo inapita hivyo tusubiri CCJ kama chama kikuu cha upinzani 2015-20.
 
Nliwajibika baada ya kushindwa kudeliver ndani ya hiko chama. Infact mimi ndie niliejitoa bada ya kuona napingana na chama hasa katika mitizamo na maono. I ve bn there as one of party think tank

Kama na wewe ulikuwa a part to the think tank Basi ndio maana mambo yanaenda halijojo. Your thinking is unable to come up with reasonable idea for propagating sustainable political stability. They must be happy that you left.

But I will issue you a point of correction, you did not differ with the Party, rather you got frustrated because your nonsense ideas and advises were dumped or properly putting it, were properly granted a deaf ear.
 
Na CHADEMA wakichemka wakamsamehe Zitto kwasababu ya hizi Propaganda za CCM na wapambe wa Zitto, baasi chama kimekufa maana kutakuwa hakuna woga tena kwamba mtu ukitenda kosa laweza kukughalimu, ilimradi tu una vicent vya kufanya Propaganda kwenye vyombo vya Habari basi. Kuna tetesi pia TISS wametoa fungu kubwa tena kwa ZZK ili aanze kucheza na wajumbe wa kamati kuu kwamba ikitokea inaletwa hoja ya kufukuzwa uanachama waigomee, kweli Chadema safari hii mpo kwenye Mtihani mkubwa sana ambao inatakiwa kuufaulu ili TISS wapate hasara hayo mapesa yao na iwakatishe tamaa kwamba pesa siyo kila kitu

Mtazamo wako ni sawasawa na wangu kabisa.
Kama CC ya Chadema itashindwa kuwafukuza akina ZZK na wenzake kwa sababu za aina yoyote basi Chadema hata kama hakitakufa leo kitakuwa Chama legelege miaka yote ya uhai wake. Na hao mamluki na wasaliti watachekelea sana kwani watatunga mbinu mmbadala kukisambaratisha kabisa,kwa msaada wa CCM na TISS chama hakitakuwa na jinsi ya kujikwamua tena.
My God Forbid....! Kuwafukuza uanachama ni jambo la muhimu kabisa kwa wakati huu,ili kukiimarisha Chama,bila kufanya hivyo ni kunyong'onyeza mapambano dhidi ya utawala wa KIFISADI wa CCM na serikali yake.
CHADEMA NDIO TUMAINI LA WANYONGE - YUWAFUKUZE TUSIOGOPE.
 
Usituletee tetesi hapa tupe facts, zitto hahitaji msamaha wala kuonewa huruma na yeyote CDM, isitoshe hakuna direct allegations zinazomlenga zitto mana usaliti unaosemwa kupitia waraka ameshakujibu haujui na aliyeuandaa huo waraka kathibitisha zitto alikua hajui lolote. Wengi wenu ni comment za chuki binafsi na kufata mkumbo. History ya CDM wote tunaijua so haya yanayotokea c jambo geni kwny hiki chama, ni maamuzi ya wachache wenye ulafi na uchu wa pesa na madaraka. Mtu umegombea urais umecheka, umekuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama for several years still bado unang'ang'ania uwe juu tuuu. Huu ni ubinafsi na uroho wa madaraka na pesa. Wakinyanyuka wengine mnawapiga nyundo kichwani warudi chini. Mnaboa bana na mnajifanya hamjui kama mmepoteza mvuto ndani na nje ya chama mnang'ang'ana tuuu pisheni watu wenye mawazo na mtazamo mpya nao wajaribu kama kweli CDM kuna demokrasia ya kweli. Mbona wakina MCcain na Romney wanagombea once kwani wao hawahitaji fame+authority? Watu wakisema kuna ukanda + udini mnawashambulia kua niwabaguzi. Tulianza na NCCR, tukaja CUF na sasa CDM ndo inapita hivyo tusubiri CCJ kama chama kikuu cha upinzani 2015-20.
Najua umejiunga leo kumtetea Zitto but it is too late the dude has gone already,

Chama kilipofikia sio tena cha kufanyia majaribio aende Chauma kisicho na misingi akajaribu demokrasia ya sirisiri anayoitaka.
 
