Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Inawezekana kukawa na connection baina ya afisa na vishoka ila sio kwa utawala wa huyu mama kamishna.

Nakumbuka mara ya mwisho watu wanaohisiwa vishoka karibu 8 walikamatwa pale kupigwa picha na kuamriwa kutofika eneo hilo na iwapo wataonekana watakamatwa na kufikishwa mahakamani


NI kweli huyo Mama ni msaada ana commitment isipokuwa kuna watu wa ngazi za chini wanamharibia, kuna ndugu yangu alikuwa anahitaji kusafiri akaambiwa na maafisa wa dirishani pass ingepatikana siku ya pili, nikamdirect kwa ofisa mmoja kule ofisi zao za mjini, akamwambia arudi kwa aliyemjazisha forms amwambie ampe pass siku hiyohiyo kabla ya saa ya kufunga ofisi, muda mfupi tu maafisa wa Kurasini wakaanza kumtafuta kwenye simu aende akachukue pass, kwahiyo kilichopo ni ujanjaujanja wa hao wa chini
 
Passport nimeomba toka September 2017, nimefuata taratibu zote kama walivyo nielekeza nikaweka viambatanisho vyote, fomu wakaikagua wakaniambia iko sawa... na Bank nikalipia, wakanichukua na finger prints kabisa...

Ila sasa toka hiyo September hadi hivi leo Passport yangu bado haijatoka..... Alafu kuna mtu anatoa laki tatu anapata ndani ya wiki.
Fuatilia kama imetoka. Kuna jamaa yangu nae alikuwa anadai haijatoka nikamshauri afuatilie akaambiwa ishatoka siku nyingi akaenda ofisi ya mkoa kuichukua. Hawana utaratibu wa kukujulisha kama imetoka. Fiatilia mama
 
Fuatilia kama imetoka. Kuna jamaa yangu nae alikuwa anadai haijatoka nikamshauri afuatilie akaambiwa ishatoka siku nyingi akaenda ofisi ya mkoa kuichukua. Hawana utaratibu wa kukujulisha kama imetoka. Fiatilia mama

Mimi mwenyewe ni Mkenya. Nilipoona maswala ya ku-apply passport yamechukua mkondo mpya kama Kenya (online platform), nilidhani itakuwa nafuu na itarahisisha mambo. Huku Tz mlolongo ni mrefu na makaratasi ni mengi sana. Inasikitisha sana hamna hata Twitter ama Facebook Accounts ambazo wateja wanaweza kufuatilia hatma za passports.


Yaani hawa jamaa wa immigration ni wazinguaji tu. Hata ufuate taratibu zote zilizowekwa , lazima watakuzungusha tu ilimradi wapate chao. Mke wangu na binti yangu wali-apply passport tangu October 2017,aliambiwa mwezi Disemba,,,,,,,kaenda Disemba 1, akaambiwa Januari 2018. Akarudi Kurasini alikochukulia, akaambiwa aelekee Posta, Alikuwa huko wiki iliyopita, akaambiwa aende Kurasini. Alienda Kurasini Jumanne, ameambiwa fomu hazionekani n na majina hayapo kwenye orodha,,,,aandike majina upya fomu zitafutwe halafu atapigiwa simu Alhamisi jana. Ni kimya tu...............Dah!
 
Kama kawaida watu wa kanda (maalum) ya ziwa huwa tunasahau hata salamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye mada,
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu vitabu vya hati ya kusafiria, kila mtu anasema lake leo nimekosa kazi nikaenda mapema kujionea makao makuu ya uhamiaji kurasini Dar es salaam, nilikaa kwa masaa mawili nikagundua yafuatayo vile vibanda vya kutoa copy pale nje ni biashara cover up kiuhalisia wale bila kumung'unya maneno nawaita mawakala wa pass port, niliingia duka la kwanza kutoa copy nikakuta kuna watu kadhaa nao wana subiri huduma hiyo yule dada mtoa copy anaongea na simu nanukuu "unataka express ama ya kawaida, kama ni express ni laki tatu inatoka ndani ya wiki" mwisho wa kunukuu yaani alikuwa anaongea bila uwoga na kwa ujasiri ukiangalia dukani humo kuna watu wengi kila mmoja anakukaribisha tena wababa wazima nikabahatika kumuona mmoja anamuhuri wa mwanasheria tayari kwa kutengeneza affidavity sh 15000.

