Afisa Uhamiaji ni wala Rushwa waliokithiri

Godfirst

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
406
468
Habari wanajamvi,

Leo asubuhi tumepata ugeni wa afisa Toka uhamiaji. Hapo ndiyo nlipojua madudu ya Hawa jamaa.

Ofisi ni ya wachina wameonyeshwa passport wakajiridhisha ila wakawa wanatuhoji Kwa nguvu Kwa kufoka pili wanaongeza vitu vingine ilimradi tu wapate pakuwakawamata Ili watoe fedha.

Wakaona mchina kawashinda wamemchukua mfanyakazi tokea saa sita mpaka mda huu hawajamuachia Kwa kigezo Cha kwamba aliwapiga picha hivyo wanataka laki tano ili wamuachie simu.

Waliingia ofisi ya pili jirani na hapa waliwakuta wachina wawili hawajatembea na passport na sizani kama Wana vibali sababu ni wageni wakapozwa na laki mbili wakawaachia.

Sisi mtu wetu Bado kabebwa na hao maafisa uhamiaji sijui wanampeleka wapi.

Sawa Tanzania imekua nyumba ya mchumia tumbo ila Bora wange deal na huyu mchina wakamuacha huyu wa kwetu.

Wamemfanya kama chambo mpaka tutakapotoa laki tano ndio watamuachia.

Shame on those migration officers who don't work accordingly they work for their pockets.
 
Sasa hivi kila mahali ni rushwa tena ya wazi wazi maana jamaa hawana hata haja ya kujificha tena. Nchi inanuka rushwa hii aisee!

Kuna wahamiaji wengi tu wana kadi za NIDA na passport na siyo raia wa nchi hii. Kwa sasa ni pesa zako tu unafanya cho chote unachotaka katika nchi hii!
 
Tatizo lipo na wenye mamlaka wanajua ila matamshi Yao yanasaidia kulikuwa tatizo. Mfano- waziri uwekezaji anasimama mbele ya kadamnasi nakusema mwekezaji akifeli tutafukuza mchana kweupe Jana Bashe anaagiza mkandarasi awekwe lokapu. Yaani utaratibu na mikataba haiheshimiwi. Ni ubabe ubabe tu. So ajabu Uhamiaji wanatumia ubabe tu
 
Halafu mhabeshi jirani tena mwafrika mwenzetu anafungwa kisa kapita border na wengine wanasema ooh wanahatarisha usalama.

Masikini ya Mungu wana nini hao watafuta maisha

Ila mchina mwenye uchumi mkubwa na wataalamu wa kila aina anaulizwa rushwa na wazalendo wanapokea na kusepa tena ni police hao

Hao wachina wanauwezo wa kutengeneza hata silaha za maangamizi lakini jamaa zetu wanauza nchi kwa Laki 5
Inasikitisha sana
 
Sasa hivi kila mahali ni rushwa tena ya wazi wazi maana jamaa hawana
hata haja ya kujificha tena. Nchi inanuka rushwa hii aisee!

Kuna wahamiaji wengi tu wana kadi za NIDA na passport na siyo raia wa nchi hii. Kwa sasa ni pesa zako tu unafanya cho chote unachotaka katika nchi hii!
Rushwa sahv imepamba moto
Jamaa wa chini nao hawataki kupitwa
Maana washaona huko juu mabilion kwa matrilion yanaliwaa,na wao wameamua wachangamke

Ova
 
Watendaji wengi wa serikali ni wala rushwa.
Wengine wanadai rushwa ni kama tabia, Imesambaa kwa watumishi wengi sio wakubwa sio wadogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom