Inasikitisha lakini tuangalie hali halisi kwanza. Wabongo wengi ni magumashi when it comes to kufanya kazi. Sisi ni wavivu na watoro wa kazi, wazembe, waongo, na wengi wetu hawana ujuzi wa kazi na wana vyeti bandia. Najuwa wengi wenu mtakasirika ila hizi habari alinitonya mtu muhimu sana maishani mwangu nami nilipo chunguza nikaona ukweli wake. Utakuta mtu kaajiriwa serikalini ila hana taaluma yeyote na hajuwi why yuko pale. Matokeo yake raia unakwenda tafuta huduma unamkuta mtu yuko bize kwenye Istagram na Fesibuku wakati wa kazi na watu kibao wamejaa kusubiri huduma, ukiuliza huduma anakuambia anayeshughulika na hilo suala katoka kumbe ni yeye mwenyewe ila anashindwa tu kukuambia kuwa yuko incompetent. Kingine, utakuta mtumishi wa serikali asiyejuwa jukumu lake, anakwenda kazini kusaini tu kisha anarudi kwenye mataptap, muda wa kazi kwisha ukikaribia ndipo anarudi kusaini out. Who needs to hire ppl like these? We need to change our mentality ya kupenda kufanya kazi bila visingizio na wizara husika kuajiri watu wenye ufanisi na waliosoma si tu watoto wa mjomba na kutuletea madhara haya tuliyonayo sasa ya uzembe na uvivu. Haya makampuni ya kigeni yanajuwa kuwa watanzania ni wazembe na waongo ndiyo maana hawataki ku deal nasi. Je, hata kama wewe mleta mada ni muwekezaji hapa nchini, utapenda kuwekeza kwa watu wavivu na wazembe? Nini lengo lako la kuwekeza, kuingiza pesa au kujipa hasara? Mi nasema, rais Magufuli atumbue watu wa dizaini hii serikalini, wanatuhaibisha watanzania.