Nikatoka nikaenda duka la pili baada ya kuona pale kuna msururu wa watu yule dada alikuwa ananitolea copy huku ameweka simu masikioni naye anaongea na mtu "ya wiki ni laki 3, wiki mbili laki 2 ya kawaida laki na nusu, kwa wewe unayesafiri haraka ntakupa hii ya laki tatu hiyo haipungui na kama uko serious njoo haraka manake naenda kumuona afisa mkubwa" kilichokuwa kinaendelea pale ni kwamba watu waliokuwa wanafika pale uhamiaji kwa ajili ya ku process passport wanaanza kupokelewa kwa kukatishwa tamaa na yule ndugu anayekaa pale kwenye dawati la huduma kwa wateja hivyo wanashawishika kurudi pale kwa wale watoa copy nje.

Swali langu kama mimi niliyeenda pale kwa mara moja nimejionea hayo niliyoona, hakuna wahusika ambao wanajua kuna biashara hii haramu? na je nani ni wanufaika wa mradi huu. Ntakuwa nikileta mrejesho ambapo kwa ukiwepo ushahidi wa picha na video Kama kuna watu wamekataa kuwajibika ngoja sasa tuwawajibishe [HASHTAG]#unokoniuzalendo[/HASHTAG]
Sidhani kama iko hivyo mbona jamaa zetu wawili waliomba pasi bila rushwa na ndani ya wiki wakapa na walienda ufaransa ktk meeting na wamerudi salama.
 
Watanzania wengi ZIMAMOTO. Na wengi ujuaji mwingi, tena aiku hiz ndo kujazia online hizo application bado nashangaa watu wanatoa rushwa. Maajabu haya. Sitoi rushwa, hata makosa ya barabarani, kama nina kosa niandikie faini nilipe.
Mkuu huko barabarani mtu anatoa rushwa kama ipo chini ya adhabu, amount ya rushwa ni ndogo kuliko adhabu otherwise hakuna logic.
 
Hayo madudu yalikuwa kwa sana kipindi cha JK.
Kumbe hao ma ofsa wa uhamiaji bado hawajabadilika?
Tiss watawasambaratisha wote hao.
Just matter of time
 
Online ppt form
Kutoa rushwa immigration utake mwenyewe tu. Mambo yote online, utaenda ofisini kwao kuchukuliwa alama za vidole na kukabidhi viambatanisho tu, na siku ya kuchukua passport yako.
 
hapo ni shida aisee.
mpaka nimepata pass yangu ilibidi nijiongeze sana nimefika U.S wazungu wameninunia nilivyochelewa kufika,nusura waniharibie hao Uhamiaji,na mimi sitoagi hela kwenye haki yangu,nilibanana nao hadi wakasanda,ila walinichelewesha sana.
 
Online ppt form
Kutoa rushwa immigration utake mwenyewe tu. Mambo yote online, utaenda ofisini kwao kuchukuliwa alama za vidole na kukabidhi viambatanisho tu, na siku ya kuchukua passport yako.
Jidanganye. Hiyo form ukienda nayo utaambiwa haina reference # na utarudishwa kule kule kwa watu wa stationaries ukajibu tena maswali yale yale. Huko utatozwa pesa pia na process itabidi ianze upya. Sijui hata wameweka hizi fomu online za nini kama hazina reference #. Kidogo niwatemee mate waliponiambia eti fomu niliyojaza haina ref. Namba wakati ndiyo hiyo katika website yao. Pathetic !!!
 
Kwa madhumuni ya masomo baadhi ya vyuo application form au scholarship zinahitaji poassport ID hivyo ukisubmitt zile form badala ya admission letter zinakubalika???
 
Watanzania wengi tuna shida sana. Labda nikwambie kitu, Passport ni kitambulisho cha raia wa kigeni ndani ya nchi ambayo mwenye pasipoti sio raia. Pamoja na kwamba pasipoti anapewa mtu lakin bado inabaki ni mali ya serikali kwa maana matumizi ya hio pasipoti yaendane na kufuata sheria na taratibu za kiuhamiaji kwa nchi unayokwenda.

