Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Nipe ufafanuzi hapa kama mtu anaomba passport kwa madhumuni ya masomo baadhi ya vyuo application form huwa zinahitaji passport No hivyo mwombaji akitumia application form badala ya admission letter inakubalika??
Utaratibu mwingine ni mzazi kuandika barua kwa kamishna jenerali kukuombea pasipoti ww binti yake akieleza situation, unapata bila shida. Ile ya kuleta admission ndio ipo kwenye regulations zao labda ni kuwaomba kuzifanyia marekebisho ili ziendane na wakati
 
Uhamiaji kuna tatizo kubwa,nina mtoto anatakiwa akafanye interview ya kujoin shule nchini Africa Kusini mwezi huu January,pamoja na kueleza uharaka uliopo lakini tangu tumelipia passport mwanzoni mwa December tunaambiwa bado.
Ukienda kule mambo ya ndani watu wengine wanaofuatilia wanakwambia passport zao tangu mwezi wa May wanafuatilia.
Endelea kufuatilia
 
Kama kawaida watu wa kanda (maalum) ya ziwa huwa tunasahau hata salamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye mada,
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu vitabu vya hati ya kusafiria, kila mtu anasema lake leo nimekosa kazi nikaenda mapema kujionea makao makuu ya uhamiaji kurasini Dar es salaam, nilikaa kwa masaa mawili nikagundua yafuatayo vile vibanda vya kutoa copy pale nje ni biashara cover up kiuhalisia wale bila kumung'unya maneno nawaita mawakala wa pass port, niliingia duka la kwanza kutoa copy nikakuta kuna watu kadhaa nao wana subiri huduma hiyo yule dada mtoa copy anaongea na simu nanukuu "unataka express ama ya kawaida, kama ni express ni laki tatu inatoka ndani ya wiki" mwisho wa kunukuu yaani alikuwa anaongea bila uwoga na kwa ujasiri ukiangalia dukani humo kuna watu wengi kila mmoja anakukaribisha tena wababa wazima nikabahatika kumuona mmoja anamuhuri wa mwanasheria tayari kwa kutengeneza affidavity sh 15000.

Nikatoka nikaenda duka la pili baada ya kuona pale kuna msururu wa watu yule dada alikuwa ananitolea copy huku ameweka simu masikioni naye anaongea na mtu "ya wiki ni laki 3, wiki mbili laki 2 ya kawaida laki na nusu, kwa wewe unayesafiri haraka ntakupa hii ya laki tatu hiyo haipungui na kama uko serious njoo haraka manake naenda kumuona afisa mkubwa" kilichokuwa kinaendelea pale ni kwamba watu waliokuwa wanafika pale uhamiaji kwa ajili ya ku process passport wanaanza kupokelewa kwa kukatishwa tamaa na yule ndugu anayekaa pale kwenye dawati la huduma kwa wateja hivyo wanashawishika kurudi pale kwa wale watoa copy nje.

Swali langu kama mimi niliyeenda pale kwa mara moja nimejionea hayo niliyoona, hakuna wahusika ambao wanajua kuna biashara hii haramu? na je nani ni wanufaika wa mradi huu. Ntakuwa nikileta mrejesho ambapo kwa ukiwepo ushahidi wa picha na video Kama kuna watu wamekataa kuwajibika ngoja sasa tuwawajibishe [HASHTAG]#unokoniuzalendo[/HASHTAG]
Passport ni 50,000. Anza mipango yako mapema, ukitaka haraka ndo utaumia
 
Ukiingia katika lile jengo.utakayokutana nayo. Lazma uwatafute wale wa nje.
passport ya Tanzania INA masharti mengi.hasa kwa sisi ambao uwa tunaamua kutoka kutafuta maisha.kuna mlolongo was vitu vingi. Mpaka unakata tamaa.
Mimi nilishawahi kupitia hyo hali.na kama viambatanisho havijakamilika.unanyima.sasa kwa nini usitoe rushwa ili upate??
Kama vimabatanisho havijatosha utapataje kihalali. Tatizo watu tunataka shortcut, chukua form, soma.,jaza vinavyotakiwa, na kama huna,tafuta.
 
Kama vimabatanisho havijatosha utapataje kihalali. Tatizo watu tunataka shortcut, chukua form, soma.,jaza vinavyotakiwa, na kama huna,tafuta.
Acha utani.unataka kwenda kutafuta maisha labda Zambia na unataka passport kubwa
.unaambiwa upeleke barua ya mwaliko utaipata wapi?
Vyeti vya kuzaliwa vya wazazi utavipata wapi?
Barua za wadhamini utazipata wapi?
Bado haujamtafuta wakili.akupigie muhuri.yaani ni mambo mengi mengi.
 
Passport ni 50,000. Anza mipango yako mapema, ukitaka haraka ndo utaumia
Usifiche matatizo ambayo yapo, tafadhali tunataka kuondoa tatizo la vishoka kama ilivyokuwa pale TRA miaka ya 2000 kwenue leseni za udereva
 
Kwanza kabisa nakupongeza mtoa post kwa kueleza kile ulichokiona pale Uhamiaji na kuamua kushea nasi!

