Mkuu katika bandiko lako umetaka kujua maana ya uhuru katika mahusiano ni nini?
Ukweli ni kuwa, hakuna maana inayoeleweka na iliyoandikwa ya neno uhuru katika mahusiano nini.
Na hakuna kamusi, wala tume iliyo wahi kuundwa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi ili tupate tafsiri ya neno uhuru katika mahusiano.
Matokeo yake, kila mtu ana tafsiri yake ya neno uhuru katika mahusiano kutokana na mtizamo wake na hisia zake kulingana na mahitaji yake, misimamo yake na utamaduni aliokulia.
Umesema jamaa yako hataki umpigie simu kwa sabb anaona unamuingilia uhuru wake, lakini kuna jamii hapa Tanzania mwanaume hataki akiwa anatoka nyumbani au anarudi kutoka mizungukoni mwanamke amuulize unaenda wapi au unatoka wapi, vinginevyo anaingilia uhuru wa mwanaume. Mifano ni mingi sana.
Kwa hiyo kuna "unwritten rules" kibao zilizojengwa katika msingi wa hisia na mtizamo inayochochewa na dhana, mahitaji binafsi, misimamo na tamaduni juu ya kipi ni sahihi na kipi si sahihi kuhusu uhuru katika mahusiano.
Na kwa mtindo huu wa kila mtu kutafsiri anavyojisikia, matokeo yake ndio mnatumbukia katika migogoro kama hii.
Wewe kimitizamo unaona hakuna shida kumpigia ila mwenzako anaona shida. Na huenda hata sio kwa sabb anakudharau lakn ni misimamo aliojiwekea, mitizamo aliyonayo na hisia alizonazo juu ya suala fulani.
And this is for sure, hutokaa upate mtu mnaye match misimamo, mitizamo, na utamaduni hata kama mnahisia za mapenzi kwa sabb tunatoka sehemu tofauti na tumbo inclusive.
Ndio wenye hekima wakasema ili mahusiano yadumu ni lazima tujifunze kutokubalina vinginevyo utahangaika asubuhi mpaka jioni ikukute.
Kwa hiyo Mkuu "ni kweli mapenzi ni hisia" lakn bila kuzingatia misimamo, mitizamo na utamaduni wa mtu utaendelea kupata tabu sana.
Turudi kwenye hoja ya muongozo unaoeleweka,
Katika muktadha huo, kama hoja ni tafsiri ya uhuru katika mahusiano, we must eliminate all unwritten rules na kuunda written rules ambazo zitakuwa standard na ndio utakuwa muongozo unaoeleweka ninao uzungumzia hapa ili kuondoa misunderstanding zote na diversity.
Na nyezo pekee ninayoijua ambayo hutumika kuondoa misunderstanding ni KATIBA.
So tuwe na "Katiba ya mahusiano ya kimapenzi na ndoa".