Sasa pamoja na kwamba pasipoti ni haki ya kila raia lakin lazima ukidhi vigezo vilivyowekwa kisheria ili kuweza kupatq pasipoti. Pamoja na kuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, afidavit na vitambulisho vyote lakin lazima ulete documents za MADHUMUNI ya safari ambazo wengi hapo huwa wanakwama.

Madhumuni ya safari ndio yanayopelekea raia wa Tanzania upewe pasipoti kwani sio kitambulisho cha kukaa nacho ndani ni kitambulisho chako ukiwa nje ya nchi.

1.Madhumuni yanaweza kuwa ni Matembezi Binafsi hapa utatakiwa kuleta bank statement ili kujiridhisha kuwa huko uendako hutoigharimu serikali kukuridisha nchini baada ya kuwa Destitute huko. Binafsi ingine unaweza kuwa unaenda kumtembelea nduguyo nje ya nchi hivyo utatakiwa kuleta barua ya mwaliko na pasipoti na permit ya nduguyo huko aliko kama ni mtanzania, kama ni raia wa huko basi anatakiwa aandike barua ya mwaliko pamoja na kitambulisho cha uraia wake au paspoti.

2. Madhumini ya kibiashara unatakiwa kuwa na leseni na tin namba

3. Madhumini ya kimasomo unatakiwa kuwa na admission letter toka chuo unachokwenda kusoma.

4. Madhumini ya kidini, barua ya bakwata kwa mahujaji na barua zingine toka taasisi za kidini kama kanisani kwa ziara za kwenda israel.

Mengine utaongezea na ww ila jua kuwa vijana wengi wanadanganya wamealikwa na ndugu zao arabuni kumbe wanaenda kuwa watumwa wa kingono na mahausigeli tu. Watanzania wengi wanaoenda Sauzi wanakuwa mapusha na mateja kiti kinachoitia aibu serikali kila mara na pia kuigharimu kuwaridisha nchini.
Nipe ufafanuzi hapa kama mtu anaomba passport kwa madhumuni ya masomo baadhi ya vyuo application form huwa zinahitaji passport No hivyo mwombaji akitumia application form badala ya admission letter inakubalika??
 
Uhamiaji kuna tatizo kubwa,nina mtoto anatakiwa akafanye interview ya kujoin shule nchini Africa Kusini mwezi huu January,pamoja na kueleza uharaka uliopo lakini tangu tumelipia passport mwanzoni mwa December tunaambiwa bado.
Ukienda kule mambo ya ndani watu wengine wanaofuatilia wanakwambia passport zao tangu mwezi wa May wanafuatilia.
 
Passport nimeomba toka September 2017, nimefuata taratibu zote kama walivyo nielekeza nikaweka viambatanisho vyote, fomu wakaikagua wakaniambia iko sawa... na Bank nikalipia, wakanichukua na finger prints kabisa...

Ila sasa toka hiyo September hadi hivi leo Passport yangu bado haijatoka..... Alafu kuna mtu anatoa laki tatu anapata ndani ya wiki.
Nchi hii sijui kama juhudi za JPM pekee zitazaa matunda na huu mwezi January ndio tutaisoma namba kwa rushwa.
 
We umejua kabisa mtoa copy sio afisa uhamiaji i mean ni kishoka sasa kwa nini utake kuhudumiwa nae na unajua kabisa yule lazima awe kama kishoka ambae ameongeza kiasi chake kwa juu.Yaani mi ninachoona hapa ni kama kupewa kazi ya kupigisha mswaki mamba so usishangae kumezwa.
Mkuu yanayosemwa yanaweza kua na ukweli,mim niliomba passport tangu mwaka jana mwezi wa saba hadi leo nakuambia sijaipata kila nikienda wananipa kalenda tena wanakwambia kama unaharaka kachukue ile ya temporary sasa unajiuliza kama ningeitaka ya tempo ningelipia kubwaa imefikia hadi nimeamua kukaa tu kimya maana sasa hivi hawaruhusu hata kwenda ndani mwisho pale mapokezi tu sasa hilo nalo liangaliwe vizuri maana linaaribu sana future za watu
 
Back
Top Bottom