Inashangaza kuona vichwa mbalimbali vya habari vikishabikia sakata la akina Zitto Kabwe kama ndio anguko au mpasuko ndani ya CHADEMA. Binafsi sioni kama kuna mpasuko wala vipande ndani ya CHADEMA ila naona kinazidi kuimarika baada ya kugundua mbinu za usaliti na hujuma ambazo zingefanikiwa zingechangia kukivuruga chama.

uzuri magazeti yote yanayoshabikia yanajulikana pro CCM, Mwananchi ni Msaky huyu piga ua ataandika mpaka lipoteze unamba one kwenye soko, RAI- rostam ndio aliyemtuma na kumfadhili kuvuruga vyama, Jambo Leo -Ridhiwani Jakaya Kikwete shemeji wa zitto na mshirika mkuu kwenye uvurugaji, Habari leo lazima wajikombe kwa IKULU maana gazeti linaishi kwa ruzuku hakuna mwenye akili ya kukuza gazeti pale,UHURU gazeti la CCM what do you expect
 
Usituletee tetesi hapa tupe facts, zitto hahitaji msamaha wala kuonewa huruma na yeyote CDM, isitoshe hakuna direct allegations zinazomlenga zitto mana usaliti unaosemwa kupitia waraka ameshakujibu haujui na aliyeuandaa huo waraka kathibitisha zitto alikua hajui lolote. Wengi wenu ni comment za chuki binafsi na kufata mkumbo. History ya CDM wote tunaijua so haya yanayotokea c jambo geni kwny hiki chama, ni maamuzi ya wachache wenye ulafi na uchu wa pesa na madaraka. Mtu umegombea urais umecheka, umekuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama for several years still bado unang'ang'ania uwe juu tuuu. Huu ni ubinafsi na uroho wa madaraka na pesa. Wakinyanyuka wengine mnawapiga nyundo kichwani warudi chini. Mnaboa bana na mnajifanya hamjui kama mmepoteza mvuto ndani na nje ya chama mnang'ang'ana tuuu pisheni watu wenye mawazo na mtazamo mpya nao wajaribu kama kweli CDM kuna demokrasia ya kweli. Mbona wakina MCcain na Romney wanagombea once kwani wao hawahitaji fame+authority? Watu wakisema kuna ukanda + udini mnawashambulia kua niwabaguzi. Tulianza na NCCR, tukaja CUF na sasa CDM ndo inapita hivyo tusubiri CCJ kama chama kikuu cha upinzani 2015-20.

wakati mwingine wat munashangaza sana munataka mutuaminshe zitto eti alikuwa hajui habari za waraka kama alikuwa hajui mbona press yake iliconfrm kamba alikuwa na mpango mbaya kwanza aliandaa press waikuwa UVCCM, tuulize alishindwa kutumia angle nyingine au alikuwa anthibitisha yeye ndio anayoyafanya halafu amejibatiza kwamba yeye ni mfia chama kwa kuropoka ropoka kutegenez mitandao ndani ya chama ka kuwa kiungo cha TISS ,halafu anaita CC wahafidhina huyo zitto merelyhna adabu a kutupa mtoni nitashangaa kama CC watamuacha bila kumfukuza, CCM walimfukuza shibuda kwa kumnyima kugombea na Kikwete Uraisi, kwani hayo huyaoni, Yupo seif Lipumba , Kikwete kagombea uraisi tangu 1995 na mkapa na msuya mbona 2005 aligombea na kushirikisha familia kwa kutumia fedha za Barrick ,usijifanye kipofu wewe w roho wa madaraka ,wasio na demkrasia ni CCM ,wanaoapa kuwawatatawala milele CCM chama mfu wapo kwa mgongo wa dola
 
Usituletee tetesi hapa tupe facts, zitto hahitaji msamaha wala kuonewa huruma na yeyote CDM, isitoshe hakuna direct allegations zinazomlenga zitto mana usaliti unaosemwa kupitia waraka ameshakujibu haujui na aliyeuandaa huo waraka kathibitisha zitto alikua hajui lolote. Wengi wenu ni comment za chuki binafsi na kufata mkumbo. History ya CDM wote tunaijua so haya yanayotokea c jambo geni kwny hiki chama, ni maamuzi ya wachache wenye ulafi na uchu wa pesa na madaraka. Mtu umegombea urais umecheka, umekuwa na wadhifa mkubwa ndani ya chama for several years still bado unang'ang'ania uwe juu tuuu. Huu ni ubinafsi na uroho wa madaraka na pesa. Wakinyanyuka wengine mnawapiga nyundo kichwani warudi chini. Mnaboa bana na mnajifanya hamjui kama mmepoteza mvuto ndani na nje ya chama mnang'ang'ana tuuu pisheni watu wenye mawazo na mtazamo mpya nao wajaribu kama kweli CDM kuna demokrasia ya kweli. Mbona wakina MCcain na Romney wanagombea once kwani wao hawahitaji fame+authority? Watu wakisema kuna ukanda + udini mnawashambulia kua niwabaguzi. Tulianza na NCCR, tukaja CUF na sasa CDM ndo inapita hivyo tusubiri CCJ kama chama kikuu cha upinzani 2015-20.

Pesa ya TISS imeanza kufanya kazi, zitafunguliwa ID hapa hata elfu kumi
Join Date : 29th November 2013
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received 0

Likes Given 0
 
Back
Top Bottom