Mimi sio afisa uhamiaji au mhusika kwa namna yoyotr ile na uhamiaji ila naomba nikujibu kwa ufafanuzi ufuatao;
1. Idara ya Uhamiaji kama utakumbuka mwaka jana ilizindua huduma za e-Services ambapo waombaji wa passport na permit walielekezwa wafanye maombi kupitia website ya idara hio www.immigration.go.tz. wakati huo huo utaratibu wa kujaza fomu za kawaida (hard copy) ukiendelea mpaka stock ya form hizo utakapokwisha na hakuna form zingine kuchapishwa.
2. Stationery zilizopo hapo sio mradi wala hazihusiani na afisa yeyote wa uhamiaji, ni ofisi zilizoanzishwa na watanzania wajasiriamali kujitaftia rizki zao kwa kutoa fotokopi, kupiga picha za passport na wengine wanasheria kufungua ofisi zao humo.

3. Fomu ya passport imewekwa kisheria ndani ya Passport and Travel Documents Act Namba 20 ya Mwaka 2002 ambapo mojawapo ya sharti la fomu kukamilika na kupokelewa na afisa uhamiaji lazima isainiwe na mahakama, mwanasheria au wakili aliyesalijiwa.

4. Affidavid ni suala linalohusika na Mahakama/Wakili/Mwanasheria hivyo afisa uhamiaji ni kuhakikisha kuwa kwenye viambato vyako kama kunahitajika affidavit anakupa maelekezo ukailete, suala la wapi na nani katoa sio la uhamiaji, muhim afisa atajiridhisha kuwa aliyetoa kasajiliwa.

5. Yawezekana kwa sasa form za kawaida (hard copy) zimekwisha ndio maana yule afisa wa kaunta kakuelekeza uende mtandaoni kujaza fomu na ww pamoja na wananchi wengine wakiambiwa hivyo huishia kwenye vibanda hivyo kupata huduma tena kwa bei anayotaka mhudumu ambapo uhamiaji haihusiki kwa namna yoyote ile.

7. Kwa uzoefu wangu najua kwamba passport hutolewa ndani ya siku saba hadi 14 lakini pia huwa kuna wahitaji wanaotakiwa kupata passport kwa haraka zaidi mfano kuwahishwa kwenye matibabu nchini India, Uhamiaji kwa kuwajali wananchi hutoa kipaumbele kwa watu wa namna hio.

8. Asilimia kubwa wa wateja wa huduma za uhamiaji huwa waoga na hivyo kuomba kusaidiwa hata kujaza fomu tu ya maombi, mfano ninao kuna dogo mmoja alikuwa kwenye stationery moja kazi yake kujaza fomu tu na kila fomu akijaza kwa elfu 2. Sasa leo kiti kipo mtandaoni unategemea dogo atakuwa anapiga bei gani?

I stand to be criticized

6.
Hata sisi tunayajua uliyoyaeleza ila uhalisia ni tofauti kabisa na haya maelezo. Kurasini pale rushwa inanadiwa bila uoga kabisa.
 
Usifiche matatizo ambayo yapo, tafadhali tunataka kuondoa tatizo la vishoka kama ilivyokuwa pale TRA miaka ya 2000 kwenue leseni za udereva
Ok, kama ni kuondoa vishoka ni sisi kufuata tu taratibu za uhamiaji na kuachana nao. Mi toka 2002 nina passport na wala sijawahi kutumia kishoka. Nimerenew hapohapo kurasini na wala sijasumbuliwa na sijaonana na kishoka.

Sent from my PHANTOM5 using JamiiForums mobile app
 
Acha utani.unataka kwenda kutafuta maisha labda Zambia na unataka passport kubwa
.unaambiwa upeleke barua ya mwaliko utaipata wapi?
Vyeti vya kuzaliwa vya wazazi utavipata wapi?
Barua za wadhamini utazipata wapi?
Bado haujamtafuta wakili.akupigie muhuri.yaani ni mambo mengi mengi.
Vyeti vya kuzaliwa vya wazazi hata kesho nenda Rita utapewa

Sent from my PHANTOM5 using JamiiForums mobile app
 
Passport nimeomba toka September 2017, nimefuata taratibu zote kama walivyo nielekeza nikaweka viambatanisho vyote, fomu wakaikagua wakaniambia iko sawa... na Bank nikalipia, wakanichukua na finger prints kabisa...

Ila sasa toka hiyo September hadi hivi leo Passport yangu bado haijatoka..... Alafu kuna mtu anatoa laki tatu anapata ndani ya wiki.
Ndani ya siku 3 kama ushajaza form na kumaliza kila kitu, printing siku 3. Hapana chezea Bongo!
 
Daah
Ushaharibu mkuu madili ya watu.lakini uko sahihi
Kuna wakati nilitaka kwenda sauzi kutafuta maisha.nikaenda pale nikajionea haya.
ukitaka ya 50,000 utaganda.
.
Aaah kumbe za serikali nazo zinauzwa kwa elfu 50000?
Sasa kuna shida gani kwa mtu kuongeza dau apate mapema kama hizi za elfu50 zinachelewa?
Mie nilidhani labda madaraja yanatofautiana kwamba ya eflu hamsini ni daraja tofauti na ya laki tatu kumbe kitu ni kile kile?
Hata kaa mie wenye haraka zao ningewapa kipaumbele kupunguza msongamano
 
Back
Top Bottom