Uhusiano wiki mbili anaanza kukuita mume wangu

Uhusiano wiki mbili anaanza kukuita mume wangu

lili jina nililomwambia wakati tunatongozana!
 
Hahahaa we ndo mswahili vitu vidogo ivooo itakuwa mgambo weeeh tena bora huyo ungenipata mie nakuita mke wangu kabisa na wee unaniita mme wangu mbona raha!!
Nampenda bby angu ye ananiita mme wangu hata mbele za watu haoni shida na mie namuitikia niambie mke wangu anafuraahi we wa wapi wewee
 
lengo halikuwa baya,sema nilishangwazwa na ile kasi ya kuitwa mume..nkaona ntazoea!
 
Sasa si umwambie kuwa hutaki akuite "mume wangu" sisi tukusaidiaje!
 
sasa kama sina mpango na wewe niitikie tu kama li ngombe?..hujui maneno yanaumba!
 
calling it off!...kama mtu haelewi status yake,ana jipa vyeo tu bila utaratibu,itakuwa rabsha baadae!
 
huyo unayemuita wa kiswahili si umempata uswahilini kwao? ungetaka wa kizungu ungefunga safari uwafuate huko kwenye nchi zao....

na kwanza unaumia wapi kuitwa mume?
wakati mnaanza ulimwambia kuwa lengo lako ni kupita njia tu?
na kama hupendi umeshamwambia?
mmmh dunia ina mambo
 
kwani jina langu analijua,basi jina softer kidogo kama darlingi kidogo hapo sasa hayo ya mume ni kurushana roho tu!
 
wiki mbili mbona nyingi hizo yan alichelewa kukuita mume mbona
 
Madem wa kiswahili bwana,yaani uhusiano wiki mbili tu,mara twende nkakuoneshe mama,mara kila baada ya dakika kumi simu hata haelewi hata kama uko kazini,hilo la kuniita mume ndio limenikera zaidi na kuamua kuchukua hatua kali za kinidhamu.

kaka shukuru mungu kwan wapo watu wanatafuta faraja kama hizo,wew kama humpendi mwache haina sababu ya kugombana.
 
Madem wa kiswahili bwana,yaani uhusiano wiki mbili tu,mara twende nkakuoneshe mama,mara kila baada ya dakika kumi simu hata haelewi hata kama uko kazini,hilo la kuniita mume ndio limenikera zaidi na kuamua kuchukua hatua kali za kinidhamu.
Kama mnafanya kile ambacho mme na mke huwa wanafanya kwanini asikuite mme wake?
Ndo maana inashauriwa usiingie kwenye mahusiano mpaka uwe na uelewa mpana wa uamzi unaotaka kuuchukua.
Tafakari chukua hatua.
 
Back
Top Bottom